Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Beyond Love (Zaidi Ya mapenzi) Sehemu Ya Kumi na Saba (17)



“Amini mpenzi wangu...mwambie basi Mchungaji aendelee kwanza, haya mambo mengine tutazungumza wenyewe baadaye,” Tom alisema akiwa haamini kama Mariam hatamkataa, akili yake ilimtuma moja kwa moja kwamba lazima Marim angemkataa ili amuumize kama ambavyo yeye alivyomuumiza siku alipokutana naye Chuo Kikuu alipokwenda kutoa semina ya Ujasiriamali. 


“Mchungaji unaweza kuendelea....” Mariam akamwambia Mchungaji.


“Nini kilitokea?” Mchungaji akauliza.


“Hakuna...” Mariam akajibu.


“Hpana...kuna kitu mnanificha. Kama kuna tatizo liwekeni wazi.”


“Hakuna Mchungaji, niamini mimi, hakuna kitu kingine zaidi ya furaha. Siamini kabisa kwamba leo naolewa na Thomas.”


“Hilo tu.”


“Kwani dogo Mchungaji? Kuolewa na mwanaume ambaye unampenda kwa moyo wako wote, nafikiri ni jambo la baraka sana!”


“Ni kweli kabisa, sasa naweza kuendelea Mariam?’


“Bila shaka.” Maram akajibu akionyesha tabasamu pana kabisa lililochanua vyema usoni mwake.


Muda wote huo Kanisa lilikuwa kimya kabisa, wakisubiri kitakachoendelea. Baadaye Mchungaji akamgeukia Mariam, ambaye sasa machozi yake yalishafutika na alikuwa akitabasamu muda wote kwa furaha. Mchungaji akamuuliza; “Je, Bi. Mariam Isaya, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji akauliza, safari hii akiwa mtulivu sana.


“Ndiyo, Mungu anisaidie!” Mariam alipojibu jibu hilo, ukumbi mzima ulilipuka kwa vigelegele, makofi na vifijo.


Tom hakuamini kama ni kweli Marim alikuwa ameamua kuolewa naye. Aliendelea kuwa na mashaka hadi pale waliposaini pamoja katika vyeti vya ndoa. Baada ya hapo sherehe iliendelea hadi usiku kabisa ambapo meli ilirudi hadi Bandarini, ikatia nanga, wageni wakaanza kushuka na kwenda kuingia moja kwa moja kwenye magari kwa safari ya kurudi majumbani mwao.


Ilikuwa sherehe iliyopendeza sana, huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya ndoa, kati ya Tom na Mariam. 


********


Maisha yao ya ndoa yalikuwa ya furaha sana, lakini tatizo lilikuwa moja tu, Tom alikuwa mtu wa starehe sana. Kila siku alikuwa haishi kwenda kwenye majumba ya starehe na kurudi usiku wa manane. Kisingizio chake siku zote kikawa ni kazi nyingi alizonazo.


Ingawa Mariam alikuwa na elimu nzuri, lakini Tom alimzuia kufanya kazi kwa kisingizio kwamba atamdharau. Siku zote Mariam alikuwa akijitahidi sana kumuelewesha Tom juu ya hilo lakini hakumuelewa.


“Na kwanini unalazimisha sana kufanya kazi?”


“Napenda mume wangu.”


Kuna unachokosa kutoka kwangu?”


“Sina maana hiyo.”


“Sasa kwanini unang’ang’ania kufanya kazi? Mimi nina uwezo na ninakutimizia kila kitu, nini kinachokufanya utafute kazi?”


“Ni vizuri kila mmoja akatoka, unajua ninapokaa hapa ndani nalemaa.”


“Unalemazwa na nini?”


“Lakini kwanini nimesoma sasa kama nilikuwa sina haja na kazi? Elimu yangu inanisaidia nini kama sitaitumikia jamii?”


“Hiyo jamii na mimi, ni nani mwenye umuhimu zaidi kwako?”


“Ni wewe mume wangu.”


“Basi sihitaji ufanye kazi.”


“Nimekuelewa ila kuna kitu kingine nataka tuzungumze.”


“Juu ya nini tena?”


“Tom mume wangu, umekuwa ukichelewa sana kurudi nyumbai, wakatiu mwingine unanikuta nimeshalala kabisa, uwe unajitahidi basi kuwahi kidogo!”


“Mariam una nini leo? Kwanza niwahi kuja kufanya nini? Mimi napika?”


“Hupiki, lakini unatakiwa kuja kula na mimi, ndiyo mapenzi hayo mume hayo mume wangu.”


“Nimekuelewa!” Tom akajibu kwa kifupi kisha akaondoka.


Maisha yao hayakuwa na furaha kama ilivyokuwa mwanzo, Tom alikuwa hana muda maalum wa kurudi nyumbani. Mbaya zaidi alirudi akiwa amelewa sana na hakutaka kula chakula cha mkewe. Jambo hilo lilimkosesha sana raha Mariam lakini hakuwa na jinsi, aliamua kuvumilia akiamini siku moja angebadilika.


*******


Ilikuwa siku ya Jumamosi usiku, ndani ya Ukumbi wa 56 Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watu walikuwa wamejaa sana kushuhudia uzinduzi wa albamu mpya ya Bendi ya Kigingi Music Band ambapo pia mbali na uzinduzi wa albamu yao mpya, pia walikuwa wakiwatambulisha wanamuziki wapya walionunuwa na Tom ambaye ambaye alikuwa akiitwa Papaa Bill.


Pesa haikuwa tatizo, Papaa Bill (Tom) aliwanunua wanamuziki hao kutoka nchini Congo ambapo walikuwa wakifanya kazi katika bendi kongwe za muziki nchini humo, lakini kwa fedha alizokuwa nazo Papaa Bill, aliweza kuwaleta Tanzania na kuwalipa fedha nyingi sana.


Baadhi ya watu walikuwa wakimsikia tu Papaa Bill kwenye vyombo vya habari hasa magazeti na redio, lakini walikuwa hawajawahi kumuona. Kati ya hao alikuwa ni Mayasa. Msichana ambaye alikuwa na hamu kubwa sana ya kumuona Tom.


Mayasa alikuwa na nia zaidi ya kumfahamu, yeye alipanga kumuweka mkononi mwake. Pamoja na kusikia kwamba alikuwa na mke, lakini kwake halikuwa tatizo, alishaandaa mbinu za kutosha kwa ajili ya kumsana Tom. Huyu ni Mayasa wa Mbagala jijini Dar es Salaam.


Usiku huo alikuwa amevalia gauni jepesi sana linaloonesha kila kitu ndani! Kwa mwanaume yeyote ambaye hana matatizo, ilikuwa lazima ashtuke sana pindi atakapokutanisha uso wake na Mayasa. Kiasili alikuwa maji ya kunde, lakini mkorogo ulifanya kazi yake ambapo alionekana mweupe sana isipokuwa kwenye viungio vya ugoko wa miguuni na mikono, ambapo kutokana na ngozi kuwa ngumu sana, haikuweza kuchunika kwa mkorogo!


“Leo lazima nimuone huyo Papaa Bill!” Rafiki yake na Mayasa alisema.


“Bora wewe unayetaka kumuona, miye naondoka naye kabisa...” Mayasa alisema akionyesha kuwa na nyodo za wazi kabisa.


“Haya tuone. Unafikiri Papaa Bill ni sawa na hao wanaume wako wa Mbagala, huyu ni matawi ya juu.”


“Sasa nitajua kama Mbagala ipo Dar es Salaam au Lindi?” Mayasa alisema akionyesha kujiamini sana.


Dakika chache baadaye, wakati wakiendelea na mazungumzo yao, Mc wa siku hiyo, alisimamisha muziki kwanza kisha akamuomba Papaa Bill atoke mbele ya jukwaa ili awatambulishe wanamuziki wapya. Papaa Bill akatoka.


“Ninayo heshima kubwa sana, kumkaribisha Papaa Bill a.k.a Tom ili aje awatambulishe wanamuziki wetu wapya. Kwa taarifa tu ni kwamba, pamoja na kwamba yeye ndiye anayewalipa wanamuziki hao mishahara pamoja na kuwanunua, pia ndiye aliyeenda kuwachukua mwenyewe Congo!” Mc aliposema maneno hayo, ukumbi mzima ukashangilia.


Tom ‘Papaa Bill’ akapanda jukwaani kwa mbwebwe sana, jioni hiyo alikuwa amevalia suruali yake ya jeans ya rangi ya blue na fulana ya kubana ya rangi nyeupe. Mikononi na shingoni alichafuka cheni za madini ya fedha!


“Sina mengi ya kuongea, naomba niwatambulishe wanamuziki wetu wageni ambayo mimi mweny....” Tom alishindwa kumalizia sentesi yake, baada ya kugonganisha macho yake na Mayasa.


“Haki ya nani tena, sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kiasi hiki! Mh...wa wapi huyu?” Tom aliwaza akiwa amezidiwa vilivyo na hisia kali za mapenzi.


Kwa hali aliyokuwa nayo, alikuwa tayari kumsaliti Mariam wake.


“Naitwa Tom....bila shaka mimi ni Tom a.k.a Papaa Bill...namuhitaji huyu mwanamke, ni lazima nilale naye, lazima...” Tom akawaza huku akimtizama kwa matamanio.


Wakati huo Mayasa ndiyo akazidisha vituko, akapandisha gauni lake juu zaidi na kuacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi. Tom akasikiza mwili wake ukipiga shoti!



Tom au Papaa Bill kama alivyojulikana na wengi amekuwa tajiri mkubwa sana nchini Tanzania, pamoja na utajiri wake amejikuta akiwa mtu wa starehe kupita kiasi. Hakuona tabu kutumia fedha nyingi katika sterehe. Alidhamini Bendi nyingi za muziki jijini Dar es Salaam kwa kutumia fedha ili kulinda heshima yake!

Siku moja katika uzinduzi wa Albamu mpya ya Kigingi Music Band, ndani ya Ukumbi wa 56 Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tom alikutana na kitu ambacho

kiliuvuruga ubongo wake kwa muda! Macho yake yalikutana na msichana mrembo sana !

Huyu ni Mayasa, binti wa Mbagala jijini Dar es Salaam, anayejua kila aina ya utundu. Tom akaapa kuondoka naye, hakujua kama Mayasa naye alikuwa akimtega.

Je, nini kitatokea? Tom ataondoka na Mayasa? SONGA NAYO.....

Tom alibaki kimya kwa nukta kadhaa akizidi kumkodolea macho Mayasa ambaye kwa wakati huo vituko ilikuwa sawa na kiitikio kwenye nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya! Alihisi mapigo ya moyo wake kubadilika, alishasahau kwamba alikuwa jukwaani na alitakiwa kuwatambulisha wanamuziki wapya kutoka nchini Congo . Mayasa alishajua udhaifu wa Tom, alichokifanya ni kugeuka nyuma kisha akaanza kutembea kwa mwendo wa madoido akiacha sehemu kubwa ya miguu yake mizuri ikionekana kwa nyuma.

“Duh! Jamani hivi huyu mwanamke yupo katika dunia hii hii ya siku zote au ameshuka? Huyu lazima nitumie fedha zangu,” Papaa Bill akawaza kisha kwa taabu akajitahidi kuanza kuzungumza kwenye kipaza sauti.

“Samahanini sana kwa ukimya wa muda mfupi uliojitokeza, unajua nilikuwa nawaza ni kiasi gani tutakuwa na mashabiki wengi katika hii bendi yetu, wanamuziki niliokuja nao kutoka Congo ni wakali sana na bila shaka watafurahia mazingira ya Tanzania .

“Mimi sitakuwa na mengi sana ya kuzungumza, acha nimpishe Kiongozi wa Bendi, Abuu Sekidevi awakaribishe ili wapenzi wa bendi yetu wawaone,” Tom au Papaa Bill akasema kisha akakabidhi kipaza sauti kwa Mc wa siku hiyo.

Watu wakashangalia sana . Abuu ambaye alikuwa ndiye Kiongozi wa Bendi, akapewa kipaza sauti na kuwakaribisha wanamuziki wapya kutoka Congo .

Walishangiliwa sana .

“Kuna binti alikuwa amesimama pale,

mzuri-mzuri hivi, mweupe sana ni wa wapi?” Tom akamuuliza Jomba ambaye alikuwa mpambe wake.

“Yupi?”

“Alikuwa amesimama pale na wenzake!”

“Amevaa nguo za rangi gani?”

“Gauni jepesi!”

“Aaah! Nilimuona, vipi kwani?”

“Kanidatisha!”

“Kakudatisha?!”

“Ndiyo mkubwa, sasa ustaarabu unakuwaje?”

“Kwa mara ya kwanza nakuona ukianza kuzungumzia wanawake wa nje ya mkeo!”

“Ni kweli lakini leo nimezidiwa, lazima nikubali, sina ujanja!”

“Sasa vipi unamtaka?”

“Tena haraka sana !”

“Nipe dakika kumi tu!”

“Kweli?!”

“Nkuhakikishia!”

“Poa kaka, nakuaminia!”

“Ni kazi ndogo sana kwangu, msubiri sasa hivi anakuja kukaa na wewe meza moja, hayo mambo mengine nakuachia wewe!”

“Mambo gani tena?”

“Kumuimbisha!!”

“Sitazungumza kitu, fedha itanisaidia!”

“Nakuamini kaka!”

Jomba akaondoka akiwa anatembea kwa mbwebwe sana , alikuwa na uhakika wa kurudi na Mayasa, siyo kwa sababu anajiamini, bali alikuwa anamfahamu vizuri sana Mayasa. Siku zote msichana huyo alijua fedha na siyo mapenzi ya kweli.

Hakutembea sana , akakutana na Mayasa akiwa na kampani yake, akasimama mbele yao . Akatabasamu. Mayasa hakupata shida sana kujua kuwa Jomba alikuwa mpambe wa Papaa Bill. Alichokifanya na yeye ni kutabasamu.

“Mambo vipi warembo?” Jomba akasalimia.

“Poaaaaa....” Wote wakaitikia.

“Naona mpo!”

“ Kama unavyotuona!”

“Samahani mrembo, naweza kuzungumza na wewe kidogo?” Jomba akamwambia Mayasa.

“Kuna nini tena?”

“Nisikilize kwanza, mbona unakuwa na wasiwasi kiasi hicho?”

“Siyo wasiwasi, ni vyema nikajua hata dondoo kwanza!”

“Ni ujumbe wako!”

“Poa!” Mayasa akakubali. Wakaenda pembeni kuzungumza.

“Unamfahamu Papaa Bill?”

“Namsikia, kwani vipi?”

“Amesema nikuite!”

“Anataka nini?”

“Mtoto wa kike vipi? Mbona unakuwa na mashaka, twende umsikilize anasemaje?” Jomba akamwambia Mayasa ambaye hakubisha zaidi. Wakaongozana hadi kwenye meza aliyokuwa amekaa Papaa Bill.

Tom alipomuona alichanganyikiwa, kwanza hakuamini kabisa kwamba Jomba alifanikiwa kumleta Mayasa. Msichana huyo akakaa kwenye kiti akitabasamu kwa manjonjo ya kimahaba.


Tom haamini kama msichana aliyekaa pembeni yake ndani ya gari lake alikuwa Mayasa. Hata yeye alijishangaa, kwani hakuwahi kupenda kama alivyompenda Mayasa. Msichana huyo alimwingia akilini mwake kwa kasi ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kupata majibu kila alipojiuliza.“Yaani sijawahi kupenda katika maisha yangu kama ninavyompenda Mayasa, huyu mwanamke ameniingia hadi mimi nashangaa, sijui kuna nini bwana? Lakini hata hvyo ni mzuri sana, naamini uzuri wake ndiyo unanizuzua.” Tom akawaza wakati akiwa anashuka katika bonde lililopo eneo la Mkwajuni, Barabara ya Kawawa, akiifuata barabara inayoelekea Magomeni.“Papaa...” Mayasa akaita.“Vipi baby?”“Naona kama una mawazo, kuna nini?”“Hapana, hakuna tatizo, nipo sawa kabisa!”“Nahisi kuna kitu unajaribu kunificha!”“Hapana...”“Sawa kama hakuna kitu lakini nahisi kama kuna kitu kinakuchanganya akilini mwako, au unamuwaza mkeo?”“Nimuwaze mke wangu wakati nipo na wewe?”“Kwani haiwezekani?”“Nitakuwa mwanaume wa ajabu sana.”“Kwanini unasema hivyo Papaa Bill?”“Kama nilikuwa naona ananifaa, ananitosha, ananiridhisha, ananivutia kwanini nihangaike kukusumbua? Lakini kwasababu kuna mapungufu katika maeneokadhaa ndiyo maana nimeona wewe unaweza kusaidia kuziba hayo mapengo!”“Kwahiyo mimi nipo na wewe kwa sababu ya kuziba mapengo tu?!”“Hapana...amini kwamba nimekupenda lakini wakati huo huo, tambua kwamba nina mke. Wewe utakuwa na nafasi yako kwangu na yeye atakuwa na nafasi yake, pia ni vizuri kila mmoja akaheshimu nafasi ya mwenzake....hasa wewe...” Tom alimwambia Mayasa akionyesha hana masihara kabisa na kilichokuwa kikitoka kinywani mwake.Pamoja na usaliti ambao alikuwa anataka kumfanyia mkewe Mariam, lakini moyo wake ulikuwa na maumivu makali sana. Hakutaka Mariam wake adharauliwe kwa sababu ya mwanamke wa nje, tena aliyekutana naye Club.Tom akaendesha gari kwa kasi alipofika Morocco, kwenye makutano ya Barabara ya Uzuri na Kawawa ambayo alikuwa anaitumia, alikata kulia na kuifuata Barabara ya Uzuri hadi Sinza Kijiweni ambapo alikata kushoto kufuata Barabaraya Shekilango.Kasi ya gari ilikuwa ni ile ile, alibadilisha gia kila baada ya muda, hakuona haja ya kupunguza mwendo kwenye matuta ya barabarani, alikuwa akipita kwa mwendo ule ule. Alipofika kwenye mataa ya Shekilango, akakata kulia akifuata Barabara ya Morogoro ambapo aliendesha gari hadi kwenye mataa ya makutano ya Barabara za Morogoro, SamNujoma na Mandela, hapo alikata kushoto akiifuata Barabara ya Mandela.Hakufika mbali sana, kabla ya kufika RiverSide, akaingiza gari ndani ya geti jekundu,katika hoteli moja nzuri sana. Moja kwa moja wakaenda hadi Mapokezi wakipitia mlango maalum, akalipia chumba na kiupandishwa ghorofa ya nne kwenye chumba chake.“Karibuni sana.” Mhudumu akasema.“Tunashukuru lakini zingatia maadili ya kazi yako.” Tom akamwambia.“Kwanini unasema hivyo bosi?”“Nafikiri unanifahamu vizuri!”“ Ndiyo....”“Ni nani?”“Papaa Bill!”“Sasa sitaki mtu yeyote ajue kuwa nimelala hapa, nenda na hilo kichwani mwako!”“Naheshimu na kuzingatia sana maadili ya kazi yangu!”“Usiku mwema!”“Nawe pia.”Tom aitumia muda mwingi sana kumwangalia Mayasa ambaye alikuwa na sura na umbo la kuvutia sana. Msichana hoyo, akipita sehemu yoyote ambapo kunamwanaume asiye na matatizo yoyote katika via vyake vya uzazi basi lazima asisimke.“Hebu simama.” Tom akamwambia Mayasa.Mayasa akasimama.“Zunguka nyuma!” Tom akamwambia huku akitabasamu na kutingisha kichwa. Mayasa akafanya hivyo.“Sasa simama upande upande!”“Kwani vipi?”“Nataka kukuona vizuri!”“Kwani hukuniona?”“Ndiyo maana nimesema vizuri.”“Sawa bwana!” Mayasa akageuka, safari hii alikuwa akigeuka kwa mapozi, huku akipandisha gauni lake na kuacha miguu yake wazi, ambayo ilianza kupandisha presha yake ya mapenzi.“Hakika wewe ni mwanamke mrembo sana, sema chochote unachotaka nikupe ilikuonyesha mapenzi yangu kwako!” Tom akamwambia Mayasa akitabasamu.Mayasa akamfuata mahali Tom alipokuwa amekaa, akakaa na kupandisha mguu wakemmoja juu ya miguu ya Tom. Tom akahisi shoti ya umeme ikipita mwilini mwake. Mayasa alikuwa mwanamke aliyemchanganya sana ubongo wake.Akasogeza kinywa chake karibu kabisa nasikio la kuume la Tom, kisha akaanza kuzungumza kama anamnong’oneza; “Ni kweli unanipenda Papaa?”“Kwanini huniamini?”“Siyo kama sikuamini Papaa!”“Sasa kumbe nini?”“Kama nilivyokuambia kule Club, wewe ni mwanaume tajiri na maarufu, kila mtu anakufahamu, nitawezaje kuwa na wewe kama sitanyang’anywa?”“Mimi ndiyo mwamuzi, na ni mimi ndiye niliyekupenda. Ndiyo maana nimekuwambia chagu chochote utakacho nikupe ili kuonyesha penzi langu la kweli kwako!”“Sawa, naona itakuwa vizuri sana kama ukinihamisha nyumbani!”“Una maana gani?”“Naishi na wazazi wangu na umri wote huuni aibu sana, kwanza nina wadogo zangu wawili wa kike na wote wanaishi na mabwana zao, nimebaki mimi tu, nyumbanikwahiyo naona itakuwa vyema kama utanipangishia chumba!”“Chumba au nyumba?”“Utakavyoona mwenyewe Bill”“Acha nikutafutie nyumba nzima, kuhusu samani za ndani niachie mimi, kila kitu utakikuta ndani ya nyumba!”“Nitafurahi sana Papaa Bill!”“Anza kufurahi kuanzia sasa!”“Sawa mpenzi wangu.” Mayasa akasema akicheka kwa sauti kubwa sana.“Nilitaka kusahau, unataka maeneo gani?”“Utakayoona yanafaa!”“Chagua mwenyewe!”“Kinondoni au Mwananyamala.”“Basi nipe muda mfupi sana, haitazidi mwezi mmoja!”“Sawa baby!” Baada ya hapo, lugha ya Kiswahili haikutumika tena.Hata hivyo lugha iliyozungumzwa badala ya Kiswahili haikuwa Kiingereza, Kifaransa wala lugha nyingine yoyote ambayo hutumika kama njia ya mawasiliano duniani. Walikuwa wakizungumza lugha ya mapenzi!*******Pamoja na kwamba Tom alikuwa anapenda sana starehe, haikuwahi kutokeahata siku moja, akaacha kurudi nyumbani. Siku hiyo hadi kufikia saa tisa na dakika zake za usiku, Mariam alikuwa hajamtia machoni mwake mumewe.Siku zote alikuwa mtu wa starehe sana lakini alipompigia simu alipopokea na kumweleza mahali alipo na wakati mwingine hadi muda aliokuwa akitarajia kurudi nyumbani. Siku hiyo ilikuwa tofauti sana, simu ya Tom ilikuwa haipatikani ka bisa!“Masikini mume wangu, sijui atakuwa amekumbwa na balaa gani tena, siyo kawaida yake kuwa hajarudi nyumbani hadimuda huu, mbaya zaidi hata simu yake haipatikani,” Mariam akawaza akiwa amejilaza kwenye sofa kubwa sebuleni akiwa hoi kwa uchovu akimsubiria mume wake bila mafanikio.Mapenzi yao sasa yalibadilika, hayakuwa sawa na ilivyokuwa awali, mara nyingi Mariam aliishia kulala mwenyewe nyumbaniakiwa hana la kufanya. Hata alipotaka kutafuta kazi, Tom alikataa akidai kuwa uwezo wa fedha alionao, haumruhusu yeyekufanya kazi, kwani ana uwezo wa kumuachia fedha za matumizi kila siku bilamatatizo.Hakupata usingizi hadi asubuhi akiwa yuposebuleni akimsubiria mumewe, hadi kufikia saa mbili za asubuhi, Tom alikuwa hajafika nyumbani, mawazo yakazidi kumjaa akilini mwake.“Lazima nifanye jambo la ziada hapa, natakiwa kwenda kutoa taarifa Polisi kwanza!” Mariam anawaza kisha akaamua kwenda kubadilisha nguo haraka na kutokanje.Akiwa ndiyo kwanza, amewasha gari, anasikia honi ikipigwa mlangoni. Mlinzi anafungua mlango, gari la Tom linaingia na kuegeshwa pembeni. Mariam haamini macho yake. Alitegemea kumuona Tom akiwa na huzuni kutokana na matatizo aliyohisi kuwa nayo, lakini alishuka akiwa na tabasamu pana.Mariam akashuka garini, akiwa ameyatulizamacho yake kwa Tom ambaye hakuonekana kuwa na chembe ya wasiwasi. Akaingia ndani na kumuacha Mariam akiwa amesimama nje, ni jambo ambalo lilichukua muda mrefu sana kuaminika akilini mwa Mariam.Mariam akamfuata Tom ndani, macho yakeyakianza kupatwa na unyevunyevu na kubadilika rangi na kuwa mekundu. Akamkuta Tom akiwa amejilaza kwenye sofa kubwa.“Vipi Tom mume wangu?”“Salama, za tangu jana?”“Mimi ndiyo natakiwa kukuuliza wewe!”“Ooooh! Hivyooeh....mimi mzima, sina matatizo!”“Lakini ulilala wapi?!”“Kitandani!”“Hayo ndiyo majibu gani Tom?”“Nimekwambia nimelala kitandani!”“Eti?”“Hujasikia au hujapenda? Halafu we’ mwanamke...naona sasa unataka kunipanda kichwani, tafadhali naomba uniache, usipende kufuatilia sana mambo yangu!” Tom akasema kwa sauti kubwa iliyoonyesha kujaa hasira.Mariam hakuwa na kitu kingine cha kuzungumza zaidi ya kwenda kujifungia chumbani, alichokifanya huko ilikuwa ni kulia akiamini alikuwa anapunguza hasira zake.Tom ameshaanza kubadilika, sasa ameanza tabia ya kulala nje na anarudi nyumbani bila woga kwa mkewe.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP BORA YA MAFANIKIO

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments