LATIFA NTANGA
0719618409
Lisa alilia sana kama amefiwa! Aliwapa kazi ya ziada wakwe zake kumbembeleza hadi alipotulia jasho liliwatoka watu wazima.
"Uchuro huo mwanangu usilie mama jikaze hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, Lisa mwanangu Alberto ni kijana wangu na nimemzaa mwenyewe najua uchungu wake kuliko wewe naumia sana yani maumivu yangu mara milioni hadi presha ilinipanda ila nimejitahidi kuvumilia na kukubali ukweli ninachokuomba mama kuwa na imani tumuombee kwa Mungu Alberto arudi salama Tanzania" Alisema kwa uchungu mzito mama yake Alberto kumwambia Lisa ambaye machozi yalikuwa yakimtoka na kwikwi ilisikika.
"Nitajitahidi mama ila naumia" Alisema Lisa.
"Najua inauma tena inauma sana mwanangu ila jitahidi sana kumbuka unae mjukuu wetu tumboni mawazo na kilio kitafanya hiyo mimba itoke tena hilo jambo sitaki kusikia kabisa Lisa ukija kutoka mimba nitakuchukia ujue hilo nishajiandaa kumpokea mjukuu wangu yani itunze hiyo mimba kuliko roho yako" Alisema kwa ukali kidogo huyo mama na maneno yake yalimtisha Lisa ambaye aliacha kulia na kujifuta machozi, kwenye familia ya mume wake alipendwa sana alivyosikia atachukiwa aliogopa sana. Basi hapo waliendelea kumpa moyo Lisa na kuongea nae sana.
"Halafu mama unaonaje ukaja kuishi hapa nyumbani?" Aliuliza baba yake Alberto.
"Kweli ingekuwa vizuri sana kama Lisa ungekuja kukaa hapa sababu huko kwako upo mwenyewe mpweke utakuwa unamkumbuka sana mumeo" Alisema mama mkwe wake.
"Nashukuru sana wazazi wangu ila mama nae alikuja kunichukua kwasasa nipo nyumbani" Alisema Lisa.
"Oh alifanya jambo zuri sana kwa sababu kukaa peke yako mpweke unaweza ukajidhuru wewe!"
"Ni kweli kabisa hafai kukaa mwenyewe huyu, ila hapa pia ni nyumbani kwenu muda wowote njoo mwanetu utaishi na sisi salama tu"
"Sawa nashukuru sana jamani nitakuja bila tatizo"
Waliongea mengi sana na baada ya hapo Lisa aliaga na kuondoka akarudi nyumbani kwao.
"Haya mwanangu ulienda wapi tena?" Aliuliza mama yake Lisa.
"Aah mama acha tu nilienda nyumbani kwa wakwe zangu!" Alisema Lisa na kukaa kwenye kochi.
"Haya za huko wazima wote?" Aliuliza bi Lucy.
"Mh shida tupu mama yani Alberto dah hata hamu sina!" Alisema Lisa na kumuelezea mama yake yote yaliyotokea.
"Oh yesu wangu! Mumeo sijui kwanini alienda huko jamani eeeh!"Alipumua kwa nguvu huyo mama na kuongea hivyo.
"Yashatokea mama yani hata nguvu sina!"Alisema kiunyonge Lisa.
"Hapana hutakiwi kukata tamaa mwanangu, inabidi ujipe moyo uwe na imani haswa simama imara ngangari hakuna kutetereka kamwe na subiri jumapili twende kanisani kuna mafundisho mazuri sana mwanangu yatakupa nguvu na ari ya kusonga mbele" Alisema bi Lucy.
"Sawa mama nashukuru" Alisema Lisa.
"Haya nenda kajimwagie maji kwanza halafu uje chakula tayari tena leo nimekuandalia ndizi mchemsho kama nakuona mate yanavyokutoka!" Alisema Bi Lucy.
"Waooo mama ndo maana nakupenda jamani hebu kwanza nile ndio nikaoge" Alisema Lisa na kusogea mezani.
"Heee muone vile bora nisingekwambia yani hata kuoga hutaki!" Alisema bi Lucy akicheka.
"Mama bwana kula lazima kuoga hiyari" Alisema Lisa na kupakua ndizi akaanza kula na kumuacha mama yake akicheka sana. Lisa alikuwa akipenda sana ndizi na hiyo mimba ndio ilimfanya kila siku atamani mchemsho wa nyama ya ng'ombe pamoja na ndizi basi ndio kilikuwa chakula chake kikubwa. Baada ya kushiba aliinuka nakwenda chumbani kwake akajimwagia maji nakujilaza kitandani usingizi mzito ukampitia.
***
Maisha mapya bila mumewe yakaanza kwa Lisa, mwanzoni alikuwa mpweke sana lakini mama yake alijitahidi sana kumchangamsha mwanae mara kwa mara alikuwa akienda naye kanisani na kumfanya Lisa akutane na wapendwa ambao walikuwa wakimpa maneno ya Mungu sana nakumtia moyo, ujauzito wa Lisa nao ulizidi kukua alianza kliniki mapema na mama yake ndio alikuwa akimpeleka mara zote, mimba ilimpenda Lisa alizidi kunenepa na kupendeza haswa. Miezi nayo ukazidi kusonga huku tumbo lake likiwa kubwa ambapo alitamani apime ajulikane anamtoto gani tumboni ila mama yake akamkatalia.
"Hiyo ni kufuru mwanangu ni sawa na kufanya baby shower ikiwa hujui utazaa kiumbe wa aina gani Mungu anaweza kukudhihirishia ukuu wake ukapima akaonekana mtoto na siku ya mwisho ukajifungua panya" Alisema hiyo mama maneno yaliyomtisha sana Lisa.
"Mama jamani!"
"Hakuna mama jamani wewe tulia siku ikifika utazaa na kumuona mwanao ila mambo ya wazungu kwenda kucheki jinsia ya mtoto ukome usiniletee uchuro mimi hapa mtoto utamuona siku utayomzaa tu!"
Itaendelea.
0 Comments