Maiko aliwaona mshangao walioupata wakina Adamu na mama yake.
MAIKO: Kwani vipi, mnamfahamu huyo??
Wakaamua kukataa kwa kujigelesha lakini ukweli ni kuwa walishamfahamu.
ADAMU: Hapana hata hatumfahamu.
MAIKO: Basi huyo mwanamke ndiye nilizaa nae huyu mtoto.
ADAMU: Na mbona huishi nae tena?
MAIKO: Ilitokea tu tukazaa ila haikupangwa kabisa.
ADAMU: Mmh!! Haya bhana.
Wakaamua kufanya mipango ya kwenda kwa kina Deborah tena kwani Adamu alimuhakikishia Maiko usalama wake na jinsi atakavyoongea na wakina Deborah ili kuwaelewesha kuhusu Maiko, laiti kama angejua aliyowatendea na jinsi wanavyomchukia hata asingejisumbua chochote.
Deborah akaamua kumuita mwanae pembeni ili kuzungumza nae.
DEBORAH: Umekuwa polisi siku hizi mwanangu?
Patrick akashtuka na kuhisi kuwa lazima kuna kitu mama yake amekishtukia, Patrick akakataa kwa ishara ya kichwa.
DEBORAH: Kama wewe sio Polisi, umewezaje kuwaokoa wote wale toka mikononi mwa watekaji?
PATRICK: Mama jamani, si nimewaokoa tu. Kwani kuna ubaya au nimefanya vibaya?
DEBORAH: Hakuna ubaya na wala hujafanya vibaya, nia yangu ni kujua una mahusiano gani na hao watekaji?
Patrick alikosa jibu la kutoa.
DEBORAH: Patrick mwanangu, nimekulea katika misingi mizuri ya dini. Sikuwa na uwezo mkubwa ila nilihangaika na maisha kwaajili yako mwanangu. Au nilifanya kosa kukulea Patrick? Mbona umebadilika sana mwanangu?
PATRICK: Nadhani mama katika maisha yako yote huwa hujutii kunizaa ila unajutia kunilea, kwanini mama kwanini? Kama usingenilea wewe unadhani angenilea nani mama? Wewe ni mama yangu wa pekee, nakupenda sana mama. Sijawahi juta kuwa mtoto wako ila nafurahia siku zote kuwa na mama kama wewe, kwanini nawe usijivunie kuwa na mimi jamani?
DEBORAH: Hivi kuna mzazi yeyote anayeweza kujivunia kuwa na mtoto jambazi?
PATRICK: Jambazi? Nani kakwambia hayo mambo mama? Umenilea mwenyewe na nimekuwa nawe siku zote na unanitambua vizuri, je umeshawahi kuniona nikitenda hayo matendo mama?
DEBORAH: Sijawahi kukuona, ila sikia Patrick lisemwalo lipo. Kwanini wasimtaje mtu mwingine kuwa jambazi wakutaje wewe Patrick? Na una mahusiano gani na Maiko?
Patrick akashtuka na kujua mama yake Tusa atakuwa ameshasema umbea tu, akajikuta akisema,
PATRICK: Wanawake bhana.
DEBORAH: Unamaana gani Patrick?
PATRICK: Sina maana yoyote mama wamekupa umbea tu. Ila nakuomba mama uniruhusu nitoke kidogo tu.
DEBORAH: Halafu utarudi au?
PATRICK: Nitarudi mama.
Mawazo ya Patrick yalikuwa ni kwa Mwita tu, alitaka amuwahi Mwita kule kule kwa Maiko kabla hajaondoka ili akamkomeshe kwa kumbaka Tusa.
Mashaka alitafuta kundi la watu ambao aliwalipa pesa na kufanya nao zoezi, nia ikiwa ni moja tu kupambana na Maiko pamoja na Patrick kwani alijua kwa vyovyote vile lazima Patrick nae atakuwa anaendelea kuwatafuta tu.
"Hapa lazima nijipange maana Maiko kanisaliti halafu Patrick nae si mtu mzuri lazima nikawasambaratishe tu."
Mashaka alikuwa na hasira sana za kuachwa mwenyewe, alimuona Maiko kuwa hamfai tena kwani amemsaliti na pia amemuumiza moyo wake.
Akawa yupo na vijana aliowanunua na kuwapa mazoezi kwaajili ya watu wawili nao ni Maiko na Patrick ila haswaa Patrick kwani ndio anayemsumbua mawazo yake.
Wale wanajeshi waliompeleka Mwita mahali alipo Maiko walishaondoka muda mrefu sana, wakati wanazunguka njiani wakakutana na Patrick.
PATRICK: Mwita yuko wapi?
MJESHI: Tumemuacha kulekule.
PATRICK: Basi sawa hakuna tatizo.
Patrick aliendelea na safari yake kwenda kumfata Mwita huku akiwa na hasira sana juu yake.
Adamu na Maiko na bi.Rehema kama walivyopanga wanaamua kuondoka kwenda kwa Deborah kama walivyopanga.
MAIKO: Jamani au twende na huyu mwanangu, kwavile ni mwanajeshi nadhani atatusaidia busara huko tuendako.
ADAMU: Itakuwa vizuri kwenda nae.
Wakiwa wanashuka kwenye ngazi za hoteli na Mwita ili waelekee kwenye gari, kufika tu mapokezi Mwita akakumbuka kuwa ameacha kofia na picha ya mama yake kwenye chumba cha Maiko anawaomba arudi kuvifata, Maiko anamkabidhi funguo na kumwambia akirudi aziache mapokezi na wao atawakuta nje wakimngoja, halafu Mwita akaenda huko chumbani.
Akiwa ameshachukua vile vitu anamsikia mtu anagonga akajua labda ni wahudumu wa hoteli ile.
Akafungua mlango na kukutana na Patrick mlangoni huku akiwa na jazba mno.
Akafungua mlango na kukutana na Patrick mlangoni huku akiwa na jazba mno.
Alichofanya Patrick ni kumkunja Mwita na kuingia nae vizuri mule ndani.
Mwita akashtukia anapewa ngumi ya sura.
MWITA: Jamani Patrick, kwani nimefanyaje?
PATRICK: Unaweza kunipa sababu ya kumbaka Tusa wewe?
MWITA: Nisamehe Patrick sikukusudi.....
Kabla hajamaliza akashtukia kapigwa ngumi nyingine na mambo yakaanza kuwa ovyo ovyo mule ndani.
Nyumbani kwa Deborah walikuwa wakimshangaa Tusa tu alivyonyorodoka.
DEBORAH: Pole sana Tusa, kwakweli nakuhurumia sana.
TUSA: Asante mama.
DEBORAH: Umekonda sana yani mvuto wako umepotea kabisa.
TUSA: Najuta kuolewa mimi, kwasababu nisingeolewa yote haya yasingenipata. Ningeendelea kuishi kwa furaha na Sele wangu, tazama sasa sitaweza kuishi na Sele tena roho yaniuma sana kwani Patrick ananitesa mimi.
DEBORAH: Jamani kwani Patrick anakufanyaje Tusa?
Tusa akainama na kuanza kulia, Pamela ikabidi nae aongee ya kwake.
PAMELA: Deborah, ungemuona huyu mwanangu alivyokuwa mwanzo kabla hajaolewa na mwanao hakika ungemuhurumia kwenye hiyo ndoa.
DEBORAH: Namuona hapa kama huyu binti amechoka sana, anatia huruma kwakweli.
Tusa aliendelea kuinama na kulia kwa uchungu. Pamela akamvuta Tusa na kusogeza kichwa cha Tusa kifuani mwake huku kiganja cha mkono kikimgonga gonga Tusa mgongoni mwake. Akaanza kusema kwa uchungu,
PAMELA: Tamaa ndio iliyotufanya tukuozeshe mama, tusamehe sie mwanangu.
DEBORAH: Kwani mlitamani nini kwa Patrick?
PAMELA: Hii yote ni tamaa ya pesa Deborah, mwanao alitulaghai na pesa zake wala sikufikiria upendo wa Tusa kwa Sele nilichotazama ni pesa aliyonayo Patrick. Ni kweli Patrick ametusaidia sana ila najilaumu kwa kumuangamiza mwanangu na pia kumnyima Sele haki yake.
TUSA: (Akainua kichwa), mama hii ni zaidi ya kuangamizwa yani natolewa mimba nne ndani ya mwaka mmoja!!
DEBORAH: Mimba nne?? Umetolewajwe?
Tusa akainama huku akiendelea kulia kwa uchungu, kwakweli Debora nae akamuhurumia Tusa. Alimtazama tatizo lake kwa uchungu.
Mashaka aliendelea kujipanga na alipatana na kijana mmoja mkorofi sana aliyejulikana kwa jina la Mporipori.
Huyu kijana alimpa moyo Mashaka wa kufanikisha kazi hiyo.
MPORIPORI: Usijari mkuu, je ungependa tuanze na yupi?
MASHAKA: Nadhani tukianza na huyu Patrick itakuwa poa zaidi maana huyu nae anataka kuniharibia mipango yangu kabisa. MPORIPORI: Hiyo ni kazi ndogo sana kwetu, ila sie huwa tunamaliza kabisa.
MASHAKA: Nyie mmalizeni tu maana huyo Patrick sitaki hata kumuona kwenye macho yangu.
MPORIPORI: Usijari mkuu, yani hapa kwetu hiyo ni kazi ndogo kabisa. Kwani huyo Patrick anakundi?
MASHAKA: Yuko peke yake hana kundi lolote, nahitaji mshughulike nae vizuri.
Mashaka akawakabidhi picha ndogo ya Patrick iliyokuwa kwenye kitamburisho ili iwe rahisi kumpata.
Wakina Maiko walimngoja sana Mwita pale chini lakini hakurejea, Maiko akataka kumfata Mwita ila Adamu akamzuia na kumwambia.
ADAMU: Wewe baki na mama hapa, ngoja niende mimi.
MAIKO: Kwanini uende wewe sasa?
ADAMU: Nina maana yangu, baki na mama hapo.
Adamu hakutaka kubaki yeye kwa kuhofia kumpoteza mama yake kama alivyompoteza Fausta na Pamela pale alipokuwa amesimama nao.
Ikabidi yeye ndio akaangalie huko chumbani kuwa Mwita amepatwa na nini.
Kufika nje ya chumba akasikia kama watu wanarumbana akaamua kuingia ndani akakutana na mpambano wa hali ya juu akajikuta akistaajabu kile kitu kilichokuwa kimetokea kwani alimkuta Mwita akiwa amezidiwa kabisa na Patrick, ikabidi aingilie kati.
Patrick aliyekuwa na hasira bado akamshindilia ngumi ya nguvu muamuliaji ambaye ndiye Adamu halafu akampiga teke lililofanya arushwe hadi mlangoni.
Adamu aliugulia sana, Patrick akamuacha Mwita aliyekuwa hoi kwa mkong'oto na kumfata Adamu ili apambane nae.
Akamfata pale chini na kumkunja, akampiga ngumi ya kwanza na kutaka kumuongeza nyingine za mfululizo, ile anataka kumshindilia ngumi nyingine tu sura yake ikamjia kuwa ni baba yake na Tusa. Patrick alishusha ile ngumi na kumuacha pale chini kisha akatoka nje haraka na kuondoka kwani tayari alishaona kitumbua kimeingia mchanga sababu alimkong'ota baba mkwe bila hata ya kumuangalia vizuri kuwa ni nani.
Ikabidi aende mahali kupumzika ili afikirie kwanza.
Deborah akamchukua Tusa ili kumuhoji vizuri kuhusu Patrick, ila Anna akaona kuwa hali ya Tusa si nzuri.
ANNA: Huyu binti atakuwa amepungukiwa na damu.
DEBORAH: Eti eeh!!
ANNA: Si unaona macho yake yalivyo meupe sana, halafu angalia ngozi yake ilivyopauka na kubabuka. Mwacheni niende nae hospitali kwanza.
DEBORAH: Hayo mambo ya utaalamu wengine hatuyajui. Wewe mpeleke tu huko hospitali.
Ikabidi Anna amwambie Tusa ajiandae na kuondoka nae kwenda hospitali.
Adamu akainuka pale chini na kwenda kumsaidia Mwita kuinuka pale alipo halafu akamkongoja na kutoka nae hadi nje, Maiko akashangaa kuwaona vile.
MAIKO: Nini kimewakumba jamani?
ADAMU: Kweli Mwanza kuna majangili, kuna jamaa ametudunda huyo si mchezo.
MAIKO: Poleni sana, kwani imekuwaje?
ADAMU: Hata sielewi kabisa, ila Mwita ndo kama hivi hali yake sio nzuri kabisa.
MAIKO: Basi tumpelekeni hospitali.
ADAMU: Itakuwa vyema.
Mwita hakuweza hata kuongea kwani aliumizwa vibaya mno.
Adamu alikuwa akijifikiria tu kuhusu kijana aliyewapiga, sura yake ikamjia kichwani mara kwa mara ila hakujua ni nani. Akajiuliza vitu vingi kuhusu yule kijana, hadi akajikuta akiropoka.
"Nadhani atakuwa gaidi yule"
MAIKO: Nani huyo?
ADAMU: Dah! Yani yule kijana kanichanganya balaa. Yule kijana aliyetupiga atakuwa mafia tu.
Adamu hakuacha kumfikiria na sura ya Patrick haikuacha kumtoka usoni.
Mashaka na Mporipori wakiwa wanakatisha eneo fulani wakamuona Patrick njiani.
MASHAKA: Kijana mwenyewe ni yule pale.
MPORIPORI: Kumbe ni yule, ngoja nishuke nimfatie.
MASHAKA: Hapana, tuwaite na wale vijana watano usaidiane nao.
MPORIPORI: Haina haja, yule namdhibiti mwenyewe kwa dakika mbili tu.
MASHAKA: Ila kuwa makini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MPORIPORI: Usijali bosi, mimi ndio Mporipori bhana.
Mporipori alijiaminia zaidi kwajinsi mwili wake ulivyojaa na misuli mingi kwahiyo alimuona Patrick ni kijana wa kawaida tu ukilinganisha na vijana wengine aliowahi kupambana nao.
Mporipori akashuka kwenye gari na kuanza kumfata Patrick alipo.
Mporipori akashuka kwenye gari na kuanza kumfata Patrick alipo.
Mporipori akamsogelea Patrick kisha akamshika bega, Patrick akageuka kuona ni nani aliyemshika bega, alipoona ni mtu asiyemfahamu akaamua kuendelea na mawazo yake.
MPORIPORI: Oya dogo vipi, mbona una dharau?
Patrick akamshangaa Mporipori na kumuuliza.
PATRICK: Nina dharau unanijua?
MPORIPORI: Swala la kukujua mi halinihusu ila kwa kifupi mi naitwa Mporipori.
PATRICK: Aah kumbe!! Na mimi naitwa msitunisituni.
MPORIPORI: Naona una kiburi sana dogo.
PATRICK: Kwani wewe shida yako nini?
MPORIPORI: Shida yangu ni wewe.
PATRICK: Kivipi?
Kwavile sehemu yenyewe ilikuwa imetulia na si sehemu ya kupitiwa na watu sana, Mporipori akaona ile ni sehemu nzuri ya kumkomesha Patrick.
Wakati wakiendelea kuongea huku Patrick akimshangaa mtu huyu, Mporipori akaandaa kumi matata ya kumshindilia nayo Patrick, akainua kumi hiyo ili ampige nayo usoni ila kabla haijafika Patrick akaudaka ule mkono wa Mporipori.
Patrick hakutaka kupoteza muda, akampiga teke tumboni na kumshindilia na kiwiko mgongoni.
Mporipori akapatwa na hasira za kupigwa na mpambano ukaanza vizuri, Mporipori alipambana na Patrick kwaajili ya pesa ila Patrick aliamua kumalizia hasira zake zote za siku hiyo kwa Mporipori.
Patrick alimsukuma kwa nguvu Mporipori hadi akaanguka chini halafu akaruka juu na kumuangukia kwa kumkanyaga tumboni hadi Mporipori akatapika damu kwa mara ya kwanza, Patrick akamshika shingo na kumshambulia kwa ngumi za sura, kisha akamuuliza.
PATRICK: Nani kakutuma kwangu?
Mporipori alikuwa kimya kabisa.
PATRICK: Hunijibu eeh!! Sasa utanijua vizuri na utajua kwanini umetumwa badala ya muhusika kuja mwenyewe.
Mporipori alikuwa hoi kabisa.
Patrick akampigia simu Yuda kuwa ampelekee bodaboda yake.
Mwita akapelekwa hospitali na kwavile alikuwa na sare za jeshi haikuwa ngumu kumuhudumia.
Wakati Mwita akihudumiwa Maiko, Adamu na Rehema walikuwa mapokezi wakingoja kusikia anaendeleaje.
REHEMA: Huyo aliyewapiga lazima atakuwa jambazi tu.
ADAMU: Hata mimi nahisi ni hivyo yani hadi kichwa kinaniuma, sijawahi kumuona mtu anayepiga kiasi kile live. Dah ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, yule kijana ni muuaji jamani.
REHEMA: Ila nani aliwasaidia?
ADAMU: Aliondoka yeye mwenyewe. Hata simjui kwakweli labda akipata nafuu huyo anaweza akawa anamjua.
Maiko alipatwa na hofu kuwa huenda kijana huyo ni Patrick ila akashindwa kuelewa uhusiano wa Patrick na Mwita na je wamefahamiana vipi.
Yuda akamfata Patrick mahali alipoelekezwa, Yuda akamshangaa yule Mporipori pale chini.
YUDA: Kaka umelikong'ota hili jitu?
PATRICK: Kwani unamjua?
YUDA: Namjua ndio, anaitwa Mporipori ni mkorofi na anaogopewa balaa.
PATRICK: Basi hakuna shida.
Patrick akachukua kamba na kuifunga kwenye boda boda halafu akaenda kumfunga Mporipori mikono, halafu akaenda kupanda kwenye bodaboda na kuanza kuendesha.
YUDA: Unataka kufanya nini kaka?
PATRICK: We ngoja hapohapo utaona tu.
Akaendesha ile bodaboda huku Mporipori akiburuzwa nayo.
Yuda aliendelea kumngoja, baada ya muda Patrick alirudi mwenyewe na bodaboda yake bila ya Mporipori, halafu akamwambia Yuda apande ili waondoke.
YUDA: Kwani umeenda kumfanyaje kaka?
PATRICK: Nimeenda kumuacha porini, yeye si ndio mporipori bhana basi kwake ni porini.
Ingawa Yuda alimchukia Mporipori ila hakufikiria kama Patrick atafanya alichofanya.
Mashaka alikimbia na gari yake baada ya kuona Mporipori anadundwa, ikabidi aende kuwatafuta wale vijana watano ili wakasaidiane na Mporipori.
Wakashangaa walipofika pale hawakuona mtu yeyote ila wakaona kama kuna kitu kilikuwa kimeburuzwa, wakaamua kufata ile alama ili wajue ni nini.
Wakamkuta Mporipori ametundikwa juu ya mti, kila mmoja alistaajabu na wote wakashangaa kuona Mporipori apigwe na mtu mmoja.
"Bosi unahakika kuwa huyo mtu alikuwa mmoja kweli?"
MASHAKA: Ndio ni mmoja ila ni mtu khatari sana.
Ikabidi wamshushe Mporipori aliyekuwa hajitambua na kachubuka mwili mzima sababu ya kuburutwa.
Yuda na Patrick wakiwa kwenye bodaboda wanamuona Anna akivuka barabara, wanaamua kusimamisha na kumfata.
YUDA: Vipi tena mamdogo?
ANNA: Bora hata nimewaona, hivi nilitaka kurudi nyumbani. Nilikuja na Tusa hospitali ila amelazwa.
PATRICK: Amelazwa?
ANNA: Ndio, amepungukiwa na damu. Inabidi aongezewe, sasa nilitaka kwenda nyumbani kuwaambia.
PATRICK: Haina haja mamdogo, mi nitamuongezea kwani damu yangu ni grupu o.
ANNA: Sawa basi twende hospitali, ila Yuda nenda nyumbani kawape taarifa.
Basi Patrick na Anna wakaenda hospitali na Yuda akarudi nyumbani.
Deborah na wenzie walibaki kustaajabu.
DEBORAH: Huko hospitali hawarudi jamani?
PAMELA: Hata na mimi nashangaa maana muda umepita sana.
DEBORAH: Hata tukisema tuwafatilie tutaenda hospitali gani?
PAMELA: Mmh!! Kazi ipo jamani.
Mara Yuda akafika na kuwapa taarifa kuhusu hali ya Tusa wote wakabaki wakishangaa tu.
Pamela na Deborah wakajiandaa kwaajili ya kwenda huko hospitali.
Adamu aliyekuwa na wenzie kumuangalia Mwita, akaamua awachomoke kidogo kwenda kuvuta sigara, hakupenda kuvuta mbele ya mama yake.
Kwahiyo akaenda upande mwingine wa hospitali hiyo, mara akaomuona Anna akikatisha nae akamshangaa na kujiuliza anafanya nini, ikabidi amuite kumuuliza.
Kila mmoja alimshangaa mwenzie, Anna akamueleza Adamu kuhusu Tusa, hapohapo Adamu akatupa na sigara chini akiwa na lengo la kwenda kumuona mwanae.
ANNA: Kwa bahati nzuri mumewe kajitolea kumtolea damu.
ADAMU: Nadhani huyo kijana atakuwa na roho nzuri sana.
Wakaenda hadi alipolazwa Tusa na pembeni alikuwepo Patrick.
Adamu alipomuona Patrick alijikuta akisema
"Mungu wangu!!!"
Adamu alipomuona Patrick alijikuta akisema,
"Mungu wangu"
Akamuangalia kwa makini, Patrick nae akainamisha kichwa chini kumuona baba yake na Tusa.
Adamu akamgeukia Anna na kumuuliza tena,
ADAMU: Umesema yule kijana ni nani?
ANNA: Khee!! Kwani humjui? Yule ni mume wake Tusa anaitwa Patrick.
ADAMU: Hapana, yule ni jambazi.
Adamu akaangalia tena pale alipokuwepo Patrick ila hakumuona tena.
ANNA: Jambazi!! Kivipi?
ADAMU: Si unaona kakimbia.
ANNA: Hajakimbia bhana, utakuwa umemfananisha tu.
Adamu na Anna wakamsogelea Tusa pale kitandani ila hawakuweza kumuona Patrick alipoelekea ingawa nae alikuwa hapo kitandani mwanzoni tu wakati wanaingia walimuona.
Mashaka akawa na lile kundi lake wakimuhudumia Mporipori.
Timmy akaanza kuwaambia wenzie.
TIMMY: Jamani huyo Patrick nadhani amechokoza moto, hata tusimuachie yani kampiga Mporipori kiasi hiki!!
DANK: Hata na mimi nimechukia sana, hapa hata tusikubali.
MASHAKA: Kama mpo tayari kupambana nae basi nitawaelekeza cha kufanya au pa kumpata.
TIMMY: Huo ndio mpango mzima, halafu nitaenda kumkodi jamaa mmoja hivi anaitwa Jangili lazima atammaliza tu huyo Patrick.
DAVID: Nilijua tu Timmy lazima ulete habari za kumkodi mtu ila mimi huko simo.
DANK: Inamaana hutaki kulipa kisasi David?
DAVID: Nilipe kisasi kwa lipi?
TIMMY: Si kampiga Mporipori, huo unaotaka kufanya David ni uoga wa kike. Usituzingue wala nini. Hata ukikataa wewe hutupunguzii kitu.
Mpango ukaanza kupangwa sasa, mpango wa kumpata Patrick na kulipiza kisasi.
Sele alitoka kwao na kwenda nyumbani kwa Deborah kumuona Tusa.
TINA: Tusa yupo hospitali, amelazwa.
SELE: Duh! Hayo majanga sasa. Hebu nambieni na mie niende.
MARIUM: Ila usiku umeshaingia Sele bora uende kesho.
SELE: Yani mama nilale bila kumuona Tusa!! Hapana siwezi mama lazima nikamuone, nimetoka nyumbani kuja hapa kumuona halafu nilale bila kumuona, siwezi.
MARIUM: Huyo Tusa mwanangu atakuingiza kwenye matatizo jamani, wewe ni Tusa, Tusa na wewe. Kumbuka yule ni mke wa ndugu yako tayari.
SELE: Ndio Tusa kaolewa na Patrick, ila siwezi kuacha kumpenda Tusa kwakuwa yeye ndiye mwanamke nimpendae.
MARIUM: Mapenzi yatakuua wewe mwanangu dah!!
Sele hakusikiliza chochote zaidi ya kwenda kwenye hospitali aliyoambiwa.
Marium alibaki kumsikitia tu mwanae.
FAUSTA: Watoto hawasikii Marium, huwa tunawaacha wafanye watakavyo maana na wao washakuwa wakubwa.
MARIUM: Yani Fausta wee acha tu, wananipa presha hawa watoto balaa. Mji wenyewe huu ushaharibika halafu yeye anang'ang'ania kwenda hospitali usiku huu, bora hata wakina Deborah wapo na Yuda sasa yeye peke yake dah!!
Patrick alitoka nje ya hospitali kwanza kwavile hakuwa na la kumwambia mkwe wake huyo.
Deborah na Pamela na Yuda wakafika alipolazwa Tusa.
Wakamkuta Adamu mahali hapo.
DEBORAH: Hivi wewe mwanaume una akili?
ADAMU: Deborah sipendi matusi.
DEBORAH: Swali na jibu tofauti, sijakutusi hapa. Mama yuko wapi?
ADAMU: Unatakiwa uniulize kistaharabu sio unafokafoka tu.
PAMELA: Ila kweli Adamu, mama umempeleka wapi unajua unatuweka roho juu jamani.
ADAMU: Yule ni mama yangu mimi, nyie roho juu za nini?
Nesi akaingia wodini na kuwaambia kuwa muda wa kutazama wagonjwa umepita kwahiyo labda warudi kesho yake.
Ikabidi Yuda awarudishe Pamela na Deborah maana Anna alijitolea kulala na mgonjwa pale hospitali.
Wakina Deborah wakarudi nyumbani huku Pamela akiuliza,
PAMELA: Mbona mdogo wako amekataa nisibaki mimi na amebaki yeye?
DEBORAH: Anna anapenda sana kuhudumia wagonjwa hata usishangae mwaya.
Marium nae akawauliza kama wamemuona Sele.
MARIUM: Vipi mmekutana na Sele njiani?
DEBORAH: Hata hatujamuona kwani nae ameenda?
MARIUM: Ndio.
DEBORBH: Basi hatujamuona.
Marium akaingiwa na mashaka ikabidi amwambie Yuda ajaribu kuwasiliana na waliopo hospitali kama watamuona Sele.
Wanajeshi Singida nao waliendelea na upelelezi wa hali ya juu kuhusiana na vifo vya ajabu na gafla vya wanajeshi hao sita.
Upelelezi uliendelea ndani na nje ya mkoa ila walishindwa kumuhisi mtu yeyote. Safari hii wakaamua kufanya upelelezi wa kimya kimya ili waone kama watagundua chochote kuhusu yale mauaji ya aina moja.
Patrick alikuwa maeneo yale yale ya kuzunguka hospitali, hakuenda mbali ili apate urahisi wa kumuona Tusa.
Kwahiyo alikuwa akizunguka maeneo ya pale pale huku akitafakari mambo mbalimbali haswaa swala zima la Adamu kutaka kumuokoa Mwita, alijiuliza sana wamejuana vipi.
Sele nae hakuwa akipoteza muda kwani alifanya safari ya haraka haraka ili aweze kufika mapema hospitali ila kwa bahati mbaya bodaboda aliyokodi ilipoteza muelekeo na kuwafanya waanguke kwahiyo Sele alijikuta akiumia na kuchubuka, ila aliinuka pale na kuendelea na safari yake ya hospitali.
Alipofika ilikuwa muda umeenda sana, akakaribia eneo la hospitali ile anataka kuingia tu akashangaa mtu akimkaba roba kwa nyuma na kumwambia
"Nimekutafuta kwa muda mrefu sana wewe kijana"
Sele akashangaa kwani hajawahi kuwa na bifu na mtu yeyote katika maisha yake na ubaya ni kuwa hata ile sauti yenyewe hakuitambua kabisa.
Yule mtu alikazana kumkaba Sele.
Yule mtu alikazana kumkaba Sele.
Sele akawa anapambana nae na kubahatika kumtazama ila kabla hajamuangalia vizuri alishtukia akipigwa ngumi nyingine, Sele aliyekuwa kashaumizwa na bodaboda akaanguka chini kwani hakuwa na nguvu yoyote ile.
Patrick alisikia yale marumbano na mapigano ikabidi aende taratibu eneo la tukio ila kabla hajafika alionwa na yule mtu na kukimbia.
Patrick akabahatika kumuona mgongoni ila alihisi ni mtu anayemfahamu kabisa, Patrick alimuhisi kuwa yule ni Maiko.
Patrick akaenda kumnyanyua Sele aliyekuwa na alama nyingi, haswa ajali iliyomfanya apate maumivu makali ya kichwa kwa wakati huo.
Patrick akamsaidia Sele na kumuingiza hospitali ili apate japo matibabu kidogo.
Maiko alikuwa akihema juu juu alienda alipokuwa Rehema.
MAIKO: Mama tuondoke.
REHEMA: Mbona sikuelewi, si ulisema kuwa unaenda kumtafuta Adamu ili turudi wote!
MAIKO: Tuondoke mama ili kesho tujipange kwenda huko kwa Deborah. Mahari hapa si pazuri kabisa.
Ikabidi waanze safari ya kuondoka.
REHEMA: Ila sasa Adamu itakuwaje?
MAIKO: Mama, Adamu anaelewa tulipo atakuja tu mwenyewe.
REHEMA: Basi sawa ila hii Mwanza wala sina imani nayo.
Mashaka na kundi lake wakapata habari kuwa Tusa amelazwa, Mashaka akawaeleza vizuri wakina Timmy ukaribu wa Tusa na Patrick pia akawaambia namna ya kumuumiza Patrick ni kumteka huyo Tusa.
TIMMY: Kazi ya kuteka tena hospitali ni kazi ndogo sana, tuachie tu utaona mambo yetu.
MASHAKA: Sawa nawaamini jamani.
Mipango ya kumteka Tusa ikaanza kupangwa kwa kasi ya ajabu.
Kesho yake Adamu alienda kwa wakina Maiko kuwaeleza kuhusu binti yake aliyelazwa.
Wakina Maiko walikuwa na Mwita pembeni ambaye alikuwa anauguza vidonda vyake.
ADAMU: Jamani jana hamjanioni sababu kule hospitali kuna binti yangu amelazwa.
MAIKO: Binti yako?? Kumbe mwanao nae yupo hapahapa Mwanza?
Kabla hajajibu wakapatwa na ugeni, ni wale wanajeshi wawili marafiki wa Mwita walienda pale na mtu mwingine jumla wakawa watatu.
Kufika pale wakamtambulisha yule mwingine kuwa ni mpelelezi na alikuwa pale kuendelea kupeleleza vifo vya wanajeshi wa Singida.
Mpelelezi huyo aliitwa Franco.
Alienda kumuhoji Mwita juu ya mtu aliyempiga na kuanza kumuhusisha mtu huyo na mauaji.
FRANCO: Je, unamtambua vizuri mtu aliyekupiga?
MWITA: Hapana, simtambui wala simjui sababu alivaa ninja.
FRANCO: Unajua Mwita, wewe ni mwanajeshi tunayekutegemea sana. Na kutokea mtu amekupiga kiasi hicho lazima atakuwa jangili tu, kama tungempata ingetupasa tumuhoji mtu huyo.
Mwita aliendelea kukataa kuwa hamfahamu kwani hakutaka kabisa Patrick ahusishwe, aliamini hausiki hata hivyo aliona kupigwa na Patrick ni haki yake kwani alimbakia mkewe ingawa nae alimchoma kisu.
Adamu akamshangaa Mwita, akatamani aseme yeye anamjua ila Mwita akamkazia macho.
Siku iliyopatia Patrick na Sele walikuwa pale pale hospitali kwaajili ya Tusa.
PATRICK: Najua Sele unampenda sana mke wangu ila ujue kuwa yule ni shemeji yako tu na ataendelea kuwa shemeji yako.
SELE: Sijakataa ila ninapenda kumjulia hali tu.
PATRICK: Hata hujionei huruma Sele, umeambiwa ukapimwe x-ray kwenda hospitali hutaki. Nadhani unataka kuzidiwa wewe.
Patrick alimuhurumia Sele ila bado akawa na maswali kichwani kuwa Sele na Maiko wamefahamiana vipi.
Pamela na Deborah walipoenda hospitali waliwakuta kulekule Patrick na Sele.
Daktari akawapa taarifa nzuri kuwa kesho yake Tusa atapewa ruhusa ya kutoka hospitali.
Wakati wanaongea yote hayo kibaraka wa Mashaka alikuwa akisikiliza kwa makini kabisa.
Hofu fulani ikamtawala Deborah, kuna kitu alikihisi ila hakujua ni kitu gani.
Timmy alirudi kwenye kundi lake na kutoa taarifa, wakaanza kujipanga kwaajili ya kumteka Tusa pale atakapotoka hospitali ili wamkomeshe Patrick.
Timmy ndio alikuwa kibaraka mmbea wa kuchukua na kusambaza taarifa.
Kesho yake Pamela na Deborah wakajiandaa kwenda hospitali kwaajili ya kwenda kumchukua Tusa.
Pamela akamshangaa Deborah akibeba kisu.
PAMELA: Kisu cha nini Deborah?
DEBORAH: Huwezi jua Pamela, tunaweza kukuta machungwa huko na kummenyea mgonjwa.
PAMELA: Ila leo si anatoka, atakuja kula nyumbani.
DEBORAH: Mi nimejisikia tu kutembea na kisu Pamela, hata usinihoji sana.
Wakaondoka na kwenda hospitali.
Kufika hospitali walikuta Tusa amesharuhusiwa na alikuwa akiwangoja wao.
Sele alitakiwa kupima x-ray, kwavile hali yake haikuwa nzuri Patrick akaamua kumpeleka hospitali inayopima maana ile haikuwa na kipimo hicho, Sele alikubali baada ya kuona kuwa Tusa ameruhusiwa.
PATRICK: Mama, tungoje hapo. Msiondoke kabla hatujarudi.
DEBORAH: Sawa nimekuelewa.
Hospitali ni hospitali, mambo mengi na muda nao ulipita bila ya Patrick na Sele kurejea.
PAMELA: Jamani hebu turudi nyumbani, Patrick atatukuta nyumbani.
DEBORAH: Basi twendeni.
ANNA: Ila Patrick atachukia akikuta tumeondoka.
PAMELA: Hebu twendeni jamani, tumekaa hapa kama mazombi.
Wakaamua kuondoka, walipotoka tu nje ya geti wakakuta gari ya kukodi mlangoni na kuwalazimisha wapande.
Wakakubaliana bei na kupanda ndani ya gari, safari ikaanza.
Wakamuelekeza wanapoelekea.
Kufika njiani ile gari ikasimama, Deborah na wenzie hawakuelewa kitu.
Dereva akashuka na kwenda kufungua buti wakatoka watu kama watatu tena waliojazia sana na kwenda kuwashusha wakina Deborah wakishirikiana na yule dereva, halafu wakamuacha Tusa ndani ya gari. Purukushani zikawa za hapa na pale ila wale ni wanaume wakawazidi nguvu wanawake.
Deborah alifanya kitendo cha haraka sana walipokuwa pale nje ya gari, alichomoa kisu chake na kutoboa kwa nguvu tairi moja wapo ya gari lile.
Ile wanataka kuondoa gari ikawagomea, ikabidi washuke wawili ila wamdhibiti Deborah aliyewatobolea tairi.
Wakati wakina Deborah wanaondoka hospitali, nyuma yao Patrick na Sele walikuwa wanarudi na bodaboda, wakawaona kwa mbali wamepanda kwenye ile gari wakaamua kuwafatilia kwa nyuma.
Patrick akashangaa mchezo ulivyokuwa pale njiani. Hapohapo akaongeza mwendo ili kuwafikia.
Ndio muda huo walikuwa wamemshikilia Deborah ili wamfunze adabu.
Patrick alifika pale akiwa amegubikwa na hasira kali kwani mama yake alimpenda sana.
Patrick alifika pale akiwa amegubikwa na hasira kali kwani mama yake alimpenda sana.
Patrick aliwarukia juu na kuwapiga mateke wale watu wawili waliokuwa wamemshikilia Deborah, kitendo hicho kiliwafanya waanguke chini na wamuachie Deborah.
Anna na Pamela walikuwa wakitetemeka tu, Patrick akawafata pale chini na kuanza kuwapa kipondo tena kwa kumuinua mmoja juu na kumtupia kwa mwenzake, waliumia sana kwa kitendo hicho.
Wale waliokuwemo ndani ya gari wakataka kufungua mlango na kukimbia ile wanafungua mlango tu Patrick akabamiza mlango ule wa gari, akasikika Pamela akipiga kelele.
PAMELA: Kuna Tusa humo.
Patrick alimvuta Tusa aliyekuwa ameshikiliwa na Timmy, wakati Patrick akishughulika na wa kwenye gari, Sele nae aliendelea kushughulika na wapale chini ingawa nae tayari alikuwa na maumivu yake mengi tu.
Patrick alimpiga Timmy ngumi moja ya shingo iliyomfanya ahisi kama vile shingo inatoka na kujikuta akianguka chini na kumuachia Tusa, huyu mwingine alitaka kukimbia ila Patrick akamuwahi kwa kumpiga mtama wa nyuma uliomfanya aanguke kifudifudi halafu Patrick akainua mguu wake na kumpiga nao kwa nguvu mgongoni na kisha kumshindilia na ngumi, yule kijana alijikuta akitoa tu damu mdomoni.
Patrick akamgeukia Sele na kumwambia kuwa awachukue wakina Tusa awarudishe nyumbani.
Sele akaenda kuwafata kuwa waondoke ila Deborah akagoma, mwanae akamuomba aondoke, Deborah akakubali kwa shingo upande.
Sele akaondoka nao na kwenda kukodi gari, kufika njiani Deborah akang'ang'ania kushuka, Sele akamzuia ila ikashindikana ukizingatia Sele nae alikuwa ni mgonjwa kwahiyo hakuwa na nguvu kivile za kuweza kumzuia Deborah, ikabidi wamuache ashuke na wao kurudi nyumbani.
Mwita aliendelea vizuri kwasasa, ila Adamu nae aliendelea kumshangaa Mwita kuwa kwanini ameficha kuhusu huyo jambazi.
ADAMU: Hivi kwanini Mwita kwanini?
MWITA: Yule ni mtu wangu wa karibu sana siwezi kumteketeza ukizingatia yeye ndio aliyenionyesha baba yangu.
ADAMU: Ila alikupiga sana na mimi alinipiga.
MWITA: Msamehe bure tu, yule alikuwa na hasira na mimi.
ADAMU: Kwani umemfanyeje?
MWITA: Aah! Mambo ya ujana tu, vipi ile safari ipo au mmeihairisha?
ADAMU: Ipo, tena nimefurahi kuona binti yangu nae amesharuhusiwa kurudi nyumbani tukienda huko utamjua.
MWITA: Itakuwa vizuri kwakweli maana ndugu zangu siwajui kabisa.
Adamu akaamua kwenda kuongea tena na Maiko kuhusu ile safari.
Patrick aliendelea kutembeza dozi ya kichapo kwa wale vijana hadi akili ikawakaa sawa, akamshika Timmy na kumkaba ili ataje aliyewatuma. Mwanzoni Timmy hakutaka kusema ukweli ila kwa maumivu ikabidi aseme kuwa ni Mashaka.
PATRICK: Mashaka, Mashaka nadhani kuna kitu anahitaji kwangu. Haya niambie alipo Mashaka.
Timmy aliendelea kutetemeka huku akisema alipo Mashaka.
Wakati Patrick akiendelea kumuhoji Timmy, mara kijana mmoja pale chini aliinuka na kuchukua jiwe ili ampige nalo Patrick, ila Patrick akagundua kabla na kukwepa, na lile jiwe likaenda kumponda Timmy.
Patrick akamuacha Timmy na kwenda kumshughulikia aliyetupa jiwe, akampa teke la maana lililomfanya hadi apoteze fahamu.
Patrick akawakusanya na kuwaingiza kwenye gari, akachukua kiberiti ambacho huwa anatembea nacho halafu akafunua tanki la mafuta kwenye gari ili awashe moto ambao utawaua taratibu wakina Timmy ndani ya gari.
Ile anataka kuwasha tu akasikia sauti nyuma ikiita,
"Patrickkkkkkk........"
Patrick akageuka nyuma haraka na kukuta mtu amebeba kisu akitaka kumchoma, Patrick akapambana na mtu yule na kumchoma na kisu chake mwenyewe, kisa akamnyanyua na kumrushia kwenye gari walipo wenzie. Halafu akachukua kiberiti chake ili awashe moto.
Mara akamuona mama yake akimsogelea na kumuita kwa hofu.
DEBORAH: Patrick!!
PATRICK: Mama!!
DEBORAH: Mwanangu.
Halafu akamfata na kumkumbatia.
PATRICK: Mama unafanya nini hapa?
DEBORAH: Nimekufuata mwanangu, umepona kweli?
Deborah akawa anampapasa papasa mwilini Patrick kuangalia kama kweli amepona kwani ni yeye aliyepiga kelele ya kumshtua baada ya kuona mtu aliyeshika kisu nyuma ya Patrick.
PATRICK: Usijari mama yangu, mimi ni mzima.
Patrick akageuka ili achome lile gari, Deborah akamzuia.
DEBORAH: Tafadhari mwanangu tafadhari, najua wewe si muuaji. Ulichofanya kinatosha, naomba tuondoke baba. Nisikilize mwanangu.
Patrick alimuangalia sana mama yake aliyeonyesha kumpenda sana, akajikuta akifata pikipiki yake na kumpakia mama yake kisha akapanda na wakaanza safari ya kwenda kwao.
Mashaka aliyekuwa amewatuma vijana wake akashangaa kuona wamekawia kurejea, ndipo alipomtuma kijana aliyebaki David ili akawaangalie kuwa labda wamekwama njiani, ndio yule kijana aliyefika na kuchomwa na kisu chake mwenyewe.
Mashaka alitafakari sana kuona watu wake hawajarejea, akajiuliza maswali mengi bila ya majibu.
"Au wamekutana na Patrick? Inamaana Patrick ndio kawapiga vijana wote wale peke yake mmh!! Labda huyu Patrick si mtu jamani. Ila nitampata tu yani hadi biashara zangu zimesimama kwaajili yake!! Dah! Huyu Patrick ni hatari"
Mashaka aliwaza mengi sana kuhusu Patrick na namna ya kumpata.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Adamu akamueleza Maiko kuhusu ile safari ya kwenda kwa Deborah.
MAIKO: Tatizo langu kubwa ni moja tu kumdhibiti mtoto wa Deborah, je tutaweza?
ADAMU: Kwani ana nini huyo mtoto wa Deborah?
MAIKO: Inamaana humjui?
ADAMU: Simjui kwakweli na hata sijui kama Deborah ana mtoto.
MAIKO: Basi ana mtoto matata sana, mtoto asiye na shukrani kabisa. Ila tutaenda hivyo hivyo naamini busara za mama zitafanya kazi.
ADAMU: Kwavile umeamua kwenda kuwaomba msamaha basi itakuwa ni vizuri.
Wakapanga kuwa kesho yake ndio waende nyumbani kwa Deborah.
ITAENDELEA

0 Comments