Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-17



LATIFA NTANGA
0719618409
Mzee Charles alikuwa ofisini kwake mbele yake kuna meza kubwa iliyojaa mafaili mengi, pembeni kuna laptop yake nzuri alikuwa na kikombe cha kahawa anakunywa taratibu huku akipitia kazi zake, hakuwa na papara Mzee huyo mwenye pesa zake. Aliondoka nyumbani na kuiacha familia yake salama kabisa kwake yeye mke na watoto wake walikuwa ndio kila kitu alimpenda sana bi Lucy mke wake, zaidi aliwapenda mno Lisa na Ayan watoto wake wa pekee. Kwake pesa haikuwa na thamani kama hao watoto ambao alijivunia sana kuwa nao. Japo kuwa Ayan alikuwa ni mdogo bado ila alimpa kila alichohitaji na hata asichohitaji na umri wake mdogo huo alikuwa na simu pamoja na laptop kabisa na alijua kuvitumia vyote. Mzee Charles alikuwa radhi apigiwe simu na mtu yoyote yule asipokee ila sio mke na wanae, yani hatakama yupo kwenye kikao simu inaita atapokea tu. Aliipenda sana familia yake. Siku hiyo akiwa anaendelea na kazi zake, akashangaa simu yake inaita na mpigaji ni Ayan alijikuta anatabasamu mwenyewe.
"Haloo mwanangu!" Alisema kwa furaha Mzee Charles.
"Baba, dada Lisa amekunywa sumu tupo hospitali" Alisema Ayan na kumfanya Mzee Charles mapigo ya moyo yapige kwa nguvu sana hapo hapo akahisi presha ikimpanda, akaanguka chini huku moyo ukimuenda mbio sana.
"Haloo..baba...baaa..baba! Haloo" Ayan alikuwa anaitwa na kuona simu ipo kimya. Hapo akamzindua mama yake ambaye hakuwa akijua kama mwanae alimpigia simu baba yake.
"Ayan unaongea na nani?" Aliuliza bi Lucy.
"Mama nilimpigia simu baba kumwambia dada Lisa amekunywa sumu" Alisema Ayan.
"Yesu wangu! Ayan kwanini umempigia simu baba unajua anapresha yule jamani oh mama wee" Bi Lucy alizidi kupagawa, alijaribu kupiga simu ya mume wake lakini hakuweza kupokea.
"Oh Mungu mlinde mume wangu mimi" Lucy alisema na kuzidi kulia kwa uchungu hakuweza kujizuia tena alitoa kilio cha maumivu sana alipomfikiria mtoto wake Lisa moyo ulimuuma sana hakujua kwanini aliamua kunywa sumu, alipomfikiria mume wake na yeye pamoja na presha yake ya kupanda alizidi kuumia na kuona dunia nzima inamuelemea yeye tu.
"Mama pole nyamaza tujue tunafanyaje" Romeo ilibidi amtulize mama Lisa.
"Naumia sana Romeo familia yangu mimi..mwanangu sijui kapatwa na kitu gani mume wangu na yeye..ooohh" Bi Lucy alizidi kulia tu.
"Mama jaribu kumpigia simu baba basi" Alishauri Romeo.
"Hapokei...simu" Alisema kwa kilio cha kwikwi Bi Lucy,
"Usilie mama, kwani hauna namba hata ya mfanyakazi wake mmoja umpigie simu" Alisema Romeo na bi Lucy akatoa simu yake na kuangalia namba za wafanyakazi wa mumewe akawapata na kuongea nao ambapo moja kwa moja walienda hadi ofisini na kumkuta Mzee Charles yupo chini basi wakamtoa hadi nje na kumuwahisha hospitali.
Itaendelea.
Ukilipa buku vipande 7 buku 2 vipande 14.
Tigo 0719618409
Voda 0763361677
halotel 0625783855
Airtel 0784072838
Namba zote jina Lisa Ntanga.

Post a Comment

0 Comments