Mwanamke kuvua nguo zake mwenyewe ni kosa kwa mabaharia wanaojua maana!
Nilimsogelea nikamkumbatia nikamnong'oneza!
"Nop baby!hakuna haja ya kuponda mawe ntapanda nikuchumie!!"
"Mmh Masu,umejifunza wapi?"
Sikumruhusu aongee sana,niliumeza ulimi wake nikaanza kumnywesha juisi ile adhimu.
Juisi ambayo ikimwagika chini inatia kinyaa ila ukiinywa kwenye kopo lake inakuwa tamu kuliko asali!!
"Mmmhhh!Sumaaaaaa!"
Aliniita Scola baada ya kuona mgeni kawa mwenyeji ghafla anajipakulia atakavyo,mgeni mtukutu anaingia chumbani bila kukaribishwa!
Nilitaka kumuonyesha Scola kuwa sikuwa mshamba tena.
Kwake yalikuwa ni maajabu hakunizoea vile!
Ile geuza geuza kama samaki sasa ilimgeukia!
Nilimchambua akachambulika,nikampepeta akapepeteka,nikamuosha akaosheka na pishi likakubali sasa ukabaki wakati wa kuliwa tu!!!
Chumba kile kilikuwa shahidi kikijionea tamthiliya nzuri ya mapenzi!
Mahaba yalikolea kulia kwa kupokezana,kushoto kulia na penye utamu tulipongezana!
"Mmmhhh!",aliguna Scola baada ya shughuli pevu hatimaye tulitua makapu yetu,kila mmoja akiwa amepata alichofuata sokoni!
"Mbona unaguna Scola?"
"Mmh!hapana nimeguna tu!"
Sikutaka kumuuliza maswali mengi,nilijua muziki wangu kaupenda Ila hawezi nisifia sababu anaamini mimi bado mshamba!
"Masu mi naondoka kesho!"
Hii kauli ilinitoa mchezoni,ikanirudisha kwenye ulimwengu wa huzuni!
Roho iliniuma nikakumbuka nilivyoteseka kipindi hayupo waubani!Nilimkumbuka sana mwandani na sasa ninayo nafasi moja tu ya kufuta upweke wa miaka miwili iliyopita kabla sijaanza safari ya upweke tena!
Nilimuangalia Scola kwa macho yaliyosema!
Macho yangu yaliongea kwa lugha iliyoeleweka!
"Masu unataka nisiende?"
Machozi yalinitoka Masumbuko,chozi la mapenzi!
"Heee!unalia??"
Scola alilishangaa chozi langu,hakuamini mvua ile ilinyesha kwa ajili yake!
"Hivi Masu unanipenda ivyo?"
"Scola tangu nikuone umefunga mboni zangu,macho yangu hayaoni tena,maskio yangu hayasikii tena na hisia zangu zote umechukua hati miliki!
Unadhani ataishije kifaranga huyu bila joto la mama yake,ataishi vipi huyu ndama bila maziwa ya mama!"
Kwa mara ya kwanza niliiona huzuni ya Scola,Ila sikuijua maana!
Sikujua maana halisi ya huzuni yake kama ananihurumia kwa kuwa nimependa pasipo au ananihurumia kwa kuwa anahisi maumivu yangu jinsi navyomkumbuka akiwa mbali!
"Masu lazima niende,biashara yangu inalegea mjini,wateja wamenizoea wanamsumbua dada!"
Moyoni nilifurahi kuona mwanamke anajituma,ni ndoto yangu kuwa na mwanamke anayejituma kutafuta maisha!
Ila laiti ningejua ni biashara gani anaifanya mjini nisingewaza kumpongeza!
Scola alinifuta machozi kwa ncha ya ulimi wake!
Hapa ndipo aliponimaliza mwanamke huyu!
Mapenzi yake alijua kuyalemba na kupaka rangi nzuri sana iliyoficha maumivu mengi ndani yake!!!
Usiku ule haukuwa wa kufumba macho,ulikuwa ni wa kubandika na kuipua,kuchemsha na kupoza,kukoboa na kusaga!
Mpaka jogoo anawika hali si hali,siyo mimi wala kipenzi changu Scola wote tulikua taabani nyang'anyang'a kwa shughuli pevu ya usiku!
"Masu hii mechi mbona batili!"
"Kwanini mpenzi!"
"Dakika tisini zimeisha za nyongeza zimeisha penati zimeisha na hakuna mshindi jamani!"
"Hahahaha!basi tuiahirishe hakuna namna!"
"Kumekucha Masu inabidi niwahi basi usafiri wetu huku unaujua!"
"Natamani kwenda mjini na mimi Scola!"
"Usjali ntakupatia namba ya simu ukimaliza shule uje!"
"Kweli baby!"
"Yeah!"
Hakukuwa na mambo mengi muda huo Ilibidi niondoke mapema kuwahi kusomewa kesi na mama Masumbuko!
Niliagana na Scola kwa mara nyingine tena,niliumia sababu sikujua lini tena macho yangu yataona tena!
Maana ni kama vile akiondoka ananiachia upofu,macho yangu hayaoni kabisa!!!
Kinyonge,nilipanda baiskeli yangu nikamshika njia ya kuanza kukitafuta Kijiji chetu!
Mwendo wangu ulikuwa wa taratibu sana,nilijikokota kama nyoka aliyejeruhiwa!
Mfukoni nilikuwa na namba ya simu ya Scola ambayo sikujua ntapata wapi simu ya kumpigia!
Kipindi hicho mtu kumiliki simu ni kazi sana!
Nilifika mapema asubuhi kabla hakujakucha sana!
Sikutaka kumsubiri mama aamke nilitafuta angalau mbinu ya kumpoza!
Niliona bora nipitie bustanini nikachukue mahitaji ya gengeni kabisa hili akiamka ayaone pengine anaweza kutuliza hasira zake!!!
Nilirudi nikamkuta kashaamka anafagia uwanja!
"Shikamoo mama!"
"Marahaba,ulilala wapi Masu?",aliitikia Salam na swali juu!
"Kwa rafiki yangu mama!"
"Scola!"
Mama alilitaja jina la Scola kiasi nikashindwa kuelewa mama kajuaje?
Hapo ndipo niliamini mkubwa hadanganywi!
"Hivi Masu unasumbukia nini kwa yule binti wa mjini,unahisi mnafanana?umetoka kupigana juzi kisa huyo binti wa mjini!"
"Mama lakini ni....!"
"Jiangalie Masu gari la petroli haliwashwi kwa mafuta ya taa,na mafuta na maji havipatani naona unajifananisha na asali ungali bado uchumvi ya mawe!"
Maneno ya mama sikuyaona maana yake,siku zote ukipenda hata Jambo jema unalitoa kasoro!
Unaweza ukaambiwa mkeo au mumeo anachepuka matokeo yake mtoa taarifa akaonekana mbaya!
"Nimekuelewa mama!",nilimjibu ili afupishe maneno yake!
Ningewezaje kuamini kuwa ile supu niliyokunywa muda si mrefu ilikuwa na sumu?
Ningewezaje unadhani?nisingeweza kuamini hata kidogo!
Scola nilimpenda na nikamtunuku moyo wangu kabisa!
"Matokeo yametoka huna habari,unahangaika na waso heshima,binti hana radhi yule ndiyo unataka kuniletea hapa Masu Masu ntakuachia laana nakwambia!"
"Mama matokeo yametoka!"
Nilichukua baiskeli yangu haraka nikaanza safari kuelekea kwenye ofisi ya Kijiji!
Nilifika nikakuta wenzangu wanaangalia majina yao!
Nilijiunga nao nikaanza kutafuta jina langu lakini sikuliona!
Nilianza kupata wasiwasi,nilihangaika sana lakini sikubahatika kuliona moyo ukaingia mashaka!
Baada ya kulitafuta jina langu bila mafanikio nilikata tamaa!
Miguu yangu ilikosa nguvu,ndoto zangu za kusoma zikaonekana kufifia!
Machozi yanililenga hasa nilipowaona wenzangu wanafurahi baada ya kupata majibu yao!
"Masu!Masu!tumetoboa mwanangu"
Said ndiye alinikurupusha kutoka kwenye dimbwi lile la mawazo!!
"Nini unasemaje Side?"
"Njoo uone!njoo uone!"
Niliamka nikamfuata Side sikuamini alinionyesha jina langu ni kweli kati ya watu kumi na tano waliofaulu katika shule yetu na sisi tulikuwemo!
"Dahhh!siamini!"
"Hahahaa!!Masuuuuu!!tumetoboaaaa!!"
Side alinikumbatia kwa furaha!hakika ilikuwa furaha sana!
Msoto wa mwanga wa kibatari ulizaa matunda!
Nilirudi nyumbani nikiwa na tabasamu pana!
Nilitamani nimfikishie habari zile njema mama Masumbuko,ndiyo maana nilipomkosa nyumbani nilifunga Safari hadi sokoni!
"Mama!mama!nimefaulu!"
Mama alinikumbatia kwa furaha machozi yakimlenga!
"Soma mwanangu,soma umuumbue baba yako alijua bila yeye haiwezekani mwanangu!"
"Kwani baba yangu yuko wapi mama!"
Swali lile lilimfanya mama aniachie hakusema neno tena!
Akaendelea na shughuli zake akipanga vitu kwenye genge lake!
"Kaa hapa leo Masu,nataka nikakupikie chakula kizuri mwanangu umenifurahisha sana leo!
Alisema mama kisha akaniacha sokoni akaelekea nyumbani!
**********
Baada ya matokeo sasa tulisubiri kupangiwa shule ambapo nilichaguliwa kujiunga na shule moja jijini Dar!
Ilikuwa ni furaha nyingine kwangu nikiamini sasa naenda kuwa Karibu na mpenzi wangu mjini!
Nilitafuta simu nikampigia kwa namba aliyonipa!
"Haloo Nani?",alipokea mwanamke upande wa pili akaniuliza!
"Haloo Scola!"
"Wee Scola simu yako hii!",niliskia upande wa pili akiongea!
"Nani tena ananiita Scola jamani mi naitwa princess!!"
Japo ni kwa mbali ila niliskia ile sauti,sikushangaa sababu habari za watu kubadilisha majina mjini ni nyingi sana!
"Halooo!",aliita Scola kwa sauti ambayo alionyesha kama siyo katoka kulala basi katoka kufanya kazi nzito!
"Scolaa!ni mimi Masu!"
"Masuuuu!!!"
"Yes baby!"
"Ooh!nambie bushman uko poa!"
"Niko poa hofu kwako mkalia ini wangu!"
"Huku kwema Masu!"
"Scola nakuja mjini!!"
"Mmh!Masu siyo saivi mi bado sijajipanga!"
"Scola nimefaulu mimi nakuja shule!!"
"Ooohh!hongera Masu karibu sana ukija unitafute please!"
"Sawa Scola nimeazima simu hapa kwaheri nimekumbuka sana tabibu maradhi yangu yamemiss sindano zako!Yananiuguza makusudi kunikumbusha utamu wa mapenzi yako!"
"Mmmh!Masu unanisisimua bhana ushakuwa muimba mashairi Bushman umeendelea!"
"Hahahahaaa!",nilicheka Ila kabla sijatia neno simu ilikata salio limekwisha!
Moyoni nilifurahi sana kuiskia sauti ya kipenzi changu!
Nilirudi nyumbani kipindi hicho maandalizi ya shule yanaendelea!
Mpaka inafika siku ya kuondoka kila kitu kilikuwa tayari!
Nakumbuka siku moja kabla ya kuondoka mama aliniita sebuleni!!
"Mwanangu safari huwa ngumu kila unapopiga hatua ya kusonga mbele!unakoanzia ni kurahisi kuliko unakomalizia!chonde mwanangu fuata kilichokupeleka!
Nakuomba siku zote utambue kuwa hakuna mwanamke yoyote atakayekupenda zaidi ya ninavyokupenda mimi mama yako.
Uwe na kiasi mwanangu mjini kuna Mambo mengi yenye kutamanisha,anasa zote unazozijua na usizozijua zipo mjini huko uendako!
Usinisahau wakati wa furaha,ukanikumbuka wakati wa huzuni tu,Masumbuko mwanangu nilikuita hili jina hili daima usisahau wewe ni nani na unapaswa kufanya nini!"
******
Mama alinipa usia ulionigusa moyoni,nikaapa kuyafanyia kazi yote aliyoniambia?
Asubuhi niliamka mapema mama akanisindikiza,nilikuwa na rafiki yangu Side maana tulichaguliwa shule moja!!
Tulipofika stendi tulikata tiketi Ila kabla sijapanda gari nilimuona mama yangu vile uso wake ulivyofunikwa na ukungu wenye huzuni!
Ilimuwia vigumu kukubaliana na hali ile,
Nilimsogelea nikamkumbatia mama yangu!
"Mama usihuzunike naenda kukupigania!"
Machozi yalinitoka siyo Mimi tu hata mama yangu!
Nimeishi chini ya kivuli chake tangu nizaliwe!Nimeishi nikimjua yeye kama baba na mama yangu!
Ilikuwa ni ngumu kumuacha mpendwa wangu bila kumbatio la matumaini!
"Nenda,nenda mwanangu!nenda ukaniletee heshima,daima nijivunie kuwa na kijana kama wewe Masumbuko!"
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya mwisho ya mama yangu pale stendi!
Nilipanda gari nikageuka nikampungia mkono naye akanipungia gari likaanza safari!
Safari ya kuitafuta ardhi ya Dar es Salaam!
Ardhi ambayo ilinipa mateso na maumivu yasiyohesabika!!!
Kama kawaida ya Dar es salaam,mgeni utambulika machoni!
Macho yangu hayakutulia kuzunguka huku na kule kushangaa magorofa na nyumba nzuri zenye kuvutia!
Kwa side yeye hakuwa mshamba sana maana haikuwa mara yake ya kwanza kuja jijini!
Tulifika stendi ya ubungo tukashuka.
Wingi wa watu na pilika pilika nyingi zilitosha kuniambia "Sasa Masu umeingia jijini!
"We Masu acha kushangaa hapa kuna wezi wakikuona mshamba mshamba wanakutapeli",aliniambia Side!
Tulichukua pikipiki kwa mpaka shuleni,tulikuwa miongoni mwa watu wachache waliofika siku moja kabla ya siku ya kuripoti!
Maisha yalianza rasmi,ilikuwa ngumu kuzoea maisha yale maana ilikuwa ni ndani kwa ndani kwa mliosoma boarding mnajua!
Mawazo yalikuwa ni mengi sana kwangu,maana ukitoa masomo kingine kilichonifanya nifurahi kuja mjini ni mpenzi wangu Scola!
Mpaka muda huo nilikuwa sijawasiliana naye kabisa!
Hatimaye mwezi ulikatika bila kupata mawasiliano yoyote na Scola wangu!
Sikuwa na furaha,huzuni ilitawala mpaka hapo sikujua nawasiliana vipi na Scola!
Siku moja nikiwa darasani nikakumbuka kuna kitabu nilikisahau bwenini!
Nilitoka darasani nikashika njia kuelekea bwenini!
Nilipofika mlangoni niliskia kama mtu anaongea bwenini!Ila ni kama alikuwa anaongea peke yake nikasita kuingia kwanza!
Kutokana na jinsi alivyokuwa anaongea moja kwa moja nikajua atakuwa anaongea na simu!
Nilifungua mlango ghafla!na yeye akashtuka akaificha simu yake!
Alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tano ila hatukuwa darasa moja yeye alikuwa anasomea masomo tofauti na Mimi!
"Unaficha nini Sasa?",nilimsogelea nikamuuliza!
"Kwani we umeona nini?"
"Nimeona simu!",nilimjibu bila hofu Wala kupepesa macho!
"Iko wapi?"
"Sikia usitake tubishane mi kusema kwa mwalimu sioni shida,nimekusikia kila kitu hadi unasema leo utatoka mkaonane!"
"Unataka nini?"
"Nataka simu yako nimpigie mpenzi wangu na pia leo tutoke wote nami nikamuone mpenzi wangu!"
Ilibidi awe mpole akanipa simu,namba ya Scola ilikuwa kichwani nikaandika nikampigia!
'namba unayopiga kwa sasa haipatikani!'
Nilishusha pumzi ndefu sana,nilijaribu kama Mara tatu nikaambiwa simu haipatikani!
"Vipi haipatikani?",aliniuliza yule jamaa!
"Ndiyo!",nilimjibu nikiwa na sura yenye kukata tamaa!
"Jaribu tena utakuwa mtandao mbovu!"
Nilipiga tena bahati nzuri ikaita kisha ikapokelewa!
"Hello!",sauti ya malikia wangu ilisikika!
"Hello Scola ni mimi Masu!"
Niliongea kwa sauti hadi yule jamaa akaniambia!
"Oya!taratibu mzee tutakamatika!"
"Masu uko mjini?"
"Ndiyo nipo shule ila nilitaka tuonane leo!"
"Ndiyo ile shule uliyoniambia?"
"Ndiyo!"
"Ok tuonane sangapi?"
Hapo sikujua ilibidi nimuulize huyu jamaa ambaye anaonekana yeye kashakuwa mzoefu!
"Eti tunatoka sangapi?"
"Mwambie saa nne usiku!"
Baada ya kupata jibu nilimwambia na Scola ambaye bila kusita aliniambia kuwa saa nne atakuwa pale shuleni!
INAENDELEA....

0 Comments