Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Singeli kitaa sehemu ya tatu (03)

 


“Ndangala Ndangala tu!”

“Yule mchizi bosi wa Rambo?” Aliuliza kwa shauku Dudukila.

“Eeeh! Huyohuyo.” Jaba alijibu.

“Daa kweli hapo umenena. Yule mwana ana mavumba kinyama.”

“Sasa dogo Cholo hii kitu sio ya kwenda nayo pupa itakutokea puani. Niachie mie, kesho kuna show ya Ronki pale club… mi najitoma kama kawa nina uwezo wa kumvaa Ndangala akanielewa.” Alijitapa Jaba ingawa dogo Cholo alionesha kutoridhika na maamuzi yale lakini alimezea.


*********


Jotojoto la utamu wa Tausi lilipenya na kumfikia njomba nchumali wa Ndangala pindi akiwa kamkumbata kwa nguvu akimpa maneno ya kumlainisha.

“Tausi… usiwe kama mtoto mng’aa asiyejua bee wala baa! Hapa jijini maisha hayaendi kama utakavyo wewe bali unapaswa kwenda yanavyotaka maisha. Tena nataka nikupe nafasi kwenye club yangu hutakuwa kama dada zako ila utakuwa na kitengo tofauti ilimradi tu uwe unanipa raha sweety” Huku akimpapasa Ndangala aliendelea kumuongelea Tausi sikioni kwa sauti mnyegeko. Lakini kwa Tausi ilikuwa tofauti kabisa! Alianza kupatwa hasira na uchungu uliomfanya machozi yamtiririke.

“Wee kaka hivi huoni haya hata huna utu wa kumpapasa maungo mwanamke pasipo hiyari yake? Tena akiwa si mkeo?” Aliuliza Tausi swali ambalo halikumstua wala kumpunguzia Ndangala kasi ya kumpapasa japo kuwa Tausi alijitahidi kujinasua.

“Tulia Tausi acha utoto, fulsa nikupayo wengi wanaililia hawaipati. Wee inakuangukia miguuni unaipiga teke? Hebu kata kiu ya Ndangala ule maisha mjini..”

Safari hii mikono ya Ndangala ilikuwa inang’ang’ana kukigusa kitudambwa cha Tausi kilichowambwa ndani ya suruali nyepesi aliyopewa na Jerida.

Lakini safari hii Tausi hakuzungumza kitu. Moyo ulimtuma kutumia nguvu. Na ndivyo alivyofanya kwa kustukiza. Alitumia ubavu wa shamb aliokuwa nao na kumsukuma ghafla kwa nguvu Ndangala. Kisogo cha Tausi kilipigiza midomo ya Ndangala na kujikuta anamuachia baada ya msukumo ule.

“Haaaa!?” alistaharuki kwa hasira Ndangala huku akimtazama kwa jicho kali Tausi sekunde zile alipofungua mlango na kutoka mbio mbio.

Kichwa chake chepesi cha kukariri ndicho kilimsaidia kupita mulemule walipopita na Ndangala pindi wanaingia clubuni pale. Mabinti waliokuwa wanamalizia kufanya usafi walimshangaa jinsi anavyotembea haraka kama askari zima moto.

“Mh! Huyu hajamuibia bosi kweli sasa anamkimbia?” mmoja wao alijiuliza na kumwita.

“Wee binti…haaiiweeeee!” Tausi hakusimama. Aliukaza mwendo kuuwahi mlango mkuu wa kutokea.

Ndangala akiwa ndani alijipangusa lipsi moja ya mdomo iliyokuwa inatoa damu baada ya kujing’ata bahati mbaya pindi aliposukumwa kimgongo mgongo na Tausi.

Aliingia bafuni huku akicheka mwenyewe na kujitazama kwenye kiooo jinsi alivyong’ata mdomo.

“the hehe! Daaah… hivi vitoto vyengine unaweza kuviona vizuri kwa nje kumbe ubongoni vindimu! Lakini mmmh! Huyu mtoto sio poa.. mvuke wa joto lake kama kuna watu wanapika mwilini mwake…! Hapana lazima nimtie nyama.”

Alitafakari na kutoa simu yake ya mkononi haraka. Alipiga namba za baunsa mmoja kati ya wale wawili waliokuwa nje punde walipokuwa wanaingia.


“Hey we! Hebu simama! Mbona mbiombio kulikoni?” Sauti ya pande la mtu ilimsimamisha Tausi pumde tu alipotoa nyayo geti la nje.

“samahani kaka, kuna kitu muhimu nimesahau nyumbani nawahi” alidanganya Tausi uongo aliompa mashaka yule baunsa na kumsogelea baada ya kubaini sauti yake ina mtetemo.

“Una uhakika?” baunsa alikaza huku akisogea.

“Ndio hivyo kaka.”

“Wee hujamkimbia bosi kweli?” Swali la baunsa lilimchosha nguvu Tausi. Aliona sasa anaweza kushikwa na kurudishwa kulekule.

Alishusha pumzi Tausi asijue afanyeje. Moyoni alijisikia aibu iliyochanganyika na hasira. Alianza kumlaumu dadaye na kuijutia nafsi yake kwa kuja Dar. Hakuwa tayari kulala kitanda kimoja na mwanaume asiyemfahamu kiundani.

“Tino… hata mie nina mashaka na huyo! Tena ngoja nikamuangalie bosi kama yuko salama kweli huko ndani sio kawaida kabisa aje na binti halafu amuache atoke mwenyewe.”

Sauti ya bidada aliyekuwa anamwita Tausi awali pasipo kusimama ilisikika ikimsisitiza baunsa aliyeitwa Tino ambae alimsimamisha Tausi pale nje .

Ndipo yule mfanya usafi akarudi ndani ya club kuelekea kule v.i.p lodge chumba alichokuwa Ndangala ili wapate uhakika ju ya mtoko wa yule binti mgeni machoni mwao.

“Mungu wangu! Nimekwisha!” alisema na moyo wake Tausi.

Wakati huohuo simu ya yule baunsa ilisikika ikiita mfukuoni mwake. Ndangala ndiye aliyekuwa anampigia. Pasipo kuangalia mpigaji baunsa aliidharau simu na kuendelea kumuuliza maswali Tausi huku akimtupia jicho la kumtamani lililomtazama kwa uchu wa kubinjuka nae.


Kwa upande wa ndani Ndangala alipoona simu haipokelewi ndipo alipovaa shati yake haraka na kufungua mlango. Ndipo uso kwa uso alikutanisha macho na mwanamama mfanya kazi aliyekuwa anakuja kwa niaba yake.

“Samahani bosi! Eti huyubinti uliyekuwa nae ulimruhusu kutoka?” aliuliza yule mama.

“Yuko wapi?” aliuliza Ndangala badala ya kujibu.

“Nje hapo amezuiliwa na Tino.”

“Vizuri ngoja nielekee mwenyewe wee endelea na kazi zako.”

“sawa bosi.” Aligeuka kuendelea na yake mfanya usafi.

Bosi Ndangala alipiga hatua za haraka kama askari mwenye kiu kuelekea upande wa nje ya club.


*********


Mdoti akiwa kwenye mishemishe zake za bajaji aliendelea ‘kula vichwa’ kama kawaida yake. Kichwani mwake mawazo juu ya Tausi hayakumkauka. Alifikiria vitu vingi sana tokea usiku wa jana yake alipomuona ambapo ndo ilikuwa mara ya kwanza.

“Nikuache Rambo club kabisa ama kituo cha daladala?” Mdoti alimuulza mteja wake punde walipokkuwa wanakaribia eneo husuika alilotakiwa kumfikisha.

“Niache Rambo kabisa kaka.” Alijibu mteja ambaye alikuwa ni mwanamke.

Na ndipo bajaji ya Mdoti iliambaa mpaka Rambo night club na kuegesha.

“Asante kaka pesa yako hii.” Alishuka mteja na kumkabidhi Mdoti noti ya shilingi elfu kumi. Lakini kipindi Mdoti akimrudishia chenji mteja wake ndipo macho yake kwa mara nyengine yalimuona Tausi akiwa amesimama akitetema mbele ya baunsa mmoja pale nje. Picha halisi ilionesha wazi kuwa ametaitishwa.

Moyo ulimlipuka Mdoti! Kwa butwaa hakuamini macho yake




“Asante kaka pesa yako hii.” Alishukuru mteja na kumkabidhi Mdoti noti ya shilingi elfu kumi. Lakini kipindi Mdoti akimrudishia chenji mteja wake ndipo macho yake kwa mara nyengine yalimuona Tausi akiwa amesimama akitetema mbele ya baunsa mmoja pale nje. Picha halisi ilionesha wazi kuwa ametaitishwa.

Moyo ulimlipuka Mdoti! Kwa butwaa hakuamini macho yake


Mteja wa mdoti alipomuona yule baunsa pale nje alifurahi na kumkumbatia kwa shangwe.

“Waaooo! Jamani Tinoo baby” Aliita bidada na kumpiga mabusu Tino hali iliyompotezea umakini juu ya binti aliyekuwa naye.

Tausi naye alitumia upenyo uleule kukimbia. Tino alistuka na kutaka kumkimbiza lakini sauti ya bosi Ndangala aliyekuwa anatokea ndani ya club ilimzuia.

“Muacheee Tino endelea na mambo mengine ya kiusalama saa nne ikifika muhakikishe yeyote aliyelala humu awe ameshaondoka.”

Aliingia kwenye gari yake Ndangala baada ya kusema hayo na kugeuza taratibu kuondoka eneo lile.

“Huyu ni kuwachimba mkwala dada zake tu! Lazima wamlegeze ili nimpochoe vizuri.” Aliwaza Ndangala kipindi anaingia barabara kuu na kuishia zake.


Mdoti aliyaona yote yale kama anatazama filamu. Ndipo naye aligeuza bajaji yake na kuambaaambaa pembeni mwa barabara ya waendao kwa miguu kuelekea upande ule ambao Tausi alikimbilia.

Alimuona na kumpigia honi alipomkaribia.

“Panda twende Tausi” Ilibidi amwite alipoona binti anazidi kuukaza mwendo ihali alishapunguza mita kadhaa tokea kule Rambo.

Aligeuka Tausi aliposikia jina lake na kuiona sura ya Mdoti ambayo hakuikumbuka pia.

“Nani wewe?”

“Duh! Mara hii umenisahau? Mi Mdoti jana ndiye niliyewabeba tokea ubungo mara ulipowasili jijini.”

“anhaa! Nimekumbuka.” Alijibu Tausi na kuingia kwenye bajaji ya Mdoti.

“Pole! Mbona hivyo vipi dadazako wako wapi?”

“Nyumbani! Naomba nipeleke dada atakupa pesa yako mi sipajui popote hapa nilikuwa nakimbia ovyo tu kujinusuru mikononi mwa shetani.”

Aliongea kwa huruma Tausi. Picha aliloliona Mdoti hakutaka kuhadithiwa sana zaidi alipata jibu moja tu.

“Tausi si malaya wala hauwezi umalaya.”

Na ndivyo alivyosema moyoni mwake Mdoti. A liingiza bajaji barabara kuu na kuitafuta njia ya Tandale kwa kina Jerida.

“Nakupa pole Tausi pia nakupongeza kwa msimamo wako. Namjua vizuri yule mchizi Ndangala. Siku moja nitakupa historia yake hata kuwa na pesa zile zinazomtia kiburi hapa mjini na kufanya mambo ya ajabu.”

Maneno ya Mdoti yalimjengea maswali Tausi na shauku ya kujua mengi kuhusu Ndangala hata dadaake Jerida.

“Eti samahani! Hivi dadaangu Jerida na Tunu nina imani unawafahamu vizuri! Unaweza kunifafanulia kazi gani wanafanya kwa yule kaka?”

“Duh! Ha ha ha ina maana wewe ndugu yako hadi anakuleta mjini hujui anafanya kazi gani?”

“Ndio sijui naomba unambie kama unajua!.”

“Kwa hiyo hata alipokwambia amekutafutia kazi ukaja bila kujua unatakiwa ufanye kazi gani?”

“Ndio sijajua kaka.” Alijibu Tausi kwa sauti ya upole yenye msisitizo.

Mdoti alifikiri kidogo kabla hajasema kitu wakati huo bajaji ilishakaribia kabisa mitaa ya bi mtumwa.

“Sikia Tausi, mi nimekuleta bure kabisa hapa huna haja ya kumwambia hata dadaako kama mie ndo nimekuleta. Nyumba yenu ileee. Simu si unayo?”

“Ndio ninayo.”

“Basi leta nikuandikie namba zangu. Naomba kesho kabla sijaja kuwachukua usiku unipigie kuna mengi muhimu sana yapaswa uyajue mapema usije kuimaliza juisi ya maisha kabla ya wakati.” Alitoa maelekezo Mdoti wakati huo bajaji aliisimamisha mbali kidogo na nyumba waliyopanga kina Jerida.

Alishuka Tausi na kumshukuru sana Mdoti mara bada ya kuandikiwa namba. Taratibu alipiga hatua kuelekea nyumbani kwa dadaye. Watu waliokuwa bombani mbele ya nyumba husika muda huo walijikuta wanamshangaa Tausi kana kwamba wamemuona malaika mtaani kwao. Aliinamia chini kwa aibu ya kutazamwa sana. Aliufikia mlango mkubwa lakini kabla hajafungua ulifunguliwa. Macho kwa macho na Jerida.


“Weee kweli mpumbavu sana Tausi! Lool…”

Hilo lilikuwa neno la kwanza alilokutana nalo toka kwa Jerida. Kabla hata ya salamu. Uso wa Jerida ulibadilika. Ndita alikunja kwa udhia alioletewa na nduguye. Udhia ambao Tausi alikuwa hajafahamu bado nini tatizo. Bosi Ndangala alishamchafua kwa kupiga simu kwa Jerida na Tunu.

“Dada! Yaani badala unipe pole unaanza kunifokea! Nimekosea wapi lakini?”

“Hujui ulipokosea? Kwa hiyo hiyo kum** yako unamletea nani? Au unamchukulia kawaida sana bosi Ndangala! Basi nikwambie Tausi yule ndiye anayetupa jeuri ya kutesa hapa mjini. Na haimaanishi eti akikufanyia usaili ndio atakusumbua tena…Lakini bibi wewe umeona kama atang’oka nayo umeirudisha huku kavukavu unataka iliwe na mapaka ya uswahilini? eeeh”

Kauli za Jerida sasa zilivuka mipaka moyoni mwa Tausi. Alijikuta anaanza kudondosha machozi huku akijilaumu kwanini amekuja Dar. Ndio kwanza siku ya pili. Wambeqa wa mtaa walitupia vijicho pembe wakiwa bombani kuutazama mchezo mzima uliokuwa unaendelea pa;e mlangoni.

“Kwa hiyo dada kumbe mlipanga kuniuza kwa yule kaka? Kwanini hujanambia kama kazi unayoniitia ndio hii. Dada mi siwezi, heri niondoke tuu!” Kilio kilimponyoka Tausi. Jerida alimtazama nduguye huruma ikamvaa tena. Alimshika mkono na kuingia nae chumbani kwake.

“Nyamaza mdogo wangu ila hebu nisikilize kwa umakini.” Alianza kumbembeleza tena na kumshushia maneno mengi ya faraja na ushawishi wa kuwa pamoja mara walipofika ndani na kumkalisha kitandani.

“Hili jiji mdogo wangu lina pesa nyingi sana ila kama utakuwa na akili ya kuzitafuta tu. Pia lina kila aina ya vishawishi na ghasia. Mimi hapa unavyoniona na Tunu kazi yetu ni pale club majira ya usiku tunajumuika tunawachuna mabuzi mpaka asubuhi hatukosi elfu sabini mpaka laki kwa kila mmoja. Hivi unadhani kwa mwezi tunaingiza shilingi ngapi? Haimaanishi sisi ni malaya! Hapana. Malaya ni wale wenye wapenzi wao ndani huku wakijifanya wastaarabu kumbe pembeni wana lundo la wapenzi wengine. Lakini tufanyacho sisi hatutengenezi wapenzi wala wachumba bali tunatengeneza pesa. Tunauza urembo wetu tunacheza na akili za walevi. Ila kuhusu Ndangala ukweli umekosea mdogo wangu, ungemuachia tu amini angekupa nafasi ya kujichanganya v.i.p ambapo huwa wanakaa watu wenye pesa na wale maarufu. Usiogope mdogo wangu unatakiwa uwe mwanamke wa shoka kama mimi dadaako. Nisikilize.” Alimshawishi zaidi. Wakati huo Tunu hakuwepo nyumbani.


Baada ya Jerida kumsomea risala ndefu ya maisha ya jiji pamoja na kumtoa mashaka nduguye juu ya kazi yao. Mwishowe Tausi alionesha kukubali. Lakini hilo alilifanya machoni tu!... Moyo wake bado uliwaza tofauti kabisa.


Dakika zilikimbia usiku ukaingia.

Alionekana Jaba akiwa na Dudukila sambamba na dogo Cholo wakipiga soga na jamaa zao kwenye ‘camp’ yao iliyoitwa Beach boys.

Siri ya pete ya almasi ilibaki kuwa siri yao tu. Walichokifikiria kesho ifike mapema ili wakapige pesa ndefu kama walivyoamini.

“Oyaa! Dogo Cholo nasikia leo umekunya! Pande zipi mwanetu? Hujafaniiwa nini?” Aliuliza mchizi mwenye kipara pindi wakiwa wanapiga soga.

“Hamna dogo rasi leo mbona tulikuwa nae geto kutwa nzima leo.” Alidakia Jaba kuzima maswali kwa Cholo.

“Jaba eeh! Turuke kwa tumbo mwanangu leo kuna washawasha huko na yule mtoa ladha wao wa Mbagala twende ukamfunike mwanangu.” Jamaa mwengine mrefu waliyemwita Tolu aliongea huku akinyonga mjani (bangi).

“Kweli boy! Ka vipi jamani tuzukeni tukakimbize.” Wengine nao walisapoti.

Ndipo jeshi zima likaunga mkono kuelekea kwenye shughuli ya kigodoro mitaa ya kwa tumbo.

Mwendo wa kijeshi waliokwenda nao uliwachukua muda mfupi sana kufika mtaa husika uliokuwa na kigodoro.


“Mama kidole changu leooooo… nasema mama kidole changu hikiiiiii…..

Mani chongo nimebadilikaaa! Mziki kaaziiii..”

Ilisikika sauti ya mc aliyekuwa anaimba kwenye shughuli hiyo ambayo haikuonesha kuchangamka sana ingawa kulikuwa na kundi la mademu maarufu sana kutoka Tandale wacheza nusu utupu walioitwa ‘washawasha’.

Nyimbo alizokuwa anaimba mc wa muda huo ambae ilisemekana anatokea Mbagara zilikuwa za taratibu ambazo ziliwakuna zaidi wamama watu wazima waliozunguka mduara. Kwa upande wa vijana walibaki kusimama na kutazama huku wengine wakikaa tu. Walipenda mziki uliochangamka ili wachangamke, lakini hawakuwa na budi sababu shughuli si yao. Madada washawasha walijitahidi kucheza kuichangamsha shughuli waliyokodiwa lakini mziki na uimbaji wa mc yule uliwazingua vichwa vyao washindwe kufanya yao kiustadi kama walivyozoea.

Lakini alipofika Mc Jaba na kundi lake ndipo watu mmoja mmoja walipoanza minong’ono.

“Jamani si yule mc Jaba mwenyewe..?”

“Ndiye..enhee na Dj wake mwenyewe ni yule mrefu…” Watu walibinyana kupashana uwepo wa Jaba. Huku wengine wakimnyooshea vidole kipindi mziki ukiendelea.

Hatimaye sasa haikuwa minong’ono tena bali sauti zilipazwa na wahuni.

“Oyaaaa! Mama shughulii mpeni maiki mwanetu Jabaa aaamshe popooo! Sio muda wa kudevela devela huu”

Sauti hizi zilipozidi kupazwa na vijana chata mbaya zilimuogopesha mama shughuli na kuona endapo akipinga zaidi inaweza kutokoe vurugu. Ndipo hapo aliposimamisha mziki kwa mc wake aliyemkodi tokea Mbagara na kutangaza.

“Jamani mc Jaba la baja, tunakuomba na kukukaribisha kwenye shughuli yetu utubarikie japo kidogo.” Alitangaza mama yule na kusababisha miluzi kwa masela na wahuni kibao wa kitaa. Mc kutoka mbagara hakupenda hata kidogo lakini ilimbidi ampishe Jaba na mtamboni akaingia Dj Dudu Kila mtaalamu wa kuchezea ‘vitual dj’ ambapo alichomeka flash yake aliyokuwa anatembea nayo muda wote na kuchagua nyimbo zao za kufanyia balaa.

“Hii hapa sasaaaaaa sauti ya Mc Jaba… Jaba wa ukweeeeeelii..Jaba la bajaaaa! Eeeh wanangu wagiliki ee wagiliki.. wapi watoto wa Bichi boooiiiz, eeh Side kichecheee wasalimie watoto wa bondeni kwa Mandeeeeeeraa! Weeee dogo Choloo wape hai watoto wa Nyamiela…bila kuwasahau wanangu wa Andalaini…..tunawasha moto kama kawa kama dawaaa…Miluzi basi kidogo wahuniiiiiii…..Wachafu kempuuuuuuu! Choooma na washa washaaa watoto wa jijiiiii! Weee dj Dudu kilaaaaa…Bwiiiiisaaaaaaaaaaaaaa..”

Alianza kufanya yake mc Jaba huku dudu kila akichagiza mbwembwe zake za kucheza na vitual dj.

Mambo sasa yakawa mambo kwenye kigodoro….Moto ukawaka!

“Hii hapa sasaaaaaa sauti ya Mc Jaba… Jaba wa ukweeeeeelii..Jaba la bajaaaa! Eeeh wanangu wagiliki ee wagiliki.. wapi watoto wa Bichi boooiiiz, eeh Side kichecheee wasalimie watoto wa bondeni kwa Mandeeeeeeraa! Weeee dogo Choloo wape hai watoto wa Nyamiela…bila kuwasahau wanangu wa Andalaini…..tunawasha moto kama kawa kama dawaaa…Miluzi basi kidogo wahuniiiiiii…..Wachafu kempuuuuuuu! Choooma na washa washaaa watoto wa jijiiiii! Weee dj Dudu kilaaaaa…Bwiiiiisaaaaaaaaaaaaaa..”

Alianza kufanya yake mc Jaba huku dudu kila akichagiza mbwembwe zake za kucheza na vitual dj.

Mambo sasa yakawa mambo kwenye kigodoro….Moto ukawaka!

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments