Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi : Mfungwa (Prisoner) Sehemu Ya Kwanza (1)



IMEANDIKWA NA : JAFARI MPOLE

*********************************************************************************

Ndani ya Gereza La Oregon nchini Marekani msafara wa magari ya Polisi likisindikiza gari la Wafungwa ambalo liliwasili na kushuka askari lukuki na kuweka ulinzi wafungwa wakafunguliwa mlango wa gari na kuanza kushuka wakiwa na pingu kila mmoja huku chini wakifungwa nmyororo wa pamoja mrefu kwenye miguu yao ya kulia. Waliongozana kwa pamoja hadi kuingia ndani ya Gereza hilo ambapo kitendo cha wao kuwasili tu mule ndani wafungwa waliokuwa humo ndani wakaanza kuwapigia makofi huku wengine wakiwazomea na kuwashangilia. Wale wafungwa wageni ikabidi washangae hali ile akiwemo kijana Albert ambaye ni raia wa kitanzania aliyekuwa akiishi huko nchini Marekani kwa miaka mingi na haikujulikana ameingia leo Gerezani hapo kwa kosa lipi.

Yeye na wenzake wageni walianza kuangalia mandhari ya pale Gerezani kwa nje,hakika lilikiwa ni gereza kubwa sana na muda huo ulikuwa wa mapumziko kwa wafungwa kuwa nje wakifanya mazoezi na michezo mengine kwa aliyehitaji. Wafungwa wageni walisogezwa sehemu na kunyoosha mstari mmoja sawa kisha akawasili Mkuu wa jela na kusimama mbele yao.


"You are welcome into the Oregon prison,here is your new home,follow the jail law and follow it all in the jail this is one of the rules and each of you knows it, so I would like to understand early each one of You, I hope for peace from you, thank you. (Mnakaribishwa gerezani ya Origon, hapa ni nyumba yenu mpya, kufuata sheria ya jela na kufuata yote ndani ya jela hii ni moja ya sheria na kila mmoja anajua, hivyo ningependa kueleweka mapema kila mmoja wenu, Nina matumaini ya amani kutoka kwenu, asante."alisema Mkuu wa Gereza aliyefahamika kwa jina la Mc.Donald na baada ya kuyasema hayo aliondoka zake huku nyuma askari watatu wakimfuata kama kumlinda.


Mkuu msaidizi alitoa amri wafungwa wale wapya wapelekwe moja kwa moja kupatiwa sare za gereza hilo pamoja na kupangwa kwenye vyumba watakavyokaa kila mmoja wapo.Kijana Albert alibaki kutazama tu ukubwa wa gereza lile wakiwa wanatembea kuelekea sehemu ya kukabidhiwa vifaa vya kuanza maisha ya gerezani. Vyumba vingi sana vya wafungwa vilionekana humo huku kila kona kukiweka Camera kuhakikisha wanaona kila kinachoendelea kwenye Gereza hilo.

Aliona wafungwa wa kizungu tu humo wengi sana wakiwatazama wakiwa wanaingia huku wengine wakiwaonesha vidole vya matusi na wengine wakiwadhihaki kama ilivyo kawaida kwenye Magereza duniani. Walipozidi kwenda mbele akabahatika kumuona mtu mweusi ambaye aliokuwa amejitoboa masikioni na kuweka vipini hata puani naye akiwa anamtazama Albert akiwa anatembea na wenzake wakiwa kwenye minyororo na pingu hadi walipofika ndani ya chumba kimoja wakafunguliwa pingu wote na minyororo mguuni na kuagizwa kupanga mstari mmoja na mmoja mmoja akaanza kuitwa na kupokea beseni lililokuwa na sare ya jela zikiwa na namba kabisa ya mtuhumiwa, taulo,sabuni ya kuogea na vitu vengine vidogo vidogo. Askari aliyekuwa akitoa huduma hiyo alikuwa akiita Namba ya sare utakayopewa hivyo halitatambulika jina lako zaidi ya namba yako tu popote pale ndani ya gereza. Walizidi kupewa vitu hivyo na kijana Albert alipofika zamu yake askari alimtazama na kumpatia vifaa vyake kisha akaongozana na wenzake waliokuwa wakipangiwa magereza ya kukaa. Aliongozana na askari mmoja hadi kwenye sero namba 141 na kufunguliwa akaingia humo kisha mlango ukafungwa.


"Stay here until your fellow back.(Ukae hapo mpaka wenzako watakaporudi)."alisema Askari yule na kugeuka kuondoka zake.

Albert alitua Beseni lake na kuanza kuangalia sero ile ilivyo kisha akaanza kutoa toa vitu vyake na kuvipanga. Alitazama pembeni na kuona kuna nguo za mfungwa mmoja zikiwa pembeni na biblia na vitabu vengine vya dini. Akajua mmoja wa wafungwa waliokuwa wanakaa mule ni mtu wa dini,hakujali sana akaendelea na mambo yake.


Dakika kumi baadae kengele ilisikika ikilia mfululizo na kuwafanya wafungwa wote waliopo nje ya gereza wakiwa kwenye michezo na wengine wakipunga upepo wakaanza kuingia ndani kila mmoja akaelekea zake kwenye chumba chake kama ilivyo kawaida. Aliingia mzungu mmoja mwenye asili ya nchi ya Russia na kumkuta Albert akiwa amekaa wakawa wanatazamana. Dakika chache akatokea mfungwa mwengine akiwa ameshikilia rozali na moja kwa moja alipoingia tu akaenda kwenye kitanda na kukaa.


