..Machozi ya Mariam yalikuwa na thamani kubwa, thamani hiyo ilitokana na kipimo cha mapenzi kilichokuwa ndani yake! Alimpenda sana Tom wake, lakini badilikola tabia yake lilimkosesha raha moyoni mwake.Mariam hakuwa na amani, alishindwa kuelewa ni shetani gani aliyemwingia mumewe na kumbadilisha kiasi kile. Hadi wakati huo hakuwa na uhakika kama aliyemjibu majibu machafu kiasi kile alikuwa Tom wake aliyemfahamu siku zote.“Sasa amezidi! Amefikia hatua ya kulala nje, Tom kwanini unanitesa lakini?” Mariamalisema maneno hayo huku akilia kwa uchungu, chumbani alipokuwa amekimbilia.Hasira zilipomzidi Mariam, alijikuta akizidisha kilio, jambo lililomuudhi sana Tom ambaye haraka alitoka na kwenda chumbani kumfuata kwa lengo la kumpa kipigo.“Pumbaaaafu....hapa siyo Klinik, umeelewa? Naomba unyamaze haraka sana!”“Sinyamazi.”“Unasema?”“Sinyamazi Tom, niache nilie hasira zanguziishe. Unanitesa sana Tom lakini sasa umeona ili kunidhibitishia kwamba ni kwelihunipendi, umeamua kulala nje kabisa, sasanina thamani gani kwako mimi?!”“Hivi wewe mwanamke, nimekuoa au umenioa?”“Tumeoana!” Mariam akajibu kwa kujiamini huku akifuta machozi machoni mwake.Hakujua ni kiasi gani lilikuwa jibu baya kwa Tom. Alimwangalia kwa jicho la hasira kisha akamsogelea polepole huku akitetemeka kwa hasira zilizoonekana dhahiri.“Hivi, hii jeuri unaipata wapi wewe mwanamke? Nakuuliza wewe...hii jeuri unaipata wapi?”“Tom mpenzi wangu, kukuliza ulilala wapi imekuwa jeuri?”“Hata kama, mimi ni mwanaume na nina mambo mengi, na kama nilikuwa nahangaika na biashara zangu, utajuaje?”“Ni lini uliwahi kulala nje Tom, kama kuchelewa ulikuwa unanipa taarifa, iweje kwenye kulala nje ushindwe kuniambia?”“Kwahiyo kila ninachokifanya lazima nikuambie siyo?”“Mimi kama mkeo, natakiwa kufahamu hayo yote, kumbuka uliahidi nini siku ya ndoa, kumbuka Tom mume wangu!”“Hata kama, lakini nimekuambia kuwa ninakazi nyingi na ndizo nilizokuwa nahangaika nazo, nilitegemea ungenipokeana kunipa pole, lakini mwenzangu ndiyo kwanza unaanza ugomvi!”“Lakini simu zilikuwa hazipatikani!”“Ziliisha chaji!”“Hapakuwa na njia nyingine ya kunijulisha Tom!”“Lakini mbona umeshikilia sana hilo jambo? Kitu kidogo unataka kiwe kikubwa?”“Natetea uhai wangu Tom, hivi unafikiri kama ukizoa maradhi huko na kuyaleta hapa nyumbani itakuwaje kama siyo kuniua?”“Unasemaje wewe mwanamke? Yaani mimini ukimwi? Sasa naona upole wangu unaniponza, unataka kunipanda kichwani sasa!” Tom akasema hayo huku akivua mkanda wake wa suruali.Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni kipigo cha nguvu, ambapo pamoja na Marim kuomba msamaha Tom aliendelea kumpiga!“Nisamehe mume wangu utaniua, naomba msamaha, tafadhali Tom...nakufaaaaa...” Mariam alipiga kelele lakini Tom aliendelea kumpiga mpaka hamu yake ilipoisha akaamua kuachana naye.******BAADA YA MIEZI SITAMapenzi ya Tom na Mayasa yalizidi kushamiri huku mateso, manyanyaso na matusi kwa Mariam yakiwa ni vitu vya kawaida kila kukicha! Tom alibadilika sana, akawa hasikii wala haambiwi kwa Mayasa.Kama ni mapenzi basi yalitakiwa kutafutiwa jina lingine maana katika penzila wawili hao yalikuwa makali zaidi ya neno lenyewe! Walikuwa kama kumbikumbi,kila mahali walikuwa pamoja.Tom alishindwa kuelewa kwanini alijikuta akizidisha mapenzi kwa yule mwanamke kwa kasi ambayo hata yeye mwenyewe hakujua ilipotokea. Alimuona Mariam kamakinyaa mbele yake, hakuwa na muda wa kukaa na Mariam hata kujadili kuhusu mambo mbalimbali ya familia yao.Muda mwingi alikuwa na Mayasa, Tom hakujua siri ya kumpenda zaidi Mayasa, kulikuwa na kitu kilichosababisha mapenzi kati yao kuongezeka! Mayasa alikwenda kwa Mtalaamu wa Kienyeji ambaye alimuwekea mambo yote sawa! Tom alikuwa mkononi mwa Mayasa na hakuwa na uwezo wa kufurukuta kwa namna yoyote ile! Alikuwa kama bendera ambayosiku zote huwa inafuata upepo.Siku moja Tom akiwa na Mayasa mjini, Tom alijikuta akifanya jambo la hatari sana. Baada ya kupungukiwa na fedha, waliamua kwenda kwenye mashine ya kutolea fedha ya CRDB Tawi la Azikiwe na kumtuma Mayasa aende akachukue pesa.“Sasa nitawezaje wakati sifahamu namba zako za siri?”“Hilo tu, nitakupa!”“Lakini ni vizuri ukaenda mwenyewe, mambo ya pesa hasa akaunti ni siri ya mhusika mpenzi wangu! Hebu shuka kwenye gari uende ukachukue pesa, acha uvivu wako!” Mayasa alimwambia Tom lakini alikuwa anamtania kwani alikuwa anajua kwamba dawa ndizo zilizokuwa zikifanya kazi.“Wewe ni mpenzi wangu siyo?” Tom akauliza.“Hata hili gari linajua hivyo.”“Umejibu vizuri sana, sasa sina haki ya kukutuma?”“Unayo!”“Namba za siri za hiyo kadi ni 1343, nenda katoe laki tano haraka!”“Sawa baba, isiwe ugomvi!” Mayasa akasema kisha akatoka kwa mwendo wa maringo kuelekea kwenye mashine.Tom alibaki hoi akikodolea macho makalio ya Mayasa, yaliyokuwa yanavutia sana. Watu waliomwona akipita, walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakimtimzama kwa macho ya matamanio.Ilibaki kidogo Mayasa azimie baada ya kuona fedha zilizokuwa kwenye akaunti yaTom, pamoja na kwamba alikuwa anafahamu Tom alikuwa na fedha nyingi sana, lakini hakuwahi kufikiria kwamba akanuti yake ingekuwa na fedha nyingi kile.Akaunti ya Tom ilikuwa na zaidi ya bilionithelathini, hata hivyo alikuwa na akaunti nyingine katika Benki za NBC na Barclays ukiachilia mbali akaunti nyingine zilizokuwa nje ya nchi. Mayasa akachukua kiasi kile cha fedha na kurudi kwenye gari.“Umefanikiwa?”“Ndiyo!”“Twende!” Tom akawasha gari na kuondoka na Mayasa, safari yao iliishia katika moja ya Hoteli za sasa iliyokuwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi.Wakiwa huko Mayasa alikumbushia ahadi ya kupangishiwa nyumba, aliyoahidiwa na Tom.“Haraka ya nini? Subiri kwanza!”“Lakini dear nitaendelea kukaa Mbagala hadi lini? Sina hadhi ya kukaa kule tena!”“Ni kweli lakini nimekuambia subiri mpenziwangu, nakuandalia kitu cha maana na muda mfupi baadaye utafurahia!”“Tutaona!” Walikula raha huko usiku mzima.******Wiki mbili baadaye Tom alimpigia simu Mayasa na kutaka wakutane kwa ajili ya kumpatia zawadi nzuri sana aliyoiandaa kwa ajili yake.“Kwani we’ uko wapi?” Mayasa akamwuliza.“Uwanja wa nyumbani 56 Club!”“Mimi nipo Mwananyama, acha nichukue taxi mara moja nakuja hapo sasa hivi!”“Nakusubiri mpenzi wangu!” Muda mfupi baadaye Mayasa akafika.Bila kupoteza muda Tom akamwambia Mayasa aingie kwenye gari. Akaingia. Wakaangaliana kwa pamoja na kuachia matabasamu mapana sana usoni mwao.“Leo ni siku ya furaha katika penzi letu, nataka kukuonyesha kwamba nakupenda, nakuthamini, nakuheshimu na nataka kuwa na wewe katika siku zote za maisha yangu!”“Mbona unanitisha mpenzi, kuna nini?”“Usijali, fumba macho yako, halafu nitakufunga kitambaa cheusi kisha nitakufungua baada ya kufika mahali zawadi ilipo, sawa?”“Hakuna shida mpenzi wangu!” Tom akatoa kitambaa na kumfunga Mayasa usoni, kisha akaondoa gari.Safari yao iliishia Kinondoni B, karibu kabisa na Shule ya Sekondari Biafra ambapo kulikuwa na nyumba nzuri ya kifahari iliyokuwa na kila kitu ndani! Nje ya nyumba hiyo, kulikuwa kumeegeshwa gari mpya aina ya Toyota Rav 4 la rangi la Buluu, ukoka ukiwa umechukua nafasi kubwa pamoja na bustani nzuri iliyokuwa pembeni ya bwawa la kuogelea.Tom alipoegesha gari lake, akafungua mlango na kumtaka Mayasa atoke. Baada ya hapo akamfungua kitambaa usoni mwake na kumpa funguo mbili, moja wa gari na mwingine wa nyumba.“Huu ni funguo wa nyumba yako, na huu ni wa gari lako, lile pale. Kuanzia leo, hii ni nyumba yako, ina kila kitu ndani, furahia maisha mpenzi wangu!” Tom akasema akitabasamu.Mayasa hakuweza kuelewa kama yaliyokuwa yakitokea yalikuwa ni ndoto autukio la kweli. Akamwangalia Tom huku akitetemeka kwa furaha, midomo yake ikaanza kutingishika!“Ni nyumba ya kupanga au...” Tom hakumuacha Mayasa amalizie sentesi hiyo, akamkatisha.“Nimeinunua na hati yake hii hapa, nimekuwa nikifanya ukarabati na kuifanya ya kisasa kwa miezi sita sasa, hii ni nyumba yako....mali yako!” Tom akamwambia Mayasa akitabasamu.Tayari macho ya Mayasa yalishajaa machozi, akamsogelea Tom na kumkumbatia kwa nguvu, mabusu motomotomashavuni mwa Tom yalitawala.“Nimeamini unanipenda Tom!”“Tena sana, kuliko hata Mariam!”“Kweli?”“Nakuhakikishia!”“Leo ni siku ya furaha ya penzi letu, ili niamini vizuri kama kweli unanipenda, twende tukalale nyumbani kwako, hapo utanifanya nione unanithamini na kunipenda na humpendi mkeo!” Mayasa akasema akiwa ameyatuliza macho yake usoni mwa Tom.Maneno yale yalizunguka kwenye ubongo wa Tom zaidi ya mara kumi bila kupata jibu la kumpa Mayasa.“Tom, nahitaji jibu lako mpenzi wangu!”Tom akafungua kichwa chake, macho yake yakitizama chini huku akionekana kuwa na mawazo mengi sana yaliyomkumba ghafla. Kila alipotaka kuzungumza alionekana kusita.
Kama ni mtihani, huu ulikuwa mkubwa kuliko yote kwa Tom! Pamoja na kumpenda sana Mayasa, lakini kitendo cha kumwambia akalale naye nyumbani kwake kilikuwa cha udhalilishaji mkubwa kwa mkewe wa ndoa Mariam.
