LATIFA NTANGA
0719618409
Akili ya Mama Lisa ilikuwa kama imeshtuka baada ya Romeo kumuuliza kama anayo namba ya mfanyakazi wa mume wake, alikuwa kavurugwa akili yote haisomi wala hakukumbuka kumpigia mfanyakazi yoyote kuongea naye.
Hapo hapo akachukua simu nakutafuta namba za wafanyakazi wa mumewe. Aliipata ya karibu nakuipiga.
"Haloo, Frank naomba nenda ofisini kwa mzee Charles.. Kamuangalie" Alisema Mama Lisa bila hata salamu.
"Mama kwema lakini?" Aliuliza Frank ambaye alishangaa siku hiyo kupigiwa simu bila hata salamu na hakumzoea mama Lisa akiwa hivyo.
"Frank mwanangu nenda kwanza kamuangalie baba yako ndani" Alisema Mama Lisa na hapo hapo Frank akakata simu na kwenda hadi ofisini kwa Mzee Charles ambapo alimkuta yupo chini, Aliogopa sana! Akatoka na kwenda kuwaita wafanyakazi wenzake ambapo wakaingia ndani na kushangaa zaidi hali aliyokuwa nayo bosi wao.
"Jamani imekuaje bosi amepatwa na nini?" Aliuliza Daud.
"Hakuna anayejua hilo, hebu tumpelekeni hospitali kwanza" Alisema Frank na kwa pamoja wakasaidiana na kumbeba bosi wao wakamtoa nje na kumpakia kwenye gari Safari ikaanza. Walifika hospitali salama na Mzee Charles akapokelewa na manesi na kupelekwa hadi ndani alipoanza kupatiwa huduma.
"Nani ndugu wa huyu mgonjwa?" Aliuliza nesi mmoja.
"Huyo ni bosi wetu tumemkuta ameanguka ofisini" Alisema Daud
"Sawa anapresha huyu baba anaangukaga mara kwa mara au?" Aliuliza nesi huyo.
"Hapana hatufahamu hii ndio mara ya kwanza" Alisema Frank.
"Oh sawa subirini hapo basi" alisema nesi na kuondoka akarudi kwenye chumba ambacho aliingizwa Mzee Charles.
"Kwani imekuaje leo sijaelewa ujue"Alisema Daud.
"Unajua nilikuwa ofisini kwangu naendelea na ile kazi ya jana kuhusu wale waarabu, sasa ghafla nashangaa simu inaita kuchek jina ni mama mke wa bosi nikashangaa kuna nini hadi anipigie na yule mama namuheshimu sana jamani mama mpole yule, anahuruma sana" Alisema Frank.
"Ni kweli bi Lucy ni Mama wa kuigwa sana yani nampenda sana yule mama" Alisema Daud.
"Basi bwana nikashangaa zaidi hakuna salamu wala nini, mama anasemaje nenda ofisini kwa baba kamuangalie, dah nilishtuka sana imekuaje bosi amepatwa na nini sikutaka kuuliza sana basi nikaenda ndio nikamkuta bosi yupo chini niliogopa sana!" Alisema Frank.
"Dah mtihani sana huo ila utakuwa kuna tatizo kwao sio rahisi hili jambo" Alisema Daud.
"Itakuwa hivyo bwana tena ngoja nimjulishe mama kuwa tupo nae hospitali" Alisema Frank na kutoa simu yake akampigia mama Lisa.
**
Mama Lisa alikuwa amekaa kajiinamia tu muda wote huo mlango wa chumba alicholazwa Lisa haikuwa umefunguliwa si Romeo wala mama Lisa ambaye alikuwa anaongea kila mmoja alikuwa kimya kajiinamia kwake na mawazo yake kichwani. Mlio wa simu ndio uliwashtua na mama Lisa akaangalia mpigaji akamuona ni Frank.
"Haloo" Aliita kwa unyonge kwani hata nguvu mwilini hakuwa nazo.
"Eeh mama, tulimkuta baba amepoteza fahamu chini ila tumewahi kumuwahisha hospitali" Alisema Frank.
"Sawa mwanangu nashukuru sana mtaniambia maendeleo yake" Alisema bi Lucy kwa unyonge haswa.
"Sawa mama usijali"Alijibu Frank na kukata simu ambapo aliona mlango wa chumba alicholazwa Mzee Charles ulifunguliwa na akashangaa Mzee Charles yupo mbele kutoka.
"Aah bosi pole sana" Alisema Daud.
"Pole mzee vipi unaendeleaje?" Aliuliza Frank.
"Asanteni nipo salama naomba nipelekeni St Anna maria hospitali" Alijibu kwa ufupi Mzee Charles.
"Lakini Mzee ungetulia uangalie hali yako kwanza haupo sawa" Alijaribu kutoa ushauri Daud.
"Kijana wangu nipeleke hospitali nikamuone mwanangu Lisa amekunywa sumu!" Alisema kwa uchungu Mzee Charles huku machozi kwa mbali yakimlenga.
"What? Lisa amekunywa sumu?"
Itaendelea.
Ukilipa buku vipande 7
Ukilipa buku mbili vipande 14, namba ya malipo
Tigo 0719618409
Voda 0763361677
Jina Lisa Ntanga.
0 Comments