Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-55



LATIFA NTANGA
0719618409
Maisha ya Romeo yalibadirika sana kutoka kuishi kwenye chumba kimoja hatimaye alinunua nyumba kubwa nzuri ya kisasa, akaanza kuishi hapo Romeo aliweka na mlinzi kabisa wa kumlindia nyumba yake pamoja na kijakazi wa kiume wa kufanya kazi za nyumba nzima pamoja na usafi ndani. Hakutaka kumuweka mfanyakazi wa kike kwa sababu alijua lazima atamgonga tu!
Ila tabia yake ya kutembea na wanawake hovyo hakuweza kuiacha kabisa, bado aliendelea kuwapa dozi tu. Ila alikuwa na akili sana kwani aliweka vitega uchumi vingi japo kuwa kazi yake ya kuchora tattoo hakuweza kuiacha kwani alifungua sehemu yake mwenyewe na kuwachora watu kwa raha zake, pia alifungua saluni nzuri ya kisasa yakiume. Alinunua bodaboda nyingi na kuweka vijana ambao kila mwisho wa wiki walikuwa wakimpeleka mahesabu. Romeo alikuwa mtu wa bata sana akila raha na watoto wazuri anaowataka, kwake ilikuwa dhambi sana kumuacha mtoto wa kike yani dhambi kubwa sana. Maisha yake yalikuwa hivyo tu bila kujali lolote, ndani ya muda mfupi alichafua hali ya hewa Tanzania kwa kutoka na wasanii wengi wa kike. Alitembea hadi na waimbaji nyimbo za injili aliwapitia Romeo alikuwa mchafuaji haswa! Hakutaka kupitwa na sketi kabisa. Siku moja akiwa matembezini kwenye supermarket moja hivi alishangaa kumuona msichana kama Lisa ila aliipuuzia baada ya kumuona huyo msichana yupo na mtoto wakiume tena mtoto akimuita mama.
"Ah nitakuwa nimemfananisha!" Alisema Romeo na kuendelea na mambo yake ila bahati nzuri alipomaliza na kwenda kulipa hapo hapo akakutana uso na macho na huyo msichana nabkumuona ni Lisa kabisa.
"Oh my god Lisa!" Alisema kwa mshtuko Romeo.
"What Romeo?" Lisa na yeye alisema kwa mshangao sana. Wakasogeleana na kukumbatia kwa nguvu sana hadi kuwashangaza watu wengine hapo supermarket.
***
Lisa alichoka maneno ya mama yake hakuweza kwenda kupima wala kujua jinsia ya mtoto wake, na miezi nayo ikazidi kusonga hadi pale alipofikisha miezi tisa nakuumwa uchungu.
"Uwiiii mama naumiaaa..." Alilalamika Lisa sana pale walipokuwa kwenye gari akapelekwa hospitali.
"Jikaze mwanangu ndio ukubwa huo" Alisema bi Lucy na hapo hapo alichukua simu na kuwapigia wakwe zake Lisa akawaambia kama mkwe wao anaumwa uchungu.
"Nakuja sasa hivi mnaenda hospitali gani?" Aliuliza mama yake Alberto.
"St Mathias" Alisema bi Lucy na hiyo ilikuwa hospitali ya mzungu ambayo walipenda sana kwenda kutibiwa hapo familia nzima basi baada ya hapo akakata simu. Njia nzima Lisa alikuwa akilalamika kuumia tu hadi walipofika akapokelewa na manesi wakarimu sana akapelekwa leba na bahati nzuri alipimwa njia mtoto alikuwa karibu hakupata shida muda huo huo akajifungua salama.
"Anti mtoto gani?" Aliuliza Lisa.
"Wa kiume" Alijibiwa.
"Oh asante Mungu wangu hatimaye nimemleta Harris duniani I hope mume wangu utafurahi sana ukimuona mwanao" Alisema Lisa kwa hisia sana, manesi wakamsafisha baada ya hapo akatolewa na kupelekwa kwenye chumba kingine kwa sababu hiyo haikuwa hospitali ya serikali basi akaingizwa chumba kingine kisafi pamoja na mtoto wake akambeba na kuanza kumnyonyesha, wazazi wake pamoja na wakwe zake ambao nao walifika hapo hospitali wakaruhusiwa kuingia ndani na kumuona mjukuu wao, ilikuwa furaha kubwa sana kumuona huyo mtoto.
"Jamani mjukuu wangu ataitwa Robson" Alisema mama yake Alberto.
"Mama jamani tangu mimba changa mume wangu alisema akiwa wakiume ataiwa Harris na akiwa wa kike ataitwa Yobness" Alisema Lisa.
"Heee kumbe tayari majina yalishapangwa" Alisema kwa mshtuko huyo mama.
"Ndio huyu ni Harris jamani naitwa mama Harris mie sio Lisa tena!" Alisema Lisa na kufanya wazazi wake wacheke sana.
"Ila mama shikamoo jamani shikamooni mama zangu...uchungu unauma yesuuuu...kuzaa kunauma jamani mama yangu mie nimekoma" Alisema Lisa na kufanya wazazi wake wacheke sana.
"Ndio umuheshimu mama yako sasa ushajua kuzaa kupoje" Alisema mama mkwe wake.
"Jamani nimekoma mimi sina hamu!" Alisema Lisa na siku hiyo alilala hapo hospitali hadi kesho yake akaruhusiwa kurudi nyumbani. Alishangaa sana baada ya kurudi nyumbani kwao na kukuta kumeandaliwa sherehe ndogo ya kumpokea Harris na mbele kulipambwa na kuandikwa. WELCOME BABY HARRIS
Lisa machozi ya furaha yalimtoka hapo hapo akamkumbuka mume wake na kutamani siku hiyo angekuwepo!
Itaendelea.
Mjitahidi kushare tu.

Post a Comment

0 Comments