Ni kweli Tom alikuwa katika mtihani mzito sana na hakuweza kufungua mdomo wake kusema chochote, hadi dakika mbili baadaye, Mayasa alimtingisha kwa nguvu na Tom kurejewa na kumbukumbu zake vizuri. Ni kama hakuwepo mahali pale.
“Mbona umenyamaza?”
“Unasema?”
“Mbona upo kimya, nahitaji jibu lako!”
“Najua Mayasa, lakini fahamu kwamba umenipa mtihani mkubwa sana!”
“Mtihani mkubwa kivipi?”
“Mayasa!” Tom akaita.
“Nakusikia mpenzi wangu!”
“Huoni kuwa huo ni mtihani mkubwa sana kwangu?”
“Labda nikuulize swali kabla ya kujibu lako!”
“Endelea...”
“Unanipenda?”
“Mayasa mpenzi wangu, hata wewe unaweza kunisaidia kujibu!”
“Pengine ninalo jibu, lakini yawezekana jibu nililonalo mimi ni tofauti na fikra zako!”
“Hapana...unavyowaza ndivyo nilivyo!”
“Kwahiyo sasa nikuambie ninavyowaza jibu yako?”
“Ndiyo!”
“Utaniamini?”
“Kwanini nishindwe?”
“Tom hunipendi, hunipen...” Mayasa akasema akilia.
Tom hakutaka kuyaona machozi ya Mayasa, haraka akaanza kumfuta machozi yake na kumbembeleza anyamaze.
“Niache nilie Tom, ni haki yangu!”
“Haki ya kuli? Kivipi?”
“Napenda nisipopendwa!”
“Usiseme hivyo mpenzi wangu, mimi nakupenda sana!”
“Kama unanipenda kwanini unanifanyia hivi?”
“Kumbe yote haya niliyoyafanya huoni thamani yake?”
“Sina maana hiyo, nataka udhihirishe penzi lako kwangu mbele ya mkeo, nataka mkeo afahamu kwamba yupo unayempenda zaidi, ambaye ni mimi. Kwanini unanitesa kiasi hicho Tom?” Mayasa alikuwa akizungumza kwa hisia sana huku machozi yakimtoka machoni mwake.
Tom hakujua kilichokuwa akilini mwa Mayasa, alifanya yote hayo kwa sababu alikuwa akihitaji Mariam afukuzwe ili aweze kuzitawala vizuri mali za Tom, hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake siku zote. Kuchota mali za Tom ingewezekana kama Mariam angeondoka ndani ya nyumba ya Tom na hatua ya kwanza kwake ilikuwa ni kwenda nyumbani kwa Tom na kulala pale.
Aliamini kwa kufanya kungemchukiza Mariam na kuamua kundoka zake kwenda kwao. Wazo lake lilikuwa zuri sana ingawa hakujua ni kiasi gani lilikuwa sumu kwa mwenzake.
Ukimya wa mrefu ukapita, wote wakiwa hawazungumzi chochote hadi Tom alipoamua kuanzisha mazungumzo.
“Nina swali moja kwako!”
“Uliza!”
“Unanipenda?”
“Saaana!”
“Sasa sikiliza, mimi ni mwanamke na wewe ni mwanaume, sawa?”
“Ndivyo ilivyo!”
“Wewe una nafasi yako kama mke na mimi nina nafasi yangu kama mume ni kweli?”
“Hujakosea kitu!”
“Lakini pia unakubali kwamba, mwanaume ndiye kichwa cha nyumba?”
“Hata kwenye maandiko ipo!”
“Sasa mimi kama mumeo, kichwa cha nyumba, msemaji wa mwisho, naomba unielewe kwamba, kwa leo haitawezekana kwenda kulala nyumbani, lakini naweza kulala na wewe hapa kwa ajili ya kuizundua nyumba, umenielewa?” Tom akasema kwa kujiamini sana ingawa alitarajia kukutana na jibu la kukataliwa.
Kinyume na matarajio yake, Mayasa alimsogelea Tom na kukumbatia kwa nguvu, kisha akausogeza mdomo wake karibu kabisa na wa Tom, akautoa ulimi wake haraka na kuutumbukiza kinywani mwa Tom. Wakaanza kufurahia mapenzi.
“Nimekuelewa mpenzi wangu, hakuna shida!”
“Nami nimefurahi sana kwa uelewa wako mpenzi wangu, naona sasa umekuwa na unatambua nafasi ya mwanaume katika mapenzi.” Tom akasema akishangulia ushindi moyoni mwake.
“Ahsante mpenzi wangu!” Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Mayasa lakini moyoni ilikuwa ni tofauti kabisa; “Huna ujanja wewe, nakulea-lea kwanza, lakini kuna siku utaingia mkenge tu.”
Tom akamshika mkono Mayasa, wakaingia ndani. Macho ya Mayasa hayakuwa tayari kuamini kilichokuwa mbele yake, ilikuwa sebule nzuri ya kisasa yenye kila kitu cha maana!
Kwanza kulikuwa na seti ya masofa mazuri, chumba maalumu cha chakula (dinning room), jokofu kubwa, redio kubwa, luninga na deki yake na kila aina ya anasa.
Hayo yangekuwa makazi mapya ya Mayasa baada ya kuishi muda mrefu katika maisha duni huko Mbagala. Hakuamini macho yake, kama kweli Tom alikuwa amedhamiria kumjengea nyumba nzuri nzuri kiasi kile. Macho yake yalizunguka kila kona ya sebele ile ya kisasa yakitizama vitu vizuri vilivyokuwepo.
“Ahsante sana mpenzi wangu, siamini macho yangu!” Mayasa akasema akimwaga machozi kama mvua.
“Amini, amini mpenzi wangu, wewe ndiye niliyekuchagua kutoka moyoni mwangu!”
“Nakuamini mpenzi!”
“Sasa twende nikakuonyeshe bed room!” Tom akamwambia na kumshika mkono kisha wote kwa pamoja wakaongozana hadi chumbani.
Huko Mayasa ndiyo alishindwa kuelewa namna gani atakavyotoa shukrani zake. Kilikuwa chumba kikubwa, kizuri na chenye kila kitu! Kwanza kulikuwa na kabati kubwa la nguo, kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita ambacho kilitengenezwa kwa kutumia ngozi, meza ya vipodozi pamoja na vikorobwezo kibao!
Choo na bafu vyote vilikuwa ndani, kukiwa na bomba la maji ya mvua ambayo hutoka ya moto, baridi na ya mchanganyiko! Kilikuwa chumba cha kisasa sana. Mayasa akamwangalia Tom, kisha akajikuta hisia zake za mapenzi zikimpanda sana, akamsogelea na kumtupia kitandani. Kilichoendelea huko ilikuwa ni shughuli nzito iliyomalizika baada ya saa moja.
Wote wakiwa na furaha wakatoka na kwenda nje kuogelea katika bwawa la kuogelea. Hakika yalikuwa maisha ya kifahari sana, kila kitu kilikuwa kipya kwa Mayasa. Siku hiyo hawakutoka kabisa, kila kitu kilikuwa ndani. Vyakula vyote vilikuwa kwenye majokofu.
Walipomaliza Tom alijipumzisha nje, wakati Mayasa akiendelea kupika chakula ndani. Mayasa alijiona mshindi katika maisha mchezo ule hatari wa kuisambaratisha ndoa ya watu.
“Haya ndiyo maisha, lakini mambo bado, nitahakikisha ananyooka, mimi ndiyo Mayasa mtoto wa mjini, niliyezaliwa, kukulia na kusomea katika jiji la wanjanja, jiji la Dar es Salaam,” Mayasa alijisemea moyoni mwake wakati akipika chakula cha usiku.
Baadaye walikula na kulala usingizi wa mapenzi mazito.
INAENDELEA
0 Comments