Alimtazama Albert kwa muda kisha akamsogelea na kumfunua shati lake bega la kulia na kukuta alama ya Nduli,alitabasamu sana.

"Karibu Oregon,mimi pia ni muafrika ila ni mkenya naitwa Simon."alijitambulisha yule kijana na kumfanya Albert atabasamu baada ya kuona ni jirani yake kabisa na anaongea kiswahili vizuri.


"Asante sana aisee. Naitwa Albert."alijitambulisha Albert.


"Ninyi ni swahili wote?"aliuliza yule Mrusi aliyekuwa akimtazama Albert pindi alipoingia na kumfanya Albert ashangae kuona ameongea kiswahili pia.


"Yes he is Tanzanian. He speak swahili well as his language, his name is Albert.(Ndio yeye ni mtanzania,anaongea Kiswahili kama lugha yake,anaitwa Albert."alisema Simon na kumfanya mrusi yule atabasamu.


"Ahaa safi, Albert jambo. Karibu Oregon. Oregon ni gereza letu,ni nyumbani,mimi jina ni Johnson nipo hapa five years ago. Siwezi toka nimehukumiwa for life until death."alisema yule mrusi aliyejitambulisha kwa jina la Johnson.

Albert alimuonea huruma Johnson baada ya kujieleza kuwa yeye ni mtu wa jela tu mpaka kifo chake, amekuhukumiwa kifungo cha maisha jela.


"Pole sana Johnson ,usijali lakini kikubwa ni uzima tu na kumuomba Mungu katika kipindi chote."alisema Albert na kunyanyuka kumshika bega Johnson kama kumfatiji.


"Okay ni muda wa kupumzika jamani huu Askari akipita akituona bado tunapiga zogo hapa ni balaa lengine."alisema Simon na kupanda kitandani akajilaza huku akiwa aeshka biblia. Johnson naye alipanda juu ya kitanda hicho vilivyo bandana(double deck) naye akajilaza ambaye alijikuta akitokwa na machozi akifikilia maisha yake.


Albert naye aligeukia pembeni na kuona kitanda kimoja pembeni akasogea na kujilaza akifuata sheria kama alivgoambiwa na wenzake. Alishusha pumzi na kukumbuka mambo yake ya nyuma na taratibu usingizi ukamchukua.

Akiwa kwenye usingizi kuna ndoto moja ilimjia.


Siku hiyo alikuwa akirudi zake kwake mjini LAS ANGLES akiwa anakaa na mpenzi wake raia wa kimarekani aitwaye Angela. Siku hiyo aliandaa zawadi ya pete ya uchumba kuweza kumvisha mpenzi wake,alipofika kwenye nyumba waliokuwa wakiishi alianza kunyata taratibi kama kumfanyia Suprise Angela bila kuwasha taa. Lakini kila alipozidi kuingia ndani zaidi ukimya uliopo mule ndani ukamfanya hata yeye awe na wasiwasi japi uso wake ulijawa na furaha ya siku hiyo. Gafla taa ikawashwa na mtu tofauti na kumfanya Albert ashtuke alipogeuka nyuma. Alihamaki baada ya kuona watu watatu wakiwa wamemteka Angela kwa kumfunga kamba mikononi huku wakimuonesha Bastola Albert kumuweka chini ya ulinzi.

"We do not have time to lose here, tell us the CSI FILE Password, otherwise cute Angela is going die.( Hatuna muda wa kupoteza hapa, tuambie neno siri la faili la CSI vinginevyo mrembo Angela anakufa."alisema kijana mmoja wa akionesha kuwa ndio mkuu wa kundi lile akiwa amenyooshea bastola Albert. Mmoja wao akatoa laptop haraka haraka na kuiwasha kisha akaanza kufungua faili lililoandikwa CSI na kumgeuzia Albert ambaye hakutaka kufanya kile wanachohitaji. Kuna siri nzito ndani ya faili hilo na ni yeye pekee ndiye anayefahamu Password za kufungua hilo file. Alimtazama Angela wake akiwa amejeruhiwa usoni damu zikimtoka,hakika anampenda sana na hakutaka kabisa adhurike.


"Please Albert please,dont tell them about it,dont think about me Albert there're many important things in CSI,Please dont show them.(chondechonde Albert usiwaambie chochote,usinifikirie mimi kwasasa kuna mambo muhimu sana humo kwenye CSI,tafadhari usiwaoneshe)."alisema Angela na kusikia ngumi ya tumbo ikitua kwa uzito wa aina yake. Hapo ndipo walipomtonesha Albert baada ya kujua mpenzi wake huyo yumjamzito wa miezi mitatu. Alipotaka kufanya fujo zilikokiwa mashinegan na kuanza kupiga risasi kadhaa pembeni ya mrembo Angela wakimaanisha hawatanii hali iliyomfanya Albert asitishe fujo.


"Okay fine...fine...i'll show you.(Sawa basi...sawa..nitawaonesha)."alikubali Albert kuwaonesha Password zile ili tu wamuache Mpenzi wake aliyekuwa akiugulia tumbo pale chini. Haraka akaichukua ile laptop na kuanza kuingiza Password za kufungua file lile huku akiwaonesha kabisa namba hizo na faili hilo likafunguka. Walimpokonya laptop hiyo na kutazama yaliyomo kweli wakakuta Documents za siri ambazo walikuwa wakizihitaji muda mrefu.

Walipiga simu kwa mkubwa wao wa kazi kumueleza kuwa wamefanikiwa,alifurahi sana kusikia hivyo.

"Just play a smart game.(Cheza mchezo wenye akili)"ilisikika sauti ya bosi huyo akiongea na mkubwa wa kikundi hicho ambaye baada ya kuambiwa hivyo akajua nini afanya.

Abert alimsogelea mpenzi wake pale na kuanza kumliwaza kwa kumpa pole. Wale watu baada ya kukamilisha zoezi lao waliweka mambo sawa na kuchukua chupa nzito ya bia na kumtwanga nayo Albert kichwani papo hapo akaenda chini na taratibi nuru ikaanza kufifia machoni. Angela kuona vile alilia sana kuona mpenzi wake ameumizwa vile na yule jamaa akanyanyua bastola yake na kumnyooshea Angela bila mwenyewe kufahamu. Albert alisikia tu sauti ya mpenzi wake kwa mbali akilia na punde tu akasikia mlio wa risasi mbili, papo hapo akaona mpenzi wake Angela akidondoka chini karibu ya Albert ambaye kwa mbali alipata kuona tukio hilo lakini hakuwa na uwezo wa kuamka na punde tu naye akapoteza fahamu.


Baada ya muda alipata kusikia sauti kwa mbali ikimuita jina lake huku akimtingisha,taratibi macho yake yakaanza kufumbua.

"Albert muda wa kula huu amka."ilikuwa ni sauti iliyomfanya Albert anyanyuke pale alipo. Alipoangalia huku na kule akapata kufahamu yupo jela kumbe. Muda wote kumbe alikuwa akiota ndoto ambayo ni tukio lililotokea hapo nyuma. Alishusha pumzi baada ya kukumbuka ya nyuma na kumkumbuka mpenzi wake Angela aliyesadikika kuuawa siku hiyo ya tukio kwa kupigwa risasi. Basi alinyanyuka na kuongozana na wenza Simon na mrusi Johnson kuelekea kula.


Ilikuwa ni sehemu kubwa sana ya wafungwa kukaa mahala hapo baada ya kupokea chakula. Simon ndio alikuwa mbele akimuonesha Albert namna ya kufuata hatua zote wakiwa hapo,na baada ya kuchukua chakula waliongozana na kwenda kukaa sehemu moja wakiwa na Johnson.

Albert alitazama pembeni na kuona kuna wafungwa mabaunsa wakiwa wanawakoromea wenzao hata kuwapokonya chakula. Simon aligeuka naye kutazama hali ile ambayo kwake alishaizoea.

"Wanaitwa #DEVIL_MOB, kila mtu anafawahamu kwa tabia zao hizo,hata hapa wanaweza wakaja na kuchukua chakula wakala wao basi tu wakukwaze ili ukiwabishia wakupige."alisema Simon na kama alitabiri, wale mabaunsa wakawa wanatembea tembea kuchagua tu chakula kipi kinawafaa. Hawakutaka kwenda kukaa kupanga foleni hata siku moja na kwenye kuangaza mbele wakasogea walipokaa wakina Simon wakiwa kimya.

Baunsa mmoja alimtazama Albert ambaye naye alikuwa akiwatazama wakiwa wamejichora matatoo kwenye miili yao meupe . Mmoja wapo alinyanyua sahani ya Johnson aliyekuwa kimya tu na mwengine akainyanyua sahani ya Albert kisha wakageuka kuondoka zao. Wakina Simon na wenzake wakawa wanawatazama tu wale watu lakini Albert alipowaangalia kwa makini akapata kuona alama ya tatoo moja ikiwa pembeni ya shingo yao. Akaikumbuka ile alama aliiona siku ile mpenzi wake Angela aliuawa na wale watu walikuwa na alama hiyo hali iliyomfanya haraka anyanyuke.


"Hey...!"aliita Albert na kuwafanya watu wote wageuka kumtazama. Hata wenzake Simon na Johnson walishangaa wakijua amewasimamisha wale mabaunsa kwasababu ya chakula kile kilichochukuliwa. Haikuwahi kutokea hata siku moja wakazuiwa au kusimamishwa hivyo sauti ile iliwafanya kundi la #DEVIL_MOB wasimame na kugeuka nyuma.


SEHEMU YA 02


Simon kuona vile akajua kutatokea vurumai muda si mrefu.

"Albert kaa chini haraka watakuja hao kukuumiza. Kaa haraka..!"alisema Simon kwa sauti ya pole pole akimtaka mwenzake akae chini.Hata Johnson ikambidi amkanyage mguu Albert kama kumtonya kuwa akae chini lakini mwenzao hakuwa akiwaza wanavyodhani. Mawazo yalikuwa kwa mpenzi wake Angela ambaye watu wenye tatoo ile ndio waliomuua mrembo hiyo hivyo alijawa kama na mshangao baada ya kuiona tattoo ile kwa yule baunsa.

Wale mabaunsa walipomuoma kuwa ni Albert wakajua kuwa amechukia kwa kuwa wamempokonya chakula. Taratibu huku sura zao zikionesha kuwa na hasira wakaanza kurudi mpaka pale Albert aliposimama Albert. Simon kuona swala hilo litakiwa ni balaa kwa mwenzake ikabidi asimame huku akielekeza rozali yake mbele kuomba amani.


"Sorry for what happened, this guy is a new prisoner so he does not know anything about you, I stay with him one room so I'll let him know everything about DEVIL MOOB. (Samahani kwa kilichotokea, huyu ni mfungwa mpya kwa hivyo hajui chochote juu yenu, nakaa pamoja naye chumba kimoja hivyo nitamjulisha kila kitu kuhusu DEVIL MOOB)"alisema Simon na kuwafanya wale mabaunsa wamgeukie yeye kumrazama akionesha kutabasamu hana wasiwasi.

"Pastor...try to rub your sheep,another day we'll kill him.(mchungaji... Jaribu kumchunga kondoo wako,siku nyengine tutamuua"alisema yule baunsa na kugeuka zake na kuondoka huku wenzake wakimkata jicho Albert kisha nao wakaondoka. Wafungwa wote pale kantini walikuwa wakiwatazama tu huku kimya kikitawala hadi walipoondoka wale DEVIL MOOB. Simon aligeuka kumtazama Albert.


"Aisee hawa watu sio wa kuwasimamisha wala kuongea nao hovyo wanakufanyia kitu mbaya dakika tu."alisema Simon huku Albert akitazama tu kule walipoelekea wale mabaunsa.Aligeuka na kumshika Simon mabegani.


"Simon hebu niambie hawa watu wana muda gani humu gerezani.?"alisema Albert na kumfanya Simon amtazame.


"Nilipofika hapa miaka sita nyuma niliwakuta. Huenda Johnson anajuwa wana muda gani hapa."alisema Simon.


"DEVIL MOOB...hawa ni miaka mingi hapa, I think like 12 years(nafikiri kama miaka 12)."alisema Johnson na maneno yale yakamfanya Albert anyon'gonyee na kukaa chini kwenye kiti. Wenzake nao wakakaa huku wakimtazama.


"Luna kitu unafikiria kuhusu wao?"aliuliza Simon na kumfanya Albert akumbuke yale mauaji ya mpenzi wake Angela kila akijaribu kivuta picha ya wale watu waliokuwepo kwenye tukio lile hakuweza kuwafananisha na hawa mabaunsa.


"Nimeona Tattoo shingoni mwa yule jamaa, na tattoo ile niliioona pia shingoni mwa watu ambao waliweza kunifanya mimi nikawa humu jela sasa, na ndio maana nilisimama baada ya kushangaa kuona tattoo ile na sio kwaajili ya chakula walicho chukua."alisema Albert na kuwafanya wenzake wajue kumbe alikuwa na maana nyengine kabisa ndio maana alisimama na kuwaita wale mabaunsa.


"Nini tatizo Albert la wewe kufika humu?"aliuliza yule Mrusi Johnson na kumfanya Albert amtazame. Alifahamu mzungu huyo yeye ni mtu wa jela tu maisha yake yote hivyo hakuona haja ya kumficha.


"Hao watu wenye hiyo tattoo walivamia nyumbani kwangu ambapo nilikuwa nikiishi na mpenzi wangu ambaye alikiwa ni mjamzito wa miezi kadhaa. Nahisi walitumwa na watu fulani ambao walikuwa wakinifuatilia sana kutaka kitu kufoka kwangu,mimi ni mtaalamu wa mambo ya mitandao na katika tafiti zangu nikapata kutambua kuna faili moja ambalo ni la siri ya watu watu watatu ambao wanataka kuipindua Kampuni kubwa hapa Amerika ifilisi kila kitu ili wapate kukaa wao waanzishe biashara zao. Hivyo kila process (hatua) walizopanga kuzifuatilia kukamilisha zoezi lao ndio zipo kwenye hilo file la CSI ambalo ni jina la hao watu watatu, Chris, Silvester na mdada Isabella ambaye ni mtoto wa tajiri maarufu hapa LOS ANGLES."alisema Albert na kuwafanya wenzake wawe makini kuendelea kusikiliza.


"Ilikuwaje hadi ukafahamu hayo yote kuhusu file hilo?"aliuliza Simon na kumfanya Albert akumbuke.


"Kuna siri kubwa hapa kati Simon ila tambua tu kwamba hawa watu wameniulia mpenzi wangu. Na mimi hadi kufika hapa ni kwaajili yao. Walipomuua mpenzi wangu walinipiga na kuzimia hivyo najikuta nipo mikononi mwa Polisi nikidaiwa kumuua eti mpenzi wangu. Inamaana walinisakizia kesi ile na kila nikipojaribu kujitetea nikaona nakosa uhuru wa kuongea na kujikuta napata kifungo cha miaka 15 jela. Wewe unadhani nitakubali kukaa humu hali ya kuwa waliofanya mauaji wapo uraiani wanakula vizuri."alisema Albert na kumfanya Simon ahamaki kwa maneno yale.


"Oh my God. So what do you want to do?(Mungu wangu.. kwahiyo unataka kufanya nini?)"aliuliza Johnson baada ya kumsikiliza Albert anbaye swali lile lilimfanya ameze funda moja la mate likashuka kooni taratibu na kushusha pumzi huku Johnson pamoja na Simon wakimsikiliza kwa makini.


"Kuna mtu mdogo wangu nilishampanga juu ya kesi hii na analifanyia kazi jambo fulani. Kuna Plan ambayo tuliipanga juu ya swala hili, hawa watu naamini watanifuata mpaka huku wanimalize maana nina kitu ambacho ni muhimu sana kwao. Na ndio maana kwa kulijua hilo mambo yote nimemuachia dogo naamini analifanyia kazi swala hili“alisema Albert akiwa anatizama sahani iliyokuwa na chakula pale mezani.


“Kuna jambo umeamua kufanya hapa jela?“aliuliza yule mzungu Johnson na kumfanya Albert amtazame huku akitabasamu.


“Mapema sana Johnson, tuleni bwana“alisema Albert na kuvuta sahani ya chakula cha Simon akaanza kula na wenzake wakaungana naye.


JOMO KENYATTA AIRPORT (KENYA)


Kijana Ernesto alikuwa akiwasili kutoka nchini Tanzania. Alipokanyaga kwenye ardhi ya Kenya moja kwa moja akaelekea kwenye Taxi na kutaka apelekwe mtaa wa Embakasi ambapo kuna mtu ambaye anahitaji kukutana naye ili wazungumze mambo fulani. Akiwa ndani ya Taxi hiyo alitoa laptop yake na kufungua kisha akaanza kusoma ramani ya mtaa huo uliopo katikati ya jiji. Kwa utundu na taaluma aliyo nayo katika swala zima la kuchezea kompyuta na vitu vengine kama hivyo aliweza kuunganisha na kifaa fulani ambacho kiliweza kuonesha Taxi ile aliyopanda inapoelekea na njia anazopotishwa. Alipohakikisha anapopelekwa ni sahihi akatoa foni zake kwenye begi na kuziwe masikioni baada ya kuunganisha kwenye simu yake kisha akaegamia kiti kujipumzisha akisikiliza muziki. Dereva alikuwa akimtazama tu kupitia kioo chake kidofo cha mbele.


“Karibu sana Kenya. Bila shaka wewe ni Mbongo?"alisema yule dereva akiwa anaendesha gari yake.


“Nahitaji kupumzika dakika 37,nadhani ndio tutakuwa tumefika Dandora."alisema kijana Ernest akionesha kutotaka kusumbuliwa.

“Atii wabongo wana dharau. Khaah."alijisemea mwenyewe yule dereva baada ya kujibiwa vile huku akiendelea kuendesha gari huku akitazama saa yake ilikuwa ikionesha imefika saa 9 na dakika 23 mchana.


Watu wa mji huo walikuwa pilika pilika za kila siku, kila mtu akipambana kutafuta riziki kwa namna yake.

Ndani kidogo na mtaa wa Dandora kulikuwa mahala ambapo ni kama madarasa ya wanafunzi kusomea, ilikuwa ni sehemu maalumu ambayo wanafunzi wanapata masomo ya ziada (tuition) baada ya kutoka mashuleni. Na baada ya muda kupita ile Taxi iliweza kuwasili maeneo hayo na kupaki sehemu. Ernest alinyanyuka baada ya kufika,aliweka vitu vyake sawa kisha akashuka zake na kumfuata dereva wake.

“Aisee unaonekana unajali muda sana, zile dakika zako 37 ndio tumefika hapa eneo husika."alisema yule dereva na kumfanya Ernest atoe wallet yake ya hela.


“Naomba nilijibu swali lako sasa hivi maana muda ule nilikuwa nahitaji kupumzika“alisema Ernest kisha akatoa noti tano za elfu kumi kumi za kitanzania na kumpatia yule dereva.

“Asante kwa usafiri wako.“alisema Ernest na kugeuka zake akaelekea maeneo ya yale madarasa. Yule dereva alipozitazama zile pesa akafahamu ni shilingi elfu 50 za kitanzania. Alibaki akimtazama tu abiria wake yule huku akitabasamu baada ya kujua amejibiwa sesi lake kwa noti ikimaanisha yule abiria ni Mtanzania. Aligeuza gari yake na kuondoka zake na muda huo huo milango ya madarasa ilifunguliwa wakaanza kutoka wanafunzi wakubwa walionekana ni wa Level ya juu. Ernest alibaki ameshikilia begi lake tu akitazama wanafunzi wengi wa rika lake wakiongozana kuondoka zao na mwishowe akatokea Mwalimu mwenyewe akiwa ameshikilia vitabu vyake akiongoza njia ya kuelekea nyumbani kwake baada ya kumaliza darasa. Ernest alijiweka sawa na kujifanya kama mwanafunzi akaanza kutembea kwa haraka hadi alipomfikia Mwalimu yule.


“Teacher wacha nikubebee books."alisema Ernest akibadili kabisa lafudhi na kuongea lafudhi ya kikenya kumtaka amsaidie mwalimu yule vitabu.


“Ohoo asante kijana. You are so kind hadi naona furaha."


“Asante teacher ni kawaida kusaidia mkubwa."


“Si kwa vijana wote hasa Kenyan. Hawana heshima ya aina hii may be itokee ni bahati tu."alisema yule mwalimu.


“Basi mimi ni tofauti na hao, naheshimu yule aliye juu yangu.“alisema Ernest wakiwa wanatembea na mwalimu huyo huku wakiendelea kuongea hadi walipofika nje ya jengo moja la kupanga ambapo mwalimu huyo alikuwa akiishi humo mwenyewe.

Kijana akamkabidhi vitabu walimu huyo na kuagana akaondoka. Erne alipifika mbele akatazama mahali ambapo ni karibu na mwalimu huyo.Pembeni upande wa pili kulikuwa na Motel kubwa yenye gorofa tatu hivyo ilimbidi aelekee na kukodi chumba kuweka makazi yake kwa muda.


Hata alipopata chumba akaingia na kuweka begi lake kwanza kitandani na kusogea kwenye dirisha akitazama kwa chini na kuona mji wa Embakasi ulivyo. Kwa mbele yake ndipo jengo ambalo Mwalimu yule alikuwa amepanga naye kwenye Hotel moja yenye gorofa zipatazo nne na kwa bahati alipata kuona chumba ambacho mwalimu alikuwepo maana alionekana naye kufungua vioo vya madirisha.


“B I N G O O!"alifurahi Erne baada ya kuona vile, haraka akarejea zake pale kitandani na kuanza kufungua begi lake akatoa vitu vitu mule vikionekana vifaa vingi vya mambo ya mitambo.


Alianza kuviunga na kuviweka sawa kisha akachomeka kebo kwemye swichi na kuunganisha waya mmoja kwenye laptop yake kisha akaiwasha. Alichukua dalubini yake na kurejea pale dirishani na kuanza kuangaza kule alipo mwalimu yule huku akisogeza karibu kabisa aone vizuri kupitia darubini.

Alishuhudia tu kuona mule ndani mwalimu akizunguka zunguka kwenda huku na kurudi akionekana kuwa bize na jambo fulani. Alimuacha na kurudi zake pale kitandani akasogeza laptop yake na kuanza kupekua pekua ndani yake.Alitafuta maelezo ya ule mtaa aliofikia na kupekuwa hata lile gorofa alilofikia kwa jina na kulipata na kutambua yupo kwenye mahala pa namna gani. Alipo yakamilisha hayo alijilaza kitandani kwa kupumzika huku akitafari jambo.


Ndani ya kampuni moja ya siri iliyoundwa na Tajiri wa kimarekani Mr.Macklen ambaye ameifanya kampuni hiyo kuanza kujulikana gafla ndani ya marekani kwa kutoa ajira. Hakuishia hapo alivuka hata barani Africa na kuweka wigo la biashara zake kwa kulitangaza jina la kampuni yake ya M O L E N katika baadhi ya nchi za Africa zikiwepo Kenya na Tanzania, aliajiri vijana wengi sana wenye taaluma ya IT (Information Technology) ambao walikuwa ni wataalamu wa kucheza na teknologia ya mitandao.


Zilitolewa nafasi 6 tu nchini Tanzania za watu wanaohitaji kazi katika kampuni hiyo na miongoni mwa vijana walio wania kuhitaji kupata ajira ndani ya kampuni hiyo alikuwa ni Ernest. Alijitahidi kwa uwezo wake kuhakikisha nafasi hiyo anaipata lakini uwingi wa watu walioweza kufika mahali hapo ukamfanya ashindwe kupata nafasi hiyo na kampuni ikafanikiwa kuwapata watu wao 6 walio wahitaji.

Walipomaliza zoezi hilo Tanzania wakajiandaa siku tatu mbele waelekee sasa Kenya kumalizia zoezi hilo la kuajiri vijana kadhaa. Dodoso hizo za ajira alizipata kijana Ernest na kuona asikate tamaa. Siku ambayo anafanya mpango wa kutoka Tanzania kuelekea Kenya kwaajili ya kujaribu tena nafasi ya kupata kuajiliwa na kampuni hiyo ya M O L E N alipata kufuatwa na jamaa yake ambaye wote ni watu wa kupeana madili ya kufanya kama watoto wa mjini ili kufanikiwa kupata pesa kuendelea na maisha. Walikaa na kuongea kuhusu mpango kabambe ambao unaendelea.


“Sasa sikia Ernest. Kuna ticha mmoja anaitwa Otieno anafundisha vijana wa vyuo ni kama tution. Huyo ticha aliwahi kwenda Marekani na akafungwa kwenye gereza la Origon miaka kama 10 na amerejea nyumbani kwao Kenya na sasa ni Mwalimu mzuri tu. Huyu anafahamu vyema jengo lile lilivyo anaweza akasaidia katika harakati zetu.“alisema kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar.


"Fanya namna yeyote huyu mtu ujenge ukaribu naye kwa siku chache kabla ya kuanza mchakato wa kuajiriwa na ile kampuni. Siku hizo tumia njama yeyote hata umueleze ukweli tu akupe ramani kamili ya mchoro wa gereza lile halafu tutajua tufanye nini.“aliyasema hayo Oscer akimueleza Ernest ambaye alikuwa akiweka vitu vyake vya kubeba kwaajili ya safari ya kuelekea Kenya.


"Nimekuelewa best. Wacha nikaifanye hii kazi, nikutakie siku njema uwe karibu na System kwa mawasiliano zaidi."alisema Ernest akiwa anavaa begi lake mgongoni.


"Usijali sisi ni team hakitaharibika kitu.“alisema Oscar na kukumbatiana kisha Ernest akaanza safari ya kuondoka zake.


Yote hayo alikuwa akiyakumbuka Ernest akiwa pale kitandani amejilaza.

"Brother. They kill our family. Nimejitoa akili na ndio maana ni mzima mpaka leo, wananiita AKILI MBILI kuwa sina akili kabisa zimebaki akili ya kula na kulala, ila watalipa kwa hili walilofanya.“alisema Erne akiwa anatokwa na machozi ambayo yaliyo lowesha shuka kitandani mara baada ya kukumbuka matukio ya nyuma kuhusu familia yao.

Ernest ndiye pacha wake kabisa na kijana Albert ambaye yupo ndani ya Gereza la Oregon nchini marekani akihukumiwa kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Angela.



Kule Gerezani Oregon, Albert alikuwa akiendelea kuzoeshwa mambo na wenyeji wake Simon pamoja na Mrusi Johnson. Walimpeleka sehemu mbalimbali ndani ya lile gereza na kumuonesha baadhi ya makundi ambayo ni zaidi ya Mafia ndani ya gereza hilo hivyo anapaswa kuwa muangalifu.Wakiwa kwenye pitapita zao mule ndani lile kundi la DEVIL MOOB lilikuwa likiwatazama tu wakiwa wanapita karibu yao huku wakionekana kununa muda wote. Simon na wenzake walipita kwa upole bila kugombana na mtu hadi walipo waacha mbali.

“yaani wale jamaa si wakuwachezea kabisa humu ndani hata wakuonee vipi wewe kausha tu watafanya ubabe wao wataondoka.

“alisema Simon huku Albert akigeuka kuwatazama kwa mbali wakionekana kujenga duara wakijadili mambo yao.


"Mkubwa wao ni yupi pale kati yao?"aliuliza Albert huku akigeuka kuwaangalia wale watu bila hata kupepesa macho.

"doooh usiwaagalie hivyo sasa watashtuka watufuate tena hapa."alisema Simonna kumshika bega Albert akimgeuza watazane.

"watazame kwa kuibia ibia Albert hawa watu ni hatari sana, yule aliyejichora matatoo mengi na kipini puani ndio mkubwa wao. Juzi tu inasadikika kaua mtu huko ndani toilet lakini hakuna kilichoendelea hadi sasa."alisema Simon akiwa anamueleza Albert ambaye alikuwa akisikiliza kwa makini. Aligeuka tena na kumtazama tena yule mkubwa wa kundi lile aliyesadikika kufanya mauaji siku iliyopita.

Basi walizidi kuongea mambo mengi pale na kuda wa kurejea kwenye sero zao ulipowafia walirudi na kila mtu akapumzika baada ya usiku kuingia.Albert hakuwa hata na lepe la usingizi siku hiyo kika akikumbuka tukio la kushambuliwa siku ile ipoamka alijikuta yupo mikononi kwa Polisi na kupewa kes ya mauaje ya mpenzi wake.Aliumia saa akimkumbuka kipenzi chake hadi hasira zinampanda kuona anatumikia adhabu ambayo haimhusu.


Upande wa pili Ernest alikuwa makini sana pale alipofikia. Muda wote alikuwa akitazama kule kwa mwalimu Otieno kutumia dalubini yake aliyo iseti vyema kuielekezea chumbani kwamwaimu hiyo. Alikiwa akimtazama kila anachokifanya mule ndai kwake na hiyo ndip kazi ya awali kuifanya katika mpango waliopanga.Masaa kadhaa mbele taa ikazimwa kwa Mwalimu kuashiria anajipumzisha.Ernest naye akajiridhisha baada ya kuhikisha amelala na yeye akapanda kitandani kuutafuta usingizi.


Asubuhi kulipo pambazuka Ernest alijiandaa na kuwa na muonekano wa kisomi zaidi. Alinyanyua begi lake ambalo alipanga baadhi yq vitabu kisha akavaa miwani n kusogea kwenye kioo kujitazama na kujiweka imara. Alipohakikisha ana muonekano ulio sahihi alitoka zake chumbani na kuanza safari ya kuelekea kule dasani ambapo mwalimu yule amekuwa akifundisha hapo lengo likiwa ni kumzoea mapema.


Hata walipoingia madasani wanafunzi hao walikuwa bize kila mtu na kujifunza. Alipata kuingia mwalimu Otieno ja kuendelea na kipindi na kulichambua somo la Physics vizuri na wanafunzi hao wa chuo wakawa wanamuelewewa vizuri tu. Kwa Ernest kwake ilikuwa kama marudio tu maana yote yaliyofundishwa pale yeye alikuwa anayaelewa hivyo alikuwa akizingatia tu kama mwanafunzi lakini moyoni ana jambo lake. Kwa kujiweka katika mazingira mazuri muda mwingi alikuwa akiuliza maswali ambayo yalikuwa na maana kwenye somo hali iliyomfanya Mwalimu Otieno amtambue mapema na hata kumkumbuka kuwa jana yake tu alisaidiwa kubebewa vitabu vyake.Huo ndio ukawa mwanzo wa mazoea baina ya wawili hao.


Ndani ya Hotel moja yenye hadhi ya kipekee mjini Nairobi waonekana watu wawili wakiwa wamevalia suti zao nyeusi wakiwa na mabegi wanaelekea kwenye chumba kimoja cha hoteli hiyo ambapo ndipo walipofikia. Hata walipoingia ndani waliweka mabegi yao juu ya kitanda na kuanza kuyafungua.Walitoa silaha zao zenye uwezo wa aina yake ja kuanza kuzitandaza kitandani huku kila mmoja akionekana kuwa bize.

Hata walipomaliza wakavua nguo zao na kuvaa nguo zengine kisha kila mmoja akachukua bastola mbili ambazo zina uwezo wakufanya tukio kimya kimya bila ya mlio wa risasi kusikika kwa watu (*silence pistor*).Baada ya kuyakamilisha hayo kwa dakika chache hawakutaka kusubiri tena kujaa mule ndani wakatoka zao na kuanza safari ya kuelekea sehemu waliyo dhamiria kwenda.


Masaa mawili mbele vipindi viliweza kuisha na taratibu wanafunzi wakaonekana kutoka kwenye madarasa kila mtu akishika njia yake kurejea makwao. Ernest kama ilivyo ada yeye alimsubiri mwalimu Otieno pindi atakapotoka aongozane naye. Na ndivyo ilivyokuwa baada ya mwalimu huyo kutoka akapokelewa vitabu vyake na kijana huyo wakaanza safari.

"nimependa sana somo la leo mwalimu hakika nimeelewa kwa weledi mkubwa."alisema Ernest akiwa amejenga tabasamu.

" waooh nice boy, kama utakuwa ume enjoy somo langu naamini hata wengine wamelipenda pia,ni vizuri."alisema mwalimu Otieno na mazungumzo mengine yakaendelea.

Wakiwa wanaendelea na safari zao yao mwalimu alihisi hali ya utofauti kidogo.Machale yakamcheza na kuhisi kuna watu wanawafuatilia kwa nyuma. Hakutaka kumjuza Ernest wakaendelea na safari yao huku akiwa makini hadi walipofika sehemu ya kuachana na kila mtu akashika njia yake kuelekea kwake.

Ernest alikuwa mwenye furaha baada ya kuona tayari kashamuweka nwalimu Otueno katika rada zake za kumuamini hivyo ni muda wa yeye kufanya jambo alilopanga.Alielekea zake chumbani kwake na kuufungua mlango akaingia ndani.

Lakini muonekano wa mule ndani asubuhi alivyoondoka ni tofauti na sasa anavyoona, alihisi kuna shida imetokea humu ndani na gafla tu muda huo huo akashuhudia bastola ikiweka nyuma ya kichwa chake na kuwekwa telo.

"usithubutu kufanya jambo lolote lile maana sitakuwa na huruma kufyatua risasi ikapenya moja kwa moja kwenye ubongo wako."ilisikika sauti ya mwanaume mmoja na maneno yale Ernest aliweza kutambua kuwa mtu huyo ni mtanzania kwa jinsi alivyoongea kiswahili chake.Ilimbidi atulie tu na kuweka mikono juu kusalimu amri.

Alipita mwanaume mmoja hadi ndani na kuanza kufunga madirisha ya chumba kile huku mwenzake akiwa amemuweka chini ya ulinzi Ernest.

Walivuta kiti wakamuweka akae kisha mmoja wao akikaa naye kitandani kumtazama Ernest huku mwenzake mmoja akiwa ameweka bastola kichwani kwa Ernest.

"majibu yako ya kweli na ya kueleweka ndio yatakayo kuokoa hapa leo vinginevyo unakuwa maiti kwa muda mfupi tu."alisema yule mtu akiwa amekunja sura hali iliyomfanya Ernest ahofie.

" hebu tuambie kuna kitu gani cha siri unakijua kutoka kwa kaka yako?"

"kaka? mnamzungumzia kaka yangu yupi?"aliuliza Ernest na kumfanya yule mtu amrushie ngumi moja ya pua iliyomtoa damu puani Ernest akabaki kuishika pua yake kwa maumivu.

"nilikwambia awali majibu yako ndio yatakuokoa hapa leo, unauliza kaka gani kwani wewe humjui kaka yako Albert? hatuna masihara hapa tutakumaliza tu ukiongea utumbo, narudia tena una kitu gani cha siri unakijua kutoka kwa kaka yako?"aliuliza yule mtu na kushuhudia damu nyingi zikimtoka Ernest puani kiasi cha kumfanya ashindwe kuongea. Walitoa pamba kwenye kisanduku cha huduma ya kwanza kilichopo mule ndani kisja wakaendelea naye kutaka azungumze.

"naomba utujibu haraka."alikazia yule mtu.

"kiukweli mimi sina ninacho kifahamu kutoka kwa kaka yangu, nimepotezana naye muda tangu alipoelekea marekani kutafuta maisha na hado leo sikuweza kujua anaendeleaje, hivyo mnaponiuliza swali hili nakuwa kwenye sintofahamu niwajibu nini zaidi ya kuwaambia kuwa kaka yupo marekani ndio ninachojua."alisema Ernest akiwa ameshika pamba iliyokuwa puani kuzuia damu kushuka.

"umekuja Kenya huku kufaya nini? na ulikuwa unattafuta nafasi ya kuingia kwenye kampuni ya MOLEN ili iweje?"aliuliza yule jamaa na kumfanya Ernest atambue kuwa watu hawa huenda waliluwa wakimfuatilia kwa muda mrefu sana.

"ninahitaji kutafuta maisha, sina kazi na ndio maana niliposikia nafasi za kazi nikataka kuapply ili nifanikie, na ndio maaa sikukata tamaa kukosa nafasi Tanzania nikaamua kuja huku Kenya kujaribu bahati yangu."alisema Ernest kwa kujiamini.

" dogo sikia, sisi tumekuwa tukikufuatilia sana na kujua nyenendo zako, unajua fika kuwa Kaka yako yupo gerezani Oregon na hizi zote njia zakuja huku ni kutaka kumtoa kaka yako. Kwa maana hiyo ni kwabq utqkuwa unajua fika kuna jambo kaka yako analifahamu.Shida yetu kubwa ni kutaka kujua Password za faili la CSI na tunaamini utakuwa unafahamu tu"alisema yule mtu akionesha kuwa siriasi na.jambo hilo.Ernest kusikia habari hizo na kukumbuka matukio ya mauaji ya nyuma katika familia yao akahisi ndio hawa hawa watu waliofanya matukio hayo.

"okay sawa nitawaonyesha lakini laptop yangu ipo kwa mwalimu wangu na ndio documents zote zipo mule nilizihifadhi."

" hakuna kupotezamuda nyanyuka twende" alisema yule mtu aliyemuwekea bastola kichwani na kumnyanyua Ernest waelekee kwa huyo mwalimu kuchukua hiyo laptop.Ernest alikubali tu lakini moyoni anajua amewadanganya hivyo akili yake ni kuwa wakifika huko nje awachoropoke mikononi mwa wauaji hao ambao wanaonekana wapo makini.

💪MBINU ZA KUFUATA ILI KUPATA WAFADHIRI KUTOKA NJE YA NCHI

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments