Kufuatia sharobaro Dullah kuitwa, aliivaa chupi yake chapchap’ Doreen naye alisimama pale sofani na kuchukua nguo zake na kukimbilia chumbani.
Zakayo aliendelea kuita ndipo Dullah alitoka haraka pale sebuleni na kwenda jikoni kwa akina Doreen, Zakayo alipoona kijana huyo haitiki alijua alitoka nje ya geti akarudi kumfahamisha fundi Yassin kwamba hakuwepo.
Dullah alipoona Zakayo kaondoka alivuta pumzi na kuzishusha akafurahi kwani alijua atakapokuwa akitoka mle ndani asingeonekana, wakati akiwaza hivyo Doreen ambaye tayari alivaa nguo alikwenda na kumshika Dullah begani.
“Vipi, amejua kama upo humu ndani?” Doree ambaye macho bado yalikuwa yamemlegea alimwuliza.
“Hajaniona na kaingia ndani,” Dullah ambaye alimlaani sana Zakayo kumkatishia starehe yake alimwambia Doreen.
“Kama hajakuona vizuri, ili kuwapoteza maboya itabidi nikutoe nje kabisa kwa kutumia mlango huu wa uani, baadaye ugonge geti ujifanye ulikwenda kununua soda,” Doreen alimwambia Dullah .
“Sasa hiyo soda nitanunua na hela gani wakati kwenye suruali yangu iliyopo ndani kuna shilingi mia tano tu!” Dullah alimwambia mrembo huyo.
Baada ya kutoa kauli hiyo, Doreen alicheka akamwambia asubiri akaingia ndani kisha kutoka akiwa na soda ya kopo akamwambia atoke nayo nje ili atakapofunguliwa geti ionekane alitoka kuinunua.
“Du! Kweli wewe mjanja sana,” Dullah alimwambia Doreen kisha aliichukua ile soda ya kopo lakini kabla ya kutoka nje akaona hatakuwa amemtendea haki msichana huyo bila kumbusu.
“Jamani asante yaani busu lako limenisisimua sana,” Doreen alimwambia Dullah akiwa kamkumbatia bila kujali nguo zake zilizochafuka kwa michanga.
“Ila basi tu, huyu aliyeniita katuvurugia sana nilitaka kukuonjesha penzi langu,” Dullah alimwambia Doreen.
Wawili hao wakiwa wanazungumza, si Zakayo akiwa nyuma ya nyumba waliyokuwa wakiweka malumalu akaanza kumwita tena Dullah , kitendo cha bila kuchelewa Doreen alifungua mlango mdogo wa uani na kumtoa Dullah .
Baada ya Dullah kutoka, Zakayo akaendelea kumwita ndipo kijana huyo aliitika akiwa nje ya nyumba, Zakayo alipomsikia akiitika alikwenda kufungua geti akamkuta Dullah ameshika soda ya kopo.
“Kaka muda sasa tunakutafuta kumbe mwenzetu umeacha kazi na kwenda kununua soda, hivi utaiweza kazi hii tunayofanya?” Zakayo alimwuliza Dullah .
“Unajua muda ule sista sijui Doreen kanipa maji nikaendelea na kazi nikaona kiu bado imenishika nikaamua kwenda kununua hii soda kwani huwa nikinywa kidogo inakata kiu,” Dullah alimwambia Zakayo.
Zakayo alimtazama Dullah alivyokuwa akizungumza na ile soda yake ya kopo aliyokuwa ameishika akaishia kucheka na kujisemea moyoni;
“Kweli site imevamiwa na sharobaro wa Tandale kwa tumbo, sisi tunawaza kazi yeye tayari kisha kuwa mwenyeji mpaka kaenda kununua soda ya kopo, kweli huyu dogo ni mtoto wa mama.”
Kwa kuwa walikuwa wakizungumza wakiwa wamesimama pale getini, Zakayo alilifunga kisha wakaongozana kuingia ndani na kwenda moja kwa moja katika chumba ambacho fundi Yassin na wasaidizi wake hao walikuwa wakifanya kazi.
Fundi Yassin alipomuona Dullah kashika soda ya kopo, awali alifikiria alipewa na Doreen lakini Zakayo akamweleza jinsi Dullah alivyokuwa mwenyeji mpaka kutoka nje na kwenda kununua soda.
“Yaani alikuwa nje kabisa ya geti?” fundi Yassin alimwuliza Zakayo huku Haruni akiwa amepozi kufanya kazi akimsikiliza.
“Ndiyo maana yake, si nilikuja kuwaambia nimemwita lakini hakuitika, niliporudia kumwita kwa mara ya pili, nikamsikia akiitika nje ya geti,” Zakayo aliwaambia.
Fundi Yassin alimkanya Dullah kwamba kilichompeleka pale ni kazi na kumfahamisha jinsi tajiri yao asivyopenda watoke getini ndiyo maana aliwaambia chochote watakachohitaji wamwambie Anne ambaye ni dada wa kazi.
“Basi bro potezea sikujua, kwa hiyo nikisikia njaa nimwambie huyo dada,” Dullah aliwaambia na kusababisha wote kuangua kicheko.
Wakati mafundi hao wakizungumza hivyo, Doreen akiwa chumbani kwake mawazo yote yalikuwa kwa Dullah kwani kijana huyo alijua kumsisimua sana.
“Huyu mkaka anavyoonekana mambo anayaweza, yaani hapa kaniacha mwili wote una ninyevuanyevua, asingeitwa na yule fundi saizi angekuwa kisha nipa raha, na nilivyomisi nanii da!” Doreen aliwaza.
Baada ya Dullah kuwachekesha mafundi wake alitoka akiwa kashika soda yake ya kopo na kwenda kuendelea na kazi, ambapo aliiweka ile soda juu ya dirisha bila kujua kama Doreen alikuwa kasimama katika dirisha hilo kwa ndani akimwangalia.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dullah baada ya kuchota mchanga kama chepe kumi na kuzirushia eneo alililoelekezwa na Zakayo, akapozi kisha alijishika kiuno na kujinyoosha, kitendo hicho kilimhuzunisha sana Doreen.
“Jamani huyu kaka anaumia bure tu, ngoja kama ataendelea kuja hapa lazima nifanye mpango wa kumpa sapoti yoyote,” Doreen aliwaza.
Wakati Dullah akiendelea na kazi, Zakayo alifika kumwangalia, alivyomkuta akiwa kasimama akatabasamu na kujisemea moyoni ‘huyu kazi hii haiwezi na sijui kama kesho atakuja.’
Zakayo aliwaza hivyo bila kujua kama Dullah alipanga kufika pale site kila siku kwa vile palikuwa na mtoto mkali Doreen ambaye wao walikuwa wakimwangalia tu kama dada yao.
“Vipi, leo huu mchanga utaisha kweli?” Zakayo alimwuliza Dullah .
Dullah bila kumficha alimwambia kwa siku ile alichoka sana hivyo angemalizia siku iliyofuata, kufuatia kauli hiyo, Zakayo akacheka na kuingia ndani kumweleza fundi Yassin.
“Kwa kuwa ni mwanaume ataweza, si unajua hizi kazi unapoonza siku ya kwanza zinakuwa ngumu!” Fundi Yassin alimwambia Zakayo.
Kufuatia kuelezwa hivyo, Zakayo alipinga na kumwambia Fundi Yassin kwamba Dullah akimaliza wiki pale site atampatia shilingi elfu kumi, fundi Yassin akaishia kucheka.
Zakayo alipoingia ndani, Dullah alimalizia soda yake kisha akawafuata wenzake waliokuwa ndani na kushangaa jinsi walivyoweka marumaru katika vyumba viwili.
“Da! Nyie mnapiga kazi sana, kazi hii yote mmeifanya leo?” Dullah aliwauliza.
Fumdi Yassin amjibu kwamba mbona walifanya kazi kidogo sana siku hiyo, Dullah akabaki akishangaa, fundi Yassin alipomuuliza kama alimaliza kuhamisha mchanga, akacheka sana na kumwambia atamalizia kesho yake.
Kwa kuwa fundi huyo alikuwa anauelewa usharobaro wa Dullah , hakumsema vibaya kwani alijua atazoea taratibu lakini kwa upande wa Zakayo alijisemea moyoni kwamba Dullah hakuwa mfanyakazi, sijui kwa nini hakumpenda kijana wa watu.
Baada ya kufanya kazi hiyo, Dullah hakuendelea tena na kazi ya kuhamisha mchanga hadi wenzake walipomaliza kazi na baada kuoga kwenye bafu la nje, fundi Yassin alikwenda kuonana na Doreen ambaye alimpa bahasha iliyokuwa na hela.
Baada ya kukabidhiwa alimpatia Zakayo shilingi 30,000 halikadhalika Haruni kisha akaiweka ile bahasha mfukoni, Dullah hakuwa na wasiwasi kwani alielewa kingeeleweka mbele ya safari.
Hata hivyo, Dullah alipenda kabla ya kuondoka amuone Doreen akawa anaplani kuhakikisha anafanikisha hilo, fundi Yassin alipowaambia waondoke akamwambia alihisi kiu hivyo ngoja akaombe maji ya kunywa.
“Wewe huna lolote, unataka umuone tu Doreen,” fundi Yassin alimwambia Dullah ambaye alicheka sana na kusema:
“Siyo hivyo bro hayo ni mawazo yako tu mbona mimi nina demu wangu mkali kumpita sijui huyo Doreen halafu mimi mtoto wa kishua kama huyo nitampa nini?” Dullah aliwaambia wote wakacheka.
“Jamani muda unakwenda, hayo maji nitaenda kununulia mbele ya safari, halafu kumbuka wewe hapa ni mgeni usije ukaleta picha mbaya bure,” fundi Yassin alimwambia Dullah bila kujua kama sharobaro huyo alibakia kiduchu kula tende tamu za mtoto huyo wa kishua.
“Haya mkubwa nimekuelewa, twendeni jamani,” Dullah aliwaambia.
Baada ya kutoa kauli hiyo, fundi Yassin aliwaambia waondoke wakatoka lakini wakiwa nje fundi Yassin aliyekuwa kamzoea sana Anne akamwita dada huyo wa kazi ili amuage.
Licha ya kumwita Anne aliitika Doreen ambaye alitoka nje fasta, na kumwuliza fundi; “ Fundi ndiyo mnaondoka?”
“Eh! Leo tumefanikiwa kuweka marumaru vyumba viwili kesho tutaendelea,” fundi Yassin alimwambia Doreen bila kujua msichana huyo alikuwa na furaha moyoni ya kumuona Dullah .
“Hakuna shida, nawatakia safari njema,” Doreen ambaye alikuwa amevaa kama alivyovaa awali aliwaambia.
Baada ya kumuaga msichana huyo, fundi Yassin, Zakayo na Haruni wakatangulia Dullah alibaki nyuma ambapo aligeuka na kumkonyeza Doreen aliyeachia tabasamu pana.
Mafundi hao walipotoka getini walishika njia hadi ilipokuwa barabara kubwa ambapo Haruni ambaye alikuwa akiishi maeneo hayo aliwaaga wenzake kwamba wangekutana siku iliyofuata.
Baada ya kuagana haukupita muda mrefu daladala iliyokea Kisauke mwisho lilifika ambapo wote watatu walipanda, kwa kuwa siti zilikuwa wazi fundi Yassin na Dullah waliketi pamoja.
Kutokana na uchovu wa kazi, wakiwa kwenye daladala hilo hawakuwa na stori nyingi zaidi ya Dullah kuwatupia macho mademu wazuri aliowaona nje na wawili waliokuwa wamo ndani ya basi.
Walipofika njia panda ya Wazo Hill maarufu kama Kibaoni, Zakayo aliyekuwa akiishia Bunju alimuaga Yassin na Dullah ambapo fundi Yassin alimsisitiza kuwahi kufika kazini siku iliyofuata.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kuwa kituo cha mabasi ya Kisauke hakikuwa mbali walitumia kama dakika nne wakawa wamewasili ndipo fundi Yassin na Dullah walishuka wakaanza kuelekea Kituo cha daladala cha Kwa Ndevu kupanda gari la kwenda Mwenge ili wakaunganishe la Tandale.
Wakiwa wanatembea Dullah alikuwa akijiuliza mbona fundi Yassin hakumpatia fedha kama alivyofanya kwa wenzake!
Hata hivyo, kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu fundi huyo alijua wakifika nyumbani angempatia ndipo akaanza kuifikiria safari yao tangu asubuhi alipokutana na yule mrembo kwenye DCM la kwenda Mwenge na wale wasichana waliopandia kituo cha Jogoo walioshukia njia panda ya kwenda Kunduchi.
Kwa kuwa kichwani alikuwa na namba ya yule dada aliyekutana naye Mwenge, akazitamka kimoyomoyo, sifuri, saba, tano, nane, nne, mbili, arobaini, na kumalizia ya mwisho akaachia tabasamu lililoonwa na fundi Yassin.
“Mwenzangu kimekufurahisha nini maana naona unatabasamu?” fundi Yassin alimwuliza Dullah .
“Bro bwana, kwani hujamuona yule dada alivyotuangalia kisha kuanza kutikisa makalio yake?” Dullah alimchomokea fundi Yassin.
“Hapana sijamuona, yupo wapi kwani?” fundi Yassin alimwuliza Dullah .
Kufuatia kuulizwa hivyo, Dullah alimwambia alikwishaondoka ndipo wakaendelea na safari hadi walipofika kituoni ambapo walipanda gari la kwenda Mwenge.
“Bro kweli kuna watu wapo vizuri sana duniani, wakati sisi tunafikiria hela ya kula wengine wanaporomosha majengo namna ile?” Dullah alimwambia fundi Yassin.
Baada ya Dullah kuuliza hivyo, fundi Yassin alimweleza kwamba maisha ndivyo yalivyo na watu wote hatuwezi kufanana kauli ambayo iliungwa mkono na Dullah .
Akiwa ameketi siti ya dirishani, Dullah akaanza kumkumbuka Doreen hasa alivyokuwa akizichezea embe bolibo zake, si mkuu wake wa kaya akaanza kuchangamka.
Kijana huyo alipoangalia eneo la makazi ya mkuu wake wa kaya na kumuona alivyokuwa, akaachia tabasamu ambalo lilionwa na fundi Yassin ambaye alimwuliza alifurahishwa na nini!
Kwa haraka Dullah alimuonesha fundi Yassin mzee mmoja aliyekuwa amekaa siti ya kushoto kwao aliyekuwa amepitiwa na usingizi na kuacha kinywa wazi, Yassin alipomwangalia mzee huyo naye akaachia tabasamu bila kujua Dullah alimpiga changa la macho.
“Maisha dogo, unaweza kukuta tangu alipoondoka nyumbani kwake asubuhi hajanywa chai na huko alikokwenda hakijaeleweka hapo kajichokea mzee wa watu,” fundi Yassin alimwambia Dullah kwa kumnong’oneza.
“Ni kweli bro nakubaliana nawe,” Dullah alimwambia fundi wake.
Kama ilivyo kawaida ya mashorobaro kupenda mambo ya mademu na mambo mengine ya kivijana, wakati safari ikiendelea Dullah alikuwa akimtupia macho msichana mmoja denti aliyekuwa kabeba mkoba wake mkubwa mgongoni.
Denti huyo ambaye alivyoonekana alikuwa kidato cha tano au sita kaumbika vizuri na licha ya kuwa ndani ya sare za shule sketi aliyovaa ilionesha namna alivyojazia.
“Isingekuwa jela, mtoto mzuri kama huyu ni kulamba tu kwa kwenda mbele,” Dullah alijisemea moyoni baada ya kukitathmini kifua kitamu cha denti huyo kilichopambwa na viembe bolibo f’lani hivi.
Gari lilipofika kituo cha Interchick, waliingia watu kibao akiwemo msichana mmoja mweupe aliyekuwa kava suruali ya jeans na kitop cha njano, Dullah alipomtupia macho moyo wake ukapiga paa!
Wakati Dullah akiwa katika hali hiyo, fundi Yassin ambaye alikuwa akimfahamu vyema Dullah, alimbonyeza dogo huyo pajani, Dullah apomwangalia akamnong’oneza kwa kusema:
“Umeyaona mambo yako hayo?”
“Kaka nimeyaona, da mtoto kaumbika halafu mapigo kama haya ndiyo ugonjwa wangu mkubwa! Dullah alimwambia fundi Yassin.
“Wewe si unajifanya mkali wa viumbe hawa, ukipata namba ya huyo dada au ukifanikiwa kuchonga naye nitakupa wekundu mmoja nje ya hela ya kazi,” fundi Yassin alimtania Dullah .
“Bro, masihara hayo!” Dullah alimwambia fundi wake.
“Siyo masihara, wewe fanya kama nilivyokuambia nikupe mpunga wako,” fundi Yassin alimwambia Dullah .
Kauli ya fundi Yassin ilimuweka katika wakati mgumu sana Dullah ambaye hakuelewa ataanzaje kuzungumza na yule msichana kisha kuipata namba yake ya simu!
“Sikubali nasema sikubali, kama mimi ndiye Dullah lazima nitaipata namba ya huyo mrembo kwanza hawa wapo duniani kwa ajili yetu,” Dullah aliwaza.
Baada ya kuwaza hivyo, Dullah alimuomba fundi Yassin ahamie upande wa dirishani, fundi Yassin huku akicheka akahamia siti ya dirishani huku akisema alikuwa akijisikia vibaya hivyo kukaa dirishani ingemsaidia kupata hewa.
INAENDELEA

0 Comments