Nilifika nyumbani nikamkuta mama anafua!
"Masu mbona umechelewa hivyo?"
"Baiskeli ilinisumbua sana mama!",nilimjibu mama huku nakwepesha macho yangu maana mama ana tabia ya kuuliza huku ananiangalia machoni kama nadanganya huwa anajua!
"Aya Scola kaja hapa,ametoka muda si mrefu kasema nikusalimie!"
Nilishtuka mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda mbio maskio yangu hayakutaka kuamini kama yameskia jina la Scola!
"Mama unamaanisha Scola amekuja hapa?"
Mama alikaa kimya,inaonekana hakupenda vile nilivyolipokea suala la Scola!
Nilisimama nikapanda baiskeli yangu nikaanza kuondoka!
"Masu!Masu!we Masu!!"
"Nakuja mama!"
Nilishika njia ya kuelekea Kijiji cha kina Scola!
Nilikimbiza sana baiskeli siku ile,pengine kuliko siku zote ambazo nimewahi kutumia usafiri ule!
Nilijua ningemkuta njiani lakini wapi,nilizidi kutokomea porini mpaka nafika kijijini kwao sikumuona Scola!
Jasho lilinitiririka kama maji,mapigo ya moyo wangu yalienda mbio!
Nikaenda mpaka kwao nikasimama kwa mbali! Bahati nzuri nilimuona yule msichana aliyenipeleka kule ambako Scola alikuwa anapenda kuota moto!
"Mambo!"
"Eh we mkaka iyo baiskeli mpaka uzeeke nayo?"
"Hahaaaa!hapana bhana naona Mambo siyo mabaya kitumbo kimejaa!"
"Ndiyo mi nimeolewa tayari!"
"Ok sasa mi shida yangu kama ya siku ile nataka kumuona Scola naskia amerudi!"
"Hahahahaaa!we mkaka wa ajabu kweli aya Scola yuko kule kule nilikokupeleka siku ile!"
Moyo wangu ulishtuka,sikutaka kuamini kama Scola bado ana mahusiano na yule baunsa wake!!
"Unamaanisha yupo kule kwa yule baunsa?"
"Ndiyo yupo uko!"
Tabasamu langu lilipotea ghafla hata hamu ya kumuona ikapotea kabisa!
Niligeuza baiskeli yangu bila kumuaga yule binti aliyebaki kasimama akiniskitikia!
Nilisukuma baiskeli sikuwa na nguvu ya kuiendesha!
Sikutaka kuamini moja kwa moja,nilikatiza nikashuka njia kwenda kumuona Scola wangu kama kweli yupo kwa yule baunsa wake!
Nilifika nikasimama mbali moyo ukiniuma sana!
Nilikuwa na mawazo mengi sana,sikuwa na uwezo hata wa kuleta fujo ni wazi yule jamaa ananizidi ubavu atanipiga aniumize!
Nilipaki baiskeli yangu nikaanza kupiga hatua zangu kusogea kwenye ile nyumba!
Hatua zangu zilikuwa nzito lakini nilijitahidi nikasogea Karibu na kijumba kile cha udongo kilichoezekwa kwa nyasi!
Hakukuwa na mabadiliko yoyote,zaidi nyasi zilijaa na kufanya kutishe!
Kwa kuangalia huwezi kuamini kama mwanamke mrembo kama Scola yuko ndani kwenye kijumba kile tena uchi wa mnyama akiwa amelalia kigodoro kidogo kilichochakaa na mashuka machafu ambayo yana miezi kadhaa hayajaona maji!
Nilisogea mpaka dirishani,nikachungulia nikamuona mwanaume yule kamuinamisha Scola wangu halafu kasimama nyuma yake anamsulubisha kwa bakora yake!
Maskini Scola alikuwa anatoa kilio kuonyesha mahaba yamefika penyewe!
Tofauti na siku ya kwanza kumkuta katika hali ile Scola nilisimamisha na hisia Kali zilinijaa!
Lakini siku hii ilikuwa tofauti,hasira zilinikaba nikijiuliza inakuwaje Scola katoka nyumbani kuniulizia na saivi yuko kwa mwanaume mwingine anafanya mapenzi!
Nilipandisha hasira kiasi kwamba sikuwa na uoga,hasira ilinipa ujasiri nikajikuta nimeropoka!
"Scolaaaaa!!!"
Wote walishtuka,yule jamaa alijitoa kwa Scola nikaiona bakora yake iliyong'aa kama imetoka kupakwa mafuta!
Nilishangaa baunsa yule kwanza hakuwa na bakora kama yangu,yangu ilikuwa mashine haswa sijui Scola alimpendea nini yule jamaa!
Yule jamaa alijifunga kitaulo chake akatoka nje akanikuta nimesimama tukabaki tumetizamana!
"We fala kila siku unakuja kuharibu starehe za watu!"
Nilinyamaza sikumjibu kitu,moyoni nilikuwa na hasira hadi macho yalikuwa mekundu!
Alinisogelea yule jamaa bila kuuliza alinipiga ngumi nikaangukia pembeni damu zikinitoka mdomoni!
Kabla sijakaa sawa akaanza kunipiga mabuti ya tumboni!
"Hey!Seba muache bhana utamuua!"
Alisema Scola baada ya kuja na kunikuta nimelala chini napigwa!
"Unamjua huyu kenge?",yule jamaa aligeuka akawa anamuuliza Scola!
Nilisimama kwa hasira nikaona ubao pembeni nikauokota kabla yule jamaa hajageuka nikampiga nao kichwani!
"Masuuuuuu!!",aliita Scola huku kashika kichwa muda huo jamaa yuko chini katulia kabisa!
"Masu umeua!!"
Scola alishika kichwa na mimi sasa akili yangu ilirudi nikaanza kujutia kwa nilichofanya!
Sikutaka kukaa pale tena,niliondoka nikapanda baiskeli yangu!
Nilifika nyumbani nikamkuta mama akiwa anakula,aliponiona tu aliona kitu cha tofauti.
"We Masu umepigana?"
Nilisimama sikumjibu kitu mama,alisimama akaenda jikoni akarudi na maji moto akaanza kunikanda!
Machozi yalinitoka ndipo nikaamini hakuna mwanamke wa kunipenda kama mama!
Mama yangu hakuniuliza kitu,najua alijua kama nimepigana,na nimepigana sababu ya Scola!
Niliingia kulala nikiwa na mawazo mengi sana,kichwani nilikuwa na mawazo makubwa nikijiuliza yule jamaa alizimia au alikufa!
Nilikuwa na wasiwasi mkubwa nikiamini jela inanihusu!
Usingizi ulikuja kwa tabu sana siku ile ..
******
Kulikucha nikaamka nikiwa na wasiwasi kuwa muda wowote nakuja kuchukuliwa na polisi!
Ile siku ikapita bila chochote kutokea,na siku ya pili ikapita hatimaye wiki ikaisha kidogo nikapata matumaini!
Moyoni niliapa kuwa sitokuja kuwa Karibu na Scola!
Siku moja nikiwa bustanini napalilia palilia ghafla niliskia sauti nyuma yangu!
"Masu!"
Nilishtuka nikageuka sikuamini,alikuwa ni Scola kasimama!
Scola alikuwa kapendeza haswa!Alionekana wa mjini haswa!
Scola alivaa suruali iliyombana na kumkaa mwilini,na juu alivalia tisheti nyeupe na nywele zake alizitengeneza yani kiufupi alivutia mno!!
Nilimshangaa kwa dakika kadhaa bila kupepesa macho!
Kosa nililofanya ni kushea funguo ya moyo wangu na Scola!
Maana kila nikifunga moyo wangu Scola akija anaufungua kirahisi!
Kilichotokea hata sijui ni nini,ila nilijikuta tu Scola anarudi kwenye makazi yake moyoni mwangu!
Huwezi amini sikuwa hata na nguvu za kumkaripia Scola wala kumhoji kwanini alinisaliti!
Mdomo ulikuwa mzito sana,ghafla niligeuka bubu!
Scola alishagundua kuwa Mimi ni mdhaifu kwake!
Alinisogelea akanikumbatia na matope yangu akapitisha ulimi wake sikioni Kisha akanipiga busu ghafla!!
Nilisisimka sana nikajikuta nafumba macho yangu kwa utamu! Vinyweleo vikasimama nikajikuta nimetamka neno ambalo sikujua limetoka wapi!
"Nakupenda Scola!!"
Scola hakunijibu aliniangalia machoni huku anatabasamu!!
Mikono yangu ilitua kiunoni kwa mwali huyu,aliyeniteka moyo wangu kwa mahaba yake!
Amekuwa kama shetani anayetembea kwenye misuli inayosukuma damu mwilini mwangu!
Amejigeuza na kuwa kama mtoto mdogo machoni mwangu!Kiasi kwamba hata akiunyea mkono siukati nauosha!!
"Scola kwani umenipa nini?"
Nilimuuliza Scola sababu kwa maajabu anayonifanyia sikujua kwanini bado namng'ang'ania!
"Mahaba mpenzi!",alijibu kisha akanipiga busu mdomoni kisha akaniachia!
Jembe liliingia dosari,lilikuwa zito kuliko mlima Kilimanjaro!
Nililitupilia mbali nikajisogeza kwa kipenzi changu Scola!
"Masu mi ninaondoka kesho kutwa!"
Taarifa ile ilikuwa kama msumari wa Moto moyoni!nilihisi kunyong'onyea sana!
Nikiwaza ni miaka imepita bila kumtia machoni tabibu wa maradhi yangu ya mapenzi!
"Masu mi nitarudi!"
"Scola mbona mapema ndiyo kwanza macho yangu yameona tena n ndiyo unataka kunikimbia!
"Masu leo nataka tulale wote kuna chumba cha rafiki yangu kijijini kwetu!"
"Kulala nje?mama yangu atanielewa kweli?"
"Unatakiwa uwe mwanaume wa kweli mi mbona nalala nje Masu usiniangushe!"
Scola baada ya kuniambia vile aliniambia jioni ya siku ile niende kijijini kwao!
Nilibaki na mawazo tele kichwani,nilimpenda sana Scola lakini suala la kulala nje na nyumbani lilikuwa gumu sana!
Lakini pia ningempata wapi njiwa wangu akipeperuka,ni lini tena atakuja kutua kwenye mti huu!
Nilibaki njia panda kwa kweli sikujua niende kushoto au kulia!!!
Moyoni nilishindwa kuamua niliwaza kumkosea tena mama yangu kwa mara nyingine sababu ya Mapenzi tena Scola!
Scola aliniacha njia panda,ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwangu.
Sikutaka kumkosea mama yangu lakini pia tunda la Scola nililitaka!
Hakukulimika tena,nilijikokota taratibu kurejea kambini(nyumbani).
Kichwa kilikuwa kizito sana nilitembea huku nimeinama kama kobe!
Mwende wangu wa kinyonga ndiyo uliofanya watu kunishangaa,nilikuwa tofauti na siku nyingine!
Sikuwa Masu yule mcheshi kipenzi cha watoto,moyo wangu ni kama ulikufa kwa muda na akili yangu ikasimama kwa kuelemewa na mawazo!
Maamuzi ndicho kitu kilitakiwa muda ule,maamuzi ambayo ni lazima yalete hasara kwa upande mmoja!
Nilifika nyumbani sikumkuta mama,bado alikuwa gengeni!
Nikaenda kuoga nikala nikaanza kuchanganyua akili yangu!
Kati ya mama na Scola nani nimkosee?majibu yalikuja mengi ikawa kazi kwangu kuchagua!
Mwisho nikaamua nimkosee mama yangu,nikiwa na sababu zangu.
Nilipima upendo wa mama na Scola yupi ananipenda? jibu likaja jepesi sana kuwa hakuna mwanamke wa kunipenda kama mama yangu!
Nikajiuliza pia ni nani nikimkosea itakuwa rahisi kunisamehe?jibu likaangukia kwa mama,basi nikajiandaa muda huo kigiza kilishaanza kuingia!
Nilitoka na baiskeli yangu nikaacha ujumbe mezani kuwa naenda kwa rafiki yangu Kijiji cha pili ntarudi kesho,ivyo asiwe na wasiwasi!
Nilizungusha pedeli safari haikuwa fupi hatimaye nilifika Kijiji cha pili!
Siku hii sikupata tabu kumpata Scola ni kama alikuwa ananisubiri!!
Nilimkuta sokoni aliponiona tu alinikimbilia!
"Masu!nilijua usingekuja!"
Alinilaki kwa tabasamu pana akionyesha kufurahia ujio wangu,hii ilinipa faraja kuona kumbe Scola huwa ananifikria!
Kwa mbali nilimuona yule baunsa ambaye nilimpiga na ubao siku ile akazimia!
Niliogopa sana nikawaza pengine Scola kanileta hili nilipiziwe kisasi!
Nilimuangalia hadi Scola akashtuka akafuata uelekeo wa macho yangu!
"Achana naye yule fala tu,anachukua wasichana kibabe hapa kijijini?"
"Scola unamaanisha hata wewe alikuwa anakuchukua kinguvu?"
"Yule anaitwa Seba Kijiji hiki kinamuogopa sana huwa akimtaka binti yoyote yule anamchukua hata mbele ya wazazi wake!"
Maneno ya Scola yalinipa moyo nikaamini huenda kweli na Scola wangu hakufanya yale kwa hiyari pengine alilazimishwa!
"Karibu sana kijijini kwetu!",alisema Scola muda huo kaishika baiskeli yangu ananiongoza na njia!
"Ahsante Scola,ohh sorry baby!"
Nilijikuta nasahau sheria za Scola wangu,anapenda sana majina ya kizungu!
Safari iliishia nje ya kijumba chenye chumba kimoja tu na juu kiliezekwa kwa nyasi!
"Karibu!",alisema Scola huku anaingiza baiskeli yangu ndani ya kijumba kile!
Niliingia ndani kulikuwa na giza totoro,Scola akawasha koroboi ikarejesha mwanga ndani ya chumba kile!
Angalau ndani ya kijumba kile vitu japo vichache lakini vilipangiliwa kwa mpangilio!
Hakukuwa na vitu vya gharama zaidi ya godoro na vingine!
Kigodoro kile kilipambwa na kutandikwa vizuri sana!
"Masu mi kesho kutwa naondoka dada ameshanipigia simu huko mjini!"
"Kwani unafanya kazi gani Scola?"
"Biashara tu Masu!"
Sikutaka kumuhoji sana,haukuwa muda wa maswali.
Nilikuwa na kiu na maji nayaona naanzaje kuleta stori za msiba kwenye harusi yenye furaha!
Nilikaribia nikakaa kwenye kigodoro kile!
Scola alinisogelea akakaa karibu yangu!
"Masu leo nataka unikune nawashwa!"
Scola alionekana kuwa kiu kikali cha mahaba,kama ni koo lilimkauka haswa alihitaji japo tone la penzi langu!
Alianza kuzivua nguo zake Ila nikamzuia,ndiyo nilimzuia sababu mimi siyo Masu yule tena!
ITAENDELEA

0 Comments