LATIFA NTANGA
0719618409
Ilikuwa siku ya jumamosi ambapo Mzee Charles alirudi nyumbani kwake akiwa ameongozana na kijana wa miaka kama ishirini na moja. Alifika nae na kumtamburisha kwa familia yake mke na watoto wawili.
"Jamani huyu kijana anaitwa Romeo ndio atakuwa msaidizi wa kazi za kule nje kuhusu mazingira pamoja na mifugo humu ndani" Alisema Mzee Charles.
"Sawa hakuna shida, Romeo karibu sana mwanangu" Bi Lucy alimkaribisha Romeo.
"Nashukuru sana Mama!" Aliitikia Romeo kwa adabu zote.
"Lisa kaka yenu huyu mumpe ushirikiano" Alisema Mzee Charles.
"Sawa baba, Romeo karibu" Alisema Lisa kwa bashasha usoni.
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza Romeo kukaribishwa kwenye familia ya Mzee Charles. Alianza kazi zake rasmi huku akiishi kwa furaha na amani, kwa sababu hiyo familia ilikuwa na upendo sana. Walimpenda Romeo na kumuona ni kama kijana wao pia. Alifanya kazi zake vuzuri na kulipwa mshahara wake bila tatizo lolote, mazoea yalianza kati ya Romeo na Lisa ambapo mara nyingi walikuwa wakikaa pamoja kuongea kula na siku ambazo wazazi wake Lisa wakitoka na Lisa kubakia nyumbani alikuwa huru sana na Romeo. Ghafla mapenzi yakachipua kwao wakajikuta wanapendana sana. Lisa akamshauri Romeo aache kazi hapo kwao na pesa alizokuwa nazo Romeo na Lisa akamuongezea nyingine baada ya hapo Romeo akaondoka nyumbani kwao Lisa na kupanga chumba chake huku uhusiano wao ukiongezeka siku hadi siku, walikuwa wanapenda sana. Na kilichokuwa kinasubiriwa ni Lisa amalize masomo yake baada ya hapo Romeo akajitamburishe kwao afuate taratibu zote mwisho wafunge ndoa, Lisa ndani ya shela na Romeo ndani ya suti.
***
Moyo wa Lisa uliuma sana kila alipomfikiria Romeo, alimpenda mno huyo mwanaume lakini kitendo cha kumfumania alijisikia unyonge sana. Moyo wake uliuma haswa alilia na kulia bila kupata jibu. Akili ya haraka ilimwambia ni bora anywe sumu afe, kwa uchungu aliokuwa nao Lisa alijikuta anakubali maamuzi hayo akaingia stoo wanapohifadhia madawa na sumu za wadudu kwenye mifugo yao, hakuuliza alichukua na kukoroga kwenye maji akanywa huku akiwa analia sana.
"Romeo kwaheri mie natangulia mbinguni" Alisema Lisa akiwa anasikia maumivu makali sana alijinyonga kitandani akiugulia maumivu hadi pale alipoishiwa nguvu akalegea na kupoteza fahamu.
Mama Lisa macho yalimtoka baada ya kumuona mwanae anatokwa mapovu mdomoni huku akiwa hana nguvu amelegea mwili mzima. Alipiga kelele kali zilizomshtua Romeo ndani ambaye alitoka mbio na kwenda hadi chumbani kwa Lisa akaone kuna kitu gani, na yeye alipoingia alishangaa sana baada ya kuona Lisa anatokwa na mapovu mdomoni.
"Mungu wangu! Lisa umekunywa sumu?" Alisema Romeo kwa sauti na kuwa kama amepagawa.
"Romeo nenda chumbani kwangu kachukue funguo ya gari tumpeleke hospitali" Alisema Mama Lisa ambaye alikuwa amechanganyikiwa sana. Mdogo wake Lisa na yeye akaenda chumbani na kushangaa hali aliyokuwa nayo dada yake alianza kulia kwa sauti.
"Ayan nyamaza usilie dada atapona sawa eeeh" Alisema Mama Lisa akijikaza huku machozi yakishindwa kujizuia na kumtoka, Romeo alirudi na funguo akambeba Lisa na kutoka naye nje. Mama Lisa akachukua simu yake na kuondoka pamoja na Ayan wakapanda gari huku dereva akiwa ni Romeo akalitoa gari kwa kasi na safari ya kwenda hospitali ikaanza.
"Mama hospitali gani?" Aliuliza Romeo.
"Anna Maria hospitali twende" Alisema Mama Lisa na kumuelekeza hospitali ya masista ambayo walikuwa wanatibiwa hapo familia nzima. Basi nusu saa ilitosha wakafika na Lisa akapokelewa na kuingizwa ndani kupatiwa huduma ya kwanza, Mama Lisa alikaa chini amejiinamia. Ayan ndiye alichukua simu yake na kumpigia baba yake.
"Baba, dada Lisa amekunywa sumu tupo hospitali" alisema Ayan na kumfanya Mzee Charles aanguke kwa presha ofisini kwake.
Itaendelea.
Lipia buku sasa upate vipande 7. 0719618409 lisa ntanga.
0 Comments