Eunike aliuliza.
"Sawa Eunike ila nimeoteswa kuwa natakiwa niachie U lady Divine. Kwahio sina haja ya kuendelea kuwa Lady divine wakati maono kupitia ndoto yamenikataza nisiendelee!"
Lady Amana alisema. Maneno yake hayo yaliwafanya wanafunzi wake wote kumwangalia kwa muda kama sekunde kumi na tano bila kuzungumza Jambo lolote.
"Najua mnajisikia vibaya sana, lakini naombeni mkubalieni na hicho ambacho nimesema kuwa ni cha kweli na sistahili kuendelea kuwa Lady Divine!"
Lady Amana alizungumza tena. Alikuwa anazungumza huku machozi yakimtoka, alijisikia maumivu sana moyoni mwake. Ni kweli hakusitahili tena kuwa Lady divine lakini alichokitamka haikuwa sababu halisi ya kuuacha U Lady Divine ila ukweli wenyewe ni kwamba alifanya mapenzi na Marehemu Zayoni ambaye alikuwa mfalme kabla hajafa.
"Sawa Lady Amana. Lakini kunipa Mimi jukum kubwa hili unazani nitaweza kulihimili na wakati huo huo sijui hata kutafasili maono ya ndoto au hata maono ya Lady Divine!"
Eunike alisema.
"Sio kazi Eunike hayo nitakuelekeza tu kwasababu tuko wote, ila wewe unasitahili kuwa Lady divine na kesho nitaenda kuongea na Mfalme Yolam aweze kukutambulisha na Kukuapisha rasimi kwa watu wa Ufalme huu kuwa wewe ndiye Divine Mpya.
"Sawa Lady Amana"
Eunike aliitikia.
"Nashukuru kwa kunielewa. Sasa naomba turudi tukapumzike!"
Lady amana alisema. Alitaka wanafunzi wake warudi kulala.
"Lakini Lady Amana, kuna jambo tunahitaji msaada wako!"
Eunike alisema.
"Jambo gani Eunike?"
Lady amana aliuliza.
"Siku ambayo Prince yolam aliapishwa kuwa Mfalme, niliona maono ambayo yalinichanganya sana, lakini sikuelewa maana yake!"
"Maono yapi Eunike?"
Lady amana aliuliza, muda huo huo Eunike alianza kumsimulia maono yake aliyaona wakati anamuombea King Yolam wakati wa kuapishwa kwake.
"Tunataka tafasiri ya maono haya"
Eunike alimalizia kwa kusema hivyo baada ya kumsimulia Lady Amana maono yake.
Kabla hajaanza kuitoa maana halisi ya maono Yale Lady Amana alikuwa kama kashikwa na mshituko kidogo.
"Mbona umeshituka Lady Amana!"
Eunike aliuliza tena.
"Hapana, ila nilikuwa natafakari kuhusu maono hayo"
"Sawa Lady Amana"
Eunike alisema tena.
"Maono hayo yanamaanisha kuwa. Falme ya Iyumbwi itaungana na Falme nyingine na kuunda Falme moja kubwa sana!"
Lady Amana alisema. Muonekano wake haukuwa wa Furaha ilionekana kabisa kuwa kuna jambo kalificha katika tafasiri yake.
"Lakini kuna jambo hujatwambia maana yake. nyota iliyotoka katika nyota ya Mwanzo na kwenda kuungana na nyota nyingine, halafu wingu zito likatanda na kuzifunika zingine zote, hivyo vinamaanisha nini?"
Eunike alimuuliza tena Lady Amana baada ya kumuona kabisa kuwa alikuwa na Mashaka.
"Ni kweli Eunike, ni kwasababu ni Jambo la Mashaka, na nitawafanya muishi kwa mashaka sana!"
"Kwani ni Jambo baya sana?"
"Ndiyo lakini kwasababu ninyi ni Lady divine sina budi niwambieni yote iliyokweli kuhusu maono haya....Ni kwamba nyota iliyotoka katika Nyota nyingine ni Mtoto ambaye atazaliwa katika Ardhi ya Iyumbwi na atakulia katika Ufalme mwingine, na akifika huko atakuwa mfalme mkubwa, kisha atataka kuziunganisha Falme ya Iyumbwi na Falme hiyo nyingine. Wimbi jeusi linamaanisha kuwa lazima kutakuwa na vita kubwa sana, vita hiyo itasababisha kufariki kwa watu wengi sana. Lakini baadaye Falme hizi zitaungana na kuwa Falme Moja yenye nguvu na Amani kuliko hata ilivyo Iyumbwi ya Sasa!"
Lady Amana aliitoa tafasiri halisi ya Maono ya Eunike.
Baada ya kuipata Tafasili hiyo kila Mmoja alibaki kimya kwa muda huku wakitafakari jambo la kuzungumza.
"Je na hiyo Falme inaitwaje?"
"Hiyo Falme kwakweli siwezi kujua ni ipi lakini itakuwa ni Falme ya Nghumbi!"
Lady Amana alisema.
"Bila Shaka itakuwa ni yenyewe kwasababu niliwahi kuambiwa na Mama yangu kuwa, Iyumbwi na Nghumbi ilikuwa ni Falme Moja hapo kabla lakini ilitokea mtafaruku baina ya Maprince wawili waliotaka kila Mmoja kuwa Mfalme, hawa ndio waliouvunja Ufalme Mmoja wa Ng'umbwi na kujigawa kila Mmoja na Ufalme wake!"
Mmoja wa wanafunzi wa Lady Amana alisema.
"Ni kweli unachokisema. Eliena. Kwa maana hiyo Falme hizi mbili zitaungana tena!"
Lady Amana alisema.
"Kwahio hata huyo Mfalme Kaisha zaliwa? Na kama yupo alifika vipi katika Ufalme wa Nghumbi?"
Eunike aliuliza tena.
"Ni swala gumu sana kujua habari za Mfalme huyo, lakini hata Sasa King Joktan wa Nghumbi bado ananguvu sana, nahisi labda akitoka yeye ndiyo huyo Mfalme atakuja kuichukua nafasi yake. na Bahati mbaya sana King Joktan wa Nghumbi bado hajapata Mtoto atakaye weza kuulisi Ufalme wake!"
"Kwa maana hiyo haitokuwa wakati huu?"
"Hapana Eunike, nazani ni wakati huu huu wa King Yolam, kwani inaonekana kabisa inarudi katika Historia ya nyuma, kwani Maprince waliosababisha kugawanyika kwa Ufalme wa Ng'umbwi Majina yao Mmoja aliitwa Prince Yolam kama huyu huyu, na Mwingine aliitwa Cleopa. Wote hawa walikuwa ni Watoto wa Mfalme aliyeitwa Zilizayoni. Ukiangalia Jina La Baba yao, pia linaendana na jina la marehemu Mfalme Zayoni(Baba mzazi wa King Yolam)!"
"Kwahio Lady Amana, unamaanisha kuwa Mfalme Zayoni ameacha watoto wawili lakini Mwingine ndiye yuko huko Nghumbi na ndiye atafanya hivyo?"
Eunike aliuliza tena.
Swali hili lilimfanya Lady Amana kuinamisha kichwa Chini huku akiliangalia tumbo lake, kwani alihisi labda yeye ndiye atakuwa ameibeba mimba ya mwana wa mfalme ingawa kulikua hakuna dalili za mimba. Alishinda kuangalia kwa macho tu kwasababu bado alikuwa hajaamini kama ni kweli, aliupereka mkono wake wa kulia mpaka kwenye tumbo lake kuhakikisha kama kweli hana mimba. Alipogundua kuwa hana Mimba alimshukuru mungu kimoyo moyo huku akiomba mimba isije ikajitokeza kwani anaweza kuuliwa na Mfalme Yolam.
"Sina hakika na swala hili Eunike, lakini ninachokizungumza ni kutokana na maono yako!"
"Sawa Lady Amana!"
Eunike alikubali. Lakini hata muonekano wa Lady Amana ulibadilika na kurudi katika hali ya Mwanzo. Hakutaka tena kuendelea kukaa kulijadili swala hilo aliwaomba wanafunzi wake waingie chumbani kwao wakalale nayeye akasimama na kusogea chumbani kwake.
Wanafunzi wake walisimama kuingia Chumbani lakini walikuwa na Mashaka sana na Mwalimu wao. Kwa Jinsi alivyobadilika Ghafura kisha kuwaomba warudi wakalale iliwachanganya sana.
"Lazima kuna Jambo Lady Amana anatuficha, ndio maana anaonekana hana furaha, halafu kwanini kanikabizi Mimi majukum ghafura tu!"
Eunike akiwa chumbani na wenzake alisema.
"Ni kweli Eunike, hata Mimi ninamashaka, nilikuwa namwangalia sana. Nakumbuka ulipomuuliza kuwa, kwahio mfalme Zayoni kaacha watoto wawili, yeye amejishika tumbo lake. Mpaka sasa najiuliza kwanini amejishika tumbo lake, nahisi labda ana mimba!"
Eliena alisema.
"Ebu tayaache haya kwanza wasije wakasikia ikawa kesi!"
Eunike alisema kisha wote kwa pamoja wakanyamaza na kuendelea kulala.
******
Baada ya kufika kitandani kwake Lady Amana hakulala kabisa, mawazo yalikuwa ni mengi sana kichwani mwake. Alichokizungumza na Wanafunzi wake ndicho kilikuwa kinamtesa. Maono aliyoyaona Eunike yalimuumiza pia, aliyaamini kabisa kuwa ni ya kweli lakini huyo mtoto atakaye ziungamisha Falme hizo ni nani? Kwa jinsi alivyokuwa anamjua Mfalme Zayoni hawezi kuwepo Mtoto inje ya Ufalme, lazima huyo Mtoto atakuwa katika Tumbo lake hilo hilo kwani hata maono yalionesha nyota inameguka. Aliwaza sana Mpaka akahusanisha maono hayo na kuzipoteza fahamu zake kwa siku zaidi ya saba, kuwa ni miongoni mwa dalili za kumpata huyo Mtoto. Mawazo yaliendelea kumwandama Lady Amana usiku huo, mpaka alikuwa analishika tumbo lake Mara nyingi, huku akiomba miungu imuepushie mimba kwani ikitokea maisha yake yatakuwa ya mashaka.
******
Kesho yake nyakati za Saa mbili watu wote wakiwa macho Lady Amana aliwaomba wanafunzi wake wamsindikize kuelekea katika Chumba cha Mfalme Yolam akaongee naye!
Kwa pamoja walisimama na kuanza kuongoza kuelekea katika nyumba ya Mfalme.
Akiwa na timu yake, Lady Amana alikuwa anatembea kwa mawazo sana kuelekea katika nyumba au Chumba cha Mfalme.
Akiwa anatembekea katika varanda la Jumba la Kifalme, baadhi ya walinzi na wafanya kazi katika Ufalme walikuwa wakimshangaa, wengine walikuwa wakimfuata kumsalimia. Hiyo yote ni kwasababu walikuwa hawajamuona zaidi ya siku saba.
Walipoufikia mlango wa Kuingia katika Chumba cha Mfalme waligonga Hodi na kuruhusiwa kuingia.
Alipoingia tu hivi ndani alimkuta Mama Mfalme(Lady Sayuni au queen Sayuni) pamoja na Mfalme wamekaa wakizungumza.
Macho ya Lady Amana yalijipiga katika Uso wa Malkia sayuni kwa mshangao na Mshituko wa hali ya Juu, vile vile kwa Malkia Sayuni. Wote kwa Pamoja waliangaliana kwa muda sana.
Walipoyakutanisha macho yao, kila mmoja alishituka sana kumwangalia mwenzake, kwani kila mmoja alikuwa anamuhofia mwenzake kwa namna yake. Malkia Sayuni alikuwa anahakika kuwa Lady Amana alifanya mapenzi na Mfalme, halafu Lady Amana alikuwa anawasiwasi kuwa huwenda Mwanamke Yule Lady Sayuni au Malkia sayuni anaujua ukweli kuhusu yeye kufanya mapenzi na Mfalme Zayoni. Hapo ndipo ilikuwa ni mbinde. Walitazamana kwa muda sana, kama dakika moja kabisa, kisha Malkia Sayuni au Mama wa Mfalme ambaye mumewe King Zayoni ni marehemu, akaigeuza shingo yake upande Mwingine.
"Karibi Lady Divine Amana!"
Mfalme alimkaribisha Lady Divine kwenye kiti. wakati huo Mama mfalme alikuwa kimya.
Ndani ya Chumba cha Mfalme Lady Amana aliingia peke yake, wanafunzi wake aliwaacha inje mlangoni wakimngoja.
"Kwanza niishukuru Miungu yetu. Sijaamini kama kweli umeweza kuamka na kutembea ukiwa na nguvu hivyo. Kwanza nambie unajisikia je sasa?"
Mfalme Yolam aliuliza.
"Sasa hivi najisikia vizuri tu, wala sina tatizo lolote ambalo linisumbua"
Lady Amana alisema.
"Kama ni hivyo kwakweli Lazima nirudie kuishukuru Miungu ya Ardhi yetu.
"Ni kweli Yolam hata mimi nilikuwa namuwaza sana Lady Amana. Kwani nilikua na wasiwasi sana, sijui ni nini kilimkuta mpaka kuanguka kwenye Farasi"
Mama Mfalme(queen Sayuni) alisema huku akimwangalia Lady Amana usoni mwake. Wakati anazugumza alionekana kuwa mchangamfu na alikua akitabasamu.
Lady Amana alinyamaza tu kwanza.
"Kweli Mama ulichokisema....ngoja nimuulize kwanza Lady Amana.....ni kitu gani ambacho kiliperekea Wewe kuanguka kutoka Juu ya Farasi mpaka Chini?"
"Kwakeli sijui ni nini Mfalme Yolam!"
Lady Amana alimjibu Mfalme.
"Basi pole sana!"
Mfalme alisema tena.
Baada ya mfalme kusema hivyo Lady Divine aliinama chini, kumbe wakati huo machozi yalikuwa yanamtoka.
"Lady Amana mbona unalia?"
Mama Mfalme(Queen Sayun) aliuliza.
"Hapana Nahisi nitakuwa nimefanya kosa kubwa, kwasababu Mfalme Zayoni kafariki, halafu Mimi sijamzika!"
"Usijali Lady Amana. Hilo lishakwisha kwani ni wiki na siku sasa!"
Mfalme alimjibu.
"Nimeisha ambiwa na Wanafunzi wangu"
"Basi ndivyo ilivyo kama ushajua,.......Lady Divine Amana, ninashida kubwa sana na kwa bahati sana ndio umekuta tunaijadili Mimi na Mama.
"Ni kweli kabisa Lady Amana. Wewe ni Mtu wa muhimu sana katika Ufalme huu, tunakutegemea kwa mambo mengi!"
Malkia Sayuni naye alisema.
"Jambo gani hilo Mfalme Yolam?"
Lady Amana aliuliza.
"Ni kuhusu maono ya Eunike"
Mfalme alisema. Kwakuwa alikuwa kaisha ambiwa maono ambayo Eunike aliyaona, Lady Amana aliwambia kama alivyowambia wanafunzi wake.
"Sasa unashauri nini Lady Amana kwani hili ni Swala ambalo tunahitaji msaada wako?"
Malkia Sayuni alisema tena.
"Mpaka hapa sijapata jawabu kuhusu jambo hili, lakini Unalo liwaza wewe mfalme litakuwa ni muhimu sana kwasababu wewe ndiye Mwamuzi mkuu katika Ufalme huu!"
Lady Amana alijibu alipoulizwa na Mfalme. kuzungumza kwake kulikuwa si kama alivyokuwa amezoeleka. Muonekano wake ulikuwa unampa mashaka Malkia Sayuni au Mama wa Mfalme.
"Lengo la Mfalme ni kwamba akipatikana huyo Mtoto lazima auwawe tu, hakuna namna ya kufanya kwasababu sisi tunaishi katika usawa na hatuna haja ya kuungana na sehemu yoyote!"
Malkia Sayuni alisema. Alizungumza hivyo makusudi na alikuwa akimwangalia sana Lady Amana usoni. Ingawa maneno hayo yalikuwa mazito sana kwake, Lady Amana alijikaza kujipa Ujasiri wa kutoshituka.
"Lady divine....mbona unaonekana kuwa hauko Sawa au bado hujisikii Vizuri?"
Mfalme Yolam aliuliza kumbe hata yeye alishitushwa na hali aliyokuwa nayo Amana.
"Ni kwasababu kuna jambo nahitaji kuliomba na nahitaji lipokelewe!"
"Jambo gani hilo Lady Divine?"
"Tangu sasa sisitahili kuwa Lady Divine tena, na kwasababu hiyo nahitaji Eunike awe Lady divine mkuu wa Falme hii tangu masaa haya!"
Lady Amana alitamka maneno hayo huku Queen Sayuni na King Yolam wakimsikia.
"Kwanini umechukua maamuzi ya kushitukiza kiasi hicho?"
Mfalme aliuliza.
"Hapana ila wakati nimelala katika usingizi mzito baada ya kupoteza fahamu nilipata maono ambayo yalinikataza Mimi kuendelea kuwa Lady divine, ndio maana nimeamu kuja moja kwa moja kuusema ukweli huu mapema kwako Mtukufu Mfalme ili ukae ukijua!"
Lady Amana alisema. Aliamua kujiwahi mapema kabisa kusema sababu yake ili asikuze mada. Kwa Mfalme Alieleweka lakini kwa upande wa Mama Mfalme Queen Sayuni alibaki na Shaka sana.
"Sawa Lady Amana, lakini ningependa umuandae Lady Eunike kuwa Lady divine sasa!"
Mfalme alisema. Baada ya Mfalme kusema hivyo Lady Amana aliomba arudi sehemu yake.
Alitoka katika Chumba kile lakini alimwacha Malkia Sayuni akijiuliza maswali kibao kuhusu yeye.
*******
Baada ya wiki moja Lady Amana alianza kujisikia hali tofauti, hakutaka kula baadhi ya vyakula, kichefuchefu nacho kilianza kumwingia. Kwa dalili hizo zilitosha kabisa kumwambia kuwa anamimba tena mimba ya Marehemu Mfalme Zayoni. Hali hii ilimuumiza sana Lady Amana, kwanza hofu ilikuwa nyingi kweli kweli, aliyahofia maisha yake, alimuhofia Malkia Sayuni ambaye ndiye alikuwa Mke wa Mfalme Zayoni.
"Sasa wakiniuliza mimba nimeitoa wapi, nitajibu nini? Nitawambia kuwa nimepewa mimba na Mfalme, sasa si nitakufa!"
Alijisemea wakati huu alikuwa amekaa kitandani kwake, chumbani kwake. Mpaka hapo lady Amana alikuwa na chumba chake katika Jumba lile, hakuwa pamoja na wanawake Mabikira kwasababu yeye alikuwa kaisha jitoa na alikuwa na Uhuru wa kufanya vyovyote kama Mtu au mwanamke mwingine.
Na alikuwa aishi peke yake alipewa Mfanyakazi wa kumsaidia katika majukumu yake. Baada ya kuuacha U lady divine heshima yake katika Ufalme haikushuka, aliendelea kueshimika kama mwanamke bikira ambaye anaweza kuutoa msaada wakati wowote endapo ukihitajika, lakini kwa tatizo alilonalo itakuwaje, atafanya nini, endapo itajulikana. Kilicho muuma Aliwaza kuwa huwenda huyo Mtoto ambaye anaanza kutunga katika tumbo lake ndiye huyo Mfalme atakaye ziunganisha Falme hizo mbili, Ufalme wa Nghumbi na Ufalme wa Iyumbwi.
"Lady Amana Malkia Sayuni anahitaji kukuona!"
Akiwa Chumbani kabisa kitandani akiwaza, Mara aliisikia Sauti ya msichana ikigonga hodi. Muda huo huo Mfanya kazi wake alifika na kumuuliza kuhusu Malkia sayuni.
"Mwambie apite!"
Mfanyakazi Yule alifanya haraka na kurudi mlangoni kumuruhusu Malkia Sayuni aingie ndani.
"karibu Malkia sayuni!"
Lady Amana alisema baada ya Malkia Sayuni kuingia ndani ya nyumba au chumba Chake.
"Amana, mbona unaonekana kabisa huna Raha na leo siku ya pili sijakuona kabisa kutoka inje, unaumwa?"
Malkia Sayuni aliuliza. Wakati huu alikuwa akijaribu kumfanyia uchunguzi Lady Amana, alikuwa kaisha mtilia Mashaka.
"Nikweli, lakini napenda tu kukaa ndani!"
"Mh! Kwahio hauna tatizo kabisa linalokusumbua?"
Malkia sayuni aliuliza tena.
"Kweli sijikii vibaya niko mzima kabisa!"
Lady Amana alisema.
Aliuficha ukweli.
"Sawa, lakini nimekuja kukuharika katika sherehe fupi ya kumkaribisha Lady Divine Eunike ambayo itafanyika kesho saa nne mpaka saa sita. Itakuwa ni fupi wala haitachukua muda mrefu!"
Malkia Sayuni alisema.
Zilikuwa ni Taarifa za kushitukiza sana Kwa Lady Amana kwani alikuwa hajajipanga kwa jambo hilo. Baada ya kusema hivyo Malkia hakuendelea kukaa katika Chumba cha Lady Amana aliondoka na kurudi sehemu yake.
"Kwanini kaja yeye asije Eunike mwenyewe, Kuna nini ambacho kinaendelea, au kaisha Jua kuwa Nina Mjamzito?"
Baada ya Malkia Sayuni kutoka Chumbani kwake Lady Amana alibaki na maswali ambayo hakupata majibu. Wakati wote huu alikuwa na wasiwasi sana. Kiujumla mpaka hapo alikuwa kaisha jiweka rehani.
"Ee Mungu, tafadhali niepushie mtihani huu mzito kwangu, nilinde nisipate kugundulika au kufanyiwa jambo baya!"
Lady Amana alisema huku akiliangalia tumboni lake. Wakati huo huo aliupereka mkono wake wa kulia katika Tumbo lake ambalo lilikuwa na Dalili zote za kuwa ni Mjamzito, lakini Kijusi cha Tumboni bado ndio kilikua kinaanza kuota katika mfuko wa Mimba yaani Uterasi. Wakati analishika tumbo lake Machozi yalianza kumtoka Lady Amana.
"Lady Amana,. Usijali nimeisha kwahidi kuwa nitakulinda, hata kukutorosha kutoka katika jumba hili la kifalme nitakutorosha, na nitakupereka katika Kijiji chetu huko kuna Mjomba wangu, hawatojua kama huko huko!"
Mfanya kazi wake alisema, alimuhurumia sana. Mpaka inafikia hapo Lady Amana alikuwa kaisha msimulia ukweli kuhusu Mimba yake, kuwa ni ya Marehemu Mfalme Zayoni ambaye pia alikuwa Mume wa Lady Sayuni au Malkia Sayuni.
"Nashukuru Foibe, lakini naomba tusubili kwanza siku zikatika halafu ndio tutafanya hivyo"
Lady Amana alisema huku akiuinua mkono wake mpaka usoni na kuyafuta machozi yake.
*******
Baada ya Miezi mitatu mimba ya Lady Amana alianza kujichora kabisa, ilikuwa si ya kujificha katika upeo wa macho ya Mtu. Na Mpaka inafikia Miezi hiyo mitatu, yeye na Mfanya kazi wake Foibe ndio walikuwa wakiujua ukweli wote kuhusu mimba hiyo. Kukua kwa mimba kulikuza mawazo ya Lady Amana Mara mbili zaidi ya hawali.
"Foibe sasa naona Hali imeanza kuwa mbaya kwangu, itajulikana nahitaji, tufanye utaratibu Leo usiku nitoke hapa kwa namna yoyote ile"
"Usiku itakuwa mbaya nikushauri tutoroke kesho mapema masaa ya kawaida, tutaaga kuwa unatoka inje ya jengo la Ufalme kwa ajili ya kutembea na kuwaona Watu wa Iyumbwi kwani ni siku nyingi hujatembea!"
Foibe alisema. Alichokizungumza kilikuwa cha kweli kabisa na hata ushauri wake haukukataliwa na Lady Amana.
"Vizuri na nimegundua Jinsi ya Kuvaa, nitavaa nguo pana ambayo itanificha Tumbo, nisijulikane kuwa nimebeba Mjamzito halafu nitatoka. Nina Imani sitoshitukiwa!"
Lady Amana alisema.
"Samahani Lady Amana Malkia Sayuni anahitaji kuingia ndani kukuona!"
Wakati wakiwa katika mipango yao ya kutoroka Mara mlangoni sauti ya Mtu ilisikika ikimuombea Malkia Sayuni kuingia ndani.
Mapigo ya Moyo yaliwapiga paa! wote kwa pamoja, Lady Amana alikimbia chumbani haraka na kuvaa vazi kubwa, vazi ambalo lilimficha asionekane kama anamjamzito, halafu kichwani aliweka nguo lingine lefu pia ambalo lilikuwa limeshuka mpaka tumboni kabisa, kwa muonekano huo hakuonekana kama ni Mjamzito.
Baada ya kuvalia hivyo haraka haraka walimruhusu Malkia Sayuni Kuingia ndani.
"Karibu sana Malkia Sayuni"
Lady Amana alisema kumkaribisha Malkia Sayuni. Wakati huo Macho yote ya Malkia Sayuni yalikuwa Yameishia kwa Lady Amana hasa sehemu za Tumbo.
"Nashukuru sana!"
"Tukae"
"Asante"
Malkia Sayuni Alisema huku akikaa kwenye kiti.
"Foibe naomba utupishe kwanza"
Lady Amana alimuomba mfanyakazi wake ambaye alijulikana kwa Jina la Foibe awapishe wakati huo wote kwa pamoja walikuwa wamekaa kwenye, viti vilivyokuwa vimepangwa kuizunguka meza ya mduara.
"Nazani Karibu mwezi sasa sikuoni kabisa kutoka inje ya makazi yako. Una tatizo lolote linalokusumbua?"
Malkia sayuni aliuliza.
"Hapana, ila sioni umuhimu wa kutoka wakati sina mahara pakwenda na wala sina kazi ya kufanya huko inje"
"Sawa sawa, lakini hata kutembea tembea pia unashindwa Lady Amana!"
"Hapana wala sijashindwa kutembea tembea, ila Kesho ndio nilipanga kutoka kwenda kutembea tembea inje ya Jengo la kifalme!"
Lady Amana alisema.
"Hicho ndicho nilitarajia kukisikia kutoka kwako,...na utatoka saa ngapi hapa ili niandae ulinzi wa kuandamana na wewe huko huwendako usije kudhurika!"
Malkia Sayuni alisema. Maneno yake yalimshitua sana Lady Amana, akawaza kuwa mpango wake wa kutoroka hutafeli kama atawekewa Ulinzi.
"Lakini hakuna Haja ya kunipa ulinzi kwasababu si kwamba ni safari mahalumu bali kutembea tu"
"Sawa Lady Amana, lakini kumbuka kuwa unaheshimika vilivyo, na isitoshe hali yako hairuhusu wewe kutembea peke yako, unaweza kudhurika!"
Malkia Sayuni alitamka. Maneno yake yalimshitua sana Lady Amana.
"Kwa maana hiyo anaujua ukweli!"
Lady Amana alijisemea kimoyo moyo.
"Unamaanisha nini kusema Hali yangu hairuhusu kutembea peke yangu?"
"Nilijua toka mwanzo kabisa, yaani hata kabla sijawa mke wa Marehemu Mfalme Zayoni. Najua kabisa kuwa ninyi na Zayoni mlikuwa katika uchumba, ingawa wewe uliteuliwa kuwa Lady Divine. Najua kuwa Mfalme zayoni alikuwa akiishi kwa mateso sana kila alipokuwa anakuona, ndio maana kila ulipokuwa unaudhulia kwenye vikao vyake, hoja yoyote ambayo ulikuwa unasema Zayoni alikuwa anaipitisha tu hata kama ilikuwa mbaya. Mfalme zayoni alikuwa Anakupenda wewe kupita kiasi, alinioa mimi kwasababu tu kulikuwa amna jinsi zaidi kukubali baada ya kukuona wewe ukipewa Mamlaka ya kuwa Lady Divine. Kwanza toka hawali nilijua kuwa wewe na Marehemu Mfalme Zayoni mlikuwa mkifanya mapenzi kwa siri, lakini kumbe naye aliliinda heshima yako. Na nililigundua siku ambayo mlienda katika safu ya milima ya Mbagilwa mlifanya mapenzi na Mfalme Zayoni, hiyo ndio sababu ya kuuachia U lady divine na isitoshe wewe ni Mjazito!"
Malkia Sayuni alisema. Huyu ndiye alikuwa Mke halisi wa Marehemu Zayoni na Mama Mzazi wa Mfalme Yolam. Aliutamka ukweli wote kwa Lady Amana. Ilikuwa kama kamkamata Lady Amana roba ya shingo.
"Sikutaka kufanya hivyo, yeye ndiye alining'ang'aniza kufanya naye mapenzi, alitaka kujirusha kabisa kutoka juu ya Mlima mpaka chini, baada ya kutaka kufanya hivyo sikuwa na budu kumpa alichokuwa anakihitaji ili asife!"
Lady Amana aliusema ukweli wake kwa Malkia sayuni. Machozi yalianza kumtoka.
"Usilie Amana. Niliujua ukweli mapema kabisa kwasababu Mimi nina utambuzi na ni mzoefu. Najua kabisa wewe huna kosa, na hukufanya kwasababu ulitaka, ila nilimjua mfalme Zayoni alikuwa Mbishi na alkuwa king'ang'anizi sana....lakini hayo tuyaache kwasababu huna kosa ndio maana siri hii ninayo mimi pekee ila Mtoto atakaye zaliwa kutoka katika Tumbo lako ndiye Mwenye madhara katika Ufalme huu. Labda nikuombe kitu kimoja, kuwa nitakutunza na kukulinda kwasababu tushachelewa ila naomba ukijifungua Huyo Mtoto naomba ukamuue au mtupe shimoni. Nasema hivyo kwasababu yeye ndiye atakuja kuusumbua Ufalme huu, labda akiwa wa kike ndio itakuwa pona pona yake!"
INAENDELEA
0 Comments