Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Mke wa Bosi sehemu ya saba



Ukisomeka hiviii "HATUJAMUUA ILA TUMEMZUIA TUU AJIFUNZE NA AJUE KUCHEZA NA VIJANA CYO DILI" Mhhh niliguna kwa mshangao nisielewe nini cha kufanya.


Nikampigia tena mama simu ilikua haipatikani. Nikaamua kumpigia mzee ambaye ni boss wangu. Alipopokea simu nikataka kujua hali ya mama kwanza. lengo ilikua ni kumzuga mzee kama vile sijui safari ya mama. Cha ajabu yule mama aliaga kuwa anaenda Dar. Nikamwambia "mzee hebu jaribu kuwasiliana naye". Akajibu "sawa". Baada ya muda akanipigia simu akasema "simu zake zote hazipatikani".


Sikutaka kumshtua nikamwambia" haina tabu mzee"

akajibu "sawa lakini vipi mnarudi lini?"

nikamjibu "wiki ijayo".

Nilivyokata simu mlango wangu ulisukumwa kwa kasi ya ajabu sana. Nilishtuka kumwona Angel anaingia kwa fujo vile kisha akasema

"Yuu sina utani na wewe naomba Line yangu ya Simu". Nikaona nijibalaguze kwa kusema

"samahani Angel nilichukua kwa sababu line yangu ilikua haina hela".

Akasema kwa sauti ya ukali " nipee!! Nyangau mkubwa we" basi mi nikaifungua simu ili nimpe.


Ghafla Jane akaingia na kusema

"vipi humu ndani kuna nini kinaendelea". Angel akasema

"si huyu malaya wako anafuatilia mishe zako sasa sijui atafaidika nini?" Nilijisikia vibaya sana kuitwa malaya. Basi Jane akasema "kwa hiyo vipi tumuonyeshee kazi?" Angel akajibu "afunzwe adabu." (Mwanadarubin wetu: bro kimbiaa hii Mara ya mwisho kukunongoneza)


Haaaaaaa kusikia vile niliangalia usawa wa mlango nikatoka mbioo za ajabu. Sikumbuki jinsi gani nilizipangua ngazi za ghorofa nilijikuta nimefika chini na kuingia barabarani bila hata kugeuka nyuma. Nilikimbia nisijue pa kuelekea nikiwa ugenini. kizuri ni kwamba nilifanikiwa kukimbia na zile simu mbili za Jane na line ya Angel ikiwa katika simu yangu.

Nikakimbia hadi sehemu moja ambayo mpaka leo sijui inaitwaje ila ilikua ni msitu fulani, labda wakazi was Arusha watatuambia kwenye comment.


Baada ya kujihakikishia usalama pale nikaamua kumpigia simu mzee ambaye ni boss wangu. Nikampigia na kumwelekeza ya kuwa Jane si mtu mzuri na kumsimlia matukio yote. Basi alikua kama aliyechanganyikiwa kiasi mi nikakata simu na kuanza kufikiria jinsi ya kurudi Mbeya. Niliinuka pale chini ya mti nilipokuwepo.


Nikaamua moja kuwa niende kwanza polisi ili nikawataarifu polisi juu ya uharamia wa Jane wa kuwaua watu ovyo. Kisha niuze simu moja na kurudi Mbeya. Kwa kuwa nilishatambua kuwa nimeingia kwenye vita ambayo ilikua pengine hainihusu. Nikaamua kua tayari kupigana na kutetea nafsi yangu na nafsi za wengine waliokua kwenye orodha ya kuuwawa na Jane.


Nililala kwanza porini usiku ule asubuhi nikawahi kituo cha polisi. Nikawaeleza kila kitu kisha wakaniuliza " je una picha ya huyo mtu"

nikawajibu "ndio nikatoa simu na kuwaonyesha".

Basi wakaomba niwarushie kwa njia ya "Bluetooth'' nami nikafanya hivyo. Baada ya kumaliza wakati natoka pale kituoni nilifika barabara kuu na kushitushwa na pikipiki aina ya bajaji ikinifuata.


Ilifika na kusimama pale nilipo dereva akaitoa ile helment kichwani nikaona alikua ni dada mzuri sana. Akanisalimia "vipi kaka Yusuph?"

Nilishtuka na kumwangalia labda namfahamu lakini hakuna. Nikamwuliza " umenifahamia wapi?"

akajibu kwa kusema "nina mzigo wako"

akanipa bahasha ndogo ikiwa imefungwa. Kisha akawasha pikipiki na kuondoka kwa fujo sana.

Nilimwangalia hadi akapotea kisha nikaifungua ile bahasha na kukutana na barua fupi yenye ujumbe huu


?? "YUSUPH NAJUA UMESHAJUA SIRI ZANGU NAKUONYA KAA KIMYA HUJUI SABABU YA KWANINI MIMI NAUA KWA USALAMA WAKO ACHANA NA YASIYOKUHUSU ILI USALIMISHE MAISHA YAKO BY JANE" ??


(Mwanadarubin wetu: Ooh na ndo uko mjinga umeenda ambia police tiari unalo mzee baba)

Nilijikuta naishiwa nguvu na kulegea miguu. Nikiwa nawaza nifanye nini simu yangu ikaita nikaipokea na kusikia sauti ikisema


"polisi ni kazi bure acha kupoteza muda wako yusuph". Simu ikakatika, nilijiuliza amejuaje kwamba nimeenda polisi ama wananiona..?. Nilikua nimeanza kuhisi kifo kinanifukuzia kwa nyuma tena kwa kasi ya ajabu. Nikavuka barabara na kushika upande wa pili wa barabara.

Lakini kuna kitu nilihisi ila nikasema ngoja nizuge kwanza. Nilihisi kuna njemba mbili zilikua zinanifuatilia nyendo zangu. Niliwaona wakiwa na bastora viunoni mwao zikiwa zimezuiwa na makoti ya suti.


Kwa kuwa niliwaona nikapunguza mwendo nao wanapunguza. Na nikiongeza nao wanaongeza. Suluhisho ilikua ni kujitoa muhanga kufa na kupona ili kuwadhibiti wale jamaa. Nikaamua kuelekea kwenye msitu uliopo nyuma ya jengo la EAC (East African community) Arusha. Hapo ndipo nilipothibitisha kuwa wananifuatilia kwani walikua bado wanakuja nikaanza kukimbia nao wakawa wananikimbiza hadi katikati ya msitu kisha nikasimama na kugeuka. Walikua tayari wametoa bastora zao na kuniweka mtu kati kisha mlio ukasikika paaaaaaah...



TULIPOISHIA.....

Mlio ukasikika" paaah"

ilikua mlio wa risasi ambao ulitokea nyuma na kumpiga mmoja wa wale jamaa wawili. Alikua ni afande mmoja wa kike nilimkuta kituoni kumbe wakati naondoka alihisi kuwa hakuna usalama. Hivyo aliamua kunifuatilia kwa nyuma. yule mwingine akiwa amegeuka ameduwaa kuona mwenzie kauawa basi mimi nikamfuata kwa nyuma nikamtwisha bonge moja la ngumi ya kisogoni.


Aliyumba kidogo nikarusha teke la nguvu kwenye mkono wenye bastora ikadondoka. Nikaiwahi kisha nikamweka mtu kati. Basi afande yule wa kike akapiga simu kituoni kuomba msaada.


Basi baada ya mda wakafika wakawachukua wale watu hadi kituoni. Mmoja akiwa ameshakufa. Mwingine ilikua kwa ajili ya mahojiano. Baada ya kufika kituoni mara moja mahojiano yakaanza. Cha ajabu yule jamaa alikua hasemi chochote. Alipigwa na vitako vya bunduki kichwani lakini wapi.


Ghafla ilifika gari moja ndogo aina ya Cresta. Alishuka dada mmoja ambaye sura ilikua ngeni machoni pangu. Lakini mwendo ulikua ni wa Jane. Basi wakati nataka kuwambia polisi wajihami alirusha kitu kama kigorori kidogo mle ndani kisha kikalipuka na kutoa moshi. Ule moshi ulifanya watu wasione chochote kiufupi ukiathiri macho yetu wote tulipoteza nuru ya macho. Kila mtu alilalamika macho yangu, macho yangu huku tukiyafikicha. Baada kama ya dakika 10 hivi pakawa shwari.


Cha ajabu yule maiti na yule mwenzie hawakuonekana na lile gari halikuwepo. Polisi wakachanganyikiwa sana. Pia baadhi ya nyaraka muhimu zilibebwa. Wakiwa wanalaumiana kwa uzembe simu ikaita mle ndani. mkuu wa kituo akapokea na kuiweka loudspeaker. Tulisikia sauti ya ukali ikisema

?? Kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi mnatakiwa ofisi za TAMISEMI maafande wote wa kituo hicho ??

Simu ikakatwa.


Mkuu akasema taarifa tayari zimemfikia waziri wa ulinzi na usalama. Pale pale ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu.

Ujumbe ulitoka kwa Jane nao ulikua unasema


?? Pole sana Yuu unacheza na moto bora uache ??


Nilishtuka kiasi nikaamua kuondoka pale kituoni. Lakini nikiwa naondoka niliitwa na afande mmoja akasema

kama kutakua na chochote basi niwape taarifa kisha akaniachia namba ya simu. Kwa kuwa nilitaka kujua mama yule mke wa boss yuko wapi nikaamua kwenda kufuatilia ofisi za mtandao wake. Lengo ilikua nijue namba yake inasoma "Location" wapi.


Basi baada ya kufika ofisini nikajitambulisha na kuwaonyesha Rb ya polisi. Kisha wakanielekeza chumba cha injinia wa mawasiliano. Nilimweleza shida yangu kisha akakubali kunisaidia. Akabofya bofya pale Computer yake kisha akasema taja namba. Nikataja baada ya sekunde kadhaa akasema hii Namba inasoma Iko sehemu moja inaitwa ""Mwanga""

kisha akanipa Latitude na Longitude na zaid akaiprint ramani kunifikisha inaposoma ile line. Bila kupoteza muda nikaondoka na kuanza safari ya kuelekea huko. Kwa kuwa niliuza simu moja ya Jane kwa gharama ya Laki tatu hivyo nilikua na kiasi kidogo cha pesa. Nilipanda gari hadi eneo lile kisha nikashuka.


Baada ya kuangalia location nilishtuka sana maana pale ilikua ni msituni. Nikaangalia na kuona ramani inanielekeza upande wa kasikazini. Nikashika msitu ule na kuanza kuswampa ndani ya msitu.

Nikiwa njiani niliona kitu kama cheni ya shingoni baada ya kuiokota nikaitambua ile cheni. Kutokana kidani chake ndani kilikua na picha mbili ukikifungua. Nilipokifungua nikaona picha ya mama upande mmoja na ya baba yani boss wangu upande wa pili. Nikajua tayari niko eneo hatari. Nikaanza kuchukua tahadhari na kujihami kiasi.


Nikaiangalia ramani na kuona zimebaki mita mia mbili tu kuifikia eneo ambalo line ile ya simu inasoma. Nikachukua tahadhari kwa kujiweka sawa kukabiliana na chochote. Ghafla simu yangu ikaita kucheki alikua Jane nikamsikia akisema "Yuu acha kujitesa msituni huko utakufa buree". Simu ikakatika.


Sikujali sana japo nilijiuliza amejuaje niko msituni kule. Nikapata wazo "nimtrace" kwenye GPS nione yuko wapi. Cha ajabu niliona inaonyesha yuko Arusha eneo la Mount Meru Hotel. Nikazidi kuchanganyikiwa na kujiuliza amejuaje niko mwanga.


Basi nikajisemea moyoni potelea mbali liwalo na liwe ila wacha nijaribu kumwokoa Mama yule. Nikasonga mbele zaidi nikifuata ramani yangu. huku kichwani nikiwa na maswali hivi Jane ni nani mbona kuna barua zinaonyesha alikua muuza madawa ya kulevya na baadhi ya "document" zinaonyesha si Mtanzania. Je! na vipi kuhusu wanajeshi wa JWTz wenye uhusiano nae wa karibu? Na pia niliona baadhi ya picha akiwa Jeshini anafanya mazoezi ya kijeshi? Jane ni nani.? Maswali yote nilikua najiuliza huku natembea ghafla nikaona...




TUENDELEE...

Tulimwona mtu kwa mbele akiwa amevalia nguo rangi nyeusi na kugekia kwa mbele. Kizuri ni kwamba hakuwa ameniona.


Nikaamua kumnyatia kwa kuwa nlijua niko eneo hatari. Nikachukua kisu ?? changu na kukishika vizuri mkononi . Nilimkaribia yule mtu na kumshika kichwa vizuri sana.

Nikambana kisawasawa na kumwuliza ni wapi alipo mama yule. Alipomaliza kunielekeza kwa sauti ya kukatakata kutokana na kumbana sana shingoni. Nikaona hapa ni unyama tu hakuna kuremba.


Nilimtia kisu ?? yule jamaa shingoni kisha nikatenganisha kichwa na kiwiliwili chake. Nikamtupa pale na kusonga mahali nilipoelekezwa.

Ile Nakaribia nilipigwa teke nikaanguka chini wakati nataka kunyanyuka Nikawaona wanaume wawili waliojazia miili yao haswaa.

Nilichomoa kisu ?? kimya kimya na kumtia mmoja mguuni wakati anashtuka nikainuka na kumtia wa pili shingoni. Kisha nikamgeukia wa kwanza na kumwongezea tumboni. Nikaona nimewamudu kwa mbele wakati nasimama nikamwona yule mama akiwa amefungwa na watu wengine kama nane hivi.


Basi kwa kuwa walikua wamefungwa kwenye miti nikafungua na kuwapa pole. Walinishukuru sana hasa yule mama yangu. Alionyesha wazi hajui kama Jane ndo kahusika na utekwaji wake. Kwani alikua anaulizia "Jane hajambo?" Nikamwambia mama hili ni eneo hatari tuondokeni. Basi tukatoka pale baada ya kufika barabarani tukakubaliana tukalale Moshi.


Tulipanda ?? gari hadi Moshi tulilala pale kwenye Guest house moja hivi. Usiku tuliongea mambo mengi sana ila baadhi ya watu wale ilionekana ni viongozi wa vyeo fulani. Lakini baadhi walionekana ni maafande nilihisi hayo baada ya kuwa wanaongea na simu.


Basi sikutaka kuwadadisi japo nilikua nawaza kwanini Jane anawaandama sana Maaskari. Zaidi kwa nini anawaanda viongozi wakubwa wakubwa tena wenye vyeo haswaa hapa nchini kwetu. Nikakosa majibu ya ukweli. Basi wale wengine wakaniomba namba ya simu na kuniambia watanitafuta wana shida sana na mimi. Tuliongea mambo mengi sana na wale watu kisha tukalala.


Gari ya mama iliporwa kwa hiyo ilikua haijulikani iko wapi.Tuliamua asubuhi turudi Mbeya kwani nilishamwelekeza baadhi ya uchafu wa Jane. Mama yule alionekana kushangaa tu. Asubuhi tukapanda Bus ?? La Mbeya huku mama akiwa amenihakikishia kuwa tayari katoa taarifa polisi hivyo muda wowote Jane atatiwa nguvuni.

***


Baada ya kufika Mbeya saa nane usiku tulishitushwa na hali tuliyoikuta nyumbani. Ilikua watu wengi wamekusanyika usiku ule tena wakiashiria majonzi ??. Tulizidi kusogea ndipo mama akaamua kumwuliza mtu mmoja kwamba ni nini kinaendelea pale. Tukajibiwa kuwa kuna majambazi wa kike watatu walivamia pale na kuwaua watoto wawili wa mzee yule. Yaani Zuena na Yule wa kiume mdogo hivyo Happy ndo pekee aliyebaki.

Mama alishtuka sana akaanguka na kuzimia palepale.


Wakati anapewa huduma ya kwanza simu yangu ikaita cha ajabu ni kuwa sikuwa naiona namba. Niliogopa sana ila baada ya kuipokea nikaisikia sauti ya Jane ilisema


?? "Yuu huo ni mwanzo mpenzi wangu. Its better ukikaa mbali na vita hii"??. Nilishtuka sana kisha simu ikakatika.


Nikajiuliza ina manaa Jane ndo ameua watoto wa boss? Niliumia sana kiukweli na kujiuliza kwanini Jane anaua watu hovyo? Je! haoni kama nao ni binadamu au ni raia wenzake. Tuliomboleza usiku ule hadi asubuhi. Ikafanyika mipango ya mazishi tukawazika wale watoto. Lakini wakati tunarudi nyumbani kutoka makaburini kuna mzee mmoja akanifuata na kunambia

""kijana nina maongezi na wewe"". Nikamkubalia kisha tukatafuta sehemu tukakaa ilikua ni porini kidogo ikumbukwe tulitoka makaburini.


Baada ya watu kutupita wote yule mzee alianza kwa kusema ""Kijana mimi naitwa mzee Mwang'ondya sidhani kama utakua unanifahamu"".

Nikamjibu ""sikufahamu mzee wangu""

akasema ""sawa ila mimi nakufahamu vizuri sana""".

Nilishtuka kidogo yule mzee akazidi kusema ""mimi nilikua rafiki wa marehemu baba yako". Haaa hapo palikua patamu ilikua ni kitu nakisubiri siku nyingi sana.

Mzee akasema "niliwatafuta siku nyingi sana. Nyinyi mlizaliwa watatu. Mnadada yenu mmoja ambae hadi sasa sijui aliko japo niliwahi kusikia kuwa alikua Afrika ya kusini na baadae akaja Congo ila kwa sasa sijui aliko. Wa pili ni wewe ambae Allahamdulillah nimekuona. Watatu ni wa kiume pia huyo ninae Nyumbani. Na picha za dada yenu ninazo nyumbani. Akazidi kusema baba yenu na mama yenu waliuawa na...



Majambazi, sababu inasemekana kuna mtu ambaye alikua ni kiongozi serikalini aliwatuma waje waue. Katika tetesi ilisemekana nyinyi mlichomwa sindano za sumu ya kupoteza kumbukumbu ya ubongo. (wale wa biology na madaktari wanajua ni ubongo upi nausema)


Basi mzee akasema hali hiyo iliwafanya kutotambua lolote baada ya kumbukumbu kurejea. Kwa kuwa nilimsikia mzee akisema dada yangu aliwahi ishi Afrika ya kusini na pia Congo nikahisi huenda Jane ni dada yangu. Nikaona nimwambie yule mzee anipeleke kwake nikaione hiyo picha. Basi bila tatizo yule mzee akainuka na tukulaanza safari kuelekea kwa mzee yule. Sikujari habari za msiba ule tena wa pale nyumbani.


Tulifika kwa Yule mzee akanitolea mapicha mengi sana. Picha ya kwanza ilikua ni ya marehemu baba yangu. Niliangalia kwa makini sana nikawa kama naifananisha na mtu fulani. Sikutaka kuonyesha "doubt" palepale nikakaa kimya ila nikanote kitu. Picha nyingine ilikua ya mama yangu kiukweli chozi lilinidondoka kumwona mama. Picha nyingine ilikua ya dada yangu. Nilimwangalia kwa makini sikuona kama ni mgeni sana nachoni pangu. Nilivuta picha nilimwona wapi. Hatimaye nikakumbuka niliwahi kumwona kwenye picha za Jane kule hotelin akiwa amewekwa alama ya mkasi. Na kwa nilivojua Jane ukiwa kwenye orodha ya watu wanaotakiwa kuuawa unawekwa mkasi. Nikawaza ina maana Jane anataka kumwua dada yangu.


Palepale akili iliniruka nikajikuta kwa hasira na gadhabu natamka kwa sauti kuu """Jeeeeeeeeeeniiiiiiiiii!!!!!!!!!"" Machozi ya uchungu yakanitoka. Nilijikuta namchukia Jane na kuongeza mori ya kupambana naye. Sikujua naanzaje ila nilijiapiza kumwua Jane kabla hajamwua Dada yangu.


Japo kwa wakati huo nilikua sijui Dada yangu yuko wapi. Ila hasira juu ya Jane iliwaka ndani ya moyo wangu na kujiona nilikua naishi na kumlea mtu ambae atakuja kuiteketeza damu moja na mimi. Ila kulikua na tatizo lingine yule niliyeonyeshwa kama ndiye marehemu baba yangu nilihisi kuna mahali yupo kwani kama kuna sehemu nilimwona hivi.


Nikamwuliza yule mzee hivi maiti ya baba mlithibitisha kuwa ndie. Yule mzee akajibu maiti ya baba yako ilikua imeharibiwa vibaya na majambazi. Hivyo hata sura yake ilikua haionekani vizuri. Nikaanza kupata picha ya kuwa huenda baba hakufa. Nikajizuia kumwambia yule mzee hisia zangu. Nikamshukuru kwa kunipa sehemu ya maisha ya familia yangu.


Nikaaga kwa yule mzee na kuondoka na zile picha huku kichwani nikijiuliza dada yangu yuko wapi? Nilikaza buti njiani nilikua nabubujikwa na machozi ya uchungu. Nilijiuliza ikiwa yule niliyemwona sehemsehem ndiye baba yangu kwanini siki ile tulipopishana alinipita kama asienijua? Je! kwanini kama alipona asiitafute familia yake? maswali yalikua mengi yaliyokua yanatia uchungu sana. Nikajiuliza pia Jane na Angel walikua wanaua watu wenye vyeo katika Tanzania hii inamana na dada yangu ni mkubwa mkubwa hapa kwetu?


Nilikua natembea kama chizi barabara nzima nikitokwa na machozi yaliyosababishwa na uchungu. Uchungu ulikua unatokana na kuona Dada yangu ambae ndie angekua faraja mpya maishani anataka kuuawa. Nikiwa njiani nikakumbuka sijamwuliza yule mzee juu ya habari ya mdogo wetu aliyekua anaishi naye. Nikasema nitarudi baada ya kujipanga.


Nikiwa natembea huku nikijisemesha semesha mambo mengi sana. Nilishtushwa na mlio wa honi ya Gari ikiwa imetokea Nyuma nikaipisha. Ikanipita na kusimama kwa mbele na nikamwoma mtu ananiita. Nasi nikaenda kusikiliza baada ya kufika nilimwona dada mmoja. Akaniuliza

"" kaka unaelekea wapi?" Nikamjibu

"" huku mbele"" akasema

"" unaonekana una mawazo naomba nikupe lift hadi unapoishia usije ukagongwa na magari ni hatari sana kaka"".

Nikaona si mbaya nikikubali msaada wake. Njiani yule dada alikua anaongea mambo mengi huku akionyesha kunidadisi baadhi ya Mambo. Kwa kua nilikua nimeshaharibikiwa kutokana na hasira niliamua kushuka ila kwasababu nilimtilia shaka nikaamua kumwibia simu yake na kushuka nayo.


Alipoondosha gari simu nyuma ikaingiza ujumbe mfupi wa maneno nao ulitoka kwenye namba ambayo kiukweli nilikua naifahamu sana. Ilikua ni namba ya Jane. Na ujumbe ule ulisomeka hiviiiiiiiiiiiiiii


TUENDELEE.....

?? UNAJIONA MJANJA HUJUI IYO GARI ULOPANDA NDO MM MPENZI WAKO JANE NDO NIMEKUBEBA ??


Nilishtuka sana na kujiona mjinga sana kwani adui kaja hadi mikononi mwangu na nimeshindwa kumkamata. Nilijilaumu sana.

Nikazidi kusonga na safari hadi pale nyumbani kwa boss wangu ambako kulikua na msiba wa wanae wawili. Siku zikasonga msiba ukamalizika mimi kichwani mwangu niliamua mambo mawili. Moja kumwua Jane na wenzake. Mbili kumtafta dada yangu na pia kubwa ilikua ni kumtafta yule mtu niliemwona anafanana na baba yangu.


Baada ya kama wiki kadhaa kupita niliingia porini kujifua kisawasawa nilipotoka huko nikiwa nimejiandaa vilivyo nikaianza kazi.

Kwa kuanzia niliamua kwenda morogoro kwani hapo ndipo nilihisi kumwona mtu anayefanana na baba yangu. Nilifika pale moja kwa moja hadi mtaa wa mazimbu ambako nilielekezwa na wasamalia wema kua anaishi huko. Baada ya kumtafta kiasi bila mafanikio nikaamua kupumzika katika bar moja inayoitwa Makhirikhiri.

Nikiwa nimetulia pale nakunywa soda nilitumiwa sms na Jane ikisema

?? tazama mbele yako ?? .

Nikainua kichwa kutazama haaa nilimwona Jane akiwa amesimama pale na amevalia sare za wahudumu. Huku na yeye akihudumia wateja. Niliinuka kwa hasira na kumfuata wal chaa ajabu yeye hakuonyesha kushtuka hata kidogo.


Kwa kua nilikua na hasira Sikujali watu wala nini uchungu wangu ulinifanya nifanye maamuzi ya ajabu. Nilichomoa kisu na kumchoma Jane shingoni kisha nikachomoa na kumchoma tena tumboni. Kisha nikasikia kelele watu wakisema """"kaua kaua kaua!""" Nilikua nimeridhisha nafsi yangu kwa kiasi fulani. Japo kichwani ilikua swali

"""""kweli Jane ameshindwaje kukabiliana na mimi?"""

Wakiwa raia wameniweka mtu kati nilimwona Jane anapita kwa mbali huku akipunga mkono. Nilishituka nikatumia mabavu kujinasua pale ili nimcheki yule alielala.

Baada ya kumwangalia kumbe alikua amevalishwa sura ya bandia ya Jane. Nilianza kujihukumu kwa kuua nafsi isiyo na hatia. Ghafla polisi walifika wakanichukua na kunipeleka kituoni.

Baada ya kufika nilishtuka kumwona Jane amevalia Sare za Jeshi akiwa ananisubiri. Baada ya askari kushuka wakawa wanampigia saluti na kisha wakanikabidhi mimi kwake. Asikwambie mtu ule ulikua wakati mgumu sana kwangu mimi.

Nikajiuliza

"""" hivi mimi ni nini nafanya mbona naonekana nacheza na mtu hatari sana"""""".

Akaomba askari kadhaa wanipe chai,,,,,,,sio chai unayofikilia ndugu msomaji ila ni(kipigo kitakatifu)

Nilidundwa huku nikigombaniwa kama mpira wa kona. Baada ya mda Jane akasema ""yuu pole sana wewe ni mtoto mdogo sana si vema kuingia kwenye ma game ya uhuni haya".

Kisha akasema ""yule ulomwua pale si mtu ni mdori tuu ila alijazwa damu na akavishwa sura yangu. Na wewe bila kutumia akili umekurupuka. Sasa tunayo haki ya kukuhukumu tuwezavyo ila ilikua onyo ukae mbali na vitu hivi. Kama unaweza kupambana endelea ila sisi tutakuaibisha""". Kisha akaamuru maafande wanitoe pale na kunitupa popote.

Nilitolewa pale na kufungwa kitambaa Cheusi usoni. Nikapandishwa kwenye gari na kusafirishwa kwa umbali mrefu sana. Tulifika sehemu wakanishusha wakaniacha pale wakiwa wamenifunga kitambaa usoni. Nilifanya jitihada za kukifungua kitambaa kile usoni hatimaye nikafanikiwa. Lakini chaa ajabu sikua naona nuru tena mbele yangu zaidi ya giza.

Nilikua nashangaa ni kwanini ila sikua naona hata chembe. Nilihisi kupagawa kwasababu nilikua sijui niko wapi halafu nuru imepotea kwenye macho yangu. Nilijipa matumaini na kukaa pale kua labda ni kwasababu ya kufungwa mda mrefu. Baada kama ya dakika kumi ivi simu mfukoni ikaita. Kwa kua nilikua sioni nikaitoa na kukisia kisia mwisho nikapatia. Ndipo nikasikia sauti ikisema.

"Najua kwa sasa huoni mimi ni Jane kitambaa kilikua na sumu ya kukutia upofu ko umebugi. Kwasasa upo msituni sana na sijui utatokaje. Msaada pekee ni mimi na mimi nimekua adui yako." Nikajikuta napatwa na gadhabu ya kutaman hata kumchinjachinja Jane. Nikajiuliza hivi ni kwanini nateseka bila kipimo. Je ni upumbavu wangu? Kwanini nashindwa kumdhibiti Jane. Nilikua nawaza hayo huku simu ikiwa iko hewani kisha nikamsikia Jane akisema ""pole sana baby wangu""",

""Siku nyingine kabla ya kuvamia vita zisizokuhusu jipange. Nina uwezo wa kukufanya chochote yuu "my love" ila nakuhurumia"". Kisha simu ikakatika. Nikajikuta nanyanyuka kama vile naona na kuanza kutembea ovyo mara nikajikwaa na kuanguka. Nikiwa najiandaa kuinuka nilihisi kama nimeangukia nyoka kwani kilikua kitu laini kwa ngozi baada ya kukipapasa nikahisi nimeshika kichwa maraaaaa...



Gafla nikahisi kujikunja kunja kwa kile kitu ile natoa mkono niligongwa na kitu ambacho kiukweli bila kuona nilijua tuu ni nyoka. Niliinuka ili japo kuponya nafsi yangu nikataka kutoka gafla nikaangukia miti ambayo nadhani ilikua ni miiba kwani nilichomwa sana mwili wote ulikua umelowa damu. Maumivu ya kung'atwa na nyoka na pili kuchomwa na miiba hakika ilikua simanzi moyoni.


Nilimlaani sana Jane. Nikakata tamaa ya kutoka mle msituni maana sikua naona. Nikajisemea moyoni bora kufa. Nilikaa pale huku nikiugulia maumivu makali ya nyoka na miiba. Sikujua ni nini nifanye kwa wakati ule nilikua nimekomeshwa kisawasawa. Basi machozi yalinitoka bila kikomo nisijue nini cha kufanya. Sumu ya nyoka ilizidi kusambaa mwilini kwani nikahisi mwili wote unapata ganzi.


Nilikaa pale hadi pale nikaanguka na kupoteza fahamu. Sijui ni nini kilitokea baada ya pale ila nilikuja kushtuka nikiwa kama kwenye kitanda hivi. Nikainuka mara nikasikia sauti ikisema "pole sana". Nikajibu "Ahsante sana hapa niko wapi?"

Nikauliza. Basi sauti ikasema

"mimi ni mfanyakazi wa Jane na ndio tulienda kukutupa kule ila nimeona ni vema nikusaidie japo kidogo."

Kusikia vile matumaini yalianza kurejea taratibu.


Basi akaendelea kusema

"najua kwa sasa huoni lakini sumu aliyo kuwekea ina madhara kwa masaa 48 Tu. Hivyo kwa sasa jikaze baada ya masaa kadhaa kupita utaona tu bila matatizo. Lengo la Jane ilikua ni kukuonya". Maneno yale yalizidi kunifariji sana. Mhudumu wangu akajitambulisha kwa jina moja Amina.


Nilifurahi sana, Muda ulisonga na masaa yakaenda hatimaye nuru ya macho ikarejea. Nilipata kumwona Amina nikamshukuru sana kwa mema yote aliyonitendea. Akanishauri nisiondoke kwanza hadi niwe sawa yeye yuko tayari kugharamia maisha ya pale nyumbani.


Kwa kuwa nilikua na hali mbaya kiasi nikamkubalia ila nikataka kujua mambo fulani juu ya Jane. Alinieleza mambo mengi sana ila akasema kuwa hata yeye hajui Jane ni mtu wa namna gani kilichomwingiza kwa Jane ni ugumu wa maisha. Kubwa akasema "Inaonyesha hata Jane mwenyewe hafurahishwi na ile kazi ila analipiza kisasi". Nikajiuliza kisasi cha nini nikakosa majibu.


Nikaamua kumwuliza kama anajua mengine zaidi. Akasema "kuwa Inasemekana Jane aliwahi kupelekwa Afrika ya kusini akawa mtengenezaji na Muuzaji wa madawa ya kulevya.

Aliifanya hiyo kazi kwa kutumikishwa kama roboti. Baadae akarudishwa hapa nchini na kuanza kutumikishwa kama kahaba kwenye baadhi ya kambi za Jeshi la polisi. Mwisho sijui ni nini lakini kiukweli Jane ni mtu hatari sana. Japo anaonekana kuwa anapewa maelekezo na baadhi ya viongozi wa nchi tena wakubwa tu".


Nilianza kuogopa kusikia yale maelezo. Akazidi kusema

" tena inaonyesha ana mtandao mkubwa sana hapa Tanzania".

"Mmmh" nilijikuta naguna na kuona nilikua nacheza na mtu hatari sana. Basi maongezi yakaishia pale tukaendelea na shughuli nyingine. Kwa kuwa Amina alikua anaishi chumba kimoja na mimi sikua na Jinsi zaidi ya kuvumilia. Amina alikua akilala chini ya kitanda na mimi kitandani hakika Amina alijitoa kunisaidia.

INAENDELA

Post a Comment

0 Comments