Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu na Scola,alilipenda penzi langu tu hakunipenda Masu!
Alikuwa kila akitaka penzi langu anakuja siku yoyote ananipigia simu nitoke!!
"Scola lakini Niko shule ujue!"
"Shhhhiiiiiiiiiihhhh"
Scola hakunipa nafasi ya kujenga hoja,aliingiza mkono kwenye boksa yangu ili apate anachokitaka!
Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yake!aliweka mbele tamaa zake za kimwili kuliko mapenzi ya dhati!
Hatimaye ulifika muda wa kwenda likizo,nakumbuka matokeo yalitoka nikiwa mmoja kati ya wanafunzi kumi waliofanya vizuri japo si vizuri sana!
Side ndiye aliibuka kinara kwa kupata alama za juu katika masomo yote!
"Hivi Masu unajua hata nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali!"
Alikuwa ni Side akiniambia maneno haya!
"Unamaanisha nini Side!"
"Wewe una akili Masu,kumbuka ulivyokuwa unatubuluza kijijini lakini leo mimi nimepata alama za juu kuliko wewe!"
"Kila jambo na wakati wake Side,pengine ndiyo muda wako huu wa kutamba!"
"Masu we una akili ebhu angalia pamoja na yote unayoyafanya lakini upo miongoni mwa waliofanya vizuri!"
"Sasa ulitaka nifeli Side?"
"Hapana simaanishi ivyo!namaanisha ukiacha unayoyafanya sasa ukasoma hata mimi sitakugusa utakuwa Tanzania one!"
"Umeanza mahubiri Sasa!"
"Siyo ivyo Masu!kesho mi naenda kijijini ushajiandaa!"
"Siendi,mi nabaki huku ntakupa matokeo umpelekee mama mwambie mimi nipo napambana!"
"Masu!utaishije mjini hapa!"
"Hayakuhusu!Mimi ni mwanaume bhana!"
Nilikuwa na jeuri sababu tulishapanga na Scola nikifunga shule nikakae kwake mpaka tutakapofungua shule!!
Side hakuamini kama kweli mimegoma kwenda kijijini!
Kesho yake nilimsindikiza akapanda basi isha nikampigia simu Scola nikamuambia kuwa tumefunga shule!
Akaniambia atakuja jioni kunichukua shuleni!
Jioni kweli alikuja na bajaji nikapakia kibegi changu,sikuchukua hata daftari moja niliondoka na nguo zangu tu!
Safari ilitupeleka mpaka Mwananyamala,kule ndiko alikokuwa anaishi Scola!
"Karibu Masu!"
"Ahsante!"
Ilikuwa ni nyumba kubwa ya vyumba vitatu na sebule kubwa tu!
Bado nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza!
Pale ni kwa nani?au Scola anaishi na nani katika jumba kubwa namna ile!!
"Hahaha!bushman nilijua utakaa chini!"
Alisema Scola baada ya kuniona nimekaa kwenye moja ya masofa yaliyoipamba sebule ile kubwa!
Nilitabasamu tu maana kusema ukweli sikupenda vile ananiita Bushman!
"Bushman una juisi,maji na wine sijui unataka nini!"
"Niletee juisi!"
"Kunywa wine acha ushamba mtoto wa kiume!"
Aliniletea juisi kisha akaingia chumbani alitoka akiwa amevaa kanga peke yake!
Mdomo wangu ulikuwa kwenye glasi ya juisi Ila macho yangu yaliangalia sehemu za nyuma za Scola ambaye si mgeni kwangu ila hakuwahi nichosha machoni!
Scola alikuja akanikalia mapajani,mkono wake mmoja akaupitisha shingoni!
"Bushman!unaikumbuka ile shoo siku ile tulivyolala wote kijijini!"
"shoo gani mpenzi?"
"Unaniangusha bhana namaanisha unakumbuka siku ile tulivyofanya mapenzi hadi asubuhi kule kijijini?"
"Hahahaha!nakumbuka!"
"Sasa mpaka urudi shule mmh!nataka nipate shoo kama zile kila siku!"
"Wewe tu Scola,Masu nimenyimwa hela tu lakini mashine ipo mama!"
"Hahahaha!tafuta hela wewe,achana na shule kina Mo wale Bakhresa hawajasoma!"
"Mmhh!wamesoma wale!"
"Umeanza lini kunibishia?we nisikilize mimi hata nikikuambia Diamond ni msukuma kubali!wakusoma utakuwa wewe?"
"Unakula kwanza ndiyo ule?"
"Unamaanisha nini?",sikuelewa ile kauli.
"Hahahahaaa!namaanisha nataka hii!"
Alisema Scola huku mkono wake akiupitisha ndani ya suruali yangu!
"Mmhh!Safi sana bushman,betri yako iyo feki iko full charge!"
"Scola kwani unapenda nini kwangu naona kama tunatofautiana mawazo!"
"Masuuu!!!umeanza sitaki usumbufu nikiwa kwenye mood zangu!"
"Lakini naongelea maisha yetu,mapenzi ni maisha!"
"Maisha unayajua wewe?we mwenyewe mtoto wa mama unanuka maziwa kula kulala!"
"Ila Scola unge.....!"
"Shut up!!!!!"
Scola alipaza sauti kisha akanishika mkono akanivuta mpaka chumbani,alipofika akanisukumia kitandani!
Akanivua suruali na boksa yangu akapanda juu,hakuwa amevaa kitu ndani zaidi ya kanga yake nyepesi!!
Aliishika bakora akaizamisha pangoni,ikazama taratibu kama chupa ya soda boya zikabaki juu!
Akaanza kuzungusha nyonga yake taratibu,sikuwa na hisia lakini kama unavyojua hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Scola alikuwa kama shetani kwenye maisha yangu!
Alijua kunikasirisha na alijua kunifurahisha!
Baada ya kuridhika Scola alishuka akakaa pembeni akainamisha kichwa chake chini!!
"Aliyekupa hii bakora aliniweza,natamani atokee mtu kama wewe ila hatokei sijamuona,nakichukia Masu sijawahi kukupenda!"
"Sijui kwanini ninachokikosa kiko kwako tu na si kwingine kwanini???aaaahhh!! I hate youuuuuuu!!!!!!!"
Alisema Scola kwa sauti kisha akatoka chumbani!
Maneno yake yalinichoma moyoni,niliumia Sana kusikia Scola anasema hajawahi kunipenda!
Anasema hajawahi kunipenda na huku mimi mpaka nilipofikia nimeishi kumpenda yeye tu!
Alikuwa kwenye ndoto zangu,ila sikuwa kwenye ndoto zake!
Aliishi moyoni mwangu,lakini sijawahi kuishi Wala kuingia moyoni mwake hata kwa bahati mbaya!
Kiunyonge niliinuka nikakaa kitandani,nikauangalia uume wangu ambao ndiyo kiungo pekee kinachopendwa na Scola mwilini mwangu!
Ningekuwa na uwezo ningeukata nikamuachia abaki nao mimi niondoke zangu asinitafute!
Lakini nikiukata nataishije mimi?Na nikiondoka nao atanifuata tu kuja kumtafuta kipenzi chake!!
Nilisimama mbele ya kioo nikaanza kujikagua pengine sivutii,lakini sikuona ubaya wangu hata wanafunzi wa kike wananisifia shuleni kuwa mimi ni mzuri Mimi ni handsome sasa kwanini Scola anasema hanipendi?
Nilivaa suruali yangu nikatoka sebuleni nikamkuta Scola anapika!
Nilishika begi langu nikaliweka mgongoni,nikavaa viatu vyangu!
Sikutaka kumuaga Scola nilishika kitasa cha mlango lakini kabla sijakifungua akanishika mkono!
"Masu unaenda wapi?"
"Naenda kijijini!",nilimjibu bila kugeuza uso wangu,maana nikimuangalia tu basi hasira zitatoweka Scola aliniteka nyie acheni!
"Sasa mbona unaniacha,si ulisema utakaa hadi likizo iishe!"
"We hunipendi Mimi Scola unapenda penzi langu,leta kisu nikukatie unachokipenda ubaki nacho!"
"Unamaanisha nini Masu?"
"Okay hunielewi Towngirl ngoja nikuonyeshe ninachomaanisha!"
Niliongea kwa hasira machozi yakinitoka,nikaingia jikoni nikachukua kisu nikavua suruali yangu nikaishika bakora yangu nikapeleka kisu niiikate!
Scola alishtuka hakuelewa nachomaanisha aliogopa sana akanikimbilia akanirukia tukaanguka sakafuni.
Ikawa ni kama tunabishana Scola akawa ananinyang'anya kisu mi naking'ang'ania!
Mwanamke ni mwanamke nilimzidi nguvu nikamsukuma akaangukia pembeni nikashuka kisu nikaishika bakora nikaanza kuikata!
Kuna upumbavu mwingi nimeufanya kwenye mapenzi!
Na huu ni mojawapo ya upumbavu ambao ungekamilika sijui ingekuwaje!!
Akili yangu ni kama iliingia mdudu,sikuwa sawa kabisa!!
Huwezi amini nilidhamiria kuukata uume wangu mwenyewe kwa sababu ya mwanamke!
Halafu bado kuna mtu atasema yeye anajua kupenda,kuna watu wanapenda nyie acheni!!!
Bahati nzuri kisu kilikuwa butu kile na ile sauti aliyotoa Scola ndivyo vilinifanya niache kufanya nilichodhamiria!
"NAKUPENDA MASUUU!!"
Nilishtuka,sikuamini kama ni Scola amesema maneno yale!
Ilikuwa ni kama nimezinduka kutoka kwenye usingizi mzito sana!
Mikono ililegea kisu kikadondoka chini nikamsogelea taratibu Scola ambaye alikuwa analia machozi!!
"Scola ume...umesema u... unanipenda?"
Nilimuuliza kwa sauti ya chini Scola aliyekuwa analia tu machozi!
Nilimkumbatia Scola kwa hisia huku namuomba aseme tena lile neno!
"Scola nambie basi,nambie tena unanipenda sema basi mamaangu,ongea ongea Scolaaaa!"
Machozi yalinitoka kama mvua!kilio cha kwikwi ndicho kilichosikika!
"Nakupenda Masu,usijidhuru sababu yangu sikujua unanipenda hivi!"
"Scola nimeishi kukupenda wewe tu kama mwanamke wa maisha yangu Niko tayari kwa lolote kwako hata ukisema nijiue kwa kuwa umesema wewe ni sitosita!"
Tulikumbatiana maachozi yakitutoka, huzuni yangu iligeuka furaha nahisi hata Scola pia alihisi ivyo japo sina uhakika!
Mapenzi yalichanua kwa kiasi fulani Scola alibadilika akawa ananionyesha upendo na kunijali!
Iliisha wiki nipo mle ndani naenjoi na mpenzi wangu tu!
"Ivi Scola eti hapa ni kwako au?"
"Ndiyo ni kwangu!huamini?"
"Hapana nimeuliza sababu nakumbuka ulisema unakuja kwa dada yako!"
"Ndiyo mwanzo nilikuwa nakaa na dada ila saivi nimehama nina kwangu!"
"Scola umepata wapi pesa za kumiliki nyumba kama hivi kwa miaka mitatu tu?"
"Ooh!Mista Bushman umeshakuwa mpelelezi sasa mi sipendi tuulizane maswali yasiyo na msingi!"
"Nilikuwa nauliza tu lakini!"
"Tangu uje hapa ushamuona mwanaume anaingia humu tofauti na wewe?"
"Hapana!"
"Si tunapika na kupakuwa kila siku,nikitaka unanipa na ukitaka nakupa unakula unasaza?"
"Ndiyo laki.....!"
"Lakini nini?jiamini mwanaume mi naenda zangu jikoni!"
Scola hkunichosha machoni,kwangu ilikuwa kama kadri siku zinavyozid kusonga mbele ndivyo anazidi kuwa mrembo,ananivutia zaidi machoni!
Ndiyo maana alivyosema anaenda jikoni,alipotoka tu na mi nikaunga msafara mpaka jikoni!
Nilipofika sikumuuliza nilimkumbatia kwa nyuma huku mikono yangu ikimchenya mbavuni kwa staili isiyo kera!
Scola alivuta pumzi ndefu kwa hisia Kali kisha akazishusha na kisauti cha kumtoa nyoka pangoni!
"Aaaaassiiiii!!Masu!!!"
Scola aliujua wajibu wake aliushika usukani Sasa akawa ananipeleka anavyotaka!
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu,ngono kila dakika,kila saa na kila siku!
Zikiwa zimebaki wiki mbili tufungue shule Scola alianza tabia zake tena!
Akawa anatoka hata bila kuaga,anachelewa kurudi na muda mwingine analala huko huko!!
"Scola mbona umebadilika tena mpenzi wangu?"
"Kwani nilikuwaje mi ndivyo nilivyo!"
"Saivi unatoka tu hata huniambii na unachelewa kurudi mara unalala huko huko unarud asubuhi!"
"Aah!Sasa unadhani wakati haupo nilikuwa sitoki?kwa hiyo Mimi naishije?Unadhani hii nyumba nimeipata ndotoni?ebhu tuulizane maswali ya kiutu uzima!"
"Scola kwani kazi yako ni ipi?"
"Utaijua tu muda bado,soma ukamkomboe mama yako buuza bamia kijijini?"
Sikupenda alipomuingiza mama yangu kwenye maongezi yale!Japo namkosea lakini nampenda sana mama yangu!
Nilikaa kimya siku hiyo sikula hata chakula alichopika!
Ilifika jioni Scola akajiandaa tayari kwenda kwenye kazi zake!
Nilianza kuwa na mashaka na kazi anayofanya Scola,nilimsikia mara kwa mara aliongea na simu!
Nilihisi Scola hakuwa akienda kazini kama anavyosema,bali anaenda kwa mwanaume mwingine!
Nilianza kufanya upelelezi wangu ambao ulianza kunipa matumaini!
Usiku mmoja nikiwa nimelala Scola alirudi akiwa amelewa sana.
Aliingia chumbani akavua nguo zake kisha akajifunga kanga akatoka!
Alivyotoka hakurudi nilimsubiri sana nikaona nimfuatilie anafanya nini.
Nilifika sebuleni nikawasha taa lakini hakuwepo!
Nikaenda chooni labda kalewa kalala huko hakuwepo!
Ghafla nikaskia sauti kama watu wanafanya mapenzi zikitoka kwenye chumba cha wageni!
Taratibu nikasogea mlango ulikuwa wazi sikutaka kusubiri niliingia ndani moja kwa moja sikuamini nilichokiona!!
Scola alikuwa anaota moto tena,kama kule kijijini!
Mara ya tatu namkuta Scola yuko uchi wa mnyama tena siyo kwamba yuko peke yake,hapana!
Scola alikuwa juu,chini yake kalala mwanaume mwenye kitambi chake!
Siyo kwamba hakuniona,aliniona kabisa ila ndiyo kwanza kama mpira akaufanyia manjonjo akaupandia kwa juu kama yule Morrison wa makesi!!!!
Nguvu ziliniisha kwa yale niliyojionea!
Miguu ikafa ganzi sikuweza kusogea kabisa!
Akili ilisimama mapigo ya moyo yakaanza kutoka kwenye reli!
Scola hakunijali,ndiyo kwanza aliendelea kusaga na kukoboa!
Mkono wangu wa kulia niliuweka kifuani kupima mapigo ya moyo wangu!
Nilitoka nikarudi sebuleni nikijiuliza maswali mengi kama kweli nilistahili yale yanayonitokea!
Japo zilipaki kama siku tano tufungue shule nilisema lazima niondoke zangu!
Niliingia chumbani nikapaki kila kilichonihusu!
Nilitoa kila kilicho changu sebuleni,nikakaa nikisubiri kukuche nirudi zangu shuleni!
Usingizi ulinipitia nilikuja kushtuka Scola anamsindikiza yule jamaa huku wakiagana kwa mabusu mazito mbele yangu!
Waliagana kisha Scola akafunga mlango akageuka kwa nyodo na kanga yake moja akawa anataka kuingia chumbani!!
"Scola!",nilimuita akageuka huku kaubetua mdomo wake juu kwa dharau!!
Nilibaki kimya nikiwa siamini kama ni mimi Masu nayedharauliwa vile!!
"Sema basi nimechoka nataka kulala!",alisema Scola baada ya kuona Niko kimya namuangalia tu!
Nilisimama nikamsogelea mwanamke huyu ambaye sijui mpaka leo kama ni upendo au aliniroga kiasi kwamba nikampenda kupitiliza!
"Scola ni kweli nastahili aya?"
Nilimuangalia kwa macho yenye huruma Scola,nilitaka japo anionee huruma tu japo aniombe msamaha!
Licha ya yote yaliyotokea bado moyo wangu ulikuwa radhi kumsamehe,nilitaka niskie sauti yake tu akiniomba radhi kwa kosa alilofanya lakini haikuwa ivyo,Scola alicharuka akawa kama mbogo aliyejeruhiwa!!
"We vipi mwanaume mzima kutia tia huruma!ebhu nipishe mi nikalale!"
Alinisukuma nikaushika mkono wake!
"Scola mi naondoka zangu!"
Nilijikaza kusema maneno yale,nikijua lazima atashtuka lakini bahati mbaya ilikuwa kwangu!
"Hahahahaaa!Bushman unaondoka? kwani nimekufunga kamba?nikuonyeshe mlango?ok fine njoo huku!"
Scola alinishika mkono alipofika mlangoni akaufungua Kisha akaniletea begi langu!
"Safari njema Bushman!"
Sikuamini kama ni Scola wangu ndiyo amegeuka mbogo namna ile,yaani picha limenigeukia mimi sasa ndiyo nimekuwa mkosaji!
"Scola mi nilikuwa nakutania tu mpe...!"
"Shiiiiiiiiihhhh!ishia hapo hapo!"
Bila kupepesa macho wala kujiuliza mara mbili Scola alinisukumia nje na begi langu kieha akafunga mlango!!!
Nashukuru kulikuwa hakujakucha vizuri,pengine ningedhalilika Sana siku hiyo!
Japo miguu ilikuwa mizito lakini nilijitahid kuubeba mwili wangu.
Nilitembea kama kinyonga aliyejeruhiwa na nyoka mwenye sumu Kali!
Bora ingekuwa tumefungua shule,ilikuwa bado wiki moja nzima!
Nilijuta kukataa kwenda kijijini kwenda kumuona mama yangu kwa ajili ya mwanamke ambaye sasa kanifukuza kama mbwa!
Niliyakumbuka maneno ya mama kuwa hakuna mwanamke atakayenipenda kama yeye duniani!!
Mkono wangu mmoja ulipata kazi ya kufuta machozi yaliyokuwa yanatiririka kama maji!
Safari ilinipeleka mpaka stendi mwananyamala kuna mzee mmoja maarufu alikuwa anauza kahawa pale!
Sikuwa na sababu ya kuwahi kwenda shule,siyo kwamba sikuwa na nauli,hapana sikuwa mjinga koasi icho!
Nilienda pale kuvuta muda kabla sijapanda gari kurudi shule!!
Sikuwa nimewahi kwenda pale,sikuwa shabiki wa vikao vya wazee!
Nilikaa kwenye benchi ambapo niliwakuta wazee watatu pamoja na muuza kahawa!!
"Asalaam aleykum!",niliwasalimia vile sababu wote walivaa vibalagashia!!
"Waleyka msalam!"
Yule mzee muuza kahawa bila kuuliza aliniwekea kahawa kwenye kikombe!
Mada niliyoikuta wanaiongelea wazee wale nilitamani bora nisingekaa pale!
Ilikuwa ni mada iloyolenga maisha yangu kabisa kiasi kwamba nikahisi wananisema mimi!
"Kwa hiyo wewe ulivyomfumania ulifanya nini mzee said?"
"Hahahahaaa!nilifanya uamuzi ambao kila mtu alishangaa!
Kwanza nilimwambia yule kijana avae nguo zake kisha nikamruhusu kuondoka!"
"UKAMRUHUSU???aiseeh mi ningeua yaani kitandani kwangu?aiseeh ningeua zote!"
"Hahahahaaa!pole sana Mwita,ivi unajua kimya ni adhabu pia,tena kubwa kuliko kuua?"
Alisema mzee yule ambaye alionekana mwenye busara sana!
"Na mkeo je,ulimfanya nini?"
"Nilimwambia avae aniandalie maji nikaoge Kisha anipikie chakula ninachokipenda!"
"Haaaaaaaa!!!We mzee Said hauna akili kabisa!!"
"Subiri nimalize hadithi yangu sasa!!!"
"Eeh! Kisha ikawaje!"
"Niliongeza tabasamu kwa mkewangu na mapenzi yangu yote,jambo ambalo lilimfanya kuishi na wasiwasi mawazo yakimsumbua!
Hakula wala kunywa kwa amani tena,alitamani hata nimpige au nimfokee lakini haikuwa ivyo!
Siku moja nilivyorudi nilimkuta mkewangu kajiua kwa sumu!
"Heeee!!"
"Ndiyo maana nakuambia kuna adhabu zinauma kuliko unavyofikria!!"
Sikutaka kusikia stori zao tena,nilihisi nachefuka roho maana nimefumania na nimefukuzwa pia!
Nililipa kikombe kile Kisha nikapanda gari tayari kurudi shule!!
Nikiwa kwenye gari nilihisi mtu ananishika bega langu huku anaita jina langu!
"Masu!"
Nilipanda gari bahati nzuri nikapata siti,nilikaa nikiwa na mawazo tele kichwani!
Ghafla nilihisi mtu ananishika bega huku ananiita jina langu!
"Masu!!!"
Nilishtuka nikageuka sikutegemea kama kuna mtu anaweza kunijua zaidi ya Scola mitaa ile!
"Hee!!Jose!!"
"Yeah nambie Masu!"
Kumbe alikuwa yule rafiki yangu Jose aloyenifundisha kuruka ngome shuleni!!
"Na huku?"
"Nikuulize wewe Masu hii mitaa yetu hii kabisa home siyo mbali na hapa!"
"Dah!Mimi mwenyewe nina shangazi yangu huku,ila nimeona bora niwahi kurudi shule tu naona sielewi kabisa!!"
"Dah!yani unajua tunafanana sana tabia zetu,Mimi pia naenda zangu skonga nyumbani hapasomeki nabaniwa sana sipati hata muda wa kwenda kwa manzi wangu!"
Tulipiga stori mbili tatu,moyoni nilifurahi kupata mwenzangu tutakayekuwa wote bwenini!!
******************
Tulifika shuleni moyoni nikiapia kuwa mpya!
Sikutaka mambo ya ajabu tena,mapenzi niliyoyapa kipaumbele tayari yameshanichapa pigo!!
Nilifika bwenini nikaenda kwenye droo langu la madaftari!
Nikaanza kukagua madaftari yangu ambayo niliona mapungufu mengi sana!
Kwanza nilikuwa nimeandika notisi chache kuliko wenzangu!
Kuna mambo mengi yalinipita darasani nikiwa bize na penzi la Scola!!
Nilijiona mpumbavu nilikaa peke yangu nikaanza kulia!
Sikuamini kama ni mimi nilikuwa nachezea elimu namna ile!
Elimu ambayo mama yangu anajibana kila siku kuuza bamia na nyanya sokoni ili nisome nije nimsaidie baadae!!
Nilianza kuandika yale yote yaliyonipita nikajitahidi kujifunza kwa bidii kubwa!
Hadi tunafungua shule tayari nilikuwa nimepiga hatua kubwa!
Side alirudi na salamu nyingi kutoka kwa mama!
"Sele ulimwambia nini mama yangu?"
"Masu,wewe ni ndugu yangu,laiti ningemwambia mama yako nusu ya yote unayofanya sijui angejiskiaje?"
"Side!kwa hiyo ulimwambiaje?"
"Nilimwambia umeamua kubaki shule ujisomee!"
Jibu la Side liliniuma sana moyoni, machozi yalinitoka kwa uchungu!
Side alikuwa anajifanya anasomea kijiji basi mimi niliamua kusoma kama nasomea nchi!!
Nilisoma usiku na mchana,nilikuwa nina hasira sana,niliamini ni elimu tu inaweza kubadilisha maisha yangu!
Kipindi kile nilikuwa namuacha Side darasani Ila sasa yeye ndiyo aliniacha darasani!hakuamini!!
Niliacha tabia zote za kipuuzi,sikutaka kujihusisha na mapenzi tena japo wasichana walinisumbua kila kukicha lakini nilishkria msimamo wangu!!!
"Masu aliyekubadilisha ni nani?naona miujiza ujue!"
Alisema Side siku moja tukiwa darasani!!
"Aliyeniharibu ndiyo kanibadili Side!!"
Nilimjibu hivyo nikiamini aliyeniharibu ni Scola na penzi lake,lakini aliyenibadili ni Scola na usaliti wake!
Niliyaweka mapenzi kando,japo kuna muda nilimkumbuka Scola ila nilijikaza nikiamini siyo chaguo halisi la moyo wangu!!
Maana tangu nimempenda hakuna nilichopata ni maumivu tu!!!
"Nilikuambia Masu,wewe ni genius unaona sasa ulichotufanyia!"
Alisema Side baada ya matokeo kutoka huku nikiwa nimewazidi mbali wenzangu kwa alama za juu kuliko wote!!
Huo ndiyo ukawa muendelezo wa kupata matokeo mazuri shuleni!
Hadi niko kidato cha sita bado Masu nilikuwa tishio kwa akili pale shuleni!
Sikulewa sifa licha ya kuongoza kwa maksi za juu lakini bado nilikuwa bize kufukua kitabu!
Siku moja nikiwa darasani alikja mwanafunzi wa kidato cha kwanza akanipa kikaratasi akisema kuna mtu kanipa aniletee!!
Nilikichukua nikiwa najua moja kwa moja ni mabinti wananisumbu,maana tangu nianze kufanya vizuri darasani nimepokea barua nyingi za watoto wa kike wakinitaka kimapenzi!!
Hivyo sikuutilia maanani ujumbe ule,nilimruhusu mjumbe yule kuondoka nikiwa na maana kuwa nitaisoma baadae siyo Sasa!!
Kipindi hicho ilikuwa imebaki miezi kama mitatu tu tufanye mtihani wa mwisho wa kidato cha sita!!!
Baada ya pilika zangu za hapa na pale nilipanda kitandani.
Nikakumbuka nilipewa ujumbe nikauchukua kwenye suruali yangu Kisha nikaanza kuusoma!
Uliandikwa hivi!
"MASU,MY BUSHMAN NIMEKUMISS,TUKUTANE KESHO PALE TUNAPOKUTANAGA PLEASE USIACHE KUJA NITAFADHAIKA SANA!
Mi Mimi SCOLA kipenzi chako!"
Nilishtuka sana sikuamini kama Scola pamoja na yote aliyomfanyia bado alitaka kuonana na Mimi?
Tena kwa barua fupi ya kibabe!angekuwa mwingine angeandika hata kurasa mbili za kuomba msamaha lakini si kwa Scola!
"Ivi huyu ananichukulia ananiweza sana siyo?yani kanisaliti na kanifukuza halafu kirahisi tu nikaonane naye!ataonana na baba yake pumbavu zake!!"
Ile simu aliyonipa kwa ajili ya mawasiliano kipindi kile nilikuwa nimeizima nikaiweka kando kabisa!
Nilichukua nikaiwasha,nilikutana na meseji nyingi sana za Scola!!
Nikajua tu kanitafuta kwenye simu kanikosa sasa kaamua kunitafuta mpaka shule!!
Ile barua ni kama ilikuja na dawa ndani yake,nilijikuta naanza kumkumbuka Scola wangu sana!
Mnara ulikaza ukasimama kwa uchu mkali wa ngono baada ya kukumbuka penzi tamu la Scola!!!
Kidogo kidogo nikajikuta nalegeza msimamo wangu!
Nafsi zikawa mbili zinabishana,moja inakataa nisionane naye,nyingine inaniambia nimsamehe Scola nionane naye!!!
Kesho yake ilikuwa wikiendi,niliamka mapema nikajaribu kushika kitabu niingize japo kidogo!
Bahati mbaya akili yangu haikuwepo tena shuleni,ilimezwa na barua ile!
Scola alianza kunitawala akili yangu tena,ilikuwa ni kama alinifungulia kwa muda tu kabla hajanirudisha ndani ya jela ya penzi lake!
Ilikuwa ni hatari sana kwangu ukizingatia bado miezi michache nifanye mtihani wangu wa mwisho!!!
Nilikuwa na mawazo sana siku hii,moyoni bado nilimpenda Scola!
Ni kama Scola alikuwa amelala tu kwa muda moyoni mwangu,sasa alikuwa ameamka anaanza tena usumbufu wake!!
INAENDELEA

0 Comments