Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo : Singeli Kitaa Sehemu Ya Kwanza (1)

 


IMEANDIKWA NA : MTOTO WA BECKER


*********************************************************************************


||UBUNGO – DSM||




Ilikuwa saa tatu usiku. Basi kubwa ya abiria iliwasili na kuegesha kituo kikuu cha mabasi jijini Dar baada ya safari ndefu ikitokea Bukoba. Wasafiri walishuka kichovu kwa mchoko wa safari. Mguu mosi mguu pili kila msafiri alipiga hatua kushuka huku akimshukuru Mungu kwa kufika salama. Miongoni mwa wasafari hao alikuwamo binti mmoja mzuri sana. Kuanzia sura mpaka umbo. Hakuchosha kumtazama machoni. Alikuwa kivutio kwa kila jicho lililomtazama, si la kike si la kiume. Hakika hakuwa na kasoro ya maumbile tokea unyayo hadi unywele.


Binti huyo aliitwa Tausi. Mtoto wa Kihaya mwenye mchanganyiko wa damu ya Kitusi. Umbo lake namba nane lililobebwa na sura iliyoshiba mvuto vilitosha kuficha aibu ya nguo alizovaa. Gauni lefu jeupe mithili ya bi harusi. Mgongoni alibeba begi kubwa la nguo huku kichwani akiwa kajifunga kilemba cha kitenge. Raba nyeupe alitupia miguuni kama binti wa kihehe. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika jijini Dar es salaam. Miaka yote ishirini na mbili ya kuzaliwa kwake hakuwahi kukanyaga ardhi ya jiji hilo hapo kabla.


Alipepesa macho kulia kushoto punde aliposhuka akimtafuta mwenyeji wake. Zogo la watu na mataa ya jiji yalimchanganya na kumpa ugumu kumuona mwenyejiye.


“Mungu wangu! Jamani dada yu wapi tena?!simu yenyewe imezima.” Alijiuliza moyoni kwa woga na hofu ya kumpoteza mwenyeji wake. Alisimama nje ya basi asijue aelekee upande gani. Vijana wabeba mizigo na madereva taxi walijaribu kuzungumza nae lakini aliwanyamazia kwa kiburi cha kutotaka mazoea. Ndivyo alivyojifunza toka kwao. Asijenge mazoea ovyo na watu asiowajua hususani wanaume, vilevile alihofia kuibiwa na vijana wajanja wa jiji kama alivyowahi sikia hapo kabla. Lakini akiwa bado anatafakari vipi atamuona mwenyejie mara alishikwa bega na kugeuka haraka kwa mshtuko.


“Waaaooooo ! dadaaaaa!” Alifurahi na kukumbatiana na mtu aliyemshika bega.


Alikuwa ndiye mwenyeji wake aliyetarajia kumpokea hapo. Naye ni dadaye waliyechangia baba katika uzawa wao. Aliitwa Jerida. Binti wa kihaya aliyejaliwa makalio makubwa yaliyowachizisha wanaume kila apitapo. Ingawa kisura hakuwa mzuri kama Tausi, lakini bado Jerida hakuwa nyuma kuwatingisha vijana kila apitapo kwa kijungu chake matata, laini kama nyanya masalo.


“Karibu mdogo wangu pole na safari.” Aliongea Jerida huku akimpokea begi Tausi na kumuongoza upande wa kutokea ambapo watu wengi walielekea.


“Asante dada Jeri.” Alijibu Tausi huku akiangaza kiumakini kila pande kadri walivyopiga hatua. Amani sasa ilitawala moyoni mwake. Nafsi yake ilifurahia kufika ndani ya jiji alilokinai kuhadithiwa raha na utamu wake pindi alipokuwa Bukoba.


Mbali ya Jerida pia alikuwapo binti mwengine mwembamba mwenye weupe wa kujichubua ambae awali Tausi hakujua kama wapo safari moja. Yeye aliitwa Tunu, rafiki mkubwa wa Jerida.


“Tunu, huyu ndie mdogo wangu Tausi niliyekuwa nakupa habari zake, si unamuona mtoto mashaallah!”


“Nakwambia shoga si mchezo…pole kwa safari na karibu sana shostito!”


“Asante dada nashukuru” Alijibu Tausi huku akiachia tabasamu la haiba ya kike.


Walifika nje ya kituo na kuingia kwenye bajaji iliyokuwa inawasubiria.


“Waoo! Mama la mama huyu ndie Malkia Tausi eeh!” Aliongea kijana dereva bajaji punde kina Jerida walipoingia ndani.


“Unauliza jibu Mdoti bwana hebu tuwahishe huko.” Alidakia Tunu


“We mzungu wa kimakonde una ngenga!” Alinena dereva bajaji aliyeitwa Mdoti huku akiwasha chombo na kuondoka taratibu.


Tunu aliachia sonyo kwa utani ule wa Mdoti ambao hakuupenda na kumfanya Jerida aangue kicheko. Tausi hakutia neno zaidi ya kutabasam tu.

*******

Usiku huo huo maeneo ya Kijitonyama kwa Alimaua mziki mkubwa wa ‘kigodoro’ ulisikika ukirindima.


"Hii hapa tena sauti ya MC Jabaaaaaa, weee DJ Dudu Kilaaaa! bwisaaaa.......Ukienda mbele sawaaaa! ukirudi nyuma sawaaa!...ukiinama sawaa...! ukiinuka sawaa.... mbona kati kuna watoto mi nataka watu wazimaaaa...! mi nataka watu wazimaaa...Saula dadaaa saulaaaaaaa.... mamamamaaaa saulaaa teeena saulaaaaaa.....weeekaaaaaaaa..."


Hiyo ilikuwa sauti ya midato. Sauti ya rabsha. Sauti iliyochizika toka kwa kijana mfupi aliyesokota nywele kichwani akiwa kakamatia maiki (kipaza sauti) kishari kama mtutu wa jambazi. Mdomo aliuachama nusu kuimeza. Mishipa ya kichwa na ya shingo ilimsimama. Aliimba kwa hisia za ajabu huku akitetemesha mguu mmoja kama amekanyaga nyaya za umeme. Sauti yake iliambaa kwenye spika ikinogeshwa na midundo ya mihemuko iliyokuwa inachombezwa na Dj wake. Umati ulifurika muda huo na kuufunga mtaa. Ilikuwa hapatoshi kabisa kwa mahadhi ya mziki huo ulioshika hatamu uswahilini. Mziki wa ‘kigodoro’.


Kadiri alivyoimba alizidi kuukonga umati mzima. Watu walichizika na kufata kila alichokiimba kijana yule aliyejiita MC JABA.


Mabinti waliovaa nusu utupu katikati ya umati walizidi kucheza kihasarahasara na kuzidisha shangwe zilizomuongezea midadi Mc Jaba kuwarusha zaidi.


“…Vua dela dadaaa ubaki na chup*….. vua chup* tenaaaa ubaki mtupuuuu…. Haya tena galaagalaaaaa…galagalaaaaaa…weeekaaa! Mwaga maji tucheze kama kambaaareeee…….”


Wengine walisaula na kumwagiana maji hata kugalagala matopeni. Ilikuwa kama kituko lakini ndivyo ilivyokuwa. Burudani ya mziki alioimba Jaba ilikuwa inawakuna sana mashabiki zake hata kupelekea kukodishwa mara kwa mara mtaani kwenye shughuli za vigodoro kama ile. Tena akiwa na dj wake yule aliyeitwa Dj DUDU KILA.


