Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Ujumbe Kutoka Ndotoni (Notification From the Dream) Sehemu Ya Tatu (03)

 


"Sawa mtukufu Malkia nitajitahidi kadri ya uwezo wangu nisiharibu Sherehe za kumuapisha Mfalme mpya!"

Eunike alijibu kistaharabu sana. Baada ya mazungumzo hayo Mafupi ambayo yalifanyika usiku Malkia aliondoka ndani ya Chumba cha Lady Divine au chumba cha Mabikira au watumishi waMiungu katika Ardhi ya Iyumbwi.

"Kakwambia nini Eunike?"

Wenzake walipoingia hilo ndilo likikuwa swali la kwanza kumuuliza Eunike.

"Aliniuliza hali ya Lady Amana, na kunikumbusha kuhusu kesho kuwa nijiandaye kwakuwa Mimi ndiye nitamsimika mfalme mpya!"

"Hakuna Jinsi, tujiandae tu, kama ni majukum tutasaidizana!"

Mwingine alisema kisha wakaungana na kutiana matuamaini ya kumsaidia mwenzao kuhusu kumuapisha na kufanya taratibu za maombi kesho katika sherehe za kumuapisha Prince Yolam.

*******

"Lazima kuna Jambo Eunike atakuwa amenificha, mbona nilipomuuliza alishituka kwanza halafu kama akainamisha kichwa chini, ndio akajibu!"

Malkia akiwa Chumbani kwake alikuwa anawaza. Hata yeye alikuwa Bado hajaupata uhakika kamili ingawa alikuwa kabisa anatilia mashaka kuhusu Lady divine amana.

"Nilipokwenda kumbeba Lady Divine, mmoja wa watu wa pale alisema kuwa, nimemkuta Lady divine akiwa ametapakaa damu kwenye mapaja!"

Bado kauli aliyoambiwa na askari ilijirudia tena kichwani kwa Malkia, Mama mzazi wa Prince Yolam.

"Amna lazima watakuwa wamefanya mapenzi ndio maana Mfalme alikosa ujasiri. Kwahio atakuwa amepewa adhabu na miungu kwa kosa la kufanya uchafu wakati yeye ni Mwanamke teule!"

Malkia alijisemea pekee chumbani kwake.

********.

Siku iliyofuata mapema kabisa, nyakati za Saa mbili, mambo yalianza kubadilika katika Ufalme wa Iyumbwi, mapambo yalianza kupambwa katika uwanja halisi wa kufanyia sherehe ndani ya uwanja mkubwa uliokuwa katika ukuta mkubwa wa Jengo la Kifalme. Watu mbali mbali walianza kukusanyika kutoka sehemu mbali mbali na kuingia katika jengo la Ufalme, viongozi wa vijiji karibu vyote vilivyokuwa vinaiunda Falme ya Iyumbwi walifika katika Jumba kubwa la Ufalme.

Saa tano ndipo sherehe rasimi za kumsimika Prince Yolam kuwa mfalme katika Ufalme mkubwa wa Iyumbwi zilianza. Aliyekuwa analifanya zoezi la kumsimika mfalme hakuwa mwingine, ila alikuwa yule yule Eunike huku akishirikiana na wenzake katika lile kundi la mabikira waliokuwa chini ya Lady Amana.

Sherehe ziliendelea mpaka wakamuapisha Prince yolam kuwa mfalme. Kwa taratibu zao ilikuwa baada ya kumuapisha Mfalme lazima Lady divine amuombee kwanza kwa miungu ili apate kudumu na kama kuna matatizo miungu imuepushie.

Eunike alilianza zoezi lile la kumuombea Mfalme mpya King yolam. Akiwa anaendelea na maombi, walishangaa Eunike ambaye alikuwa kapiga magoti anashuka chini Taratibu na kuanguka kabisa Chini. Lilikuwa ni tukio la kuwashitukiza wote, hiyo ilikuwa ni ishara ya taarifa furani katika ufalme. Kila ambapo Lady divine yoyote alipokuwa anakuwa kwenye maombi maalumu akianguka chini na kupoteza Fahamu walijua kabisa kuna maono kayaona, na alipokuwa anaanguka chini alikuwa aguswi na Mtu mpaka aamke yeye kwani waliamini wakati huo alikuwa anawasiliana na Miungu wakimjulisha taarifa muhimu zilizokuwa zinahusu utawala.

Ingawa walijua hayo yote, lakini Mara zote walijua kuwa maono yale yalikuwa hayana taarifa nzuri katika Ufalme, lazima yatakuwa ni maono ambayo yatauweka Ufalme katika mashaka makubwa na wasiwasi pia. Wasiwasi mwingi ulikuwa kwa Mfalme Yolam kwani tayari taarifa za hawali ambazo alikuwa kaisha zipata kuhusu Ufalme wake na Ufalme wa Nghumbi zilimpa mashaka sana.


Bado watu karibu wote wakiwa katika maswali, wakijiuliza kuhusu jambo gani, ambalo Eunike kaliona, Eunike naye aliamka kutoka katika maono yake. Hapo kila Mmoja alikuwa na hamu ya kujua ni nini Eunike alikiona, lakini kwa bahati mbaya ni kwamba ambacho alikiona hakuna mtu mwingine ambaye alipaswa kuambiwa isipokuwa Mfalme pekee.

Baada ya kuamka, walingoja sherehe ziishe halafu Eunike akutane na Mfalme azungumze naye ni nini alichokiona katika maono yake. Lakini muonekano wa Eunike uliwapa mashaka sana watu karibu wote waliokuwepo katika mkusanyiko ule. Binti alikuwa mnyonge ghafra, mpaka sherehe za kumuapisha mfalme zinaisha Hali yake iliendelea kuwa ile ile ya unyonge na kutojiamini.


"Nimekuita ili uweze kunambia ni swala gani ambalo umeliona pindi ulipokua unafanya maombi ya mwisho baada ya kuapishwa kwangu kuwa mfalm?"

Hilo ndilo lilikuwa swali la Prince Yolam baada ya kukutana na Eunike katika Chumba cha Mfalme.

"Ni swala gumu sana Mfalme, kwani nimeiona Nyota angavu ambayo ilimeguka kutoka katika Nyota moja kubwa, kisha nyota hiyo ikaenda kuungana na Nyota nyingine, ilikuwa ni Nyota kubwa kiasi, baada ya kuungana hiyo nyota ikawa kubwa sana. Lakini ghafura likatokea wingu Jeusi na kuzifunika Nyota zote mbili, zilipokuja kuonekana nikaona zote mbili zinakutana na kuwa nyota moja kubwa, lakini Mpaka sasa sijui maana halisi ya Nyota hizo!"

Eunike alisema. Wakati huo Mfalme Yolam alikuwa amenyamaza akimsikiliza.

"Sawa, unaweza kutoka niache mwenyewe!"

Mfalme Yolam alisema.

Kwa taratibu kabisa Eunike alisimama na Kutoka katika Chumba cha Mfalme kurudi sehemu yake.


Kutoka kwa Eunike ndani ya Chumba cha Mfalme, Mfalme alibaki na Mawazo sana kwani alichoambiwa kupitia maono ni sawa na kile ambacho aliambiwa kuwa atatokea Mfalme ambaye ataziunganisha Falme mbili. Falme ya Iyumbwi na Falme ya Nghumbu.

"Hapana haitowezekana, lazima nipambane na Swala hili, kwanini nishindwe na wakati Mimi ni Mfalme!"

Mfalme Yolam alisema. Alijisikia Hasira sana. Majawabu aliyokuwa nayo yalitosha kabisa kuwa wakati wake ndio huo huo ambao Falme hizo zitaungana, hata kwa kutokana na Historia ya Taifa hilo, inaonesha kabisa Yolam na Cleopa ndio Wafalme ambao waliyatawanya mataifa hayo, na Baba yao alikuwa ni Zilizayoni, jina ambalo ikitoa herufi nne tu za mwanzo linafanana na jina la Baba yake. Kwahio hakukuwa na Haja ya kujiuliza itakuwa lini mambo hayo yatatokea wakati kila Dalili ilikuwa wazi.

"Lazima itakuwa ni kwangu, ndio maana kila jambo limefumuka wakati wa Utawala huu. Lakini huyo Mtoto ambaye atatoka katika Ufalme huu ni nani, kwa maana hiyo Baba atakuwa amemzaa mtoto inje ya Ufalme?"

Mfalme Yolam Alijisemea pekee. Maswali yalikuwa mengi na kichwani mwake, alikuwa anajitahidi sana kuyatafutia ufumbuzi mwenyewe.

"Cha kufanya ni kuanza na huyo mtoto kwanza, bila Shaka atakuwemo tu humu ndani ya Ufalme amejificha amekaa kimya tu!"

Mfalme Yolam alisema tena, wakati huu aliipiga meza yake ngumi kwa mkono wa kushoto. Alisimama kabisa akaanza kuzunguka zunguka ndani ya Nyumba au chumba chake. Mpenzi msomaji nikisema chumba simaanishi chumba kimoja ni kwamba ilikuwa ni chumba kikubwa sana ambacho kilikuwa kimegawanyika katika vyumba na sehemu ya sebule, vyumba vyote vilikuwa vimeunda Jengo moja kubwa kweli kweli.




Mfalme Yolam aliumiza kichwa chake sana kuwaza namna ya kulimaliza tatizo hilo. Kilichokuwa kinamtesa si kitu kimoja tu, cha Falme yake kuungana na Iyumbwi halafu Mfalme awe mwingine, Tatizo lingine ni kwamba hataonekana dhaifu katika uongozi wake.

"Mfalme, Malkia Sayuni anataka kuingia ndani"

Sauti ya Mlinzi wa mlangoni ilisikika ikimuombea Malkia mkuu yaani Mama wa Mfalme kuingia ndani. Huyu hakuwa mwingine ni Lady Sayuni.

"Yolam mbona unaonekana mwenye mawazo hivyo.....na ulichoambiwa na Eunike kinahusu nini?"

Malkia aliuliza maswali mawili kwa wakati mmoja.

"Hakuna kitu Mama, na najiona kawaida sana!"

Mfalme Yolam alisema.

"Yolam mwanangu kumbuka kuwa sasa wewe ni Mfalme......lazima ukumbane na Changamoto nzito, Mimi ni mama yako kama kuna Jambo naomba usinifiche, niko ladhi nikusaidie kwa namna yoyote ile ilimradi Ufalme wako uthaminike na ueshimike kwa kila Mtu ndani ya Taifa hili kubwa!"

Malkia alisema kwa msisitizo sana, alitamani kujua ni jambo gani linamsumbua kijana wake toka muda.

"Hapana Mama ila natafakari maono ya Eunike!"

Mfalme alisema. Alichokitamka kilimfanya mama yake kutaharuki kisha akasema.

"Nini ambacho kakiona Yolam?"

"Kanambia kuwa ameona Nyota ambayo imemeguka kutoka katika nyota kubwa angavu, kisha nyota hiyo ikajongea kuifuata nyota nyingine ambayo pia ilikuwa ni kubwa pia, ila nyota ile ilifika ikaungana na ile nyota na kuwa Nyota kubwa zaidi ya hii ya hawali, lakini baadaye likatanda wingu jeusi likazipoteza nyota hizo, na wingu hilo lilipoisha nyota zile kubwa mbili ziliungana na kuwa nyota moja kubwa sana!"

Mfalme yolam alimsimulia Mama maono ya Eunike.

"Umekwambia Maana yake?"

"Hapana Mama, kanambia kuwa hajui maana ya kitu hicho!"

Mfalme Yolam alisema. Alikuwa anazungumza kwa utaratibu sana, uso wake ulikuwa umejaa upole wakati anaongea na Mama yake.

"Lakini ni nani anaweza kutwambia kuhusu maono haya, Lady Divine Bado amepoteza fahamu mpaka sasa, angekuwa mzima tungepata jawabu kirahisi tu, sijui hata mimi maono hayo yanamaanisha nini!"

Malkia alisema huku akionekana kabisa kushangazwa na alichokisikia.

"Ndicho hicho tu mama kinanisumbua!"

King yolam alisema tena, hakutaka kumwambia mama alichokipokea kutoka kwa Semwali kuhusu Falme mbili kuungana.

Malkia Sayuni alinyamaza kidogo kama alikuwa anawaza jambo. Akiwa katika mawazo yale, alikumbuka alichoambiwa na askari kuhusu Lady divine, kuwa alikuwa na michirizi ya damu kwenye mapaja yake, wakati huo huo alikumbuka Mfalme alipojaribu kumkwida pindi anaongea kuhusu Lady divine kuwa msaliti wa Miungu.

"Mama mbona unaonekana kuna jambo unalijua lakini unanificha!"

Mfalme alisema.

"Hapana, ila nilikuwa namuwaza mwanamke mmoja yuko katika kijiji cha jilani hapa nasikia huwa anatafasili maono na ndoto! Kwahio tunaweza kuagiza aletwe hapa, anaweza kutusaidia maono hayo!"

Malkia Sayuni alisema. Bado aliendelea kumficha mwanaye ukweli, ila yeye alikuwa anawaza kuwa kuna mahusiano kati ya Maono hayo na kilichopo katikati ya Merehemu Mfalme Zayoni na Lady divine Amana.

"Mfalme! Waziri mkuu anahitaji kuingia ndani?"

Wakati bado wako katika majadiliano mlinzi wa mlangoni kwa mfalme alisikika akimuombea waziri mkuu ruhusa kuingia ndani.

"Mwambie apite!"

Mfalme aliagiza waziri mkuu aingie.

Moja kwa moja waziri mkuu aliingia ndani kwa Mfalme, alishangaa kumkuta Malkia mkuu(Mama mfalme) akiwa na Mwanaye.

Kwanza aliitoa salamu kisha akakalibishwa kukaa.

"Kwanza Nashukuru kwasababu Lady Sayuni naye yupo!"

Hiyo ndiyo ilikuwa sauti ya Waziri mkuu baada ya kuingia. Kwa maneno hayo ilitosha kumjulisha mfalme na Malkia mkuu kuwa kuna Jambo geni Waziri mkuu kaingia nalo!"

"Kuna jambo gani?"

Mfalme aliuliza.

"Mfalme hamjasikia kuhusu swala la Ufalme wa Iyumbwi na Nghumbi kuungana tena na kuwa Falme Moja?"

Waziri mkuu alisema kama swali. Alichokitamka kilimshitua Sana Mfalme Yolam, si Mfalme Yolam tu Bali hata Malkia Mkuu, Mama wa Mfalme Lady Sayuni.

"Umelijuaje swala hilo waziri mkuu?"

King Yolam naye aliuliza. Swali lake pia liliwafanya Mama yake pamoja na Waziri mkuu kumwangalia yeye kwa mshangao.

"Kwa maana hiyo unalijua Yolam?"

Mama aliuliza.

Yolam alibaki kimya kidogo, kwani siri yake ilionekana kuvuja.

"Ndiyo Nalijua!"

Kwa ulimi wake Mfalme Yolam alitamka.

"Mbona ujanambia kuwa Mama kuna hiki na hiki, na taarifa hizi zimetoka wapi?"

Malkia aliuliza.

"Kwakuwa tupo sisi hapa, ngoja niliweke wazi. Hili swala kweli lipo!"

Prince yolam alisema kisha akaanza kuwasimulia kila kitu alichoambiwa na Simweli.

"Kwa maana hata maono ya Eunike yanalenga huko huko?"

Malkia(lady Sayuni au Mama wa Mfalme) aliuliza.

"Ndiyo Mama, na ndilo Jambo ambalo linaniumiza kichwa changu mpaka sasa!"

"Kwani Eunike kazungumza Jambo gani ambalo linayahusanisha maneno haya?"

Waziri mkuu aliuliza ili apate kujua ni nini Eunike alikiona kupitia maono.

Mfalme hakusita kumweleza, alimueleza Jinsi maono yalivyokuwa. Hata waziri mkuu alishituka sana, hakutegemea kabisa kama angeambiwa kitu kama hicho kutoka katika maono.

"Kama limejidhihirisha katika maono ya Lady Divine lazima kuna ukweli ndani yake!"

Waziri mkuu alisema.

"Kama ninavyo waza Mimi!"

Mfalme alisema kumuunga mkono Waziri mkuu.

"Kama ni hivyo unazani tutafanya nini?"

Malkia aliuliza.

"Mama mpaka hapa ninawaza wapi nitampata huyo Kijana nimuue kabla hajafikia hiyo hatua!"

Mfalme alisema.

"Ni kweli Mfalme Yolam lakini kumbuka kuwa huyo Atazaliwa katika Ufalme wa Iyumbwi ila atalelewa na kukulia katika Ufalme wa Nghumbi, kama yupo bila Shaka atakuwa yupo Nghumbi!"

"Ni kweli Waziri mkuu lakini Mfalme alimzaa vipi Mtoto inje ya ndoa na alimtorosha vipi kumpereka katika Ufalme wa Nghumbi, au huyo Mtoto na Mama yake ndio walivuka mpaka na kuingia Nghumbi kwa kuyaofia Maisha yao katika Ufalme huu?"

Mama mfalme(Malkia sayuni) alisema.

"Nishafikiria sana Mama, nikawaza nitajaribu kujenga ukaribu na Ufalme Nghumbi halafu wakati huo huo nitawatuma vijana waingie katika Ufalme wa Nghumbi wakiwa kama wafanya kazi ndani ya Jumba la Ufalme. Na imani nitafanikiwa kwa njia hizo, lengo langu ni kumjua Huyo Mfalme Jina lake!"

Mfalme Yolam alisema.

"Kweli kabisa hata mimi naliunga mkono swala hili"

Waziri mkuu alisema.

"Mama lakini pia naomba kujua ni kipi kilichotokea kati ya Marehemu Baba yangu, na Lady divine Amana?"

Baada ya kuzungumza mambo mengine Mfalme Yolam alimrudia tena Mama yake amwambie ukweli kuhusu mfalme na Lady Divine.

"Hakuna kitu Yolam, nahisi kuna matatizo tu yaliwakuta njiani!"

Mama alisema. Hakutaka kabisa kumuweka mwanaye wazi juu ya alichokuwa anakijua baina ya Mfalme na Lady Divine. Alimficha kwasababu alijua anaweza kuyachukua maamuzi magumu.

Walijadiliana mengi kuhusu jinsi mipango yao itakavyokuwa, na walikubaliana kuwatuma watu, kwanza huku wao wakifanya utaratibu wa kutengeneza Ziara zao katika Ufalme wa Nghumbi, kwa lengo la kufanya upelelezi wa huyo kijana ambaye anasemekana atakuwa mfalme.

*******

Siku tatu baada ya Mfalme Yolam kuampishwa usiku wa manane ndio Lady Amana aliamka kutoka katika kupoteza Faham. Kwanza alijishangaa mwenyewe. Pembeni yake alikuwepo Eunike, wakati huo naye alikuwa amesinzia. Akiwa Bado amekaa kitandani kumbukumbu za matukio ambayo yalikuwa yamemtokea siku za nyuma yalianza kujirudia kichwani mwake. Alikumbuka siku ambayo alifanya mapenzi na Mfalme Zayoni katika milima ya Mbagilwa, hakuishia hapo hata pale alipoanguka kwenye farasi pia alikumbuka.

Baada ya kuyakumbuka alijishika kichwa, akaisi maumivu makari sana, hata kuhema hakaanza kuhemea juu juu, taratibu machozi yalianza kumdondoka.

alijiona kabisa alichokifanya na mfalme ameisaliti nafsi yake.

"Lady Amana!"

Wakati huo Eunike alishituka usingizini na kuliita Jina la Lady Amana. Kitendo kile kilimshitua sana Lady divine, akayafuta machozi yake haraka ili Eunike asitambue kama alikuwa Analia. Kwasababu ndani kulikuwa ni giza kwa kiasi chake.

Haraka Eunike aliwasha taa na mwangaza ukakiangaza Chumba kizima.

"Lady Amana!"

Eunike alimuita tena mwalimu wake. Alijisikia faraja kumuoma amemka. Eunike alikaa kitandani kwa mwalimu huku akimwangalia Usoni.

"Lady Amana, vipi unajisikiaje?"

Alimuuliza.

Swali lake alikujibiwa kwa wakati, Lady divine Amana alilinyamazia kwani alikuwa amezubaa sana. Bado kumbukumbu za dhambi yake zilikuwa zinajirudia kichwani.

"Lady Divine tafadhali naomba kujua unajisikiaje?"

Eunike aliuliza tena. Lakini Bado hakujibiwa. Baada ya kuona Lady Amana hamjibu Eunike alisimama atoke inje akawamshe wenzake ili waje wamuone mwalimu wao.

"Usitoke tafadhali!"

Lady Amana alisema. Hayo ndiyo yalikuwa maneno yake ya kwanza.

"Naomba Kujua unajisikiaje?"

Eunike aliuliza tena.

"Naomba Maji ya Kunywa kwanza!"

Lady Amana alisema. Haraka Eunike alitoka kitandani na kumchukulia Lady Amana maji ambayo yalikuwa mule mule chumbani kwake na kumpa. Lady Amana aliyapokea na kuyanywa maji Yale kisha akamrudishia Eunike kikombe.

"Nahitaji kuonana na Mfalme Zayoni"

Baada ya kunywa maji vizuri Lady Amana alisema hivyo. Kwanza Eunike alibaki ameganda kwa muda huku akimwangalia Usoni, ghafra machozi nayo yakaanza kumtoka.

"Mfalme kaisha fariki sasa ni wiki na siku kadhaa!"

Eunike alisema. Lady Amana alishituka sana baada ya kuambiwa hivyo.



Muda mfupi, tangu kuambiwa kuwa mfalme amefariki Lady Amana aliwaamusha wanafunzi wake na kukaa nao. Wakati huu alikuwa anaonekana katika hali ya udhuni sana.

"Nina jambo ambalo naimani litawashitua sana, ila naombeni mvumilivu wenu!"

Lady Amana alisema.

"Usijali Lady divine!"

Mmoja wa wanafunzi wake alisema.

"Tangu sasa sistahili tena kuwa Lady divine, badala yake nitabaki kuwa kama watu wengine, na Labda nitashirikiana nanyi kwa baadhi ya Vitu tu basi!"

"Kwanini Lady Divine?"

Eunike aliuliza. Kikundi kizima cha wanafunzi wake, ambao kwa Idadi walikuwa sita walishitushwa sana na alichokizungumza mwalimu wao na kiongozi wao.

"Ni kwasababu sahivi najiona sistahili tu kuwa Lady divine, na ningependa Eunike aitwe Lady Divine wa Hapa tangu sasa, Mimi msinitambue kama lady Divine ila mniite kwa jina langu la Lady Amana tu!"

Lady Amana alisema tena. Bado aliendelea kuuficha ukweli kwanini anataka kujivua u Lady Divine.

"Tafadhali naomba utwambie, bila kutwambia ukweli siku nyingine unaweza kupata matatizo tukakosa jinsi ya kukusaidia. Lakini ukitwambia tutaishi tukijua unatatizo gani?"

soma hapa kanuni tisa za mafanikio

ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments