Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-53



LATIFA NTANGA
0719618409
Ilikuwa tafrani tena baada ya mama yake Alberto kupandwa na presha ikabidi wamtoe nje haraka na kumpakia kwenye gari akakimbizwa hospitali ambapo alipatiwa tiba vizuri na baada ya muda mfupi alikuwa sawa.
"Pole mke wangu" Alisema mumewe.
"Asante mume wangu" Alijibu kwa unyonge sana na alionekana akiwa na mawazo sana.
"Usijali mume wangu ila Alberto amefanya tumbo la uzazi liniume jamani huyu mtoto kwanini lakini aliamua kwenda nje ya nchi jamani" Aliongea kwa uchungu sana.
"Pole mke wangu hata mimi naumia ila tumuombee Mungu mtoto wetu arudi salama" Alisema huyo baba, na kwa vile hali yake ilikuwa sawa aliruhusiwa kurudi nyumbani.
"Mume wangu inabidi umpe taarifa Lisa ajue kuhusu mumewe!" Alisema mamayake Alberto.
"Ni kweli ngoja nimpigie simu nimjulishe!" Alisema huyo baba na kuchukua simu yake akamtafuta Lisa.
"Haloo...eeeh Marahaba nilikuwa nakuomba uje nyumbani mara moja ndio njoo tu utajua huku huku" Alisema huyo baba na kukata simu.
"Vipi amesemaje?" Aliuliza mama yake Alberto.
"Lazima aje tuongee nae vizuri sio mambo ya kuongea kwenye simu aya" Alisema huyo baba akainuka na kwenda kwenye friji akachukua maji na kumimina kwenye glasi akanywa nakukaa chini, muda huo mkewe alikuwa amekaa kwenye sofa kwa unyonge mkono shavuni.
"Yani Alberto kajua kuninyima raha mama yake" Alisema huyo mama kwa masikitiko makubwa sana.
"Usijali mke wangu ishatokea" Alisema huyo baba. Na muda mfupi walisikia honi nje ikilia na mlinzi akaenda kufungua geti alikuwa ni Lisa aliingiza gari ndani akashuka na kwenda hadi mlangoni akagonga na mama mkwe wake alienda kufungua na kumkumbatia Lisa alishindwa kujizuia machozi yalimtoka huyo mama,
"Lisa mama karibu sana" Alikaribishwa Lisa.
"Asante mama shikamoo! Baba shikamoo!" Aliwasalimia kwa heshima na kukaa chini huku akimshangaa mama mkwe wake kwanini analia.
"Lisa unamuona mama yako hapo, alikuwa amepandwa na presha tumetoka hospitali sasa hivi ndio tumerudi nyumbani" Alisema baba mkwe wake Lisa.
"Jamani mama!" Lisa alisimama na kwenda karibu na mama mkwe wake akamkumbatia tena.
"Pole mama shida nini tena?" Aliuliza Lisa.
"Mumeo Lisa, Alberto ameniumiza sana kwanini aliamua kwenda kambini nje ya nchi sheria zao za kijinga washenzi wale Alberto!" Alisema huyo mama kwa uchungu.
"Mbona sielewi mama imekuaje tena?" Aliuliza Lisa na kukaa vizuri kwenye kiti.
"Sheria za jeshi huko alipoenda mume wako haruhusiwi kufanya mawasiliano kwenda sehemu yoyote na hana likizo miaka minne anamaliza kazi ndio anarudi Tanzania" Alisema huyo mama.
"Heeeee, mama Unasemaje?" Aliuliza Lisa kwa mshtuko na hapo hapo akaangua kilio kikubwa.
Itaendelea.

Post a Comment

0 Comments