Deborah na Fausta ikabidi wazungumze na Patrick kujua ni gharama gani ambazo anazisema kuwa kamgharamia Tusa.
PATRICK: Mama, mahali tu nilitoa shilingi milioni kumi na tano.
FAUSTA: Milioni kumi na tano!! Walikuwa wanamuuza au?
DEBORAH: Mbona pesa ni nyingi sana?
FAUSTA: Ndiomana mdogo wangu Pamela hana usemi, pesa ni nyingi mno watairudishaje pesa yote hiyo? Tunapaswa kuzungumza juu ya hili jamani.
DEBORAH: Jamani Pamela anapenda pesa sana, yani mahali milioni kumi na tano? Mahali gani hiyo? Ndiomana pesa yako inakuuma mwanangu Patrick.
Ikabidi Deborah na Fausta waingie ndani kwa mazungumzo zaidi.
Patrick alizunguka nyuma ya nyumba yao, alipopiga jicho mbele akamuona Maiko.
"Amefata nini tena huyu firauni hapa?"
Maiko hakuja kwa shari bali alienda kwa utaratibu kabisa ili kuzungumza na Patrick ila Patrick alikuwa na chuki na hasira za wazi dhidi ya Maiko haswa kitendo cha Maiko kumchinja baba yao na wakina Yuda ambaye Patrick alimuona kama baba yake pia.
Patrick alizidi kupandwa na hasira kadri Maiko alivyosogea.
Patrick alizidi kupandwa na hasira kadri Maiko alivyosogea.
Maiko nae aliendelea kumsogelea Patrick ila akaona mabadiliko ya Patrick usoni ikabidi aongee kabla hajamsogelea zaidi.
MAIKO: Tafadhari Patrick, sijaja kwa shari leo. Nina shida na mazungumzo na wewe Patrick. Nisogee hapo?
Patrick alimuangalia tu bila ya kumjibu chochote ila alitikisa kichwa kama ishara ya kukubali. Maiko nae akamsogelea zaidi ili apate kuzungumza nae.
MAIKO: Tafadhari Patrick naomba tumalize tofauti zetu.
PATRICK: Unajua wazi tofauti zetu haziwezi kuisha labda useme lingine.
MAIKO: Nataka tushirikiane kumuangamiza Mashaka.
Patrick akacheka sana, kisha akaondoka pale na kwenda mbele na kuingia ndani, Maiko akajikuta akibaki mwenyewe na kujiuliza kwanini Patrick amemcheka.
Maiko akiwa pale nje anamuona Mwita na Tulo wakifika pale.
Maiko akamshangaa Tulo kwa kumuona pale.
MAIKO: Kwani mnajuana?
MWITA: Tumejuana hapahapa, nadhani hii ni sehemu ya makutano.
MAIKO: Nadhani Tulo hapa umemfata rafiki yako Patrick, nafikiri pia itakuwa vyema kama utanisaidia kuzungumza nae.
TULO: Kuzungumza na nani, Patrick?? Hapana, namuogopa sana.
Ikabidi Maiko amuulize alichofanywa na Patrick.
MAIKO: Kwani amekufanyeje?
TULO: Nitakueleza tu usijari.
MWITA: Na mbona uliondoka bila ya kuniaga?
MAIKO: Dah!! Kuna kitu kilinichanganya bhana. Ila usijari.
Tulo alikuwa anamuelewa Maiko na anajua kuwa Maiko si mtu wa kuaga huwa anajiondokea tu.
Mwita akaingia ndani na Tulo akabakia pale nje na kumueleza kilichompata.
MAIKO: Dah! Na wewe zoba kweli, yani ulikubali kutumwa na Mashaka kwa Patrick!! Yeye mwenyewe kamshindwa.
TULO: Ndomana sijarudi Arusha hadi leo.
MAIKO: Hakuna tatizo, fanya kuwa karibu na Patrick huwezi jua, anaweza kukubali kuwa na sisi tena.
Wakaongea mawili matatu na Tulo kumfata Mwita ndani.
Fausta alimfata Adamu kwa lengo kumuuliza.
FAUSTA: Hivi kaka, unamuozesha mtoto kwa milioni kumi na tano kweli? Ulikuwa unamuuza au ni vipi?
ADAMU: Muulize mdogo wako maana posa hiyo aliipanga yeye.
FAUSTA: Na je mkafanyia nini?
ADAMU: Vitu vingi tu vya biashara ila nyingine tulikula.
FAUSTA: Ndio kipindi kile nini ambacho mlikuwa mkitanua? Kumbe mnatanulia pesa ya posa. Mtaweza kuilipa sasa maana mwananu kagoma kuishi na huyo mwanaume.
ADAMU: Tutailipa tu ila hasara yake itakuwa kubwa sana.
Pamela akawafata na kumuuliza mumewe.
PAMELA: Baba Tusa, tutailipaje hiyo pesa? Mi nadhani swala la muhimu ni kumuomba Tusa akubali tu kuishi na Patrick.
Pamela alikuwa hajielewi kabisa kwani hata alishindwa kuwaza namna ya kuipata hiyo pesa na kuirudisha.
Patrick alienda moja kwa moja kuzungumza na Tusa.
PATRICK: Hivi Tusa unajua kuwa unaipa familia yako umaskini kwa kuachana na mimi!!
TUSA: Umaskini kivipi sasa?
PATRICK: Wazazi wako unadhani watapata wapi pesa za kunilipa! Nimekutolea mahari kubwa sana Tusa. Ingekuwa laki tisa kushuka chini ningesamehe ila milioni kumi na tano!! Siwezi kuisamehe, hapa ni mimi kuendelea na wewe au wazazi wako kuilipa hiyo pesa.
TUSA: Bora wakulipe tu, sitaweza kuendelea kuishi na wewe. Mume gani nisiyetambua hata kazi yako? Bora tu tuachane.
PATRICK: Na utakula mapumba na huyo Sele wako asiyejielewa.
TUSA: Hata tusipokula poa tu.
Patrick alifanya kama vile kumtania Tusa huku akimpa maneno ya ukweli.
Marium aliamua kuondoka na familia yake ili waende kuzungumza vizuri.
SELE: Ila mama mi nitarudi tu badae.
YUDA: Hata mimi nitarudi.
Kwahiyo Mwita na Tulo hawakuwakuta watu hawa, Maiko hakutaka hata kuingia ndani aliendelea kubaki pale pale nje akitafakari mambo yake.
Mwita alitulia pale ndani akimngoja Patrick aliyekuwa chumbani ili apate kuzungumza nae.
Tulo nae alipomuona Tina amekaa mwenyewe akaona ni vyema kuzungumza nae.
Wakaongea mengi na stori za hapa na pale.
TINA: Kwani Tulo umekuja lini Mwanza?
TULO: Mbona kama wiki mbili zilizopita.
TINA: Na unalala wapi siku zote hizo?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TULO: Hotelini bhana.
TINA: Una hela za kuchezea eeh!!
TULO: Waswahili husema, tumia pesa ikuzoee. Pesa ninayo na raha ya pesa ni matumizi. Lini mtarudi Dar?
TINA: Hata sijui, vipi maisha lakini?
TULO: Yameninyookea kiasi, nina nyumba yangu. Gari mbili moja yangu na nyingine nitampa mwanamke nimpendaye.
TINA: Hongera sana, nani atapata hiyo bahati ya kukabidhiwa gari ya pili?
TULO: Unataka kumjua Tina? Tena si gari tu bali nitampa vitu vingi, kila akitakacho kwangu atapata.
TINA: Hebu nitajia huyo mwanamke ni nani na umempendea nini na kwanini umemchagua yeye na si mwinginewe.
TULO: Nampenda binti mmoja mzuri sana na anavutia, inaonyesha alipatwa na mikasa kidogo ila bado anavutia. Moyo wangu upo kwake na nitampa kila kizuri mbele yangu. Sitapenda alie, nitapenda kuona akitabasamu muda wote. Huyu binti nampenda sana.
TINA: Nitajie basi Tulo.
Tulo akaona kuwa asipoteze muda, akaanza kumueleza ukweli Tina juu ya hisia zake.
Tina akabaki kushangaa kuwa mwanamke mwenyewe ni yeye.
Maiko hakukata tamaa aliendelea kukaa pale pale nyuma akiingoja kauli ya Patrick kwani alijua wazi kuwa Patrick anamfanyia makusudi.
Maiko alijikuta akisinzia, ila alishtuliwa na ndoo ya maji aliyomwagiwa, kuangalia ni Deborah ndiye aliyeshika ndoo hiyo.
DEBORAH: Ondoka sasa hivi nyumbani kwangu sitaki kukuona shetani wewe.
MAIKO: Unanionea bure tu Deborah.
DEBORAH: Nani akuhurumie muuaji kama wewe, sitaki hata kukuona mbele ya macho yangu. Kama hao ndugu zako kutana nao hukooo ila sio hapa kwangu.
Ikambidi Maiko ajiongoze na kuondoka.
Mwita alikuwa akitafakari mambo mengi, haswaa mahali ambako wakina Patrick wanapatia pesa kwani hakuwaona hata mara moja wakienda kazini, huyo Maiko ndio kabisa hakueleweka ila alikuwa na pesa nyingi sana na hakuona shida kukodi gari kila anapokwenda. Kauli ya Tulo ikawa inatembea kichwani mwake kuwa je anajua kazi anayofanya baba yake, akajiuliza kuwa kazi hiyo inaendana vipi na usalama wake wa Taifa, kwakweli Mwita alikuwa na maswali mengi sana.
Patrick alipotoka ndani akaamua kutoka nae nje na kuzungumza nae.
MWITA: Unajua kuwa wale wanajeshi wenzangu wote waliotumika kumkamata Sele na tusa wameuwawa?
PATRICK: Kumbe wameuwawa, pole sana.
Mwita akashindwa kuelewa kwanini Patrick hana hata mshtuko.
MWITA: Hivi Patrick unafanya kazi gani?
PATRICK: Kamuulize baba yako kwanza ndipo uje kuniuliza na mimi.
Mwita alihisi kuwa lazima kuna kitu kinaendelea.
Patrick alionyesha chuki ya wazi kwa Mwita kwani huwa hapendi kuchunguzwa.
Marium alizungumza na watoto wake,
MARIUM: Hivi nyie wanangu mmerogwa jamani?
SELE: Kwanini mama?
MARIUM: Yani wote mnataka kuwa na familia ile iliyolaanika! Familia ambayo baba anambaka mwanae na kumpa mimba?
YUDA: Hatukuelewi mama?
MARIUM: Yuda mwanangu, yule Tina wa nini wewe? Hakufai yule mwanangu. Na wewe Sele, achana na Tusa si mwanamke wa kuishi nae yule.
SELE: Mama, nitakusikiliza vyote ila Tusa simuachi ng'ooo. Ananipenda ninampenda, najua ipo siku Mungu atatuweka pamoja. Haya mengine ni mapito tu.
YUDA: mama, nampenda sana Tina. Siwezi kumuacha mama.
MARIUM: Na mtawaacha tu labda mimi sio mama yenu.
Marium aliinuka kwa hasira na kusahau kuwa hata huyo Tina anayempinga ni mtoto wa rafiki yake kipenzi Fausta.
Mashaka akaamua kwenda tena nyumbani kwa Deborah ili akamuone dada yake bi.Rehema hadi akajishangaa kuwa kwanini amekuwa vile,
"Au ndio nataka kufa? Kwahiyo namuangalia angalia mara ya mwisho maana yeye ndiye ndugu yangu pekee aliyebaki.
Kufika kwa Deborah akamuona Fausta nje, kitu hiki kilimshtua Mashaka kwani hata hakujua kama Fausta anajuana na bi.Rehema.
Mashaka akabaki ameduwaa akimshangaa Fausta.
Mashaka akabaki ameduwaa akimshangaa Fausta.
Fausta hakujua kama kuna mtu anayemuangalia, aliendelea na kazi zake pale nje kama kawaida.
Bi.Rehema nae akatoka ndani na kumfata Fausta pale nje huku akizungumza nae, yote hayo Mashaka alikuwa akiyashuhudia, alitamani kumuita bi.Rehema ila alishindwa kwasababu alijua Fausta angeshtuka.
Ila mara akamuona Fausta akiingia ndani na Rehema akiwa bado pale nje, akaamua kushusha kioo cha gari alilokuwa nalo na kumuita kwani vioo vyake vilikuwa vyeusi.
Bi.Rehema alipoangalia ile sauti ilipotokea akagundua ni kwenye lile gari na akagundua kama ni ya Mashaka, akaamua kumfata.
Alipofika Mashaka akamuomba azunguke ili aingie kwenye gari na kuzungumza nae, bi.Rehema akamwamuru Mashaka asogee ule upande mwingine na yeye akaye kwenye uskani kwani hakumuamini vizuri Mashaka alihisi kuwa huenda akaondoa gari, ila Mashaka akamuomba na kumsihi sana kuwa anahitaji kusogea nae kidogo tu ili wapate kuzungumza.
REHEMA: Na ukikiuka masharti je?
MASHAKA: Nifanye chochote utakachotaka kunifanya.
REHEMA: Mmh!! Naweza kukufanya chochote kweli mimi!!
MASHAKA: Usijari dada, kiukweli najutia makosa yangu ndomana ningependa tuzungumzie hili swala kidogo.
Bi.Rehema akakubali na kupanda kwenye ile gari ya Mashaka ambaye aliiondoa mahari pale.
Fausta alipotoka tena pale nje hakumkuta bi.Rehema, akamuangalia huku na kule bila ya kumuona.
Akamfata Pamela na kumuuliza.
FAUSTA: Hivi huyu mkweo ana matatizo gani?
PAMELA: Kwanini?
FAUSTA: Ni mara ya ngapi hii anaondoka bila ya kuaga jamani?
PAMELA: Inamaana hayupo?
FAUSTA: Ndio hayupo, yani aliniagiza ndani kuzungumza na Deborah kutoka nje nilhpomuacha hayupo tena.
PAMELA: Umejaribu kumuangalia na kule nyuma maana nyumba kubwa hii.
FAUSTA: Nimemuangalia kote hayupo sijui hata ameenda wapi.
Pamela nae akajaribu kuangalia huku na kule bila hata ya kumuona bi.Rehema.
PAMELA: Halafu akirudi hata huwa hasemi alipotoka.
FAUSTA: Labda kapata buzi mzee mwenzie.
Wakaanza kucheka kwa umbea.
Deborah alifikiria maneno aliyoambiwa na kuombwa na Fausta juu ya yeye kuzungumza na Patrick kuhusu Tusa.
Deborah akaamua kumuita tena mwanae ili kuzungumza nae.
DEBORAH: Mwanangu, me nadhani tuwaachie tu mtoto wao waende nae.
PATRICK: Yani mama kirahisi hivyo!!
DEBORAH: Sasa mwanangu unadhani itakuwaje jamani?
PATRICK: Mama, mimi nahitaji kuwakomesha hawa haswaa wazazi wa Tusa ili wazazi wenye tabia kama yao ya kupenda pesa na kufanya mabinti zao kama kitega uchumi waache.
DEBORAH: Ila anaeteseka ni Tusa mwanangu!!
PATRICK: Nataka wanilipe posa yangu, gharama zingine nitahesabu hasara ila wanilipe posa yangu tu. Si waliona fahari kumuozesha mtoto wao kwa milioni kumi na tano!! Sasa nataka wailipe tena sina masikhara kwa hilo, bora hiyo pesa uitumie mama yangu utakavyo ila sio wao. Wazazi wa Tusa hawana akili kabisa, na bora huyo baba yake Tusa si baba yangu maana akili zake fupi kama mchanga.
DEBORAH: Ila mwanangu si watakuwa maskini sasa?
PATRICK: Mama, binti yao si wamemfanya mtaji basi watapata pedeshee lingine litawajengea nyumba ila sidhani kama huyo Sele watamkubali na ukapuku wake.
DEBORAH: Patrick mwanangu umebadilika sana, sinabudi kukwambia ukweli wa maisha yako labda ukawa umefanana na ndugu zako tabia, haswaa baba yako nadhani utakuwa umefanana nae na sasa imeanza kujionyesha.
PATRICK: Inamaana mama wewe humjui baba yangu kabisaaa?
DEBORAH: Hivi karibuni utaujua ukweli tu maana Patrick niliyemnyonyesha ziwa langu na kumlea kwa kukimbizana ndani kwa fujo na utundu wake sidhani kama ni wewe. Kwakweli natamani arudi Patrick wangu yule wa zamani.
Deborah akamuacha Patrick na kutoka nje ya chumba na kwenda sebleni kwani machozi yalikuwa yakimlenga lenga.
Mashaka akaanza kuzungumza na bi.Rehema kuhusu Fausta.
MASHAKA: Fausta ni nani yako dada?
REHEMA: Khee swali gani hilo? Fausta ni mtoto wa baba wa wanangu pia ni dada wa mkwe wangu.
MASHAKA: Nadhani humjui Fausta vile ninavyomjua mimi, unamkumbuka Neema?
REHEMA: Neema yupi?
MASHAKA: Yule mtoto wa bamdogo aliyekuwa pacha wa baba yetu.
REHEMA: Sawasawa nimemkumbuka.
MASHAKA: Basi yule Fausta ana mdogo wake anaitwa Pamela na Neema ndio mama yao mzazi.
REHEMA: Kheee! Kumbe wale watoto ni ndugu zangu kabisa, Mungu wangu. Mbona ukoo wetu umesambaratika sana? Unajua huyo Pamela kaolewa na mwanangu mie!!
MASHAKA: Ndio mambo ya kutokufahamiana hayo, ila si mbaya sababu mtoto wa dada mkubwa na mdogo wameoana.
Halafu akawa anacheka,
REHEMA: Kinachokuchekesha sasa? Hebu nirudishe huko.
MASHAKA: Usipanic bhana dada yangu, nenda ukawaeleweshe ila mimi sikuja kuzungumza nawe kuhusu hilo.
REHEMA: Ulitaka kusema nini? Nirudishe bhana.
Mashaka akaendesha gari na kufika pale kwa Deborah kisha akamgeukia Rehema na kumwambia.
MASHAKA: Dada, usihangaike kumtafuta mchawi au mtu mbaya kwa kifo cha mzee Ayubu.
REHEMA: Unamaana gani?
MASHAKA: Aliyemuua mzee Ayubu si mwingine bali ni mwanao Maiko.
Mashaka akajihisi kupumua kwa kumtwisha Maiko mzigo wa lawama, bi.Rehema akahisi kuchanganyikiwa kwani ilikuwa ngumu kuamini kuwa mwanae angefanya ukatili wa kiasi kile kwa mzee Ayubu.
Bi.Rehema alishuka kwenye lile gari akiwa amenyong'onyea sana.
Tulo na Mwita wakaondoka tena kwana Mwita hakupata majibu mazuri toka kwa Patrick nao wakapanga kurudi tena.
MWITA: Vipi na wewe Tulo mbona unafuraha sana?
TULO: Mtoto anaonyesha kunielewa kabisa maana hata jibu la kunipa alikosa.
MWITA: Sasa umeamua vipi?
TULO: Tunavyoenda mjini hivi nitaenda kumnunulia zawadi nzuri sana, najua Tina ataipenda na atanipa jibu zuri na la uhakika.
MWITA: Na kuaminia bhana.
Tulo alikuwa na furaha kweli kwani aliamini kuwa lazima Tina atamkubalia tu.
Adamu alimfata mkewe Pamela kwani alishachoka kuishi pale Mwanza.
ADAMU: Unajua nimechoka, kwakweli tumekuwa mzigo kwenye mikono ya Deborah bora turudi kwetu tu.
PAMELA: Kwetu ambako una mpango wa kuuza nyumba ili kuweza kulipa posa ya mtoto? Mmh! Sikujua mambo yote haya kabla laiti ningejua nisingepanga mahari kubwa kiasi kile.
ADAMU: Majuto ni mjukuu mke wangu, hatuna la kufanya inabidi tu tukubaliane na halihalisi. Ninge ni kauli ya majuto na huja baada ya maji kumwagika.
PAMELA: Natamani kama vile siku zirudishwe nyuma, kwakweli hali ni mbaya.
Wakamuona bi.Rehema akirudi huku akiwa amenywea sana.
ADAMU: Nini tatizo mama?
REHEMA: Bora tukio hili angelifanya mtu yeyote duniani ila si mwanangu Juma. Kwanini lakini? Kwanini imekuwa hivi?
Wote wakamshangaa na kumuangalia tu.
Mashaka alijiona kafanikiwa kiasi fulani kwani alikuwa kashamvurugia Maiko kuwa tena karibu na bi.Rehema na alijua wazi kuwa lazima Maiko agome kubeba mzigo na atamtupia Patrick.
"Na hapo ndio patamu, maana Patrick anajifanya mwema sana. Ngoja tu na wao waumbuke na waogopwe na kujificha kama ambavyo mimi ninafanya"
Akaishia kwa kicheko cha kujipongeza.
Ilibidi Tina amueleze Tusa kuhusu Tulo kuwa anampenda.
TINA: Anaonyesha kunipenda kweli halafu anapesa tofauti na Yuda.
TUSA: Sikushauri kuwa nae, sidhani kama huyo Tulo atakuwa tofauti na Patrick. Wanaume wote ni sawa Tina.
TINA: Hapana bhana si sawa, Tulo kashajipanga kimaisha ana nyumba na magari. Nikiwa nae nitaishi maisha ya kifahari, sijawahi kufikiria kuwa na gari ila Tulo kasema atanipa. Unajua nikiwa nae nitaanza na mia tofauti na Yuda itabidi nianze nae na moja.
TUSA: Ngoja nikuulize Tina, unachoangalia wewe ni pesa ya mtu au upendo wa mtu kwako? Angalia Mapenzi Tina, pesa kitu gani bhana. Mi mwenzio nateseka hapa sababu ya pesa.
TINA: Jamani sasa nifanyeje?
TUSA: Akili kichwani mwako, wewe ni mtu mzima sasa na ushapitia mengi. Usifikirie nakuonea wivu la hasha, nakuhurumia Tina.
Tina akatulia akitafakari kauli ya Tusa kuwa aangalie mapenzi au pesa.
Maiko aliendelea kuhitaji kuzungumza na Patrick ingawa alimwagiwa maji na Deborah ila hakuacha kwenda kuchungulia nyumbani kwa Deborah maana alitambua wazi lazima kuna muda atakaosikiliza tu.
Akaamua kwenda tena nyumbani kwa Deborah.
Bi.Rehema alizunguka nyuma ya nyumba akitafakari aliyoambiwa, alikaa na kujiinamia.
Akatokea mtu na kumshika bega, kumtazama alikuwa ni Maiko.
Akashikwa bega, alipogeuka kumtazama alikuwa ni Maiko.
Bi.Rehema akamuangalia kwa macho makali sana kisha akainama na kulia, ikabidi Maiko nae achuchumae chini kumuuliza.
MAIKO: Nini tatizo mama?
REHEMA: Siamini kama kweli nimezaa mtoto muuaji, siku zote nimekuwa nikimbia kuhusu mauaji uyafanyayo kumbe ni kweli dah!!
Maiko akaona kuwa sasa ishakuwa soo, akaamua kuuliza kwa kujigeresha.
MAIKO: Kwani nini tena?
REHEMA: Unauliza hujui? Hujui mauaji uyafanyayo? Yani wewe ni wa kumuua babako mwenyewe! Hata kama humfahamu hukustahili kumuua.
MAIKO: Unamuongelea mzee Ayubu?
REHEMA: Unauliza majibu? Kwanini umemuua mzee Ayubu? Mzee wa watu tena asiye na hatia amekukosea nini hadi umuue?
MAIKO: Unanilaumu bure mama, sijamuua mimi bhana.
REHEMA: Sasa nani kamuua?
MAIKO: Ni Mashaka ndiye aliyetutuma na aliyeenda kumuua ni Patrick.
REHEMA: Patrick!! Patrick yupi?
Kabla hajajibu akatokea Deborah kule nyuma,
DEBORAH: Yani wewe shetani Maiko umekuja tena nyumbani kwangu? Haya ondoka upesi kabla sijafanya kitu kibaya.
Maiko akawa anasuasua tu huku bi.Rehema akimtetea.
REHEMA: Jamani Deborah, hajaja kwa ubaya huyu.
DEBORAH: Wewe si ushakuwa kiziwi husikii unapoambiwa ondoka, sasa endelea kukaa hapo hapo.
Deborah akaingia ndani, Maiko na bi.Rehema hawakujua Deborah alikuwa na maana gani.
Deborah alipotoka alitoka na jagi lenye maji mkononi na kwenda kummwagia Maiko mgongoni, maji yale yalikuwa ya moto sana na kumfanya Maiko aruke ruke na kuanza kukimbia.
DEBORAH: Hiyo trailer, njoo tena uone picha yake mwehu wewe.
Halafu akaingia ndani.
Deborah alipoingia ndani alimkuta Patrick yupo sebleni akijiandaa kutoka.
DEBORAH: Shetani alikuja tena mwanangu. Nadhani anafata ndugu zake hao.
PATRICK: Nani tena huyo??
DEBORAH: Maiko huyo, kaja hapa tumbo mbele mbele nimemmwagia maji ya moto akome. Mwanangu bora hapa tuhame tu, hili shetani litaendelea kusumbua kila siku.
PATRICK: Sawa mama nimekuelewa.
DEBORAH: Waachie tu binti yao warudi nae kwao tupumzike, kwakweli nimechoka.
PATRICK: Sawa mama ila lazima niwakomeshe, lazima walipe mahari yangu na iwe fundisho kufanya binti zao kama kitega uchumi.
DEBORAH: Ila mwanangu nimeshachoka mamako.
PATRICK: Usijari mama, yote yataisha tu.
Patrick akamuaga mama yake na kuondoka.
Bi.Rehema alikuwa akiwaza kuhusu Patrick kuwa je ni Patrick anayemjua au ni yupi.
Adamu akamkuta mama yake pale pale alipokaa.
ADAMU: Mbona umnyonge sana mama?
REHEMA: Muda sio mrefu Maiko alikuwa mahali hapa ila alichofanywa na Deborah mmh!! Ni khatari sana.
ADAMU: Kafanywaje tena?
REHEMA: Yani Deborah kammwagia maji ya moto Maiko mgongoni, dah huwezi amini kwakweli. Kumbe Deborah ana roho mbaya kiasi hiki!
ADAMU: Ulikuwa humjui Deborah ndomana ukawa unamtetea, Deborah amewahi kumkata mtu miguu kwa upanga. Achana na Deborah kabisa.
Rehema akasikitika na kuanza kumwambia alichoelezwa na Mashaka kuhusu kifo cha mzee Ayubu na jinsi alivyoambiwa na Maiko.
ADAMU: Sasa ni Patrick yupi?
REHEMA: Hata mi mwenyewe simjui.
Wakaamua kutafuta mawasiliano ya Maiko ili waende wakapate ukweli.
Tusa aliamua kumuuliza tena Tina juu ya alipofikia na maamuzi yake.
TUSA: Kwahiyo Tina umeamuaje?
TINA: Hata sielewi.
TUSA: Unampenda nani kati yao?
TINA: Nawapenda wote.
TUSA: Acha uongo Tina, utawapenda vipi wote. Inaonyesha mmoja wapo unampendea pesa wewe. Tulo umempendea pesa zake.
TINA: Naangalia future bhana, sasa Yuda pale alipo mmh! Nitafika nae wapi?
TUSA: Yuda ni mwanaume anayependa kujishughulisha halafu ana mapenzi ya dhati. Sidhani kama Tulo ni mwanaume sahii kwako. Nakushauri uwe na Yuda, fanya maamuzi sahihi sasa usije kujutia badae.
Tamaa ya pesa ilimtawala Tina na kusahau kuwa amewahi kubakwa kwa tamaa.
Anna aliwakaribisha Tulo na Mwita nyumbani kwake, akakaa nao na kufanya maongezi nao.
Akamuona Tulo amebeba zawadi alipomuuliza akagundua kuwa anaipeleka kwa Tina na akagundua kuwa kuna kitu kinaendelea.
Baada ya maongezi ya hapa na pale wakaaga na kuondoka, muda kidogo akafika Marium.
MARIUM: Nimekuja kukutembelea leo mdogo wangu.
ANNA: Karibu dada.
MARIUM: Mwenzio naona wanangu wote wamechanganyikiwa na ule ukoo uliolaaniwa.
Anna akampa moyo kuwa asiwe na shaka kwa Tina kwani kuna mwanaume mwingine anayemfatilia.
MARIUM: Bora, maana Yuda nae anataka kuleta uchizi kama ya ndugu yake Sele.
Patrick nae akaenda kumtembelea mamake mdogo na kumkuta Marium huku ambae alikazana kumshauri na kumshawishi Patrick kuwa asimuache Tusa.
Maiko aliyekuwa akiugulia donda alilopata kwa yale maji ya moto aliyomwagiwa na Deborah, akafatwa na Rehema na Adamu kwaajili ya kumuuliza.
REHEMA: Ila mwanangu na wewe umezidi kuwachanganya hao wanawake watakuua wewe.
MAIKO: Kweli kabisa mama, wataniua.
Walipomuuliza kuhusu huyo Patrick akawahakikishia kuwa ni Patrick wanaemjua wao.
REHEMA: Mbona hafananii?
MAIKO: Kweli hafananii ila ni yeye.
ADAMU: Dah! Kijana mbaya sana yule.
MAIKO: Ila mbaya ni Mashaka maana yeye ndiye aliyesema mzee Ayubu auwawe na sikujua kama ni baba.
REHEMA: Kwahiyo nyie kazi yenu kubwa ni uuaji?
Maiko hakutaka kujibu na kujifanya kuwa kazidiwa na maumivu, hivyo bi.Rehema na Adamu wakaondoka.
Mashaka aliamua kujipongeza kwa habari aliyompa dada yake kwani alijua lazima italeta mvurugano kati yao.
Akaamua kwenda baa kujipongeza.
Wakati anakunywa akamuona Tulo na mwenzie wakipita akaamua kuwaita ili ajumuike nao, na wala hakujua nini kilimpata Tulo.
Bi.Rehema na Adamu waliporudi kwa Deborah wakaamua kumuita Fausta na Pamela na kuwaeleza hawakutaka kumwambia Tina na Tusa kwanza kwani hata hivyo Tusa hakujua kama babu yake amekufa.
FAUSTA: Mmh! Hata siamini, Patrick anaweza kuua kweli?
PAMELA: Hata mimi mwenyewe siamini.
ADAMU: Mimi naamini, yule kijana ni mbaya sana, anapiga mtu kama vile anatwanga lazima atakuwa muuaji tu.
REHEMA: Pengine ukatili huo karithi kwa mama yake.
Bi.Rehema akawaelezea jinsi Deborah alivyommwagia maji ya moto Maiko.
FAUSTA: Kwa hilo nampongeza, kama ni mimi ningemwagia moto kabisa aungue vizuri.
REHEMA: Mmh! Ila ndio hivyo jamani, Patrick ndiye aliyemuua mzee Ayubu.
Deborah aliwasikia na kuwafata.
DEBORAH: Nani muuaji?
PAMELA: Eti mwanao Patrick.
DEBORAH: Kamuua nani?
REHEMA: Mzee Ayubu.
DEBORAH: Mna uhakika?
ADAMU: Ndio uhakika upo asilimia zote.
DEBORAH: Mimi nakataa, mwanangu si muuaji na hajawahi kumuua yeyote.
REHEMA: Sadiki tuyasemayo Deborah, mwanao Patrick kamuua mzee Ayubu.
Muda huo Patrick nae ndio alikuwa amerudi nyumbani kwao.
Muda huo Patrick nae ndio alikuwa amerudi nyumbani kwao.
Waliendelea kumjadili Patrick bila ya kujua kuwa yupo nje anawasikiliza wanavyosema.
DEBORAH: Nyie nani kawaambia kama Patrick ndiye aliyeua?
PAMELA: Wameambiwa na Maiko.
DEBORAH: Tatizo hamumjui Maiko vizuri, hata siwashangai.
REHEMA: Ila ni kweli, Patrick ndiye aliyeua.
Mara Patrick akaingia ndani na kufanya wote washtuke na kunyamaza.
PATRICK: Mnashangaa nini? Endeleeni kuongea.
Wakawa kimya tu wanatazamana bila ya kusema chochote.
PATRICK: Huwa sipendi kuishi na watu wanafki, kama nimefanya kitu niambie mwenyewe sio kukaa na kunijadili bila sababu za msingi. Semeni mnachosema juu yangu.
REHEMA: Hakuna chochote baba.
PATRICK: Hiyo ni nidhani ya uoga, mama nakuomba mara moja.
Ikabidi Deborah afatane na mwanae na kuwaacha wale wengine pale sebleni.
Bi.Rehema na wengine wakabaki kutazamana.
FAUSTA: (Akacheka), kweli nidhamu ya uoga yani hata wewe kaka umeshindwa kusema!!
ADAMU: Sijajiandaa bado, huyo kijana hatabiriki bhana.
PAMELA: Kwahiyo unamuogopa?
ADAMU: Hapana simuogopi.
FAUSTA: Mbona ulinyamaza sasa wakati wewe ndio mwanaume tunayekutegemea!
ADAMU: Dah! Haya mambo nyie acheni tu ila mi nadhani kuwa cha msingi ni kufata sheria juu ya swala hili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
PAMELA: Mmh!! Tutakuza mambo jamani, je tutayaweza? Hebu tufikirie kwanza.
REHEMA: Ila mi nadhani itakuwa bora kama tutaenda kuongelea nje maana humu ndani hapafai.
Wakaamua kutoka nje kwenda kuzungumzia hilo swala.
Patrick aliamua kuzungumza na mama yake.
PATRICK: Mama, kwanini mamkubwa ananisisitiza kuwa nisiachane na Tusa?
DEBORAH: Yule kashavurugwa mwanangu, kwa kifupi hata hajielewi.
PATRICK: Halafu mama wasisitizie hao watu, kuwa mi sipendi kusemwa semwa kama kuna tatizo wameliona basi wanifate mwenyewe sio kunisema pembeni.
DEBORAH: Usijari mwanangu.
Hata Deborah nae alishindwa kumuuliza mwanae kuhusiana na hiyo tetesi ya mauaji.
Tina na Tusa wala walikuwa hawaelewi kinachoendelea kwani wao walijifungia chumbani tu.
TUSA: Tina, leo Tulo anakuja. Jibu lako ni nini?
TINA: Hivi wewe Tusa huna habari zingine zaidi ya hizo? Nitaangalia kwanza akishakuja.
TUSA: Wanaume wana vishawishi vingi Tina, ni bora kuwa na jibu kabla hajafika.
TINA: Tusa, mi ni mkubwa sasa hakuna tatizo hata awe na vishawishi vya aina gani.
TUSA: Akikuletea zawadi hapo utakataa?
TINA: Kwani zawadi ina tatizo gani Tusa? Hakuna tatizo mdogo wangu niamini.
TUSA: Sawa ila nakuhurumia, je kwa mfano akifika Yuda na Tulo kwa muda mmoja utafanyaje?
TINA: Usijari Tusa, nitajua cha kufanya kama ikitokea hivyo ila najua haiwezi kutokea bhana.
Bado Tina alikuwa mgumu kuelewa.
Mashaka aliwanunulia pombe za kutosha Mwita na Tulo, wakanywa hadi kujisahau kabisa.
TULO: Itabidi ile safari yetu twende kesho Mwita.
MWITA: Sawa sawa hakuna tatizo.
Mashaka alikuwa akifurahia ushindi wake ila Mwita na Tulo hawakuelewa na waliendelea kunywa tu.
Usiku ulipofika ikabidi waende kulala hotelini, Mwita na Tulo wakalala hoteli ya karibu na Mashaka na kesho yake wakawa wakwanza kwenda kuzimua ile pombe kwa supu ili kuushtua mwili.
MWITA: Kwani Tulo unafanya kazi gani?
TULO: Kwanini?
MWITA: Tangu nimekufahamu, tunalala hoteli, kula vizuri na kukodi usafiri yaonyesha una pesa ya kutosha maana kila nikitaka kutoa pesa unanizuia na kutoa wewe. Hebu nihabarishe mwenzangu, kazi gani unafanya?
TULO: Aaah! Mi mchimba madini wewe, huko Arusha Mererani. Sisi ndio matajiri wadogo wadogo.
MWITA: Nadhani kazi yenu si ngumu ndomana hamna uchungu na pesa zenu. Inamaana unafanya kazi pamoja na Patrick maana na yeye aliniambia kuwa ni mchimba madini.
TULO: Ndio nafanya nae kazi moja, kazi yetu ukiwa unaanza ni ngumu sana ila ukiizoea inakuwa laini kama ugali na mrenda vile.
MWITA: Duh!! Haya bhana, si wengine tunahenyeka na serikali kwa mshahara kiduchu sana.
Mwita bado alikuwa na maswali kichwani mwake ila kidogo jibu la uchimbaji madini lilimridhisha kwani anajua jinsi gani madini yalivyo na pesa.
Yuda na Sele wakakaa na kujadili kauli ya mama yao.
YUDA: Unajua mama yetu utu uzima wake unampeleka vibaya sana, yani wanaume wakubwa kama sie ni wa kutuambia mwanamke anayefaa na asiyefaa kweli?
SELE: Mama kavurugwa bhana, mi badae nitaenda kwa mamdogo kusikilizia yale mambo ya Tusa na Patrick yameishia wapi.
YUDA: Kwahiyo hapo unatamani kweli Tusa apewe taraka!
SELE: Ndio ili nimpate kiurahisi.
YUDA: Bora hata mimi Tina uhakika kuliko wewe, nataka nikamnunulie Tina zawadi.
SELE: Zawadi gani?
YUDA: Yoyote nitakayopata, zawadi ni zawadi bhana.
SELE: Ila dah! Kwa huyo Tina hata mimi nakuhurumia, nakumbuka kipindi nipo na Tusa huyo Tina ndio alikuwa namba moja kumshawishi Tusa aachane na mimi. Yani Tina na mama yake Tusa wako sawasawa, wanapenda pesa balaa.
YUDA: Tina kabadilika bhana, si unakumbuka kipindi kile wakati namtongoza akaniambia nitafute pesa kwanza, mbona saivi hajaniambia? Inaonyesha kuwa ameshajifunza na kubadilika.
SELE: Kama kabadilika basi itakuwa vizuri.
Wote wawili wakajiandaa na kutoka.
Patrick alitulia kwao na kupanga cha kumfanya Maiko.
"Hivi mwanaume mzima kama Maiko bila hata aibu kuja kuwaambia hawa wasiojielewa eti Patrick kamuua mzee Ayubu. Hivi kweli mimi ningemuua mzee Ayubu bila ya yeye kunituma? Nadhani Maiko ananitafuta sasa. Na pia hawa nduguze hawamjui na hawanijui vizuri, sasa nitaenda kumchukua huyo Maiko wao na kumtoboa toboa mwili mzima mbele ya macho yao."
Patrick akaondoka nyumbani kwa lengo moja tu la kumpata Maiko.
Bi.Rehema akawaita tena watoto wake kujadili.
REHEMA: Hivi kweli tutakaa kimya hivi hivi bila kufanya chochote? Iko wapi haki ya mzee Ayubu?
PAMELA: Sasa mama tutafanyaje kwa unavyodhani?
REHEMA: Patrick achukuliwe hatua. Adamu acha kulala jamani wewe ni mwanaume unatakiwa usimame kwa hili.
ADAMU: Naona Deborah hatuamini, itabidi tumlete Maiko hapa aje kueleza.
FAUSTA: Jamani jamani naomba nitoe onyo, wengine hapa tuna aleji na huyo Maiko sasa mkija nae chochote nitakachofanya msinilaumu.
Halafu akainuka na kuondoka.
PAMELA: Achaneni na huyo kavurugwa, hebu tujadili wenyewe.
Wakaendelea kujadili yanayowasibu.
Fausta akaenda kuzungumza na Deborah.
FAUSTA: Wanavyojifanya wema utafikiri wao hawajawahi kutenda vitu vibaya.
DEBORAH: Kwani wao walifanya nini?
Fausta akaanza kumsimulia Deborah kuhusu kipindi kile cha yeye alivyokuwa mke wa Jumanne ambaye ndio huyo Adamu.
Stori aliyoambiwa ilimsisimua sana Deborah na kumfumbua macho na masikio na hata asijue itakuwaje pale ukweli wa mambo yote ukijulikana.
Kufika mjini, Yuda akaona viatu vizuri sana na kuamua kumnunulia Tina ili akamfurahishe.
Yuda na Sele wakaachana njiani kwani Sele alitaka kwenda kwanza kwa mama yao mdogo Anna halafu na Yuda akatangulia kwa Deborah.
Tulo na Mwita wakaenda nyumbani kwa Deborah, nia ya Tulo ni kuzungumza na Tina na kumkabidhi zawadi aliyomletea.
Tina alitoka sebleni akiwa na furaha ila Tusa alimuangalia kwa msononeko sana.
Wakati Tina akizungumza na Tulo pale sebleni, Yuda nae akaingia pale sebleni.
Wakati Tina akizungumza na Tulo pale sebleni, Yuda nae alingia pale sebleni.
Tina akashtuka kumuona Yuda, Yuda nae akashangaa kuuona ukaribu wa Tulo na Tina.
Yuda akamtazama Tina na kuwa kama vile anamuuliza jambo fulani kwa macho, Tina akashusha macho chini.
Mara Tusa akatokea ndani na kumuona Yuda akiwa amesimama na mfuko wake mkononi, akamfata kwa mbwembwe.
TUSA: Wow, shemeji yangu wa ukweli. Karibu sana.
Akaenda na kumpokea ule mfuko na kuuchungulia,
TUSA: Mmh!! Shemeji, umeniletea zawadi nini?
Yuda akaushangaa sana uchangamfu ule wa Tusa kwani hajawahi kumuona akiwa hivyo kabla.
TUSA: Mbona hujibu shem? Karibu tukae.
Tusa akamshika mkono Yuda na kwenda kukaa nae palepale karibu na alipokaa Tina na Tulo.
Kwakweli Tina aliona kuharibiwa siku vibaya mno kwani yeye hakupanga kabisa kuwakutanisha watu wale wawili pale.
Yuda aliendelea kumuangalia Tina kwa umakini mkubwa huku Tusa nae akiendelea kumuongelesha, Tina alijionea aibu kwani alitambua anachofanya.
Tulo hakuelewa kinachoendelea, ikabidi amuulize Tina.
TULO: Mbona umebadilika gafla Tina?
TINA: Naombe twende tukazungumze nje.
TULO: Kwanini? Mbona sielewi jamani?
TINA: Utaelewa tu tukitoka nje.
Tulo akainuka, Tina nae akainuka na Yuda nae akainuka.
YUDA: Unaenda wapi Tina? Si unajua kuwa nimekufata wewe!
Tina alikaa kimya tu, Tulo nae akamgeukia Tina na kumuuliza.
TULO: Amekufata wewe kivipi?
TINA: Twende nje bhana tukazungumze.
Wakawa wanatoka nje, na Yuda nae akawa anawafata kwa nyuma.
Patrick alifanikiwa kumuona Maiko, alimkuta akiwa amelala mgongo wazi kwani alikuwa amebabuka sana mgongoni.
Patrick akacheka sana,
PATRICK: Vipi gaidi? Umemwagiwa tindikali nini?
MAIKO: Nimemwagiwa maji ya moto na mama yako.
PATRICK: (Akacheka), kazi nzuri sana aliyofanya mama yangu. Nitaenda kumpongeza.
MAIKO: Yani, Patrick umefurahi kiasi hicho!
PATRICK: Tena nimefurahi mno, nia yangu kwako ilikuwa ni kukumaliza leo ila nitangoja kwanza hayo maumivu yako yapoe halafu ndio nije kukuongeza na maumivu mengine. Kweli mama yangu anafaa jamani.
MAIKO: Sawa, ila nitapona tu.
PATRICK: Na ukipona utakuwa mikononi mwangu. Haya niambie, nani amekutuma kuwaambia kuwa mimi ndiye nimemuua mzee Ayubu?
MAIKO: Unanionea bure Patrick, sikuwa na nia ya kusema ila yote haya ameyaanzisha Mashaka. Huyu ndio mtu mbaya Patrick.
PATRICK: Hata kama, wewe hukutakiwa kunitaja mimi. Muone ulivyo na ushetani wako hadi unaua baba yako mzazi.
Patrick aliondoka na kwenda kumtafuta Mashaka kwani alijua kuwa huyu ndiye msumbufu namba moja.
Tina na Tulo wakatoka nje na Yuda nae akawafata.
YUDA: Nahitaji kujua kuna nini kinaendelea kati yenu wawili?
TULO: Ujue wewe kama nani?
YUDA: Mimi kama nani? Kivipi?
Tina akaona mambo yatamgeukia sasa, akaamua kukimbilia ndani na kumuacha Tulo na Yuda pale nje.
Tulo na Yuda wakaanza kurumbana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
YUDA: Tina ni mpenzi wangu, nakuomba ukae mbali nae.
TULO: Mimi ndiye mpenzi wake, wewe ndio unatakiwa ukae mbali nae.
Wakaanza kugombana na kupigana, Mwita akawaona na kuwafata.
MWITA: Acheni ujinga nyie, hebu angalieni mwanamke mwenyewe kawakimbia na kuwaona wapumbavu. Nyie mnaendelea kugombana wakati mnayemgombania katulia ndani.
YUDA: Huyu jamaa ni muharibifu tu na hajui wapi nimetoka na Tina.
TULO: Hata mimi pia hujui nilipotoka na Tina.
Mwita aliendelea kuwasihi waache kugombana ila hawakusikia.
Mara Deborah nae akatoka ndani na kukutana na yale marumbano kati ya Yuda na Tulo.
Ikabidi na yeye aingilie kati kwani hakujua wanagombea nini.
DEBORAH: Sitaki matatizo nyumbani kwangu, kwani mnagombea nini na nyie hapa? Semeni mnachogombea.
Ikabidi Mwita amueleze kuwa wale wawili wanamgombea Tina.
Deborah hakutaka majibishano, aliamua kumuita Tina mara moja.
ITAENDELEA

0 Comments