Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Mume gaidi sehemu ya kumi na tatu (13)



Patrick na mama yake walifika nyumbani, Deborah alikuwa akitafakari tu jinsi Patrick alivyokuwa anapigana, akajikuta akijisemea

"Au jambazi kweli?"

Kumbe Patrick alimsikia na kumuuliza

PATRICK: Nani jambazi mama?

DEBORAH: Mmmmh aaaah hata sijui ni nani nimejisemea tu, ni wale vijana waliotuteka.

Patrick aliona kama vile mama yake ana kiwewe tu. Akaenda chumbani kwake na kuendelea kutafakari kuhusu Mashaka. Ingawa alishajua alipo ila hakutaka kuondoka siku hiyo ili kuepusha kuhisiwa vibaya na mama yake.

Deborah hakuacha kutafakari yale mapigano ya Patrick.

Marium ilibidi aondoke na Sele ili akapate kutibiwa vizuri yale majeraha ya ajari aliyopata.


Patrick alikuwa chumbani kwake akitafakari vitu vingi hasa upendo wa mama yake kwake.

"Dah! Mama yangu ananipenda sana, sijui kwavile mimi ni mtoto wake wa pekee au ni mapenzi yake tu kwangu!! Nadhani hapa duniani ni mama tu anayenipenda"

Patrick alikuwa akijaribu kuangalia lile tukio la mama yake kurudi wakati anapambana, ingawa hakupenda kumuona mama yake pale ila kwa upande mwingine alifurahia kuona anapendwa vile na mama yake.

"Natamani Tusa nae angenipenda japo kidogo tu, najua hawezi fikia upendo wa mama basi hata angenipenda kidogo tu ningefurahi sana"

Mara akasikia mtu akigonga mlango wake.

Patrick akatoka na kumkuta Tusa mlangoni.

PATRICK: Tusa!!

TUSA: Asante sana Patrick kwa kuniokoa.

Patrick alitabasamu hadi hakuamini ile shukrani aliyoitoa Tusa.


Kama walivyopanga Rehema, Adamu, Maiko na Mwita walienda nyumbani kwa Deborah.

Wakashuka kwenye gari huku Maiko akiwa na tahadhari kubwa ya kukutana na Patrick.

Anna aliyekuwa anafagia, ile kuwaona tu macho yake moja kwa moja yalienda kugonga sura ya mtu mmoja tu, akajikuta akiangusha fagio chini na kusema kwa mshangao,

"Maiko!!"

Deborah aliyekuwa anatoka ndani akashangaa sana, kilichomshangaza ni kuwa Anna amemjulia wapi Maiko.


Deborah aliyekuwa anatoka ndani akashangaa sana, kilichomshangaza ni kuwa Anna amemjulia wapi Maiko.

Deborah akamsogelea Anna na kumuuliza.

DEBORAH: Umemjulia wapi huyo mdogo wangu?

Anna alizidi kumuangalia Maiko kwa hasira hadi pale alipomuona Mwita akajikuta akimkimbilia na kumkumbatia,

ANNA: Jamani Frank, umemtolea wapi huyo shetani?

Frank nae akawa amemkumbatia Anna bila ya kusema chochote.

Deborah akaenda mlangoni kwake.

DEBORAH: Sidhani kama itakuwa busara kwa wewe Maiko kuingia humu ndani kwangu.

REHEMA: Hana nia mbaya Deborah, amekuja ili muweze kumsikiliza japo kidogo tu.

Deborah aliwaangalia sana na kuona kuwa hawajamuelewa tu, akaamua kuwaachia mlango wapite ili wajuane humo ndani.

Halafu Deborah akaamua kwenda kumuita Patrick ili aone kama kweli Patrick na Maiko wanaukaribu wowote.


Fausta na mwanae Tina siku hiyo walienda hospitali kwaajili ya uchunguzi wa hapa na pale, Fausta alitaka kujua maendeleo yake na kuonekana kuwa anaendelea vizuri na kumpima mwanae Tina, walifanya safari hii ya hospitali wakiwa wamesindikizwa na Yuda.

Tina nae alipopimwa akagundulika kuwa anaujauzito, Tina alishtuka sana na kuanza kulia, mama yake akawa anambembeleza.

TINA: Mama sitaki mimba ya kubakwa mimi sitaki kabisa.

FAUSTA: Nyamaza mwanangu, kumbe ulibakwa! Mbona hukusema mama?

TINA: Niliona aibu mama, nilibakwa na wanaume mashetani tena walinibaka kwa kupokezana. Mama sitaki hii mimba sitaki mama.

Yuda nae akasikia na kuwasogelea.

YUDA: Mimba? Nani ana mimba tena hapa?

Tina alizidi kulia na kushindwa kujielezea.

FAUSTA: Yani hapa ni tatizo juu ya tatizo jamani, sijui hata tufanyeje!

YUDA: Tina ana mimba au?

FAUSTA: Ndio, Tina ana mimba.

YUDA: Aaah!! Hapana kwakweli nasema hapana jamani yani.... Aaah! Hapana.

Tina alizidi kulia pale alipoinama.

FAUSTA: Mwanangu, haya mambo twende tukayajadili nyumbani hapa hospitali hatutaelewa cha kufanya. Twende nyumbani ili tuweze kupata maamuzi sahihi.

YUDA: Sikuzote nampenda Tina na sijawahi mlazimisha kufanya nae kitu chochote kumbe wenzangu walikuwa wanajibakia!! Aaah! Imeniuma sana.

FAUSTA: Najua kama inauma, ila turudi nyumbani kwanza jamani. Kwani mimba kitu gani bhana, cha muhimu kwasasa ni uhai. Twendeni nyumbani tukajadili.

Tina alijawa na machozi tu usoni, wakaamua wafanye safari ya kurudi nyumbani.


Marium alipotoka kumsindikiza mwanae Sele hospitali na kurudi nyumbani.

SELE: Mama, nataka kwenda kumuona Tusa.

MARIUM: Hivi mwanangu, unajua huyo mwanamke atakuu wewe!!

SELE: Hawezi kuniua mama tunapendana sana.

MARIUM: Hata kama mnapendana mwanangu, kuna kipindi kwenye mapenzi ni bora kusema inatosha sasa. Wanawake wangapi hapa mtaani wanakupenda mwanangu? Kuna wakina Sara na Maria, wanatamani hata leo utamke kuwa unawahitaji ila hawapati hiyo nafasi. Yani wewe na ndugu yako mnamng'ang'ania Tusa kama vile yeye ndiye mwanamke pekee duniani.

SELE: Mama, hao unaowasema wananipenda hawawezi kuwa kama Tusa. Nampenda sana Tusa na pia najua kuwa Tusa ananipenda, sina nia ya kumpora Tusa kwa Patrick kwasasa ila najua penzi la kweli halifi mama haijalishi nini kitatokea.

MARIUM: Penzi la kweli halifi labda kwa mwanamke na mwanaume wa kizungu ila sio sisi wenye ngozi nyeusi, tumeumbiwa tamaa na hatuna hiyo kitu mapenzi. Tusa angekupenda kweli asingekuwa na Patrick.

SELE: Inamaana wewe mama hukumpenda baba?

MARIUM: Mimi na baba yako tulipendana kweli ndomana tukadumu ila huyo Tusa hakupendi acha kujidanganya mwanangu.

Sele aliyatafakari maneno ya mama yake ila kwajinsi alivyokuwa anampenda Tusa yale maneno hayakumkaa kichwani hata kidogo.

SELE: Hivi mama unajua mimi nilimngoja sana Tusa, tangu anasoma hadi alipomaliza kama kunisaliti si angenisaliti kipindi kile jamani!

MARIUM: Hebu acha ulimbukeni wa mapenzi mwanangu, Tusa kashakuwa skrepa pale alipo. Mwanamke gani yule sasa, mimba nne ndani ya mwaka mmoja halafu wewe bado upo na msemo wa kumpenda!! Acha ujinga mwanangu, Tusa hakufai tena muachie tu Patrick maradhi yake yale. Yule Tusa pale alipo spana mkononi bora akae na Patrick atasaidiwa na pesa sasa kwako si atajifia tu? Acha kung'ang'ania mitumba iliyochoka mwanangu.

Sele akamuangalia sana mama yake halafu akaondoka, Marium akabaki akijisemea,

"Sijui karogwa jamani mwanangu mmh!! Mapenzi mabaya sana ukiyaendekeza."


Patrick alipokuwa akizungumza na Tusa pale mlangoni akaona itakuwa vyema sana kama wakikaa chumbani, kwahiyo akamuomba Tusa akae nae chumbani.

PATRICK: Kwanza pole sana Tusa kwa yote yaliyokupata, umebadilika sana Tusa yani umekuwa tofauti kabisa kama vile sio wewe niliyekuona facebook.

TUSA: Umenipitisha mapito ambayo sikuwahi kuyawaza maishani mwangu, umenifanya niwe mtu wa kilio na mateso. Nimebaki mwanamke picha tu ila si mwanamke kama nilivyotamani kuwa.

PATRICK: Naelewa Tusa ila yote hayo kwavile hukupenda kunielewa vile ninavyokupenda Tusa.

TUSA: Ubaya ni kuwa hata wewe hukupenda kunielewa kama sikupendi Patrick, umetumia nguvu nyingi na pesa nyingi sana kwaajili yangu Patrick ila kila nikitafakari yaliyopita nakuweka wewe kwenye kundi la wanaume wenye roho mbaya, ila kwasasa umenisaidia sana Patrick sinabudi.....

PATRICK: Hunabudi nini? Niambie Tusa, hunabudi kuniambia kuwa wanipenda?

Mlango wa Patrick ukagongwa ikabidi aende kufungua na kumkuta mama yake akigonga.

DEBORAH: Kuna wageni sebleni naomba twende ukaongee nao.

PATRICK: Nije na Tusa?

DEBORAH: Ndio njoo nae tena yeye anahusika zaidi.

PATRICK: Wageni gani hao mama?

DEBORAH: Nyie njoeni tu mtawaona.

PATRICK: Sawa mama tunakuja.

Ikabidi Patrick amwambie Tusa kuwa waende.

PATRICK: Halafu tutarudi kuzungumza vizuri sawa Tusa?

TUSA: Sawa, hakuna tatizo.

Patrick na Tusa wakatoka chumbani na kwenda sebleni.


Mashaka alikuwa na mawazo tu baada ya kuwakuta wale vijana wake wakiwa na hali mbaya sana, ikabidi aamue kusafiri na kwenda Arusha kuchukua baadhi ya vijana wao kwaajili ya Patrick.

Kule Arusha walimshangaa sana Mashaka kwani mawazo yalianza kumkondesha, Tulo ndio aliyempokea kwani ndio aliyeachwa kwenye himaya ya Maiko kwa muda.

TULO: Kwakweli tumeshangaa sana, kimya kirefu kwani huko Mwanza kuna tatizo gani?

MASHAKA: Mwanza hakuna tatizo ila Patrick amekuwa tatizo kubwa sana kwetu, Patrick ameua vijana wengi tu. Kwakifupi Patrick hafai, inabidi kujipanga kweli ili kwenda kupambana nae hata sijui Patrick amejifunzia wapi yale mambo ya mapigano.

TULO: Itakuwa China tu, ila Patrick inatakiwa tumuendee taratibu. Unajua yule jamaa ni jasiri sana halafu yupo kamili kila idara. Ngoja tufanye maamuzi ya taratibu tutampata tu.

MASHAKA: Tatizo muda, kazi nyingi zimelala kwaajili yake.

TULO: Hakuna tatizo, mi namjua Patrick vizuri niachie hiyo kazi kwa muda utaona majibu yake.

Mashaka akazungumza mengi na Tulo huku akiwaza hasara alizopewa na Patrick.


Patrick na Tusa walienda sebleni, Patrick ile anatokeza akabambana na sura ya Mwita, kuangalia pembeni anamuona Maiko halafu akamuona Adamu hapo akanywea na kurudi kwenye korido haraka.

TUSA: Mbona umerudi nyuma gafla?

PATRICK: Aaah! Hata sielewi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

TUSA: Twende bhana, hivi hadi wewe Patrick unakuwa na aibu kwa wageni? Twende bhana.

Patrick akaona njia bora ni kujifanya kuwa wote wale hawafahamu, kwanza aliona Maiko ni longolongo tu pale alitamani akutane nae kwenye anga zake amfundishe adabu.

Patrick na Tusa wakajitokeza, na kitendo cha kwanza ni Tusa kumkimbilia baba yake na kumkumbatia huku machozi yakimtoka ilikuwa ndio anamuona kwani kule hospitali wakati Adamu alienda kumtazama alikuwa amelala.

TUSA: Jamani baba, nimefurahi kukuona baba.

Patrick alikaa na kuwasalimia kama vile watu asiowajua halafu akainuka na kutoka nje, Deborah akawa anastaajabu kuona hali ile na kujiuliza kuwa inamaana hawajuani kweli na Maiko.

Wakati Patrick alipokuwa anatoka nje akakutana na Sele mlangoni wakasalimiana halafu Sele akaingia ndani.

Patrick alikaa pale nje akitafakari uwepo wa Maiko mule ndani na kitu gani akamfanye mara gafla akamuona Sele akitoka nje kwa jazba na kubeba jiwe, Patrick akashangaa kwani alimjua Sele vizuri kuwa si mtu wa hasira kiasi kile akaamua kumfatilia Sele ndani.

Lengo la Sele lilikuwa ni kumponda Maiko na lile jiwe kwani alijua wazi asingeweza kupambana nae kwa yale maumivu yake, akalishika lile jiwe kisawasawa na kulirusha mahali alipokuwa Maiko.


Akalishika lile jiwe kisawasawa na kulirusha mahali alipokuwa Maiko.

Patrick akakimbia mbele gafla na kulidaka lile jiwe, Tusa nae akainuka pale alipokuwa amekaa na baba yake akawa anaongea kwa jazba.

TUSA: Patrick umelizuia kwanini hilo jiwe kumponda huyu shetani? Tena sikuwaona ni mashetani mawili yapo hapa, umezuia kwavile tabia zao na zako zinaendana?

Wakati Tusa alikuwa akizungumza hayo, Sele nae alikuwa amekazana kutaka kupambana na Maiko ila Patrick akawa anamzuia hata Maiko alishangaa leo kutetewa na Patrick.

PATRICK: Punguzeni hasira Sele na Tusa.

SELE: Unajua alichonifanya huyu Patrick? Unajua huyu alichonitenda?

PATRICK: Punguza hasira kwanza Sele tuzungumze, kumbuka hasira hasara.

TUSA: Yani unavyoongea Patrick kamavile na wewe ni mtu mwemaaa kumbe ndio walewale kasoro majina.

PATRICK: Tusa, usiwaze mabaya yangu tu, kumbuka na mema yangu.

TUSA: Katika wanaume ninaowachukia humu duniani ninyi watatu mnaongoza, siwapendi siwapendi siwapendi.

Tusa akatoka nje, Deborah akashangaa kuona Tusa ni muongeaji kiasi kile kwani mara nyingi huwa akimshuhudia anapolia tu. Patrick nae akaamua kutoka kumfata Tusa nje.

Deborah akamshika Sele mkono na kutoka nae nje pia.


Patrick akaamua kuzungumza na Tusa.

PATRICK: Tusa, nakuomba usinichukie. Mimi Patrick wa leo si Patrick uliyemfahamu kipindi kile nakupenda Tusa na sina roho mbaya kama unavyonifikiria na wala sina tena ushirika wowote na Maiko.

TUSA: Kama huna ushirika na Maiko mbona umemzuia Sele asimponde na jiwe?

PATRICK: Tusa, pale ndani si mahali sahihi pa kufanya hivyo. Sele angeweza kumuua Maiko na je angefunguliwa kesi ya mauaji si angefungwa maisha? Je, uko tayari kuona Sele akifungwa maisha?

TUSA: Inamaana Patrick unampenda Sele?

PATRICK: Ndio nampenda, Sele ni ndugu yangu siwezi kumchukia. Swala la Maiko ni dogo sana kwangu, hiyo kazi niachieni mimi.

TUSA: Sitapenda kuona Sele anafungwa sababu nampenda.

PATRICK: Hapo ndipo unapokosea Tusa, unatakiwa unipende mimi. Mimi Patrick ndio mumeo wa maisha.

Halafu Patrick akaenda kumfata Sele aliyekuwa ametolewa nje na Deborah.

Tusa alimuangalia Patrick na kuona kama mtu wa tofauti, akashangaa Patrick kumuhurumia mtu kufungwa, ila Tusa akajisemea,

"Sijawahi kuua katika maisha yangu ila huyo Maiko lazima nitamuua"


Anna aliyeachwa mule ndani na wale wageni.

ANNA: Kwakweli Maiko wewe ni shetani, hakuna binadamu atakayeweza kukupenda baada ya kugundua uyafanyayo. Najua wazi hata hao walioongozana na wewe hawakujui kuwa wewe ni mwanaume wa aina gani ila wakijua mambo yako watakuonea kinyaa.

ADAMU: Maiko, hebu tuweke wazi tafadhari ni mambo gani uliyoyafanya na iweje hadi binti yangu akuchukie?

Akatokea Deborah na kusema,

DEBORAH: Si binti yako tu anayemchukia, huyo Maiko unayemuona hapo mbele anachukiwa hadi na sisimizi nadhani ukimjua vizuri hata wewe mwenyewe utamchukia huyo shetani.

REHEMA: Mungu wangu, najua yote haya sababu ya kutokumlea mwanangu mimi mwenyewe, ona mambo yalivyo sasa.

PAMELA: Majuto ni mjukuu mama, huyo Maiko hapa Fausta bado hajarudi nae akirudi ana yake.

ADAMU: Hadi Fausta? Una matatizo gani Maiko? Ndugu yangu niliyekujua ukubwani, nini tatizo Maiko?

Maiko alikuwa ameinama tu kwa aibu.


Patrick akaenda kuzungumza pia na Sele.

PATRICK: Kwani yule jamaa umemjulia wapi Sele?

SELE: Kwanza ungeniachia yule mtu nimponde na jiwe, amekuwa akiniwinda muda mrefu sana. Yule ni adui yangu namba moja humu duniani.

PATRICK: Kwakweli mnanishangaza, hivi huyu Maiko ni mtu wa aina gani? Na kwanini ametenda matukio mengi ya ajabu kwa watu wengi?

SELE: Nina hasira nae sana, na siwezi kumsamehe hadi naingia kaburini.

Patrick alimtafakari sana Maiko ila alikosa jibu la kwanini Maiko amehusika kwenye matukio mengi ya ajabu.


Tina na mama yake walirudi huku macho ya Tina yakiwa yamejaa machozi.

Tusa ndiye aliyewapokea na kuwauliza kwanini Tina analia.

TINA: Nina mimba Tusa, tena mimba ya kubakwa. Naichukia Mwanza Tusa.

Tusa nae akajikuta akilia na kukumbuka mikasa yake yote ya mimba.

Ikabidi Patrick na Sele nao wawasogelee na kuamua kuingia nao ndani, Patrick alitaka kupata maelezo yakinifu juu ya uwepo wa Patrick mule ndani wakati anaonyesha kuwa ameshaumiza watu wengi.

TUSA: Pole sana Tina ndugu yangu.

Walipoingia ndani, Tina akamuona Maiko akamgeukia mama yake na kumwambia.

TINA: Mama, mwanaume mwenyewe aliyenibaka ni yule pale.

Wote wakamtazama Maiko na kumshangaa.

FAUSTA: Maiko, Maiko, Maiko yani umenibakia mwanangu? Hivi unajua kama umembaka mwanao shetani mkubwa wewe?

Fausta akaenda kumvaa Maiko mwilini, kukawa na varangati ndani ya nyumba kwani Fausta hakutaka kumuachia Maiko.

ADAMU: Haya makubwa sasa mi hata sielewi, yani Maiko umembaka Tina mtoto wetu dah!!

TUSA: Sio Tina tu hata mimi mwenyewe alinibaka.

PAMELA: Nini? Khe khe khe, Mungu wangu laana gani hii jamani!!

Wakajaribu kumtoa Fausta alipomshikilia Maiko ilikuwa ni kazi ngumu, ikabidi Maiko atumie nguvu zake mwenyewe na kutaka kukimbilia nje ila alikutana na Tusa mlangoni akiwa ameshika kisu na kumchoma nacho begani.

Damu nyingi zikamtoka Maiko ila akampushi Tusa na kutoka huku kisu kikiwa begani.

TUSA: Na bahati yako ningekubebea panga wewe.

Ikabidi Rehema nae atoke na kumfata Maiko aliyekuwa akivuja damu.


Tulo kama alivyomuahidi Mashaka akaamua kufunga safari kuelekea Mwanza ili kuweza kuonana na Patrick kwani Patrick alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana kwahiyo alijua atampata tu.


Patrick bado alikuwa haelewi kitu, akaomba aelekezwe na Pamela akamwambia jinsi ilivyo ila bado hakuelewa.

PATRICK: Hii familia sasa imeanza kunichosha siielewi, siielewi, siielewi. Hivi inakuwaje mzazi hadi anashindwa kukaa na watoto wake hadi mambo kama haya yanatokea?

PAMELA: Sasa wewe Patrick unamlaumu nani?

PATRICK: Namlaumu huyo bibi, ila kiukweli familia ya Tusa imenichosha. Kwanza haieleweki. Familia haina mwanzo wala mwisho.

PAMELA: Usimlaumu Tusa tu, je wewe familia yako inaeleweka?

PATRICK: Ndio familia yangu inaeleweka na wote tunafahamiana sio kama familia yenu.

PAMELA: Kama inaeleweka mbona wewe na nduguyo kumgombea mke mmoja? Je ulifahamu kama Mwita ni mtoto wa Anna? Na je baba yako mzazi unamjua? Hata wewe familia yako haieleweki.

Kwenye swala la baba mzazi Patrick akawa ameguswa vilivyo na kuamua kumfata mama yake Deborah.

PATRICK: Mama, naomba na mimi leo unitajie baba yangu alipo sitaki mambo kama haya yatokee na kwangu. Sitaki kuwa na familia isiyoeleweka.

Deborah akajikuta akihema kwa nguvu na kuanguka.


Deborah alijikuta akihema kwa nguvu na kuanguka.

Ikabidi Patrick aanze kumpepea mama yake, Pamela nae akaenda kumsaidia hadi pale Deborah alipojisikia vizuri, akahitaji maji na Pamela akaenda kumletea.

PATRICK: Pole sana mama.

DEBORAH: Asante Patrick.

Pamela alipoyaleta yale maji, Deborah akayanywa na mengine kujimwagia kichwani.

Tusa nae akatoka ndani na kuwafata pale nje.

Patrick aliwaacha pale na kwenye nyuma ya nyumba yao kutuliza mawazo, alikuwa akifikiria kuwa kwanini mama yake hapendi kumwambia ukweli kuhusu baba yake.

PATRICK: Hii ni haki yangu, lazima niujue ukweli kama mtoto.

Kumbe Tusa alikuwa nyuma yake,

TUSA: Ukweli gani?

PATRICK: Ukweli kuhusu baba yangu, sitapenda familia yangu ikose uleleo kama familia yenu.

TUSA: Familia yetu haina uelekeo kivipi?

PATRICK: Familia yenu haieleweki, eti Maiko ni babako mdogo.

TUSA: Hapana, haiwezekani kabisa. Maiko hawezi kuwa ndugu yangu hata kidogo.

Patrick akajaribu kumuelekeza kama vile alivyoelekezwa ila Tusa akakataa kabisa, ikabidi aende ndani ili kupata ukweli wa mambo.


Rehema aliyekuwa ameongozana na Maiko akawa anajaribu kumshawishi Maiko ili warudi tena kwa Deborah na waweze kuweka mambo yote sawa.

MAIKO: Angalia mkono wangu ulivyojaa damu, unataka niende wakanichinje kabisa? Siwezi.

REHEMA: Sikia nikwambie, marumbano si mazuri kwa wanandugu. Tunatakiwa kukaa chini na kumaliza tofauti zote na kujuana, kwa mtindo huu unadhani utawajuaje ndugu zako wengine?

MAIKO: Mmh! Kurudi tena kule ni kujitakia kifo tu.

REHEMA: Hapana mwanangu, mimi mama yenu nipo.

MAIKO: Vipi baba, yuko wapi yeye? Maana nadhani itakuwa vyema nikianza kufahamiana na yeye kwanza.

REHEMA: Aliuwawa, tena alikufa kifo cha kikatili sana. Alikuwa anaishi Morogoro.

Maiko hofu ikamtanda kidogo kusikia kuwa baba yake aliuwawa tena ni Morogoro.

MAIKO: Aliitwa nani?

REHEMA: Walipendelea sana kumuita mzee Ayubu na Ayubu ndio jina lake.

Maiko akamuomba bi.Rehema warudi tena nyumbani kwa Deborah, nia yake ni kwenda kuzungumza na Patrick ili apate kujua ukweli.


Tusa aliingia ndani na kuanza kumwambia baba yake kuwa amwambie ukweli kuhusu Maiko.

Adamu akamueleza Tusa juu ya undugu wao.

Tusa akashangaa sana, kisha akamgeukia Mwita na kumuangalia tena baba yake.

TUSA: Usiniambie kuwa na huyu ni ndugu yetu.

ADAMU: Ndio ni ndugu yetu kwani ni mtoto wa Maiko.

TUSA: Baba, yani watu wote wameshindwa kuwa ndugu zetu zaidi ya hawa? Kwakweli siwapendi, siwataki na sitawakubali kamwe katika maisha yangu.

ADAMU: Mwanangu Tusa, hawa ni ndugu zetu tu hatuwezi kuwaepuka.

TUSA: Hao ni ndugu zako wewe na mama, mimi siwataki kabisa. Na laiti ungejua walivyonitenda hata usingewatetea hivyo.

Tusa akaenda chumbani, hakutaka tena kukaa pale sebleni kwani alihisi kuchanganyikiwa.

Anna alimuangalia Mwita kwa makini, kisha akamwambia.

ANNA: Natumai, matendo yako si sawa na matendo ya Maiko.

Mwita alikuwa kimya tu kwani aliona aibu kwa vitendo alivyowafanyia ndugu zake.


Fausta aliamua kumueleza Tina ukweli kuhusu Maiko, akamueleza kuwa Maiko ni baba yake.

Kwakweli Tina alilia sana na mama yake pia alilia.

PAMELA: Ila haya ni madhara ya kumficha mtoto kwa baba yake kwa kipindi kirefu.

FAUSTA: Hujui kitu wewe Pamela, unaongeaongea tu. Najua kwasababu hiki kilio ni kwangu ila kingekuwa kwako ungeyahisi maumivu yangu.

PAMELA: Basi yaishe jamani.

FAUSTA: Hujawahi umia kama hivi Pamela, mimi nimeumia. Inaniuma sana.

Tina kila alipoifikiria ile mimba alijikuta akizidi kulia zaidi na zaidi.


Patrick akaamua kumfata tena mama yake ili azungumze nae japo kidogo.

PATRICK: Ila mama nina haki ya kujua ukweli kuhusu mimi.

DEBORAH: Kweli unataka kuujua ukweli? Unataka kujijua wewe ni nani?

PATRICK: Ndio mama, nahitaji kujua.

DEBORAH: Nitakueleza ukweli, ila je ungependa nikueleze mbele ya nani?

PATRICK: Mbele ya wote wanaokufanya ulie kila unapokumbuka zamani, na mimi nitakuwa pembeni yako nikiyafuta machozi yako.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

DEBORAH: Kweli mwanangu?

PATRICK: Kweli mama kwani natambua kama mimi ndio faraja yako.

DEBORAH: Basi......

Wakajikuta wakishangaa kumuona bi.Rehema na Maiko wakija, Patrick akajiandaa kumdhibiti Maiko kama ataleta fujo.


Maiko akashukuru kumuona Patrick pale nje kwani ndio ilikuwa shida yake iliyompeleka pale.

Akamuomba Patrick kwaajili ya mazungumzo, mwanzoni Patrick alikuwa anasita ila badae akakubali na wakasogea kuzungumza.

MAIKO: Samahani Patrick, eti yule mzee aliyeuliwa na kundi letu kule Morogoro aliitwa nani?

PATRICK: Kwani umekumbuka nini? Yule mzee tulimuua bila hatia, roho yangu inanisuda hadi leo. Aliitwa mzee Ayubu.

MAIKO: Mungu wangu, dah nimeshiriki kumuua baba yangu.

PATRICK: Baba yako? Nani baba yako?

MAIKO: Yule mzee Ayubu ni baba yangu mzazi, ndio nimejua leo. Dah! Mashaka amemaliza familia yangu.

PATRICK: Inamaana tulimuua babu yake na Tusa! Dah!

Patrick alihisi kutokuwa sawa kimawazo, muda huohuo Maiko akaondoka akiwa amenywea bila ya bi.Rehema kujua kama kaondoka kwani yeye alibaki kuzungumza na Deborah.

Patrick nae akapigiwa simu na rafiki yake kuwa aende mjini, Patrick akaondoka nyumbani na kwenda mjini ili kupunguza mawazo kidogo.


Tulo ndiye aliyempigia simu Patrick, na alikuwa mjini akimngoja.

Patrick alipofika walipokeana vizuri na kuongea hili na lile kama marafiki, wakaagiza na vinywaji wakawa wanakunywa huku wakiendelea na maongezi.

Simu ya Patrick iliita tena na alitakiwa kwenda kuongea mbali kidogo, kumbe huku nyuma Tulo akamuwekea Patrick madawa kwenye kinywaji chake.

Patrick aliporudi akakaa na kuinua kile kinywaji ili anywe ile kukifikisha mdomoni tu akasita na kushusha chupa chini, kisha akamtazama Tulo na kumuuliza.

PATRICK: Umeniwekea nini humu?

Tulo akabaki anashangaa kuwa Patrick kajuaje.


Tulo akabaki anashangaa kuwa Patrick kajuaje.

Patrick akamuangalia tena Tulo kwa umakini kabisa,

PATRICK: Umeweka nini kwenye kinywaji changu Tulo?

TULO: Hapana, sijaweka chochote.

PATRICK: Sipendi kudanganywa Tulo, niambie ukweli kwa usalama wako.

Tulo alimwangalia Patrick aliyeonekana kubadilika usoni na kushindwa kujibu.

PATRICK: Natumai unajipenda Tulo, sema ukweli umeweka nini humu?

TULO: Nisamehe Patrick.

PATRICK: (Akacheka), Tulo wewe ni mpumbavu sana. Haya sema umeweka nini humu?

TULO: (Huku akitetemeka), nimeweka madawa ya kulevya.

PATRICK: Ili iweje?

TULO: Ili ulewe na niweze kwenda nawe Arusha kukukabidhi kwa Mashaka.

PATRICK: Kweli kuna watu hamna akili kabisa, hivi hujiulizi kwanini huyo Mashaka alishindwa kunichukua mwenyewe? Hujiulizi kabisaa yani? Halafu unajiletaleta tu.

TULO: Kwani umejuaje kama nimeweka kitu humo?

PATRICK: Sijakuona ukiweka ila nimekisia tu, kumbe hisia zangu ni za kweli. Ila wewe Tulo ni mpumbavu sana na siwezi kukusamehe kwa hili.

Sura ya Patrick ilionyesha kuchukizwa sana na kitendo hicho.

Tulo alikuwa akitetemeka tu.

TULO: Nisamehe Patrick.

PATRICK: Sikia Tulo, msamaha wangu kwako ni huu, mimi na wewe twende mahali tukapambane na kupimishana ubavu. Tafadhari usikatae ofa hii huwezi jua, unaweza jikuta umefanikiwa kunipiga sana hadi kunipeleka kwa huyo Mashaka wako.

TULO: Patrick hapana, nikishindwa mpambano je?

PATRICK: Basi utakuwa kibaraka wangu bila malipo. Na hakuna kukataa, lazima ukubali kupambana na mimi.

Tulo aliamua kukubali ili akajaribu bahati yake, huku Patrick akifurahi kumpata mtu wa kumkong'ota na kupunguza hasira yake.

Patrick akakodi usafiri na kuondoka yeye na Tulo kuelekea porini kidogo.


Tusa alienda kumbembeleza Tina kwani hata yeye alishapitia mapito kama yale na kuanza kuzungumza ya pale na hapa.

TINA: Natamani hata hii mimba itoke.

TUSA: Tina, usije ukawa kama mimi tafadhari.

TINA: Tusa, kwani wewe una tatizo gani? Wazazi wako wote wawili wapo bega kwa bega na wewe, tofauti na mie niliyebakwa na kupewa mimba na mtu ambaye naambiwa ni baba yangu. Tusa, una mume mzuri na mwenye mapenzi ya dhati, tatizo lako nini hapo?

TUSA: Huyo mume huyo unayemsema ni nyoka. Kwakweli wewe Tina na mama yangu ndio mlioniponza hadi mimi kuangukia mikononi mwa Patrick.

TINA: Tusa sikia, Patrick ni mwanaume mzuri sana. Najua wadada wengi wanatamani kuwa nae ila hawajapata hiyo bahati kwavile amekupenda wewe. Mi nadhani uache kulaumu ila ujivunie kwa kumpata mwanaume kama Patrick.

TUSA: Tina unasema kwavile hujui nini ambacho kilinipata wakati nipo Arusha na Patrick, usimuone vile Patrick, yule ni mwanaume katili sana hafai kuigwa na jamii. Ingawa ndoa yangu na Patrick ilikuwa ya kulazimisha ila kuna kipindi nilikubaliana na hali halisi na kuanza kujifunza kumpenda Patrick kama mume. Ila Patrick, ana roho mbaya, ni katili wa kutupwa kwa kifupi Patrick hana tofauti yoyote na magaidi. Patrick ni mume gaidi siwezi kumpenda hata kidogo, hata anifanyie nini sitampenda kamwe. Ukatili alionifanyia Patrick kule Arusha hautafutika kamwe kwenye mawazo yangu hadi naingia kaburini.

TINA: Ila ndio mumeo Tusa, mi sioni ubaya wowote kwa Patrick. Ni mpole, mcheshi na mkarimu. Pia anapenda kusaidia watu. Patrick ni mume mwema unaetakiwa kujivunia Tusa.

TUSA: Usilolijua Tina ni sawa na usiku wa giza, laiti ningekuwa na video nikuonyeshe matendo ya Patrick na wenzie ungenielewa.

TINA: Mmh! Hapana bhana, Patrick ni mume mwema. Jivunie kumpata Tusa.

Tusa alimuangalia sana Tina huku akisema kimoyomoyo,

"Uliniponza Tina nikatumbukia kwenye shimo lenye miiba, ila Mungu amekulaani na wewe umetumbukia kwenye shimo lenye moto"


Adamu alikuwa na wakati mgumu sana wa kuelewa.

Pale nyumbani wakashangaa kutokuonekana kwa Patrick wala Maiko.

Rehema alijikuta akiwa mwenyewe na Deborah.

Ikabidi Adamu akaongee na mama yake.

ADAMU: Mama, hata sioni umuhimu wa kuendelea kubaki hapa Mwanza, bora turudi Dar tu.

REHEMA: Ni kweli mwanangu ila itapendeza kama tukirudi wakati tumeyaweka mambo yote sawa.

ADAMU: Kwakweli mama nimechoka, hadi nahisi kuchanganyikiwa kwakifupi sielewi kitu kabisa.

REHEMA: Hata mimi sielewi ila Mungu atasaidia kila kitu kitakuwa peupe na tutaelewana tu.

Bi.Rehema alikuwa mgumu kuondoka kwani alihisi kuwa kuna vitu vingi ambavyo hawajavijua na wanatakiwa kuvijua.


Hofu ikamtanda Deborah kwani tangu alipomuona Patrick akiongea na Maiko hakuwaona tena, wasiwasi wake ni kuwa wameenda njia moja. Akaenda kumuuliza maswali Tusa. Ambapo Tusa alimweleza jinsi kulivyokuwa na ukaribu kati ya Patrick na Maiko.

DEBORAH: Inamaana Patrick na Maiko walikuwa wakifanya kazi wote?

TUSA: Ndio, walikuwa wakifanya kazi pamoja.

Deborah akajikuta akitafakari sana na kukosa jibu.

DEBORAH: Tusa, mbona hukuniambia kwa kipindi chote hiki?

TUSA: Patrick alinikataza, hakutaka wewe ujue chochote kuhusu yeye na Maiko.

Sasa Deborah akaanza kutengeneza picha mbalimbali katika akili yake.


Patrick na Tulo walifika kwenye sehemu ambayo Patrick aliona ni njema kwa wao kupambana.

PATRICK: Naomba tupambane, tumia nguvu zako zote kwaajili ya kunidhibiti hadi ufanikiwe kunipeleka kwa Mashaka.

TULO: Kwanini Patrick unasema hivyo?

PATRICK: Hakuna cha kwanini hapa, hilo si ndio lilikuwa lengo lako!

Tulo akatulia tu, Patrick akaamua kulianzisha kwa kumpiga Tulo ngumi moja ya pua, ngumi hii iliamsha hasira, maumivu na ghadhabu kwenye mwili wa Tulo na mpambano kati yao ukaanza sasa.

Patrick alikuwa anapambana kawaida tu ili kumpa nafasi Tulo kujidai kwanza kabla hajaanza kazi yake.


Maiko alipoondoka nyumbani kwa Deborah, mpango wake ulikuwa ni mmoja tu. Kwenda Arusha kupambana na Mashaka kwa kumuulia baba yake.

Maiko alijikuta akiwa na hasira za ajabu ambazo hajawahi kuwa nazo hapo kabla.

Alishajipanga kuwa huko Arusha ama zake au Mashaka na alitaka kujua kwanini Mashaka alitoa oda ya kumuua mzee huyo.


Hadi kesho yake Patrick hakuonekana nyumbani, hofu ikamtanda sana Deborah na kukosa raha kuwa ni kweli Patrick amefatana na Maiko.

Mara Adamu nae akamfata Deborah kumuuliza.

ADAMU: Niambie Deborah, hivi yule mtoto mkubwa vile umezaa na nani? Au ulitoka na mimba kwangu, niambie ukweli bhana.

DEBORAH: Hayakuhusu.

ADAMU: Yani hata kama ulitoka na mimba kwangu hayanihusu?

DEBORAH: Nadhani umeanza kupagawa wewe, kwako nilitoka na mimba? Halafu nikaenda nayo wapi? Hebu nitolee balaa mie.

Deborah alikuwa na mawazo ya kutafakari alipo Patrick tu.


Kule porini baada ya Patrick kupambana sana na Tulo bila ya Tulo kufanikiwa, Patrick akaanza sasa kumpitishia kichapo Tulo hadi Tulo akazimia halafu Patrick akatafuta sehemu kulekule porini na kulala.

Wakati amelala akatokewa na mzimu wa mzee Ayubu.


Wakati amelala akatokewa na mzimu wa mzee Ayubu.

Patrick akaanza kutetemeka kwa hofu kwani ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa. Ule mzimu ukamwambia,

"Usiogope Patrick, sijaja kulipa kisasi na siwezi kulipa kisasi juu yako"

Patrick alikuwa bado na hofu, akatamani kuongea ila akashindwa na ule mzimu ukaendelea kusema,

"Kuna mengi unayotakiwa kufahamu Patrick, rudi kwenu na usipendelee kulala porini"

Halafu ule mzimu ukatoweka, Patrick akashtuka pale alipokuwa amelala na kujikuta akikimbia sana, alikimbilia mahali hata asipofahamu.


Maiko alifika Arusha akiwa na lengo moja tu kukutana na Mashaka.

Alipofika nyumbani kwake, aliingia moja kwa moja ndani, alienda kuangalia lile friji analohifadhia vitu vyake na kujikuta akiingiwa na huruma na kujiuliza kwanini alikuwa vile alivyokuwa.

Alienda chumba kingine na kujiandaa namna ya kukabiliana na Mashaka, alikuwa na hasira sana juu ya Mashaka.


Patrick alijikuta akikimbilia sehemu ya mbali sana, kulipokucha alijishangaa pale alipokuwa, akarudisha akili yake vizuri kwanza.

"Hivi naota au ni nini? Iweje mtu aliyekufa akanitokea na kuongea nami? Mbona mambo haya ya ajabu jamani. Ni vitu gani ninavyotakiwa kufahamu au ni kuhusu baba yangu? Mbona sielewi sasa?"

Akajikuta akijiuliza maswali mengi bila ya majibu na alikuwa ameshajichokea kwa kukimbia sana.


Deborah aliendelea kuwa na mawazo ila hayakumsaidia chochote. Kwanza alimuwaza Patrick, pia akamuwaza Maiko kwani mahusiano ya Maiko na Patrick tayari yalishamchanganya.

Kitu kingine ni vipi Maiko aliweza kuwachanganya wanawake wote wale na kuwatesa vilivyo.

Ikabidi amfate Fausta na kwenda kumuuliza, Fausta akawaambia kuwa angependa kuwaelezea wote ili wajue kwanini anamchukia Maiko na hawezi kumsamehe kamwe katika maisha yake.

Adamu nae akawa makini kumsikiliza kwani hata yeye alihitaji kujua ukweli wa kwanini Maiko anachukiwa vile.

Fausta aliamua kuelezea kwanza jinsi alivyo kutana na Maiko na vitendo ambavyo Maiko alimfanyia.


"Nilikutana na Maiko nikiwa bado msichana na si mmama kama hivi.

Maiko alikuwa na pesa sana na kuniambia kuwa ananipenda, sikujua kama pesa yake ilitumika kumnunua mwanamke yeyote amtakaye. Alinilaghai kwa pesa yake na kujikuta nikiwa kama mtumwa wake wa mapenzi sababu ya pesa, kipindi hicho niliishi nae Morogoro kwani alinipangia nyumba kubwa sana ya kuishi. Pamela hakuwahi kumjua Maiko kwani Maiko hakuwa mkaaji sana wa pale, alikuwa akija leo basi ataondoka kesho.

Nikapata ujauzito, nilipomwambia akanishauri nitoe na kusema kuwa nikishatoa vile vipande nimwambie daktari aniwekee sehemu nzuri ili nije kumkabidhi yeye, nilijua ananitania. Hatahivyo nilikataa kutoa ile mimba kwani sikutaka kufanya kitendo kama nilichofanya na mdogo wangu Pamela hapo kabla. Sikutaka ile kitu ijurudie tena katika maisha yetu kwani tulishatenda dhambi tayari ya kukitoa kiumbe kisicho na hatia.

Siku hiyo nikiwa sijui hili wala lile, alikuja Maiko na mtu mwingine pale nilipokuwa naishi, machale yakanicheza, nikatoka nje kwa muda na kutokomea moja kwa moja, nilienda kuishi kwa baba mzee Ayubu kwa muda kwani mimba yangu ilishakuwa kubwa, kumbe kitendo kile kilimchukiza sana Maiko.

Siku niliporudi kwenye ile nyumba nilikuwa tayari nimeshajifungua watoto wawili mapacha Tina na Thomas. Nikajua kuwa labda Maiko alichukia mimba ila atafurahia watoto.

Nilipofika pale nilikuta barua nyingi sana alizoacha Maiko, tena aliacha na pesa nyingi tu mule ndani huku akisema kuwa alichukizwa na kitendo cha mimi kutoroka ila yupo tayari kunisamehe.

Nilipoona vile nikaamua kumtumia ujumbe kuwa nisharudi na tayari nimejifungua ila sikumwambia kama nimejifungua mapacha kwa lengo la kumfanyia surplise.

Siku hiyo ambayo siwezi kuisahau, alikuja mdogo wangu Pamela pale nilipokuwa naishi ambapo na yeye alikuwa na mimba ila changa, aliniomba aondoke kidogo na mtoto mmoja akakae nae kwake japo siku mbili akamchangamshe, sikumkatalia kwani nae aliishi Morogoro kwa kipindi hicho na alimchukua Tina kwani Tina alikuwa mwepesi wa kukubali kushinda Thomas ambaye alikuwa akilia kila alipochukuliwa kwangu.

Pamela alipoondoka tu, huku nyuma alikuja Maiko bila hata ya taarifa yoyote ile.

Alinikuta nikimvalisha Thomas ambaye nilitoka kumuogesha, kufika pale nilifurahi sana na kumkaribisha.

Alipokuwa ndani alimnyanyua mtoto na kumbeba, sikumkatalia kwavile alikuwa mwanae ila sikujua kama Maiko ni mtu katili kiasi kile alichofanya, aliniambia kuwa amekuja kumchukua mwanae, mimi nikashtuka sana na kumkatalia kwa kumwambia kuwa mtoto bado mdogo angoje akue kwanza.

Akaniangalia kwa dharau kisha akasema,

"Huyu mtoto umemkatalia tumboni hadi ametoka bado wamkatalia!!"

Sikumuelewa kuwa alikuwa na maana gani kusema vile, alikuwa na begi mgongoni akafungua na kutoa pesa nyingi kisha akaziweka mezani na kuniambia kuwa nimuachie mtoto aende nae ila nikagoma kwani pesa si mtoto, nikashangaa gafla akimuweka yule mtoto chini na kutoa kamba kwenye begi lake kisha kunifunga mikono na miguu huku akiniziba mdomo kwa zile solotepu kubwa ili nisiweze sema chochote, mwanangu Thomasi alikuwa akilia sana, Maiko alitoa kisu kwenye begi lake na kumchinja yule mtoto mbele ya macho yangu bila hata huruma kwakweli sikuamini kabisa, nilijihisi kama niko ndotoni.

Maiko ni mume gaidi, ana roho mbaya iliyopitiliza sijawahi kuifikilia maishani mwangu roho ya namna ile. Maiko ni shetani tena yule shetani mwenye mapembe saba.

Akaona ile kumchinja haitoshi, akamkatakata vipande na kuweka kwenye mfuko na kutumbukiza kwenye begi lake kisha akaniambia

"Hii ndio dawa ya kiburi chako, siku nyingine ukiambiwa kitu na mtu mwenye pesa kama mimi tekeleza"

akaondoka na kunifungia mlango kwa nje, nyumba yote ilinuka damu ya mwanangu.

Kwakweli siwezi kusahau, nililia sana hadi kupoteza fahamu, hata niliposhtuka bado sikuamini, sikuweza kwenda popote kwani alinifunga pale chini.

Nashukuru Mungu, kesho yake alikuja Pamela nyumbani pale ambapo nae alikuwa na funguo za ziada za mule ndani, hakuamini kuniona pale chini huku damu nyingi zikiwa zimeganda pale ndani.

Nilimsimulia kilichonikuta na tulilia sana na mdogo wangu, tulienda kutoa taarifa polisi ila haikusaidia chochote kwani Maiko ni mtu ambaye sikumfahamu ndugu, jamaa wala rafiki yake hata mmoja. Tuliamua kuamua kuondoka kabisa eneo lile na kuihama Morogoro, tangia hapo ilikuwa nikienda Morogoro basi naenda kwa mzee Ayubu tu.

Niliona Tanzania ya uchungu na ndio kipindi hicho nikasafiri na kukaa muda mrefu bila ya kurudi, mwanangu Tina alilelewa na Pamela mdogo wangu"


Habari ile iliwasikitisha sana, Deborah nae alijikuta akilia kwa uchungu na kukumbuka mambo ambayo na yeye yalimtokea hapo nyuma akiwa kwa Adamu na akiwa kwa Maiko pia.

DEBORAH: Maiko sio mtu jamani, Maiko ni shetani. Mama umeyasikia hayo?

Bi.Rehema alikuwa akilia tu bila kuamini kama mwanae wa kumzaa mwenyewe anaweza kufanya kitendo kama kile alichosimuliwa.

Adamu akajikuta akimchukia Maiko sasa kwa kitendo alichomfanyia Fausta na vile alivyoambiwa na Tusa kuwa alimbaka.

ADAMU: Mama, nadhani mwanao Juma sio huo Maiko. Nadhani tuendelee tu kumtafuta huyo pacha wangu, siwezi kuwa na ndugu mwenye roho mbaya kiasi hiki.

PAMELA: Kumbuka na matendo yako pia Adamu, nadhani wewe na yeye mmetofautiana ila kumbuka ulichonifanyia kipindi kile Adamu kama kilikuwa sahihi.

DEBORAH: Hii familia ina makubwa sana, na huyu Maiko ni mtu mbaya sana kwenye ukoo wenu.

Kila mmoja aliwaza chake juu ya Maiko kwani hakufikiriwa kuwa kama binadamu wa kawaida.


Patrick akiwa eneo asilolitambua, anaamua kuuliza watu alipo ili aweze kurudi kwao.

Anamuona kijana mmoja akiwa amesimama kamgeuzia mgongo, akaenda kumshtua ili amuulize. Yule kijana kugeuka alikuwa ni Mporipori, wakajikuta wakitazamana na Patrick.

Mporipori hakuweza kumtazama zaidi Patrick ila alianza kumkimbia ili kumkimbia Patrick kwa kuhofia kipigo, Patrick aliamua kumkimbilia Mporipori kwa nyuma kwani aliona kuwa yeye ndiye mtu pekee atakayemsaidia ukizingatia pale alipokuwa karibia watu wote waliongea kilugha na hawakujua kiswahili.


Maiko akiwa Arusha, aliwaulizia vibaraka wake alipo Mashaka. Akaelekezwa mahali ambapo Mashaka yupo. Maiko alikuwa na hasira na Mashaka kwa kumsababishia amuue baba yake mwenyewe, huku Mashaka akiwa na hasira ya kusalitiwa na Maiko.

Wakati Maiko akimfata Mashaka, kumbe Mashaka nae alikuwa akimngoja kwa hamu mahali hapo.


Wakati Maiko akimfata Mashaka, kumbe Mashaka nae alikuwa akimngoja kwa hamu mahali hapo.

Maiko alipomuona Mashaka akamuangalia kwa jicho kali sana na kumuuliza.

MAIKO: Kwanini ulitoa oda ya kumuua mzee Ayubu?

MASHAKA: Ushajua kuwa Ayubu ni baba yako eeh!! Hata hivyo umemuua mwenyewe sababu mi nilitoa oda tu.

MAIKO: Shida yangu ni kujua, kwanini basi.

MASHAKA: Kwasababu nilikuwa simpendi, namchukia sana Ayubu.

MAIKO: Kwanini ulikuwa unamchukia?

MASHAKA: Kipindi yupo kwenye mahusiano na dadangu nilimkataza sana ila hakusikia hadi akampa mimba ndio wazazi wakaingilia kati halafu mi na yeye tushawahi kugombaniana mwanamke. Ila usisikitike sana, yule kaenda na sie tumebaki.

MAIKO: Hivi wewe Mashaka unajua umenipandikiza roho ya ajabu sana! Nimeua watu wengi kwaajili yako ila sasa sioni faida, nimeharibu familia yangu na kila kitu.

MASHAKA: Kuhusu familia hata mimi sina familia, nilikutegemea sana Maiko ila sikutegemea kama ungenisaliti.

Maiko alimuangalia sana Mashaka, alitamani amrarue ila aliona njia nzuri ni kumvizia kwani hapo Mashaka nae alikuwa na yake kwa Maiko.


Deborah na wengine wote wakawa wanasikitikia habari ya Fausta kwakweli iliwatisha na kuwasisimua sana, Deborah akafikiria mengi aliyotendewa na Maiko na kuona wote wana haki ya kumchukia Maiko.

Ikabidi wapange kikao cha familia kwajili ya kujadili kuhusu Maiko, ikabidi Deborah ampigie simu dada yake bi.Marium kuwa naye awepo kwenye kikao hicho ili aeleze alichotendewa na Patrick hadi kumchukia kiasi kile ambacho anamchukia.


Patrick aliendelea kumkimbilia Mporipori huku Mporipori nae akizidi kukimbia.

PATRICK: Tafadhari Mporipori simama, sina ubaya wowote na wewe.

Mporipori alikuwa na uoga sana juu ya Patrick, ikabidi asimame eneo lenye watu ili kama Patrick atahitaji kumdhuru basi wale watu waweze kumsaidia.

Patrick alimsogelea Mporipori na kumsalimia ila Mporipori alisita kuitikia.

PATRICK: Nisaidie ndugu yangu nimepotea.

MPORIPORI: Wewe unaomba msaada kwangu!!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

PATRICK: Ndio Mporipori naomba unisaidie.

MPORIPORI: Ningekufa je kule porini angekusaidia nani?

PATRICK: Ndiomana hukufa Mporipori ili uweze kunisaidia.

Mporipori alimuangalia sana Patrick na kuamua kumuelekeza, ila akamueleza njia isiyo sahihi ili kumpoteza tu.


Walikaa kwenye kikao na kuanza kujadili matendo ya Maiko ambayo amewafanyia.

Rehema alikuwa makini kusikiliza huku moyo ukimuuma sana kama mzazi.

Anna aliamua kuelezea na yeye hadi kuzaa na Maiko.

"Kuna kipindi nilienda kuishi kwa baba yetu mdogo aliyekuwa akiishi Arusha, huko ndipo nilipokutana na Maiko alinipa kila nilichohitaji, kwakweli nikajikuta nikimpenda sana.

Nikapata ujauzito, Maiko alipojua akanichukua na kunipeleka kwa daktari ambapo nilitolewa ile mimba kinguvu. Tokea hapo sikutaka tena kuendelea na Maiko ila akanitishia kuwa nikiachana nae ataniua eti kisa nimeshakula vitu vyake vingi.

Nikapata mimba nyingine, sikutaka kumwambia nikawa kimya kabisa.

Sikuweza kuendelea kuishi pale kwa bamdogo na ile mimba na huku Mwanza niliogopa kurudi na mimba wala mtoto.

Sikuwa na mahali pa kwenda, kama ilivyo kawaida mimba haina siri, tumbo likakua na kufanya Maiko agundue kuwa mimi ni mjamzito, akanilazimisha niende nae kule tulipotoa ya Mwanzo nikagoma akanipiga sana na kusema atanitoa tena kwa nguvu, bahati nzuri nilipata upenyo na kutoroka.

Niliomba msaada kwa watu wa usafiri hadi nikajikuta naingia Tanga.

Niliteseka sana na ile mimba hadi nilijikuta nikijifungulia njiani ila walipita watu wema na kunisaidia kunipeleka hospitali.

Nilipotoka hospitali sikuwa na pa kwenda,

kulikuwa na watu flani waliojitolea kulea watoto wasio na baba, nikaamua kumpeleka huko mwanangu na kumuacha akiwa na miaka miwili, mimi nikarudi Mwanza, sikusema ukweli kwani nilimjua shangazi lazima angechukizwa na kitendo cha mimi kuzaa bila ndoa.

Mara ya pili kumuona mwanangu alikuwa na miaka kumi na tano, nilifurahi na kushukuru kwa kulelewa mtoto, hawakuwa watoto wengi walioamua kuwalea pale ila nashukuru katika hao wachache na mwanangu alikuwa mmoja wao.

Ni siku hiyo aliponiuliza kuhusu baba yake nami nikampa picha ya Maiko, nikamwambia angoje kwanza atakapo pambazuka vizuri akili ndio amtafute.

Nikarudi tena Mwanza na kukutana na Maiko, sikujua alifata nini Mwanza ila alinikamata na kuniteka huko alinipiga sana kwa kusema kuwa ananifundisha adabu kwa kumkatalia mtoto wake, alinidadisi sana alipo ila sikusema.

Nilirudi nikiwa nimetenguka mkono na mguu kwa kipigo chake, ndio toka siku hiyo sijaonana nae tena hadi siku aliyokuja hapa"


Deborah alimuangalia sana Anna bila kummaliza.

DEBORAH: Kumbe uliposema umevamiwa na majambazi huyo jambazi mwenyewe ndio Maiko!!

ANNA: Maiko ni jambazi kweli.

PAMELA: Jamani, ngoja niulize swali. Huyo Maiko yeye hizo mimba changa anaenda kufanyia nini?

DEBORAH: Maiko ni shetani na huo ni ushetani mmoja wapo aliokuwa akipenda kufanya.

FAUSTA: Mi naona huyu Maiko akija tena atujibu, watoto wetu wachanga huwa anawafanya nini. Anakula nyama au anauza?

Rehema alishindwa kuelewa kama mwanae Maiko ni mtu wa kawaida kweli.


Patrick alijikuta njia aliyoenda nayo sio kabisa yani, alijiona kuzidi kupotea.

Kwa bahati akaliona gari la mkaa akalisimamisha na kuomba lifti.

Nia yake ni kufika mahali ambapo atapata uelekeo wa maana wa kurudi nyumbani kwao.

Moyoni alikuwa akijilaumu sana kwani mbio za kuukimbia mzimu ndio zilizomponza.


Maiko akamnyemelea Mashaka akiwa na lengo moja tu la kummaliza, ila wakati anamnyemelea Mashaka alishtuka na kugundua kitu.

Hapo hapo akaanza kupambana.

Mashaka na Maiko walikuwa katika mpambano wa hali ya juu yani kufa na kupona.


Yuda nae aliamua kumsimulia Sele kuhusu kichwa cha baba yao.

SELE: Dah! Yule Maiko anastahili kufa kwakweli. Simpendi hakuna mfano, yani kumkata baba yetu kichwa dah!!

YUDA: Ndo hivyo, ila dawa ya moto ni moto. Yule nae tumkate kichwa tena kichwa chake tukiache kiliwe na kunguru.

Wakaamua kwenda kwa mama yao mdogo ili kuangalia kama Maiko kaja tena na safari hii wakajipanga kwa ajili ya kupambana nae.

YUDA: Hakuna kumuachia akimbie.

SELE: Nina hasira nae sana yule jamaa.


Baada ya Anna kuelezea yake, Tusa nae akaamua kufunguka mambo aliyofanyiwa na Patrick na Maiko alivyokuwa Arusha.

Wakati Tusa anasimulia kila mtu alipigwa na butwaa na kushangaa kuwa hata Patrick waliyemuamini nae kumbe hafai.

Muda huo Patrick nae alikuwa amefika nyumbani kwao, kusogelea mlango akawa anamsikia Tusa akisimulia.

INAENDELEA.....

Post a Comment

0 Comments