Mtindo aliotumia kuimba Mc Jaba ulikuwa tofauti na walivyokuwa wanaimba wenzake. Lakini pia ulimsaidia kupata umaarufu wa haraka tokea kwao Tandale na sehemu jirani za uswahilini. Mziki wake ulipendwa sana na wahuni mitaani. Awe wa kike ama wa kiume. Haikujulikana haraka ni sababu ya lugha za ajabu alizokuwa anazitumia ndizo zilikuwa kivutio kwa watu..! ama sauti yake kubwa ya ukali pindi aimbapo..! ama ni vile dj wake anavyotumia ‘program’ ya ‘vitual dj’ kwenye kompyuta kutengeneza midundo ya ajabu!? Hilo halikujulikana haraka.


Lakini kipindi watu midadi ikiwa imepamba moto, kigodoro kimenoga… Mara umeme ulikatika ghafla. Mziki ukazima giza likatanda. Na hapo ndipo hekaheka ikazuka kwenye shughuli……



Lakini kipindi watu midadi ikiwa imepamba moto, kigodoro kimenoga… Mara umeme ulikatika ghafla. Mziki ukazima giza likatanda. Na hapo ndipo hekaheka ikazuka kwenye shughuli.


Wazee wa zana wakatoa zana zao. Visu, bisibisi na viwembe. Kiza kilifunika utu machoni mwao na kuufunua unyama. Vijana warandukaji waliokuwa wanacheza na kuchizika sasa walibadilika.


Uso nnya, jicho nyanya. Walivaa sura za kazi.


Nyonde nyonde walikabwa na kuibiwa palepale. Wabishi walijeruhiwa vibaya kwa visu na bisibisi. Zogo likazuka na wengine walikimbia hasa baada ya kubaini kuwa walijichanganya katikati ya PAKA WEUSI.


Jina la kikundi cha vijana wahalifu waliopinda kutoka Mwananyamala. Umaarufu wao ulichagizwa na matukio yao ya kuvamia kwenye miziki, kupora hata kubaka. Na ndivyo walivyofanya hapo mara baada ya umeme kukatika. Mabinti waliokuwa nusu utupu walichezewa nyeti zao na kubinywa binywa makalio na hata kunyonywa matiti pasipo ridhaa yao. Wenye shughuli walishindwa kufanya chochote zaidi ya kujificha.


Hekaheka zilichukua zaidi ya robo saa kabla ya kikundi kile kutimka. Shughuli ikawa si shughuli tena.


“Mc Jaba dogo letu, wee muhuni wetu unaturusha ileile.. Dudukila pamoja sana…” Aliongea Paka mweusi mmoja punde walipofanya yao na kuingia mitini.


Nyuma waliacha migumio ya maumivu kwa wale waliowajeruhi.


“Dudu Kila huu mti mkavu mwanangu tesepe!” Mc Jaba alimwambia Dj wake huku akimvutia pembeni.


“Kivipi Jaba, si umeona mwanetu mmoja wamemtoboa! Inabidi tuungane na washkaji.” Alisema Dudukila huku akiwatazama vijana wenye mziki waliokodiwa wakiwa wanamsaidia mwenzao mmoja aliyechomwa bisibisi ya tumbo.


“Usiwe matak* dudu! Basi jifanye malaika wangojee mamwera uone kama utashukuriwa…” Aliongea kwa hasira kidogo Jaba huku akiishia zake uchochoroni pasipo kuaga.


Dudu Kila aliwatazama kwa huruma washkaji wenye mziki wanavyohaha na wenye shughuli kuwasaidia walioumia lakini alikosa jinsi. Aliteleza nae kama kambale kumfata Mc Jaba.




****




Bajaji ya Mdoti iliambaa mpaka maeneo ya Tandale kwa bi Mtumwa. Mbele ya nyumba moja iliyokuwa na tenki la maji nje. Hapo ndipo alipokuwa anaishi Jerida na Tunu. Kila mmoja alipanga chumba chake.


“Asante baba la baba Mdoti, basi tufate keshokutwa si unajua ugeni tena! kesho tupo ‘off’.” Jerida alisema, Mdoti aliitika kwa kichwa na kugeuza bajaji yake kuishia.


Jerida na Tunu walimkaribisha rasmi Tausi kwenye makazi kitaani kwao.


“Tausi, najua umechoka kwasasa unahitaji kupumzika. Basi mlale salama kesho tutaonana.” Aliaga Tunu na kuingia chumbani kwake. Tausi na dadaye wakaingia chumbani kwao pia.




Kwa upande wa Mdoti aliendeesha bajaji huku mawazo yake yakihama kabisa na kutuama kwa Tausi.


“Daah! Hakika Mungu kuna wanawake kawaumba bwana..mmmh! Hapana huyu sitamuacha adumbukie kwenye kisima cha Jerida! Itakuwa dhambi sana.” Alijisemea mwenyewe Mdoti akiwa njiani kurudi kijiweni kwake.




* * * *


“Dudu Kila narudia tena kukutonya mwanangu, biashara za kujipendekeza kwenye majanga utajangaluka siku moja nami natembea tu nakuacha mwenyewe.”


Aliwaka MC Jaba pindi wakiwa njiani.


“Nimekusoma Jaba basi shusha mzuka.” Dudu kila alimtuliza.


Walikatiza vichochoro na kuvuka mifereji kabla hawajaibukia kipande walichokuwa wanaishi. Ilikuwa tayari yapata saa sita usiku.


Ni katika nyumba ileile waliyoingia kina Jerida ndipo walipoingia kina Jaba.


Tofauti ilikuwa wao wapo upande wa nyuma, vyumba vya nje na kina Jerida wapo upande wa mbele, vyumba vya ndani.


Lakini kumbe wakati kina Jaba wanarudi, Jerida alikuwa msalani kujisaidia.


Vyoo vilikuwa upande uleule wa nyuma.


“Shika kiberiti nyonga kabisa dawa Jaba la baja mi nazama kushusha kitu kwanza.” Aliongea Dudu Kila huku akimpa kiberiti Jaba na kumuacha akiingia Getto huku yeye akielekea msalani pasi kujua kama kuna mtu.


Hamadi! Uso kwa uso wanagongana kwenye kigunia kilichotundikwa mlango wa chooni.


Dudu kila akitaka kuingia huku Jerida akitoka.


“Jamaniiii.. Ubishi hodi? Lione dudu lake” aling’aka kidogo Jerida na kumshika sehemu za kazi Dudu Kila kama utani.


Dudu Kila alistuka, Jerida alicheka na kumpita huku akimpiga kikumbi cha makalio yake na kumtingishia wowowo lililofichwa ndani ya kanga moja tu.


“Aaaaagh! We Jerida hebu simama!” Dudu kila alijikuta uzarendo unamshinda na kumfata. Tayari alishachanganyikiwa kijana. Macho yake yalishamchorea picha tofauti huku mwili wake ukijmjengea hisia za mchoro wa taswira nzima. Alihisi utakuwa ujinga uliokithiri kuuacha utamu umpite hivihivi.


“Leo kanasa huyu!” Jerida nae alijisemea moyoni na kugeuka kwa madaha kama yuko kwenye jukwaa la ulimbwende.


“Enhee sema!”


“Kwanini umenifanyia hivi lakini?”


“Nimekufanyaje tenaa?


“Kwa hiyo ulivyonishika huku we umeona sawa?”


“Oooh! Kumbe unasemea nilivyokushika huku? Poole nirudishie basi.!” aliongea Jerida huku akimshika tena Dudu kila eneo lake la kazi na kulifanya Dudu Kila lenyewe listuke maradufu.


Huku moyo wa Dudukila ukibadili kasi ya mapigo, Jerida alitumia nafasi hiyo kuuchukua mkono mmoja wa Dudu Kila na kuupenyesha pembeni ya kanga na kumgusisha kitumbua chake.


“Haaa! Kumbe uliumia kweli..polee! basi bila bila” Jerida alifanya kituko ambacho Dudu kila alishindwa kukivumilia kabisa na kujikuta akimkamata mikono kwa nguvu na kumvuta.


Hamadi! Kanga ya Jerida ilifunguka na kumuacha mtupu kabisa. Mambo yote hadharani. Shanga nje njeeee…!






Huku moyo wa Dudukila ukibadili kasi ya mapigo, Jerida alitumia nafasi hiyo kuuchukua mkono mmoja wa Dudu Kila na kuupenyesha pembeni ya kanga na kumgusisha kitumbua chake.


“Haaa! Kumbe uliumia kweli..polee! basi bila bila” Jerida alifanya kituko ambacho Dudu kila alishindwa kukivumilia kabisa na kujikuta akimkamata mikono kwa nguvu na kumvuta.


Hamadi! Kanga ya Jerida ilifunguka na kumuacha mtupu kabisa. Mambo yote hadharani. Shanga nje njeeee…!


“Haaa! Jamani Dudu Kila mmmnnnn…!”


Kabla hajamalizia sentensi yake tayari mdomo wa Dudukila ulifika kwenye lipsi za Jerida na kuanza kuzinyonya.


Joto la muwasho wa ngono lilimfanya Jerida akipokee kinywa cha Dudu Kila na kunyonyana ndimi kwa pupa. Uchu wa matamanio ya kungonoka ulimvaa zaidi Dudukila. Msambwanda wa Jerida ndio ulimpagawisha zaidi kila alivyoupapasa na kuubinyabinya.


“Tulia basi mbona una pupa hivyo? Kama hujawahi!” Kwa sauti ya puani Jerida alisema huku akiitoa mikono ya Dudukila aliyezidisha kumpekechua makalioni na kumshika.


“Sikiliza bwana Dudu, kula nanasi kwahitaji nafasi.” Aliongea tena huku akiinama kuikota kanga yake.


“Una maanisha nini sasa?” Aliuliza Dudukila huku akimtazama Jerida kwa jicho la uchu. Alifungua zipu ya pensi yake ya ‘jeans’ na kumtoa jongoo wake aliyevimba na kugangamala vilivyo.


“Heeeeeeh! Dudu…? Kumbe kweli we mtoto?” Alishangaa kwa sauti Jerida mara baada ya kujifunga kanga na kumuona jongoo wa Dudukila aliyesimama dede nje ya pensi.


Kabla Dudukila hajajibu kitu Jerida alikimbia haraka huku akicheka kuuelekea mlango mkubwa na kuingia ndani akimuacha Dudukila amekodoa kwa hasira.


“Kum**lama***ako! Siku ya kukutia nyama ndio utajua kama kweli ama si kweli.” Alishusha matusi Dudukila na kuelekea chooni huku mashine ikiwa bado nje imesimama vilevile.


Alitumia zaidi ya nusu saa chooni akiwa anafikiria alichofanyiwa na Jerida.


“Lazima nimtie mashine huyu malaya! Na nitamsongomeka yote hadi ajue kwanini wameniita dudukila.” Alijiapiza huku akikumbuka chanzo cha jina lake lililokuzwa na makahaba wa uwanja wa fisi miaka kadhaa iliyopita na kuleta gumzo kwa mabinti wengi hali iliyopelekea aogopwe. Ni ukubwa wa jongoo wake ambae ilisemekana alimsababishia kifo kahaba mmoja baada ya kushindwa vumilia vishindo vyake ingawa hizo hazikuwa habari rasmi. Ila ukweli ukabaki maumbile yake hayakuwa ya kawaida. Jongoo aliyeshiba, kipisi cha ukuni, zaidi ya nchi nane alijaaliwa. Na ndicho alichobaini kuwa Jerida alitaka kumlaghai ili ahakikishe ukubwa wa jongoo wake.




Baada ya muwasho kupoa na jongoo kusinyaa, alirudi getto na kukuta Jaba amelala fofofo akikoroma.


“Daaah! Huyu msen*e nae kavuta dawa zote.!” Alisema pekeake baada ya kugundua bangi zote zimevutwa na Jaba. Hakuwa na chaguo zaidi ya kujibwaga kwenye godoro na kuuvuta usingizi.




* * * *




Asubuhi na mapema kulikucha. mlango wa chumba cha Jerida uligongwa. Tausi alikuwa wa kwanza kusikia, aligeuka kumtazama dadaye alikuwa bado kalala.


“dada…dadaa…dada kuna mtu anagonga.” Alimuamsha.


“Mfungulie Tunu huyo.” Aliongea kivivu Jerida na ndipo Tausi aliposhuka kitandani kuuelekea mlango kufungua na kweli alikuwa Tunu.


“Waaooo! Malaika! Huyo kibonge bado anakoroma tu?” Aliongea Tunu huku akiingia ndani.


“Wee Jeri hadi saa hizi umelala kama tulitoka jana bwana? Hebu amka au umesahau tena kuhusu leo?” Tunu alisema huku akikaa kitandani. Na ndipo Jerida aliamka baada ya kukumbuka ahadi yao na Tunu.


“Anhaa sawa! Sasa Tausi mdongo wangu inabidi tujiandae twende kwenye ule mchongo muhimu sana kwako niliokuunganishia.”


“Ooooh! Sawa dada.”


“Kazi kazi shostito! Hamna kuzubaa” Alichombeza Tunu na kumfanya Tausi atabasamu huku moyoni akimshukuru Mungu kuwa na dada kama Jerida anayeonesha kujali sana maendeleo yake hata kwenda sawa na ahadi zake hususani hiyo ya mpango wa kazi aliomuahidi.




Baada ya kuoga na kujiandaa, walielekea kituo cha daladala Mtogole.


Safari hii Tausi alionekana tofauti na mwanzo kimavazi. Nguo alizopewa na Jerida zilimpa muonekano wa kimjini mjini ingawa moyoni alihisi aibu. Blauzi nyeupe na suruali ya pink iliyobana hayakuwa mavazi aliyozoea. Lakini kwa heshima ya dadaye alivaa hivyo na kutoka pamoja.


“Tausi achana na magauni mdogo wangu yamepitwa na wakati, tukitoka huku itabidi tupitie saluni ukatengenezwe nywele zako pia twende kariakoo nikakununulie nguo mbili tatu na viatu.”


“sawa dada asante.” Alijibu Tausi.




Walipanda daladala ya Msasani na safari yao ilikomea Kinondoni studio.


“Hallow! Eeh bosi wangu tumefika hapa… niko na Tausi yule mdogo wangu niliyekwambia. Vipi tuje moja kwa moja ama?”


Aliongea kwa simu Jerida baada ya kushuka na kusimama pembeni ya kituo cha daladala.


“Sawa bosi nimeelewa! Tupo hapahapa kituoni…sawa!” Alikata simu na kuwageukia kina Tunu.


“Itabidi tuvuke tukasimamie kituo kile maana anakuja shoga, eeh! tena anaelekea kiwanja nasikia Zungu yuko kituoni kampasua mtu jana.” Alisema Jerida kumwambia Tunu.


“Eeeeh! Usinambie!”


“Ndivyo hivyo.”


Walivuka barabara upende wa pili na haukuchukua muda mwingi gari ndogo aina ya Toyota Prado ilisimama kituoni. Jerida na Tunu waliitambua haraka na kuielekea huku Tausi akiwa kama tela tu.


“Waaooo! Jerida naona uko na cheupe” Sauti ya kijana mtanashati aliyekamatia usukani ilisikika kipindi Jerida na wenzake wakiingia.


“Eeeh kama kawaida yetu! Umeona kazikazi?”


“Aaaagh! Nimeona kweli sio powa.”


“Ndio hivyo, sasa Tausi huyu ndiye bosi wetu na bosi wako mtarajiwa, anaitwa bosi Ndangala Ndangala”


Jerida alitambulisha baada ya kuingia garini na gari kuondoka eneo lile.


“Shikamoo.” Aliamkia Tausi kwa heshima kubwa kumsaliumu yule kijana baada ya kugundua ndiye bosi mwenyewe.


“ha ha ha h Tausi, huna haja ya kuniamkia kijana mwenzako au unataka kuninyima nini?” Alicheka bosi Ndangala huku akiendelea kuchochea mwendo wa gari. Hata Jerida alijikuta akicheka kwa kugundua salamu ya Tausi ilitokana na shauku ya ajira.


“Kuwa huru Tausi karibu sana, dada zako walishanambia kila kitu na kwa kuwa sasa kuna mambo nafatilia, nitawaacha kwanza kina Jerida ila wewe itabidi ubaki nami twende wote ili tupate fursa nzuri ya kufahamiana kwa kufanya usaili wote ya ofisi.”


Aliongezea bosi Ndangala huku akimtazama Tausi aliyekaa siti za nyuma kwa kuibia kupitia kioo cha ndani. Hakika kwa namna moja moyo ulimpasuka kumuona binti mzuri namna ile.


“Hilo hamna shida bosi Ndangala, tunachotaka umfanyie kweli ndugu yetu hata umuweke V.I.P japo atakuwa mpya lakini mwenyewe unaona mambo!” Tunu aliongezea huku Jerida akiitika na kuunga mkono.


“Msijali kabisa, nitamsaidia kwa heshima yenu bila tabu na kesho itabidi mje nae. Ila afanye poa kwenye usaili wangu…Tausi kama utakuwa kazikazi utafurahi mwenyewe.”


“Nitashukuru sana kaka.” Alisema Tausi kwa sauti ya upole mkubwa kama anataka kulia kwa furaha aliyokuwa nayo.


Furaha ya kupata kazi. Ingawa bado hakufahamu aina ya kazi yenyewe japo hilo halikumtia hofu. Moyoni alishajiapiza kutochagua kazi punde akifika jijini.




Dakika chache baadae walifika Tandale na gari iliwasogeza hadi eneo la bi Mtumwa.


Jerida na Tunu walishuka huku wakimsihi Tausi atulize akili kwenye usaili anaoenda kufanyiwa na bosi Ndangala.


“Tuliza akili mdogo wangu ufaulu usaili ili nawe ufaidi maisha. Ukifeli hapo utakuwa umefele kila kitu. Msikilize sana bosi Ndangala…sawa?”


“Sawa dada, nakuahidi kutokuangusha.” Aliahidi Tausi.


“Zunguka ukae mbele huku.” Bosi Ndangala alimuelewesha Tausi. Bila maswali alitii na kukaa siti ya mbele.


Gari iliondoka huku ndani yake sasa kukiwa na watu wawili tu. Bosi Ndangala na Tausi mwenyewe.


“Huyu mtoto mmh! Sijui nikampochoe kabisaaa! Ama nivute subira nimpochoe usiku kucha… kha! Sasa nakubali sifa alizokuwa ananambia Jerida kweli hiki kifaa.”


Alisema na moyo wake bosi Ndangala huku akikanyaga mafuta kuelekea barabara ya Sinza.








“Zunguka ukae mbele huku.” Bosi Ndangala alimuelewesha Tausi. Bila maswali alitii na kukaa siti ya mbele.


Gari iliondoka huku ndani yake sasa kukiwa na watu wawili tu. Bosi Ndangala na Tausi mwenyewe.


“Huyu mtoto mmh! Sijui nikampochoe kabisaaa! Ama nivute subira nimpochoe usiku kucha… kha! Sasa nakubali sifa alizokuwa ananambia Jerida kweli hiki kifaa.”


Alisema na moyo wake bosi Ndangala huku akikanyaga mafuta kuelekea barabara ya Sinza.


“Nikipita kwenye usaili hakika sitazembea kwenye kazi. Mungu nisaidie.”


Tausi naye aliwaza yake kichwani.


Gari iliendelea kuambaa na njia hadi Sinza kijiweni na kukamata njia ya Shekilango ambapo safari ilikomea maeneo ya Lego. Mbele ya mgahawa mmoja.


“Nifate mrembo, kuwa huru usiniogope sawa?” Aliongea bosi Ndangala huku akimshika kiganja Tausi baada ya kuegesha gari. Walishuka na kuingia mgahawani.


“Tuletee supu ya kuku mzima.” Aliongea bosi Ndangala na kumgeukia Tausi mara baada ya muhudumu kufika mezani walipoketi.


“Tausi, agiza mamaa chochote unachojisikia kula asubuhi hii ama kunywa! Kuwa huru.”


“Asante bosi mi sina njaa.”


“Hapana sio kweli, kama hupendi supu ya kuku agiza ya ng’ombe ili tukiwa kwenye usaili usichoshwe kwa njaa.”


Aliongea bosi Ndangala na kumfanya Tausi acheke na kubinya binya kucha za vidoleni.




Muda mfupi muhudumu alileta walichoagiza. Sahani kubwa iliyokuwa na bakuli mbili za mchuzi wa kuku huku katikati ya sahani kukiwa na nyama za kutosha za kuku, visu, vijiko, uma na mazagazaga mengine.


Ilikuwa ni mara yake ya kwanza Tausi kwa kile alichokiona pale japo haikuwa mara ya kwanza kuona nyama ya kuku.


Kwa ucheshi wa bosi Ndangala kidogo ulimpunguzia hofu Tausi japo haukumshushia umakini wa heshima.


Baada ya supu nzito iliyowatoa chemchem za jasho la vinyolewo hatimae waliondoka huku wakiwa wamechangamka miili.


Safari hii gari ilielekea hadi maeneo ya Manzese tiptop. Mbele ya jengo lililokuwa na maandishi yaliyosomeka ‘RAMBO NIGHT CLUB’


Hapo waliposhuka kama kawaida bosi Ndangala alikuwa mbele huku Tausi akiwa kama mkia. Nje kulikuwa wamesimama vijana wawili wenye miili mikubwa (mabaunsa) wakiteta jambo na mama mmoja mnene mfupi. Walikatisha mazungumzo na wote kumsalimu Ndangala.


“Habari za asubuhi bosi!”


“Safi, vizuri nimewakuta. Mama Agy itakupasa uelekee kituoni kumfatilia Zungu, kamata hii ikulinde kama wakileta ngenga hao polisi nipigie nizungumze nao.” Aliongea Ndangala huku akitoa kibunda cha noti kadhaa za elfu kumi kumi na kumkabidhi yule mama mfupi.


Baada ya hapo alimshika mkono Tausi na kuingia nae ndani ya club. Mazingira yalikuwa tofauti sana kwa Tausi na kuanza mjengea hofu. Michoro ya kuta za club zinazoonyesha wanawake wenye vibikini ilimtisha kiasi. Ingawa hakukuwa na watu wengi zaidi ya wahudumu waliokuwa wanaendelea kufanya usafi alizidi kuingiwa mashaka Tausi hususani baada ya kuingia ndani kabisa ya club upande kulipokuwa na lodge ya kulala.


“Naomba ufunguo wa V.I.P” Sauti ya Ndangala ilimuamuru dada aliyekuwa mapokezi upande wa lodge. Dakika chache baada ya kupewa funguo alimkokota Tausi mpaka upande wa ndani na kufungua mlango wa chumba kimoja.


“Bosi huku tunaenda wapi?” Alisita na kuuliza Tausi punde alipoona mapigo ya moyo wake yakizidisha kasi kutokana na utulivu mkubwa wa eneo lile.


Alishatia mashaka hasa baada ya kugundua eneo lile lilikuwa ni zaidi ya Baa na Gesti za kawaida alizozijua Bukoba.


INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments