Sikupata nafasi ya kwenda Dar,mjomba ndiye aliyeenda Mara kwa mara!!!
Baada ya kufanya kazi miezi sita nilikuwa tayari na mtaji wa kutosha!!
Niliamua kuacha kazi nikaanza kununua madini kutoka kwa wachimbaji wadogo Kisha nayasafirisha!!
Siyo hilo tu pia nikajishughulisha na kilimo cha biashara!!
Mungu alinibariki biashara zangu zikaenda vizuri!
Mtaji wangu ukakua mara kumi zaidi,faida ikaingia kila siku!
Kwa mbali nikaanza kuziona ndoto zangu zinaenda kutimia!!
Mwaka mmoja tu baadae nilikuwa miongoni mwa matajiri wachache vijana Tanzania!!
Nilifungua kampuni iliyojihusisha na kununua korosho,Kisha kuzisafirisha nje ya nchi!
Nilijenga nyumba yangu kubwa maeneo ya Mbagala Kijichi nikamiliki gari kadhaa!
Tabia yangu kuchepuka na Scola iliendelea,tuliendelea kukutana kwa siri!!
"Ivi maisha Aya mpaka lini?"
"Kwanini Masu!!"
"Scola wewe huwezi nigeuza mimi mchepuko wako!"
"Sasa unataka nifanyeje jamani!!"
"Muache mjomba uje uishi na mimi!ulitaka pesa ninazo saivi unataka nini kingine Scola!"
Huo ndiyo ulikuwa mgogoro wangu na Scola,sikuweza kuvumilia kumuona aliendelea kuishi na mjomba wangu!!
Scola ni kama kitu alikipanga kukifanya maana licha ya kumbembeleza sana bado aliendelea kuishi kwa mjomba huku akitaka tuendelee kufanya uhusiano wa Siri!!
Siku moja nikiwa ofisini kwangu,mjomba alinipigia simu!
"Haloo Mjomba!"
"Naam mjomba shikamoo!"
"Marhaba mjomba,Sasa kuna jambo moja tulilisubiri kwa hamu Sasa naona ni muda muafaka!"
"Jambo gani mjomba!!"
"Ni kuhusu kufunga ndoa mjomba,nadhani mwezi ujao nitafunga pingu za maisha na kipenzi changu Princess!!"
Taarifa zile zilinishtua,yani mjomba anataka kumuoa Scola!Nilikata simu huku jasho linanitoka,nililegeza tai maana niliona inanibana nashindwa kupumua!!
Niliona haiwezekan kabisa!!!
"HAIWEZEKANI SCOLA NI WANGU,HUWEZI KUMUOA SCOLA HUWEZI LABDA MWINGINE SIYO SCOLAAAA NOOO!!"
Nilijikuta nimeropoka kwa sauti kubwa hadi sekretari wangu akaskia!!
"Boss kuna nini!!!???"
Nilichanganyikiwa! Sikuwa tayari kumkosa Scola maishani mwangu.
Nilichukua simu nikampigia Scola lakini namba yake haikupatikana kabisa!!
Kati ya taarifa mbaya nilizowahi kupokea nadhani hii imo kwenye tatu bora ya habari zangu mbaya !
Kumuona Scola anaolewa ni jambo ambalo sikulikubali kabisa!
Tena mbaya zaidi anaolewa na mjomba wangu, hapana haiwezekani!
Ofisini palikuwa pachungu siku ile,hakuna nilichoshika kikaenda sawia,akili yangu ilipagawa!
"Najiskia vibaya kila unachoweza kufanya utafanya vinavyonihitaji mimi ntafanya siku nyingine siko vizuri!"
"Sawa,pole sana boss!"
Sikumjibu,niliubamiza mlango wa ofisi nikaenda kwenye maegesho ya magari nikajipakia kwenye ndinga yangu ya kifahari nikarudi nyumbani!!
Maisha yangu yalikuwa yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana!
Pesa ilinitakatisha,sikuwa Masu yule tena,nilikuwa Masu mwingine kabisa,kilichonisaidia ni kuwa nilijua kuzitumia fursa na kujiongeza!!
Nilifika nyumbani,nikaingia moja kwa moja chumbani,hata mfanyakazi wangu wa ndani alinishangaa sikuwa mchangamfu kama siku zote!
Niliitafuta namba ya Scola bila mafanikio,niliona kama dunia nzima nimebebeshwa kichwani!
"WHY MEEEE!!!",
Nilipaza sauti kwa hasira huku nikivuruga vitu vilivyomo chumbani,nilichanganyikiwa!
Hakuna nilichokula kikapita siku hiyo,usingizi nao ulinikimbia!
Nikabaki na kazi ya kuzungusha macho huku na kule kama mgeni ndani ya chumba kile nilicholala kila siku!!
Sikuona faida ya pesa bila furaha,kwangu niliitafuta pesa ili mama yangu afurahie matunda yangu na hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa!
Kwani sasa kijijini mama yangu anaishi kama malikia,nimemjengea nyumba nzuri na pia nimemfungulia biashara ya duka kubwa kuliko maduka yote kijijini!!!
Lakini pia niliitafuta pesa ili niishi na mwanamke ninayempenda,na si mwingine ni Scola!!!
Mapigo ya moyo wangu yanadunda yakiimba jina la Scola kila uchwao,jinsi navyoivuta pumzi na kuitoa ndivyo navyozidi kumpenda Scola!
Mawazo yalikuwa mengi,kila simu ikiita niliangalia japo nione kama ni Scola ananipigia lakini hakuwa yeye!!
"Masu uko wapi rafiki yangu!"
"Niko nyumbani!"
"Njoo tukutane pale mtakuja bar kuna mchongo wa hela mshkaji wangu!"
"Hapana siko poa mshikaji wangu!!"
"Masu,leo we unakataa fursa,mzee wa fursa una nini leo?"
Nilikata simu,kwangu ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa!
Sijui usingizi ulinipitia sangapi,nilikuja kushtuka alfajiri simu yangu ikiita!!
Sababu ya usingizi nilipokea bila kufumbua macho!
Sauti niliyoisikia ilinishtua sana,haraka nikaamka nikakaa huku nikiwa siamini!
"Scola!!!"
"Masu!!"
"Nimekutafuta kweli mbona ulizima simu mpenzi!!"
"Tuachane na hayo Masu nina habari mbaya!!"
"Nilishaziskia Scola,mjomba kaniambia mwezi ujao mnafunga ndoa!!"
"Masuuu,acha papara hizo habari njema nina habari mbaya!!"
"Kuna nini, una mimba?ni yangu?au ya mjomba?"
"Mjomba wako amefariki!!"
"Unasema kweli!!!???"
"Ndiyo Masu!!"
Sijui kwanini nilionekana kufurahia habari zile,Ila nilijikuta ninatabasamu tu!!!
"Kwani si alikuwa mzima?"
"Ndiyo daktari anasema ni presha tu!"
"Okay mi ntakuja hapo muda si mrefu pia ntawataharifu ndugu tukutane tufanye mipango ya mazishi!!!
"Sawa Masu!!"
Mazishi yakifanyika huku kila mmoja akiamini mjomba John alifariki kwa presha!
Baada ya mazishi,ndugu tulikaa ili kujadili Mali za marehemu,lakini jambo la kushangaza Scola alikuja na karatasi zote zikimuonyesha yeye ndiye mmiliki wa mali zile na si mjomba!
"Samahani unamaanisha wewe ndiye ulikuwa mmliki wa mali au marehemu alikubali ubadilishe majina na hati za mali zake?",mama alimuuliza!!
"Mimi ndiyo mwenye mali ndugu yenu nilikuwa namfuga tu!!"
"Haa!we mtoto muogope Mungu,we siumetoka kijijini juzi tu hizi mali umetoa wapi?"
"Mama lakini yawezekana kweli!!"
"Kelele unamtetea huyu kahaba?na ole wako nikuskie una mahusiano na huyu mwanamke Masu ntakulaani,atakuwa kamuua na Kaka yangu kwa tamaa ya Mali!"
"Usiniite kahaba,Kaka yako alinipenda hivyohivyo!!"
"Wewe ni kahaba,umetoka na mwa....!"
Mama ni kama alitaka kumwaga mtama kwenye kuku wengi,alitaka kusema kuhusu mahusiano yangu ya zamani na Scola!!
Kikao kilivurugika,hakuna aliyeamini kuwa mjomba John hakuwa na nyumba eti alifugwa!!
Hata mimi nilijua Scola atakuwa amefanya umafia kwenye kifo cha Kaka!
Baada ya kikao mama aliniita pembeni akaniambia!!
"Mwanangu kila mwanamke saivi anakuona wewe kama wewe ni mwanaume wa ndoto zake!unajua kwanini?"
"Hapana mama!"
"Sababu wewe ni tajiri,jichunge usianguke kama mjomba wako,kukosea chaguo ni kukosea maisha.
Ni mara mia kupotea njia utaelekezwa,lakini ukipotea penzini ni umepotea mwanangu, huyu mwanamke ni shetani nina wasiwasi kamuua Kaka yangu,kaa mbali naye!"
"Sawa mama,nimekuelewa!!"
Mama aliondoka na ndugu wengine pia waliondoka!
Bado maneno ya mama yalikuwa na nguvu moyoni!
Niliamua kukaa mbali na Scola,sikutaka kumuangusha mama yangu!!
Ilipita wiki nzima nikiwa nimemkaushia kabisa Scola sikumtumia meseji wala kumpigia simu!!
Siku moja nikiwa nyumbani nimepumzika sina hili wala lile Scola alinitumia meseji!!
"MASU,NAKUJA KWAKO LEO!!NIMEMISS JOTO LAKO MPENZI NA VILE UNANIPATIAGA WE MWANAUME KIBOKO YANGU KABISA!!!"
Kama kawaida,meseji ile iliamsha hisia zilizokuwa zimelala!
Nikajikuta natamani kuijibu lakini nikifkria maneno ya mama nashindwa vidole vinatetemeka kwa hofu!!
Nikiwa bado najifkiria nijibu nini Scola alituma meseji nyingine!!
"NIJIBU MASU AU NITAFUTE MWINGINE!!"
***********
Nilishtuka kauli ya Scola kuwa kama sipo tayari atafute mwanaume mwingine sikukubaliana nayo!!
Sikuwa radhi kumuona Scola akitoka na mwanaume mwingine tena katika maisha yangu!
Nilikuwa tayari kumpa chochote ili mradi tu hasiondoke kabisa mikononi mwangu!!!
"NJOO SCOLA UTANIKUTA MPENZI!"
Maneno ya mama yalifutika kabisa kichwani,nilikuwa radhi nimkosee mama yangu lakini sio kulikosa penzi la Scola!!
Mapenzi yana nguvu sana,ukipenda unakuwa chizi!
Hakuna mtu anajiona yuko sahihi kama mtu aliyependa,katika wakati huu hata umwambie nini hawezi kukuelewa!!!
Hakuna binadamu mbishi kama aliyepotea penzini,unaweza kumwambia hii ni rangi akasema hapana haya ni maziwa!!!
Scola alikuja nyumbani nikamkaribisha nikiamini sasa ni muda muafaka kabisa wa mimi na yeye kufurahia mapenzi yetu!!
Maana kama pesa ninazo na yeye pia anazo!!!
Naam ukurasa mpya ukafunguliwa,mapenzi yakachanua pika pakuwa!
Haikuwa na haja ya kujificha tena,Scola alipangisha nyumba aliyomdhulumu marehemu mjomba wangu akaja kuishi kwangu!!
Kwa ndugu zangu nilifanya siri kubwa sikutaka hata mama yangu ajue kuhusu jambo lile!!!
Baadhi waliokuwa wanafahamu uhusiano wa marehemu mjomba na Scola walinilaumu na kunipa maneno makali sana!
Baadhi walikuwa rafiki zangu na wengine walikuwa watu baki tu!!!
"Masu lakini huyu si ndiye yule mwanamke ambaye tulimkuta msibani mpaka akagombana na mama yako kisa Mali za mjomba wako?"
Alijiuliza rafiki yangu Patrick ambaye tumefahamiana kutokana na kufanya biashara moja ya madini!
"Patrick umekuja kunichunguza kwangu?au umekuja kunitembelea?"
"Masu una nini huyu ni sawa na mama yako mke wa mjomba wako!!"
"Patrick!stop!"
"Hapana siwezi kukuona unapotea nakuangalia this is too much Masu!"
"Enough!!!!!inatosha Patrick toka nje ya nyumba yangu!!"
"Masu unanifuku.....!!"
"Nimesema toka nje ya nyumba yangu!!"
Siku zote nilikuwa mkali sana nikishauriwa chochote kuhusu Scola!
Niliamini mimi ndiyo nina haki ya kuishi na Scola,niliamini hata mjomba aliniibia penzi langu!!
Nilikuwa kipofu na Scola alikuwa fimbo yangu!
Bado niliendelea kufanya siri mama hasijue kuhusu Scola, watu wote nilikuwa nawakaripia wakinipa ushauri dhidi ya Scola, Ila sikujua siku mama akijua nitamjibu nini?
Scola alitulia akawa mama wa nyumbani,japo alikuwa na safari zake za ajabu ajabu!
Muda mwingine anaweza kutoka kisha anatoa taarifa kuwa hatorudi nyumbani!!
Hilo halikunifanya niache kumpenda Scola,niliamini hakuna mkamilifu chini ya jua ivyo kama niliamua kumpenda basi nimpenda na madhaifu yake!
Siku moja nikiwa sebuleni Scola alikuja akakaa pembeni yangu!
Alionyesha kama hayuko sawa kuna kitu kinamkwaza!
"Masu!",aliniita!
"Naam!"
"Mimi ni nani?"
"Wewe ni mkewangu!!"
"Mkeo unaweza kumficha kitu!!"
"Hapana sidhani!"
"Sasa mbona hunionyeshi hati ya mali zako kampuni na miradi yako mingine!!"
Nilishangaa sana na swali lile lakini sikuonyesha utofauti mbele yake!
Lilikuwa jambo la ghafla lilinipa maswali mengi kichwani!!
"Kwanini unauliza ivyo?",nilimuuliza huku nikimdadisi machoni!"
"Nataka kujua hati zako ziko wapi?"
"Lakini mbona mi sijauliza hati zako ziko wapi na kodi zako unapelekaga wapi?"
"Masu!!umeanza lini kunipeleleza?"
Scola alibadilika akakunja sura yake kwa hasira jambo lililoniogopesha hata Mimi!
Nilitaka kumuuliza kama mimi kumuuliza vile ni kumpelekeza kwa hiyo hata yeye pia ananipeleleza!!
"Sina maana hiyo Scola!!"
"Ila una maana gani??hela zote unazopata bado unaulizia vijisenti vyangu vya urithi?"
"Scola mbona unaenda mbali?"
"Shut up!na nakuapia Masu usiponionyesha au kuniambia hati zako zilipo kuanzia leo hutonigusa chumba chako chumba changu!!"
Alisema Scola kisha akaingia chumbani,sijui ndiyo limbwata au ni nini mpaka leo sielewi kule kulikuwa kupenda gani???
Nilijaribu kuingia chumbani nikidhani labda Scola angebadili msimamo wake lakini mambo yalikuwa magumu haswa!!
Scola alinifukuza kama mbwa kisa tu nimeshindwa kumwambia zilipo hati za nyumba yangu!!!
Nyumba yangu,chumba changu mwenyewe lakini huwezi amini sikuwa na uhuru nayo tena!
Nilianza kulala chumba cha wageni,Scola hakutaka hata nimsogelee!!
Alianza tabia za kutoka usiku anarudi asubuhi akiwa amelewa sana!
Alinifanyia Mambo mengi ya ajabu mpaka nikaona siwezi kuendelea kuteseka kisa hati tu!
Kuhusu hati zangu zote zilikuwa kwa mama,nilifanya vile tangu naanza kutafuta mali zangu, niliamini mama yangu ni mtunzaji mzuri ivyo yeye ndiye ana hati za mali zangu zote kasoro magari mawili niliyonunua hivi karibuni!!
Nilichukua uamuzi wa kumpigia mama,nikimpa taarifa kuwa wikiendi ntaenda kuzichukua hati zangu!
"Mama ntakuja wikiendi kuchukua hati zangu nimezitengenezea kabati imara naimani zitakuwa Salama!"
"Masu mwanangu hata daftari zako hukuweza kutunza sembuse hizi karatasi mwanangu?"
"Hapana mama nimekuwa saivi mama usijali kuhusu hilo,ondoa shaka mama!"
"Sawa!"
Mama alinijibu lakini kishingo upande,hakuonyesha kuridhika kabisa na maamuzi yangu!
Kidogo nilipata matumaini ya kuirudisha amani ndani y nyumba!
Niliendelea kulala chumba cha wageni,Scola alinikazia haswa hakutaka kulegeza kamba,mpaka nikajiuliza ni kwa ajili ya makaratasi yale tu au ni nini??
Siku zilikatika,nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa,kesho yake yani jumamosi ndiyo nilipanga kwenda kijinini kufuata hati ili nimalize ugomvi na Scola!
Siku hiyo nilitoka ofisini mapema nikapita sehemu kwa ajili ya kutuliza akili kidogo maana nyumbani hakukaliki!
Sikuwa mlevi wala mvutaji hivyo nilienda kupunguza mawazo tu kidogo kisha nikarudi nyumbani!
Nilifika mlinzi akanifungulia geti nikaingiza gari ndani!
Sikuamini nilipoingia sebuleni,nilimkuta mama akiwa amekaa ananisubiri kwa hamu huku Scola naye akiwa amekaa kwenye sofa lingine anachezea simu akionyesha kutokujali chochote!!!
Nilihisi kuishiwa ngumu,ndipo nikaamini dunia haina siri!
Nilitamani ardhi ifunguke inifukie au mbingu ishuke inifunike!!
Nilisimama nikaganda kama sanamu,miguu haikuweza kupiga hatua tena,ilikuwa mizito!
Nilitamani ningekuwa muigizaji walau ningejifanya nimezimia!
Nikatamani ningekuwa jini nikapotea ghafla nisionekane!
Ama ningekuwa na uwezo wa kurudisha mshale wa muda nyuma nisiwe nimerudi nyumbani walau wiki nzima,mama angechoka kunisubiri akaondoka zake!!!
Mama alisimama akanisogelea huku ananitizama machoni!!
"Wewe ni mwanangu kweli!!??"
Aliniuliza swali ambalo sikuwa na jibu niliinama chini kwa aibu na aya!
"Nakuuliza wewe ni Masumbuko wangu kweli?"
Muda huo Scola hana habari anachezea simu yake akionekana kuchat na mtu tena anacheka kabisa!!
"Masumbuko!wewe ni wa kutembea na aliyekuwa mke wa mjomba wako,tena kama haitoshi unamuweka ndani kabisa??"
Bado sikuwa na jibu,hakuna siku nilijihisi kuaibika kama ile,japo nilikuwa nimevaa nguo Ila nilijihisi niko uchi mbele ya mama!!!
"Masumbuko nambie ukweli ni wewe unataka hati au huyu mwanamke aliyedhulumu mali za mjomba wako?"
Nikiwa sina hili wala lile Scola akaingilia kati akatia neno!!!
"Sikumdhulum Kaka yako alinipa mwenyewe!!"
"Ssshhiiiiiihhh!"
Mama alimnyamazisha Scola akiweka kidole kimoja mdomoni!
Macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira!!!
"Nikiwa naongea na mwanangu,sitaki kusikia sauti ya ngedere anachonga,hukunisaidia leba wewe naongea na yai langu taga lako ulifanye unavyotaka!"
"Ndiyo lakini usinitaje kwenye.....!!"
"Ivi unajua maana ya kukaa kimya we kidudumtu?unataka kunyamaza kama ulivyomnyamazisha Kaka yangu?sikia binti Nina roho mbaya shetani mwenyewe ananiogopa!!"
Scola aliona hali imekuwa mbaya akatulia kama maji ya mtungini!
"Nimekuuliza wewe Masu ,hati unazitaka wewe au huyu mwanaharamu?"
Kimya changu kilimpa jibu mama,moja kwa moja akajua anayetaka hati ni Scola!
'paaaaaaaah"
Kofi zito lilitua kwenye shavu langu,niliamini kweli mama amekasirika!!
"Nije nikuskie unakuja kwangu unataka hati,utaniambia kama nimekuzaa au ulinizaa!na kingine naondoka ila kama Mimi ni mama yako utamuacha huyu mwanamke Ila kama unaendelea naye basi ulijizaa na ntakupa hongera kwa hilo!!!
Mama aliondoka akaubamiza mlango kwa nguvu kisha akatokomea zake akiniacha nyuma nikimuita bila mafanikio!!
"Mamaa!mama!mama!"
Nilitamani kumkimbilia Ila Scola aliniwahi akanishika mkono!
"Unaenda wapi muache aende!!"
"Scola mama anaondoka!"
"Kwa hiyo unataka umkate miguu au nini??muache aende kwanza katuharibia siku tu!!"
Sikuwa na uhakika kama maamuzi yangu yalikuwa sahihi!!
Nilitamani kumfuata mama lakini mzani ukaegemea kwa Scola!
Scola alikuwa shetani anayeishi kama binadamu, huwezi amini katika hali ile alianza kunipapasa akionyesha wazi uhitaji wa kufanya mapenzi na mimi!!
Ningesema nini unadhani,naanzaje kumpinga Scola?
Kwake nilikuwa bubu nakosa kabisa uwezo wa kusema!
Scola aliujua udhaifu wangu!na alijua kuutumia vizuri!
"Masu nataka!"
Sauti ya Scola ilitoka muda huo mkono wake ukiwa ndani ya boksa yangu!!
"Chu...chu...chukua!!"
Ulimi wa Scola uligeuka mdudu mnyevuaji!
Alijua kuutumia vizuri,ulitambaa mwilini mwangu na kunipa wakati mgumu sana!
Joto la mwili lilipanda msisimko ulikuwa mkubwa sana!
Na vile alininyima haki yangu kwa majuma kadhaa,nilikuwa na hamu Sana ya tendo!!
"Ooohhshhh!oooohh!!oooohhh!!"
Nilijikuta natoa sauti bila kuongeleshwa!!
Sikutaka Mambo mengi muda ule nilimbeba Scola mpaka chumbani!
Kumbuka nilikuwa sijaingia kwenye chumba changu kwa muda mrefu!!!
Hivyo ni kama vile nilikuwa mgeni mle ndani,mazingira yalivyopambwa yaliongeza hamasa na hamu Kali ya ngono!
Nilimbwaga chini Scola ambaye sikutaka autawale mchezo!
Linapokuja suala la maandalizi katika bustani ya huba Masu huwa nakuwa makini kuliko kawaida!
Huwa naamini huwezi shinda mechi bila maandalizi,labda uloge kama yanga siku ile!!
Maandalizi mema yanaleta matokeo mema mchezoni!
Scola hakujua nguo zilitoka sangapi,alijikuta yuko kama alivyotoka tumboni kwa mama yake!!
Muda huo jogoo anataka kufanya majabu yake!
"Aasiiiihhhh!Masuuuuu!taratibuuuu,asiiiiiih!Masu nakupenda!!"
Alilamika Scola jogoo akijifungia bandani!
Kwa hali ilivyokuwa ni wazi kila mmoja alimmiss mwenzie maana siyo kwa utamu wa mechi ile!!
Mechi ilikuwa kali dakika tisini ziliisha zikaongezwa therathini nazo zikaisha bila mshindi!!
Ukafika muda wa penati sasa,ambapo sikutaka kufanya makosa!!
Kila shuti nilihakikisha mpira unaingia nyavuni!
"Masu!"
"Naam!"
"Nakupenda!"
Ilikuwa ni kama mwanafunzi aliyepokea matokeo yake ya mtihani!!
Kwangu ilikuwa kama ndoto bado nilijiuliza ivi Scola alikuwa ananiambia mimi au kuna mtu mwingine alikuwa anaongea naye!!
"Scola unaongea na mimi?"
Swali lile hakulipenda Scola aliniangalia Kisha akanisonya akainuka akaenda zake kwenye kioo akiwa mtupu!!
Moyoni nilijua nina haki ya kuuliza swali lile tangu tuanze mahusiano yetu ni Mimi ndiyo nilikuwa nikitamka maneno yale!
Ilikuwa ajabu kwa Scola maana ni Mara yake ya kwanza!
Scola alikuwa kwenye kioo aliniangalia huku anachana nywele zake!!
Scola hakuwahi kunichosha machoni,urembo wake ni kama ulizidi siku hadi siku!!
Siku zote nilikuwa nasema Mungu alitumia muda wake vizuri kumuumba Scola wangu!
Rangi yake nyeupe,kiuno chake kidogo huku kikibeba mzigo mkubwa ulioleta maana halisi ya umbo namba nane!!!
Nilisimama nikamsogelea Scola huku nikimkumbatia kwa nyuma!
Scola kwa kuniahamasisha zaidi akaanza kuzungusha kiuno chake kama anacheza segele!
Hamasa ile ilitupeleka tena ulingoni,tukaanza kupigana ngumi bila refa!
Afya ya mapenzi yetu iliimarika kwa kiasi kikubwa!!
Sikujua ni kwanini Scola alibadilika ghafla baada ya mama yangu kuja!!
Akaniruhusu nilale chumbani huku akinipa uhuru mkubwa na haki yangu niliipata bila malumbano!!
Kiufupi ilikuwa ni amani iliyonishangaza hata mimi!
Siku moja tukiwa chumbani Scola aliniambia!!
"Baby kuna kitu nataka nikuambie!!"
"Nambie mpenzi usijali!"
"Nataka twende Zanzibar mpenzi hata wiki moja!!"
"Kufanya nini mpenzi wangu!"
"Baby tunaenda kupumzika na kutalii kidogo kupunguza haya mawazo mawazo ya maisha!"
"Sawa basi,tutaenda wiki ijayo!"
Kuhusu kupumzika kwangu niliona ni jambo jema sana!
Maana siku zote nimekuwa bize kutafuta pesa,sijawahi kutenga muda wa kuzitumia!!
Tulienda Zanzibar nakumbuka tulifikia kwenye hoteli kubwa ya nyota tano!!
Mandhari yalikuwa mazuri na yenye kuvutia sana!!
Kilichonishangaza ni mabadiliko ya ghafla ya Scola tukiwa Zanzibar!
Muda mwingi aliongea na simu,tena hakuongea mbele yangu!!
Siku moja nilimuomba twende kuogelea...
"Baby nimemiss kuogelea leo jiandae twende basi!!"
"We nenda tu mi sijiskii kutoka leo!!"
Sikuwa na sababu ya kumlazimisha niliinuka nikajiandaa nikatoka nikimuacha kajilaza kitandani!!
Nilifika mpaka beach,kulikuwa na watu wengi hasa wazungu na waafrika!
Ila kabla sijaenda kuoga simu yangu iliita!!
Namba ilikuwa ngeni nilitaka kuipotezea lakini moyo ukasita nikaamua kuipokea!!
"Halooo!"
"Halooo naongea na Masumbuko!?"
"Ndiyo nani mwenzangu??"
"Ni jirani huku kijijini nimepewa namba na mama yako!"
"Kwanini akupe wewe si ana simu!!"
"Kuna tukio limetokea hapa,majambazi yamemvamia mama yako yamemshambulia na kumpiga bahati nzuri leo kulikuwa na ziara ya waziri mchana huu hivyo maaskari walikuwa wengi sana wamekimbia!!"
"Unasema!!!?"
Moyo uliingia ubaridi nikatetemeka kwa hofu,habari ile iliniumiza sana moyo nikajikuta machozi yananitoka bila kutegemea!!
"Kaka huu si muda wa maswali wahi mama ana hali mbaya!!"
"Nakutumia pesa saivi mpelekeni hospitali!"
"Tayari yuko hospitalini Ila kwa hali ilivyo anahitaji uangalizi mkubwa!!"
Hakukuwa na hamu ya kuogelea tena,nguvu ziliniisha nikakaa chini kwenye mchanga!!
Watu waliokuwa wanaogelea na kufurahi niliwaona kama wananicheka mimi!
Sawa,nilikuwa mtukutu na mkaidi mbele ya mama yangu,nikichukua maamuzi ambayo hakukubaliana nayo,lakini haikumaanisha kuwa sikumpenda!!!
Niliinuka nikaanza safari ya kurudi hotelini ili nikamwambie Scola supu imeingia nzi!
Nilifika hotelini nikapanda lift mpaka ghorofa namba tatu ambapo ndipo kuna chumba chetu!!
Nilifika mlango wa chumba changu nikashika kitasa mlango ukakubali!!!
"Hamadi!!!!"
Sauti ilinitoka bila kutarajia,macho nikayakodoa kama chura aliyebanwa na mlango, mdomo ukawa wazi kwa mshangao!!
Lilikuwa fumanizi la nne katika maisha yangu,na fumanizi zote nilikuwa namfumania Scola mwanamke wa maisha yangu!!!
INAENDELEA

0 Comments