Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-56



LATIFA NTANGA
0719618409
"Mama Harris tatizo nini leo siku ya furaha bwana sio huzuni" Alisema bi Lucy.
"Mama naumia natamani mume wangu angekuwepo leo" Alisema Lisa.
"Bwana hebu achana na hayo tufurahie leo" Alisema huyo mama akamfuta machozi mwanae. Siku hiyo walikula vyakula na kunywa sana ilikuwa furaha kwao. Hadi jioni wakwe zake Lisa wakaondoka, maisha ya uzazi akayaanza Lisa na kumlea mwanae vizuri, kwake Harris alikuwa zaidi ya kila kitu alimpenda sana mtoto wake, Harris alikuwa ndio Faraja yake kwani alifanana sana na Alberto na kumfanya Lisa afarijike sana kila alipomuona mtoto wake. Siku nazo zikazidi kusonga hatimaye Harris akatoka arobaini na kufanyiwa sherehe kubwa wakajumuika ndugu na marafiki, baada ya hapo malezi ya mtoto yakaendelea vizuri Lisa alinenepa na kupendeza sana uzazi ulimkubali haswa! Alikuwa kama hajazaa vile nyonga zake zilitanuka zaidi alikuwa na shepu nzuri urembo wake uliongezeka sana. Hatimaye mwaka wa kwanza ukapita bila Alberto kurudi Tanzania. Harris alizidi kuchangamka, na kuwa mtoto mwenye afya njema. Lisa aliamua kutafuta kazi ya kufanya kwanza kwa sababu hakupenda kukaa tu nyumbani na hapo akaamua kurudi nyumbani kwake hakuona haja kuendelea kuishi kwa wazazi wake alishazoea hali ya kuwa mwenyewe bila mume wake. Basi akaanza kazi huku akiwa na mwanaye Harris ambaye hakuwa msumbufu kabisa alikuwa mtoto mpole mzuri sana, Harris alitokea kupendwa sana na watu.
BAADA YA MIAKA MITATU
Harris alishakua mkubwa na kuanza shule ya awali ambapo alikuwa akishinda hadi jioni mama yake anaenda kumchukua na kurudi nae nyumbani kwao, kila siku swali kubwa la Harris ni juu ya baba yake.
"Mama baba yangu atarudi lini?" Aliuliza Harris swali ambalo lilikuwa linamuumiza sana Lisa.
"Harris, baba atarudi usijali sawa?" Alisema Lisa.
"Mama shule kila mtu anaye baba yake wanawaongelea ila mimi baba simjui, au amekufa?" Aliuliza Harris ambaye alikuwa muongeaji sana.
"Hapana baba yako mzima kabisa ameenda jeshini atarudi mwanangu usijali sawa?"
"Sawa mama nakupenda"
"Nakupenda pia mwanangu" Alisema Lisa na kumkumbatia mwanae huyo. Basi walirudi nyumbani na kuendelea na maisha yao japo kuwa Harris aliambiwa baba yake ameenda jeshini lakini hakuacha kumuulizia kila siku. Na siku moja ilikuwa jumamosi Harris alikuwa nyumbani na hata mama yake hakwenda kazini basi waliamua kwenda kwenye supermarket moja kununua mahitaji ya nyumbani ambapo walichagua vitu vyote baada ya hapo wakaendea sehemu ya malipo ambapo Lisa alishangaa sana kumsikia mwanaume akimuita jina lake alipomuangalia vizuri alimgundua ni Romeo.
"Oh my god Lisa ni wewe?" Alisema Romeo.
"What Romeo?" Alisema Lisa na hapo hapo wakakumbatiana kwa nguvu na kufanya watu wengine washangae.
"Yani nimefurahi sana kukuona hebu ngoja, Anti bei gani vitu vyote hivi unganisha na vyangu nitajie bei yake" Alisema Romeo na akapigiwa hesabu na kutajiwa bei akatoa wallet yake na kulipa pesa zote baada ya hapo akatoka na Lisa hadi nje akaingiza vitu vya Lisa kwenye gari lake na kumuomba waingie kwenye gari lake Romeo.
"Sio siri nimefurahi sana kukuona mama'ngu" Alisema Romeo.
"Hata mimi pia nimefurahi sana kukuona Romeo umebadirika sana baba hongera sana!" Alisema Lisa.
"Asante mama, ila kila kitu ni kwajili yako yani sababu ni wewe mama'ngu Lisa bila wewe mimi nisingekuwa hapa" Alissm Romeo.
"Yamepita hayo Romeo" Alisema Lisa.
"Mama huyu ndio baba yangu?" Aliuliza Harris akimuangalia Romeo.
"Yes mimi ndio baba yako" Alisema Romeo na kumbeba Harris ambaye alifurahi sana.
"Waaoo na mimi nimempata baba yangu" Alifurahi sana Harris na kumkumbatia Romeo.
"Hapana Romeo usimdanganye mwanangu, Harris he is not your Dad, Nilikwambia baba yako yupo jeshini nje ya nchi sawa?" Alisema Lisa.
"Lisa mbona sielewi" Alisema Romeo na muda huo Harris alikuwa amepoteza furaha yake.
"Romeo nimeolewa na huyu ni mwanangu tafadhari naomba niende nashukuru kuonana na wewe" Alisema Lisa na kufungua mlango wa gari akatoka na kumbeba mwanae.
"Noo...Lisa listen to me please..." Alisema Romeo na kujaribu kumuita Lisa ambaye hakutaka kumsikiliza aliingia kwenye gari akamuweka Harris pembeni na kumfunga mkanda vizuri na yeye akajifunga wake akalitoa gari kwa kasi sana Romeo hakutaka kukubali na yeye akaliondoa gari lake na kuanza kumfuatilia Lisa ajue anaishi wapi.
"Sijali umeolewa wala umezaa Lisa wewe ni mke wangu mimi tu!" Alisema Romeo na kuongeza spidi Lisa asimpotee.
Itaendelea.

Post a Comment

0 Comments