LATIFA NTANGA
0719618409
Moyo wa Lisa ulikuwa kwenye maumivu makali sana, aliumia na kujiona hana thamani kabisa yote kwa sababu ya mpenzi wake, Alimpenda sana Romeo sana kutoka moyoni mwake, Alimuona ndio mwanaume wa maisha yake matokeo yake kila siku anamfumania na wanawake, Lisa aliumia sana. Aliendesha gari hadi nyumbani kwao akaingia ndani na kujifungia chumbani kwake huko akaanza kulia sana tena kwa uchungu. Alijisikia maumivu makali sana tena makubwa haswa Lisa alilia na kulia kwa uchungu.
"Romeo kwanini unanifanyia hivi kwanini?" Alilia sana Lisa. Usingizi mzito ulimpitia baada ya kilio cha muda mrefu.
***
Romeo alimtizama Mwanakombo na kujikuta hisia zinapanda na nyoka wake taratibu anainuka. Ila alipomkumbuka Lisa tu moyo wake ulijisikia hatia kubwa sana.
"Mwakambombo inuka" Alisema Romeo.
"Baby njoo jamani" Mwanakombo alisema kwa sauti ya mahaba haswa!
"Nisikie inuka" Alisema Romeo kwa sauti ya kuamrisha.
Basi Mwanakombo akainuka na kukaa kitako.
"Vaa kanga yako!" Alisema Romeo kwa sauti kavu isiyo na masihara kabisa.
"Kuna nini mpenzi wangu jamani?" Aliuliza kwa uoga Mwanakombo sababu hali aliyokuwa nayo Romeo ilimtisha.
"Hivi Mwanakombo unaakili timamu wewe kitendo alichokifanya leo ni kizuri?" Aliuliza Romeo.
"Kitendo gani tena mpenzi?" Aliuliza Mwanakombo.
"Usijisahaulishe nasema usijitoe ufahamu! Hivi ulikuwa hujui kuhusu Lisa siku ya kwanza sikukwambia na tulikubaliana nini? Kwanini uniharibie kwake unajua nimetoka naye wapi yule?" Aliuliza Romeo akiwa amechukia haswa, Alikuwa mhuni ila alimpenda sana Lisa yani alikuwa akiyafanya ila moyo wake upo kwa Lisa pekee hao wengine alitembea nao kwa tamaa tu hakuna msichana aliyempenda kama Lisa, kikubwa mno Lisa alikuwa na akili ya maisha si mwanamke wa starehe, Alimtakia mema awe na maendeleo yake tofauti na wanwake wengine wao wanawaza starehe tu wakikutana wafanye mapenzi bila kumshauri mambo ya maana.
"Babu weee usinichanganye yule mwanamke na mie mwanamke kama yeye anayo k na mie ninayo shida nini tusichoshane hapa, umetoka naye mbali mmetoka tumboni wote mkazaliwa siku moja kwanza mimi mzuri najiamini huyo Lisa wako anakitu gani mweusi mfyuuu" Mwanakombo alisema kwa kujitapa na kumfanya Romeo azidishe hasira zaidi.
"Mwanakombo inuka na utoke humu ndani" alisema Romeo kwa sauti ya chini.
"Sasa niende wapi mbona sikuelewi kama Lisa ushaachana nae tukae tupange maisha yetu yatakuwaje"
"Narudia kwa mara ya mwisho inuka na utoke humu ndani"
"Bwana eeeh usinitishe mimi sitoki hapa ndio.... Paaaaah!" Kabla hajaendelea kuongea alishtukia kapigwa kofi zito usoni Mwanakombo akaanza kuona nyota na hapo hapo Romeo akamshika mkono na kumvuta akamtoa nje na kufunga mlango wake.
"Tena iwe mwanzo na mwisho leo kunifahamu" alisema Romeo baada ya kufungua mlango na akaufunga na kujilaza kitandani. Hapo akili yote ilikuwa haisomi, akachukua simu na kuanza kumpigia Lisa ambaye hakuwa akipokea.
"Dah sijui nifanyaje? Hivi Lisa si anaweza kujidhuru yule" aliwaza Romeo na hakutaka kusubiria akavaa nguo zake vizuri na kutoka. Nje akapanda bodaboda ikampeleka hadi nyumbani kwao Lisa kwa sababu alikuwa akijulikana haikuwa shida akafika na kuingia ndani bahati nzuri alimkuta mama yake Lisa na baba yake hakuwepo.
"Ooh Romeo, za siku nyingi naona leo umetukumbuka jamani?" Alipokelewa kwa furaha na bi Lucy mama yake Lisa.
"Nipo mama, shikamoo!" Alisalimia kwa heshima na adabu Romeo sababu alimuheshimu sana huyo mama alikuwa na roho nzuri sana, mpole mcheshi mwenye kujali sana.
"Marahaba mwanangu, haya za masiku tele"
"Salama mama Mungu anasaidia"
"Oh sasa hivi unafanya kazi gani kwani?" Aliuliza bi Lucy na Romeo akaogopa kusema ni mchora Tattoo.
"Ah mama nimefungua duka la nguo nauza" Romeo alidanganya.
"Oh ni vizuri sana mwanangu unajua maisha magumu inabidi kuhangaika kufanya kazi kwa bidii"
"Ni kweli kabisa mama"
"Eeh unisamehe mwanangu yani mgeni hata maji sijakupa"
"Hapana mama usijali hapa nyumbani mbon"
"Subiri bwana hapa kwako Romeo" Alisema huyo mama akainuka na kwenda jikoni ambapo akasaidiana na msichana wa kazi wakatenga chai mezani.
"Romeo karibu mezani tupate kifungua kinywa"
"Haya mama asante sana" Romeo alisimama na kwenda mezani akamimina chai nusu kwa sababu hata hamu ya kula hakuwa nayo ila alimuheshimu huyo mama aliishi naye vizuri sana wakati akifanya kazi hapo ndani. Alikuwa ni kama mama yake sababu bi Lucy alikuwa na upendo sana kwa wote.
"Lisa leo sijui anaumwa hajaamka hadi sasa" alisema bi Lucy akainuka na kwenda chumbani kwa Lisa akafungua mlango na kuingia ndani.
"Mwanangu..Lisa wewee unalala hadi sasa kwanini?" Aliuliza mama Lisa na kuanza kumuamsha mwanae alishangaa anamuamsha muda mrefu bila kuamka, ikabidi amgeuze upande wa pili alipolala.
"Mamaaaaaaaaaaa!"
Sauti kali ya mshtuko ilimtoka bi Lucy na kufanya Romeo asikie na kutoka mbio hadi chumbani kwa Lisa alichokiona hakuamini.!!
Itaendelea.
Lipia buku sasa upate vipande 7. 0719618409 jina lisa ntanga.
0 Comments