Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Ujumbe Kutoka Ndotoni (Notifacation From The Heaven) Sehemu Ya Tano

 


Malkia Sayuni alisema. Maneno yake yalikuwa mazito kweli kweli, mpigo ya moyo wa Lady Amana yalikuwa yanakimbia mbio sana. Machozi yalianza kumvuja tena kwa mara nyingine huku macho yake yalikuwa yameishia katika uso wa Malkia Sayuni.

"Mbona unalia wakati nimeisha kwambia kuwa nitakulinda, na siri hii itabaki ya kwangu na Wewe mh....... Halafu umenambia kesho utaenda kuitembelea mitaa ya Iyumbwi, kweli nimeisha kwahidi kuwa nitakupa Ulinzi, kwahio nitaanza kesho kuonesha kuwa nakulinda na kukujali!"

Malkia Sayuni alisema tena kisha akasimama na kuondoka katika nyumba au chumba cha Lady Amana.


"Lady...!"

Ilikuwa ni sauti ya Foibe Mfanyakazi wa Lady Amana, baada ya kuingia ndani na kumkuta Lady Amana akiwa analia machozi.

"Kwani umekuwaje?"

Foibe aliuliza lakini Lady Amana hakujibu chochote, mikwara aliyopigwa ilikuwa ya Maana kweli kweli.

"Kwani kaisha ujua ukweli kuwa wewe ni Mjazito?"

Foibe aliuliza tena kwa Mara nyingine.

Bado Lady amana hakumjibu wala kusema neno lolote aliendelea kunyamaza huku machozi yakimtoka.

"Najua kuwa ameisha ujua ukweli, lakini naomba usijiumize kwa alichokisema. Wala usijali kwa lolote Lady Amana, Mimi niko pamoja na wewe mpaka mwisho na hutodhurika kwa chochote. Nitakulinda na nitakutorosha hapa!"

Foibe alisema kwa kujiamini kabisa.

Maneno yake yalimfanya Lady Amana kuinua uso wake na kumwangalia Foibe usoni.

"Sijui ni kwanini yananikuta haya wakati Mimi sikuyataka!"

Lady amana alisema.

"Pole Lady Amana, ila alichokwambia naomba ukisahau hapa hapa na niamini Mimi kuwa nitakusaidia na tutafanya kila mbinu nikutoroshe hapa kesho kama tulivyopanga"

Foibe alisema, maneno yake yaliazidi kumfanya Lady amana matumaini. Ingawa alikuwa anajisikia Machungu alimshika Foibe mkono na kusema.

"Sawa Foibe hata Mimi naamua kujitoa kwa lolote lakini kesho tutoke hapa, siwezi kuishi katika mazingiira ya wasiwasi. Nahitaji nimzaye mwanangua salama bila hofu!"

"Usijali Lady Amana, naimani Miungu iko na wewe, siku za kujifungua zikifika utajifungua kwa usalama kabisa!"

"Kweli Foibe, hata Mimi nitajitoa kama ulivyojitoa kwangu!"

Lady Amana alisema kisha akayafuta Machozi yake. Ingawa alichoambiwa na Malkia kilikuwa ni cha kuogopesha lakini yeye aliona ni Bora kupambana hivyo hivyo.


Baada ya kuachana na Lady Amana Malkia Sayuni alikuwa amekaa ndani kwake alionekana mwenye mawazo pia.

"Ufalme wa Iyumbwi utakuwa katika hali ngumu sana baadaye, na bila Shaka huyo Mfalme hajazaliwa. Mwanamke ambaye hatamzaa Mfalme huyo bado atakuwemo humu ndani ya Ufalme, kwahio fanya juu chini umtafute kama ni kumuua umuue haraka......... Ebu fanya yote ukimuhurumia mwanao Mfalme Yolam kwani lazima akutane na Changamoto za kutosha au kupoteza Maisha yake!"

Hayo ni Maneno ambayo Malkia Sayuni aliyakumbuka. Maneno hayo yalisemwa na Mwanaume ambaye anaishi inje kabisa ya Ufalme, Mwanaume huyo alikuwa ni mtabili wa mambo ambayo yanakuja kutokea. Na Malkia Sayuni alimfuata baada ya maono ya Lady Amana kumtisha.

"Hapana lazima nifanye mpango wa kukuua, sina jinsi kwasababu nisipolitekeleza hili nitashindwa kuulinda ufalme wa Mwanangu Yolam!"

Malkia Sayuni alijisemea mwenyewe baada ya kuyakumbuka maneno ya mtabili aliyeongea naye. Hasira alizokuwa nazo zilianza kujichora usoni mwake kwa kuonesha mikunjano, kwamaana hiyo kaamua kubadilika juu ya maamuzi aliyokuwa ameyatoa kwa Lady Amana muda mfupi.

*******

Wakati mambo Yale yanaendelea katika Ufalme wa Iyumbwi, Yolam hakuwepo katika Falme yake, yeye alikuwa yupo katika Ufalme wa Nghumbi kuongea na Mfalme Joktan. Alikuwa huko kwa sababu kuu moja ambayo ni kulijua jina la Mfalme ambaye katabiliwa. Jina hilo limo ndani ya kitabu cha Hadithi ya kweli ambayo itakuja kutokea. Wakiwa katika Mazungumzo yao ambayo yalikuwa kama sehemu ya kuzipatanisha Falme hizo mbili, King Yolam alisema.

"Nasikia kuna kitabu cha Hadithi nzuri kweli katika Maktaba yako ya Vitabu, hadithi hiyo ambayo inasemekana kuwa aliwahi kuwepo mfalme ambaye aliziunganisha Falme mbili. Natamani kujua jina la Mfalme huyo maana nikizaa Mtoto nitamuita Jina hilo, kwasababu anaonekana huyo Mfalme alikuwa shujaa kweli kweli!"

Maneno yake yalimfanya King Joktan wa Nghumbi kushituka kidogo, kisha akacheka, hakuelewa King yolam wa Iyumbwi alisema hivyo kwa maana ipi!"

"Vipi unataka kuzifanya Falme ya Iyumbwi na Nghumbi kurudi kama zamani?"

King Joktan naye aliuliza pia.


Kabla sijaimaliza Hadithi hii nikukumbushe kuwa Mcha mungu.



Swali lake kidogo lilimshitua King yolam. Lakini alilijibu hivi.

"Hapana najua kabisa kuwa Nghumbi na Iyumbwi ni Watoto wa Baba Mmoja, kwahio kila mmoja akikua huwa anakuwa na Majukumu yake na Familia yake, lakini Undugu utabaki kuwa pale pale!"

King Yolam alisema.

"Unamaanisha nini King Yolam?"

King Joktan aliuliza.

"Namaanisha kuwa Iyumbwi na Nghumbi zitabaki kama zilivyo, na hakutokuwepo na Uhasama kwasababu sisi ni watu wamoja, na tutashirikiana kwa kila Jambo!"

"Nimekuelewa, kwanini unataka jina la kwenye Hadithi wakati hayo ni maandishi ya watu walikuwa na vipaji vya kusimulia hadithi watu wakasoma na kujisikia raha!"

"Ni Kweli King Joktan lakini.....kwa imani yangu huwa najua kuwa waandishi Mara nyingi huwa ni Watu ambao wamepewa maono Fulani na Mungu juu ya mambo ambayo yalikuwepo na Ambayo yatakuja kutokea. Huwa ni Watabili wazuri na Mara zote wanamaarifa sana. Nishasoma vitabu vingi sana vya Hadithi lakini baada ya kusimuliwa kidogo hadithi hiyo nilipenda sana. Nilipouliza kuwa Kitabu cha hadithi hiyo kiko wapi? niliambiwa kuwa kinasadikika kipo katika Ufalme wa Nghumbi na ni kimoja tu, niliamasika sana baada ya kusikia kuwa ni Nghumbi. Kwasababu Ardhi ya Nghumbi na Iyumbwi ni Ndugu siku moja nitawatembelea na nitaomba hicho kitabu nikisome, na ikiwezekana nimuombe King Joktan anisaidie kiandikwe kingine nami nikipate ili kizazi cha Ufalme wa Iyumbwi nacho kiwe kinakisoma"

King Yolam alisema. Alizungumza maneno mengi ili kumfanya Mfalme Joktan kukubaliana naye, ilimradi tu ampe kitabu hicho akisome au Amtajie Jina la Huyo mfalme aliyeandikwa ndani ya hicho kitabu cha hadithi ya Kweli, hadithi ambayo Mfalme wa Nghumbi King Joktan alikuwa aujui ukweli kuwa ni Kitabu kilichobeba Hadithi ya Kweli.

"Nimekubali ulichokizungumza lakini nikutajie Jina au nimtume Mtu akakilete hicho kitabu ukisome mwenyewe. Ila sitokuruhusu uondoke nacho kwasababu hata Mimi nakipenda sana kitabu hicho!"

King Joktan alisema.

"Sawa nitafurahi sana, kuisoma Hadithi hiyo, halafu na hilo Jina La huyo Mfalme nalihitaji sana. Tena naomba Mke wangu Queen Eda akipata Mimba ya Mtoto wa Kwanza awe mwanaume nimuite Jina hilo!"

"Ha ha ha ha!"

King Joktan alicheka baada ya kuyasikia maneno ya Mfalme mwenzake wa Iyumbwi King Yolam.

"Jina lake ni KING ZILEOPA!" Baada ya kucheka hatimaye Mfalme Joktan alilitamka jina la Mfalme alieandikwa kwenye kitabu.

"Si umeona, ni Jina zuri na nimelipenda sana. Lazima nitamuita Mwanangu wa kwanza wa kiume Jina hilo, nitakuwa namuita Prince Zileopa!"

Mfalme Yolam alisema kwa furaha sana. Wakati huo huo kitabu cha Hadithi ile ya kweli kililetwa kwa ajili ya yeye kukisoma. Hakuwa na nia ya kukisoma Kitabu hicho chote ila shida yake ilikuwa ni kulijua Jina la Mfalme ambaye ataziunganisha Falme za Iyumbwi na Nghumbi. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ilikuwa ni kumjua haraka ili uwezekano wa kumuua upatikane kwa namna yoyote ile.

Taratibu alianza kukifungua kitabu hicho kwa ajili ya kukisoma. Wakati huo Mfalme mwenzake King Joktan alikuwa akimwangalia tu Mfalme huyo kijana wa Iyumbwi. Umri wa Mfalme Joktan ulitofautiana sana na Umri wa King Yolam, King Joktan alikuwa na Umri zaidi ya Miaka 35 lakini Yolam yeye alikuwa na umri usiopungia Miaka 23, alikuwa bado ni kijana kabisa.

Alitumia nusu saa tu kukisoma kitabu kile kisha akakifunika. Hakikuwa kitabu kikubwa kiasi hicho kilikuwa kitabu cha kurasa kama ishirini tu, maana yake ni kwamba karatasi zenye maandishi zilikuwa hazipungui karatasi kumi, hiyo ni kwa hesabu ya haraka haraka.

"Kwakweli ni kitabu kizuri haswa, ni hadithi nzuri sana. Kwakuwa nimekisoma Mimi mwenyewe nitakiandika kitabu kingine kwa ajili ya Kizazi cha Kifalme katika Ufalme wa Iyumbwi. Lakini Jina la Mfalme Zileopa hili nimelipenda kuliko kitu chochote, ni Jina zuri kweli kweli!"

Baada ya kukisoma kitabu kile King yolam alisema maneno hayo kama mapambio kwa Mfalme Mwenzake.

"Safi sana. Sasa nina imani umefurahi vya kutosha. Kiujumla hata mimi nilifurahi sana baada ya kukisoma kitabu hiki kwa mara ya kwanza, lakini kinanisikitisha hasa pale Zileopa alipoota ndoto ya kumuua mama yake, na hatimaye kweli anamuua kwasababu ilipaswa iwe hivyo!"

"Ni kweli Kabisa King Joktan, lakini pia inaonesha udhaifu sana kwake, kwasababu watu wengi sana waliuwawa wakati yeye alikuwa kaisha pata taarifa za ukweli kupitia ndoto!"

"Hapo kweli Udhaifu aliuonesha lakini kumbuka pia naye alijitahidi sana, maana si kazi rahisi kumuua Mama mzazi, basi kwasababu ilimpasa afanye hivyo lakini mh inauma sana!"

"Ndio maana hata mimi nimelipenda Jina lake kwasababu ni Jasiri kweli, hata Mama yake pia alikuwa Jasiri sana, yaani kukubali mwanaye amuue ili watu wasiendelee kufa, kwakweli alikuwa ni Mwanamke wa aina yake. Bahati mbaya hajatajwa humu jina lake, ningeliona humu ningempa Mwanangu wa Kike kwani naamini hata yeye angekuwa Malkia Jasiri kama Mama mzazi wa King zileopa!"

King Yolam alisema.

"Kuhusu Mama mzazi wa Kingi Zileopa kutotajwa si imeandikwa kuwa ni Mama katika kizazi cha watu wa Mungu!"

King Joktan alisema.

"Nimeona ila sasa wanawake wema wapo wengi sana!"

King yolam wa Iyumbwi alisema. Mazungumzo ya wafalme wale wawili yaliendelea kudumu huku wakijadili maswala muhimu kuhusu Falme hizo.

*******

Kwakuwa ziara ya King Yolam katika Ardhi ya Nghumbi haikuwa ya masaa kumi bali ya siku nzima, alilazimika kulala katika Ufalme wa Ngumbi. Alifanya hivyo ili kuonesha kuwa alikuwa na shida ya kudumisha mahusiano baina ya Falme yake na Falme ya Nghumbi, lakini lengo kubwa lilikuwa ni kwa Ajili ya King Zileopa aliyetajwa katika Kitabu cha hadithi ya ukweli.

King yolam alikuwa na mawazo makubwa mawili.

Wazo la kwanza lilikuwa Kwamba; Zileopa aliyeandikwa akija kuwa Mfalme basi akute uhusiano mzuri baina Falme hizo mbili ukiwepo. Kwa maana hiyo hata kumuua itakuwa rahisi kwasababu wangemuarika katika Ufalme wa Iyumbwi kabla hajaanza kuyafanya mambo ambayo atayafanya. Njia hiyo itakuwa rahisi sana kwao. Hiyo ilikuwa ni plani ya mbali lakini ilikuwa nzuri sana.

Plani ya pill ilikuwa kwamba; urafiki wao ungeweza kusaidia kumgundua King Zileopa aliyetajwa kwenye kitabu mapema. Hii nayo ni nzuri kwasababu inaenda kusababisha kumuua Zileopa Mapema kabla hajawa Mfalme.


Nyakati za usiku, ndani ya Jumba la Kifalme la Nghumbi katika Chumba alichopewa kulala King Yolam alionekana mwenye mawazo sana. Kulikuwa na Jambo kubwa ambalo lilikuwa linamsumbua kichwa.

"Ni kwamba Ufalme wa King Zileopa ni Ufalme ambao baadaye watu wake waliufurahia sana, inasadikika kuwa Ufalme huo ulikuwa ni Ufalme wa aina yake, vyakula vilipatikana kwa wingi sana katika Falme hiyo......... Jina la Mfalme Zileopa limejificha katika Maneno hayo kwasababu ni Mfalme wa pekee na hakuwahi kushindwa kwa Jambo lolote!"

Akiwa mwenye mawazo chumbani King Yolam aliyakumbuka maandishi ambayo aliyasoma kwenye kitabu cha hadithi ya Kweli kabisa.

"Lakini Bado sijashindwa nitamjua tu, hata kama jina lililotajwa kwenye hiki kitabu sio ila nitalipata"

King yolam alijisemea. Inaonekana aliyaelewa aliyosoma kuwa.. Jina la Mfalme Zileopa limejificha katika Maneno hayo, kwasababu ni Mfalme wa pekee na hakuwahi kushindwa kwa Jambo lolote.

Maneno hayo yalikuwa na maana kubwa sana, kwani ni kweli Kabisa kuwa Jina hilo ndilo jina lililolibeba Jina la Mfalme alieandikwa kwenye kitabu cha hadithi ya kweli, lakini jina lake siyo Zileopa kama lilivyo andikwa, ila ndani ya hayo maneno ndimo litatoka jina la Mfalme huyo.

Mawazo yalikuwa Mengi sana kwa Mfalme Yolam. Ingawa kweli imeandikwa kuwa Mfalme Zileopa atakuwa Mfalme wa pekee na Ufalme wake hutokumbwa na Matatizo yoyote, lakini Kitendo cha watu kufa pia kilimuumiza King yolam halafu wakati huo huo naye alikuwa ni Mfalme aliye jiona kuwa yuko katika Ubora. Hicho ndicho kilikuwa kinamfanya King yolam kufanya kila namna ili apate kumwangamiza mfalme aliendikwa kwenye Kitabu cha Hadithi ya Kweli.

Kwa kuisoma tu hadithi hiyo bila kujua kuwa ni Hadithi ya ukweli, ilikuwa ni Vigumu kugundua kuwa ni hadithi ya ukweli ambayo iliandikwa kutokana na maono kupitia ndoto za watu wa zamani. Mwandishi wa Hadithi hiyo aliufikisha ujumbe wake kwa njia hiyo kwasababu aliogopa kufa na wakati huo Vita baina ya King Cleopa wa Kwanza na Yolam wa kwanza vilikuwa vimeshamili kweli kweli.

Usiku wa siku Hiyo Kwa King Yolam ulikuwa hauna furaha kwa kiasi chake, lakini alipata kupumzika mpaka kukacha.

********

Siku iliyofuata katika Ufalme wa Iyumbwi, Asubuhi na nyakati za Saa nne watu walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kumpokea Mfalme wao King Yolam ambaye alikuwa anatoka katika Ziara ya Siku Moja huko katika Ufalme wa Nghumbi.

"Kama tulivyokuwa tumepanga, Jana Leo ndio siku ya pekee ya kutoroka hapa, wakati Mfalme anaingia katika geti la utawala sisi tutatoka, hatutopitia kwenye geti kubwa tutapitia katika Geti ndogo, huko hakutokuwepo na Ulinzi Mkubwa atakuwepo Mlinzi Mmoja na nishaongea naye, amekubali!"

"Sawa tu Foibe tujiandae tu tuweze kutoroka!"

"Ndio, ila tusubili tu ule wakati wa Mfalme kuingia ndani ya geti nasi tutoke, najua watu watakuwa wengi sana kumpokea na macho yataishia kwakwe!"

Wakiwa ndani kwao, Lady Amana na Foibe Mfanya kazi wake, walikuwa wakijadiliana Jinsi ya kutoroka na kuitoka mikono hiyo kwa hofu ya kuuliwa yeye pamoja na Mwanaye wa tumboni siku sijazo.

"Samahani Lady Amana Malkia Sayuni anahitaji kuingia ndani!"

Wakiwa katika Maandalizi yao ya Mwisho kabisa mara mlangoni Malkia sayuni aliombewa Kuingia ndani.


Kabla Sijaimaliza Hadithi hii ninakuomba kuwa Mcha mungu.



kusikia tu kuwa Malkia Sayuni anaomba kuingia ndani Mapigo ya Moyo wa Lady Amana yalipiga Paa! Kisha akaanza kuhemea juu juu.

"Mwambie aingie!"

Walimruhusu Malkia Sayuni kuingia ndani.

"Naona unafanya mandalizi ya kumpokea Mfalme Yolam. Huyo ndio moyo ambao nautaka, ila natamani nifanye Jambo kwako, lakini kila nikifika katika nyumba yako hii, moyo wangu unaniambia Lady Amana ni Dhahabu kwako. Mkumbatie sana mwanamke huyo na usiache akateseka kabisa. Lady Amana, wewe ni Mwanamke mwenzangu, mke wa pili wa marehemu Mfalme Zayoni, lakini masikini Ufalme utambui kuwa wewe pia ni Malkia katika Ufalme huu. Ila kwasababu Mimi natambua lazima nikupe heshima yako ya Umalkia. Sasa nimekuja tuongozane kumpokea Mfalme Yolam, anatoka katika Ufalme wa Nghumbi. Fanya tu matayarisho Mimi nakungoja hapa hapa!"

Malkia sayuni alisema tena alikuwa akitabasamu kweli kweli. Mawazo yake makubwa ilikuwa kutaka kumuaibisha Lady Amana mbele ya Kadamnasi ya watu, lakini pia alikuwa kama kikwazo cha kuikwamisha safari ya Lady Amana ya kuhitaji kutoroka kutoka katika Jengo la utawala wa Iyumbwi na kwenda kuishi mbali.

"Lakini sijajiandaa kwa swala hili!"

Lady Amana alisema.

"Maandalizi makubwa hayana tija kwasababu ni hapa hapa tu, we vaa nguo za kawaida tu tutoke pamoja nje tukampokee Mfalme!"

Malkia Sayuni alisema tena. Wakati huo Lady Amana Alianza kujiangalia tumbo lake, huku machozi yakimminika mashavuni. Masikini Lady Amana kila alipokuwa anakuwa katika wakati Mgumu alikuwa analiangalia Tumbo lake ambalo lilikuwa limembeba Mtoto.

"Isingekuwa hii Mimba nisingekutana na Matatizo ya namna hii!"

Lady Amana alijisemea tena kimoyomoyo huku macho yake yakimwangalia Malkia Sayuni.

"Amna Jinsi Lady Amana, najua ni Kwasababu Ishatokea....nakumbuka kuwa jana nilikuahidi kuwa nitakulinda na nitalifanya jambo hili kuwa siri, ila kukulinda nitakulinda, lakini kulifanya jambo hili siri haitowezekana kabisa, kwasababu wewe ni Malkia katika Ufalme, lazima Watu pia wakujue. Si kwamba nimekurupuka kukwambia haya, nimekaa nikatafakari nikapata mawazo hayo"

Malkia sayuni alisema tena. Wakati huo alisogea kabisa alipokua amesimama Lady Amana.

Baada ya kumfikia Lady Amana, Malkia Sayuni aliisogeza midomo yake na kumnong'oneza Lady Amana maneno haya.

"Najua unaumia sana, lakini sina Jinsi Amana, namuhurumia Mwanangu Mfalme Yolam!"

Maneno hayo yalimuingia vizuri Lady Amana, hakuwa na Jinsi ya kufanya kwasababu alifanya makosa yeye mwenyewe. Mpaka hapo alikuwa anajutia kwanini alikubali kufanya mapenzi na marehemu Mfalme Zayoni. Lakini pia alisitahili kufanya hivyo ili kuulinda Uhai wa mfalme, hata kama asingefanya, Kesi ingemgeukia kuwa yeye ndiye alimuua Mfalme, kwasababu walikuwa wawili tu katika milima ya Mbagilwa.

"Foibe!"

"Abee Mtukufu Malkia!"

Malkia alimuita mfanyakazi wa Lady Amana naye akaitika kwa Adabu sana. Foibe hakuwa inje wakati hayo yanaendelea, alisikia kila neno ambalo lilikuwa linazungumzwa na Malkia Sayuni.

"Naomba umwandaye Malkia mtukufu wa Falme hii, Lady Amana kwa ajili ya Kumpokea Mfalme Yolam!"

Malkia Sayuni alisema. Jinsi alivyomuita Lady Amana kuwa Malkia, iliwashitua sana lakini hawakuweza kutamka chochote. Kwa haraka Foibe aliimshika Lady Amana mkono na kuingia Chumbani kwa ajili ya kumwandaa ili akampokee Mfalme.

"Usiwaze Lady Amana, hata leo ikishindikana kutoka hapa, ila Lazima hapa tutoke hata kesho!"

Foibe alisema baada ya kufika chumbani yeye na Lady Amana huku akimwandaa.

"Kwa Jinsi inavyoonekana sizani kama tutafanikiwa Foibe"

"Kwanini Lady Amana?"

"Nasema hivyo kwasababu huyu mwanamke kanijia juu sana!"

"Usijali Lady Amana,......na nimepata wazo jingine, wakati Mfalme anaingia tu hivi naomba utoroke pale pale uzunguke mpaka nyuma ya jumba la Ufalme kwenye ule mlango Mdogo, najua wakati huo Malkia Sayuni atakuwa bize kumpokea Mfalme"

"Ni kweli Foibe Lakini Kumbuka kuwa mimi ni Mjamzito, macho ya watu yatakuwa yameishia kwangu, na Unajua kabisa kuwa Mimi ndiye Lady Divine wa Kwanza kubeba mimba!"

Lady amana alisema.

"Hakuna atakae gundua kuwa wewe ni Mjamzito, mimba yako bado ndogo haionekani kwa kiasi cha kwamba inaweza kugundulika katika macho ya Watu kama utakuwa umevaa mavazi haya"

Foibe alisema huku akimfunga Lady Amana nguo.

Foibe alikuwa Binti wa Umri wa miaka kumi na Tisa. Alikuwa na akili za kutosha, kwa mawazo yake hayo alionekana kabisa kuwa alikuwa ni Mama wa miaka thelathini. Kweli alimaliza kumwandaa Lady Amana vizuri, kisha wakatoka chumbani wakamkuta Malkia Sayuni akimngoja Lady Amana.

"Kumbe Foibe unajua kulemba umemvisha Lady Amana utafikiri si mjamzito!....lakini sawa twende tukampokee Mfalme Yolam"

Malkia Sayuni alisema kisha wakatoka inje na kuelekea walipokuwa wamekusanyika watu karibu wote ndani ya Ufalme kwa ajili ya Mapokezi ya Mfalme. Watu waliokua wanamuona Lady Amana walikuwa wanamfuata pia kumsalimia, ni Mwanamke ambaye alikuwa anathaminiwa sana katika Ufalme ule. Hali hiyo ilikuwa ikimfanya ajisikie uzuni sana.


Wakati inje huku watu wakimsubilia Mfalme Foibe yeye alikuwa kaisha kusanya vitu vya muhimu na anaanza kuutoroka taratibu kutoka ndani. Alifanikiwa kutoka bila kuonwa kabisa, na kuzunguka upande wa nyuma ambako kulikuwa na Mlango mdogo, ilikuwa ni Mapema kabisa masaa ya Saa nne, kama alivyokuwa amepanga alimkuta Mlinzi Mmoja tu ndiye kakaa upende huo.

"Lady Amana yuko wapi?"

Mlinzi alimuuliza.

"Usijali Anakuja muda si mrefu!"

"Mnafanya nini sasa, amuoni kuwa unaniweka Mimi matatani! Ningewaruhusu mkapita sasa hivi mkaondoka zenu!"

"Usijali kama nilivyokwambia yupo anakuja, Malkia Sayuni ndiye kamchukua kwa ajili ya kumpokea Mfalme, lakini hachelewi!"

Foibe alijitetea kwa mlinzi wa mlango wa nyuma. Ulikuwa si Mlango mkubwa kiasi hicho, ulikuwa ni Mlango mdogo kabisa, tena mtu alikuwa anapita ameinama. Mlango huo ulikuwa wa njia kubwa iliyokuwa inapitia chini ya Ardhi na kutokea upande wa pill ambako kulikuwa na Milima. Uliwekwa kwasababu ya Dharula kama itatokea katika Ufalme.

"Haya njoo ujifiche huku usije kuonekana ikawa kesi kwangu!"

Mlinzi alimwambia Foibe. Kwa umakini Kabisa Foibe naye alielekea sehemu aliyoambiwa kujificha huku akimsubili Lady Amana.

*******

Dakika chache kupita tangu Malkia na Lady Amana kufika sehemu ya mkusanyiko wa kumpokea Mfalme, geti nalo lilifunguliwa kuashilia kuwa Msafara wa Mfalme unafika.

Watu karibu wote walikaa sitandi bayi kwa ajili ya kumpokea Mfalme.

Malkia Sayuni alijisahau kabisa kuwa alikuwa ameandamana na Lady Amana, alijikuta anasogea mbele kabisa kwa ajili ya kumpokea Mwanaye, ambaye alikuwa anaingia ndani ya Ufalme wake.

Hiyo ilikuwa kama nafasi ya dhahabu kwa Lady Amana, alianza kuzipiga hatua haraka haraka kutoka mahala pale ili asigundulike.

Kama alivyokuwa ameambiwa na Foibe kuwa ajiamini tu hatoonekana katika Macho ya Watu kwasababu watakuwa wanamwangalia Mfalme, Masikini Lady Amana naye alifanikiwa kutoka kabisa sehemu hiyo na kuianza safari ya kwenda nyuma kwa ajili ya kutoroka.

Kwa usiri mkubwa na makini Alifika sehemu hiyo.

"Lady Amana!"

Faibe ndiye alikuwa wa kwanza kumuona na kumuita. Mlinzi wa sehemu hiyo alishituka baada ya kusikia.

"Haya njooni mpite haraka. Lakini nimewafungulia kwasababu naamini kuwa Lady Amana ni Mwanamke Mwema!"

Mlinzi alisema, baada ya kuwaruhusu wapite katika njia hiyo ya Siri katika ufalme.

Walipita haraka na safari ya kutokezea upande mwingine ikaanza.

*******

Baada ya kumpokea Mwanaye Malkia Sayuni alianza kumtafuta Lady Amana ili amsalimie mfalme, lakini hakufanikiwa kumuona. Hapo alianza kuwa na Mashaka lakini aliamini Labda Lady Amana kazidiwa na kurudi ndani. Aliingia ndani kwa Mfalme ili kumpongeza Mwanaye kurudi salama, huku akitaka kujua ni nini ambacho kimezungumzwa huko.

Wakati anaingia ndani kwa Mfalme alikuwa amemtuma Mfanya kazi wake akamwangalia Lady Amana ndani kwake.

"Yolam unajisikiaje Mwanangu?"

Hilo ndilo lilikuwa swali la Malkia Sayuni kwa Mfalme Yolam.

Alikuwa hayuko peke yake hata Mke wa Mfalme Malkia Eda alikuwepo pia.

"Mama Usijali, najisikia vizuri sana. Na Kitu ambacho sikukitarajia kabisa ni Mapokezi ya King Joktan. Ni Mtu wa tofauti sana, naimani hayuko kama Wafalme wengine, na kakubali ushirikiano wetu uwe wa kudumu na kudumu!"

King Yolam alisema.

"Ndio maana nilikuwa nakupenda Mwanangu. Unaweza kulienzi vizuri Jina la Muhasisi wa Falme hii King Yolam wa kwanza. Naamini hakuna Mtu ambaye atayapokea haya kwa Namna tofauti na nilivyo yapokea mimi!"

Malkia sayuni alisema.

"Kweli King Yolam, hata mimi nimefurahi sana. Wewe ni Mfalme wa aina yake na Mwenye busara nyingi!"

Queen Eda mke wa Mfalme Yolam alisema. Maneno yake yalimfanya Mumewe kutabasamu.

"Samahani Mfalme kuna Mgeni wako!"

Wakiwa katika mazungumzo mlangoni ilisikika sauti ya Mlinzi ikimuombea Mtu kuingia.

"Mruhusu apite!"

Lady Sayuni alisema. Alijua kabisa kuwa ndiye Mfanyakazi wake aliyemtuma kumwangalia Lady Amana ndani kwake.

Kweli kama alivyokuwa anazania, alikuwa ni Mfanyakazi wake.

"Vipi anakuja?"

Kitendo cha mfanyakazi wake kutia uso wake ndani Malkia sayuni alimuuliza.

"Hapana na hayumo ndani mwake, na hata Mfanyakazi wake hayupo pia!"

"Unasema?"

Malkia aliitikia kwa mshituko sana, hakutarajia kulipokea Jawabu la namna hiyo.

"Nani Mama?"

Mfalme naye aliuliza.

"Lady Amana,......bila Shaka atakuwa ametoroka!"

"Kwanini unasema kuwa atakuwa ametoroka?"

Mfalme aliuliza tena.

"Kwasababu ni Mjamzito!"


Mfalme alishituka sana baada ya kutamkiwa moja kwa moja kuwa Lady Amana ni mjamzito.

Hakutaka kuendelea kuzungumza tena, alitoka inje na kuwaita Askari wake kisha akawaamuru wazunguke kumsaka Lady Amana na wamrudishe katika mikono yake.

Haraka sana Askari walianza kumtafuta Lady Amana. Ulikuwa ni masako wa hali ya Juu katika Ufalme wa Iyumbwi.

Walifika mpaka sehemu ya mlango wa nyuma na kumkuta Askari aliyekuwa sehemu hiyo ametulia kabisa akiwa hana wasiwasi.

"Lady Amana amefika sehemu hii?"

Hilo ndilo swali ambalo askari wa njia ile ya siri aliulizwa na Askari waliokuwa wanaufanya msako.

"Hapana na sijamuona kabisa maeneo haya"

Askari yule alijibu kwa kujiamini kabisa. Baada ya kujibiwa hivyo Askari walirudi tena kwa mfalme kuwa wamemkosa. Mfalme yolam hakutaka jawabu la namna hiyo aliamuru askari zake waanze kuzunguka mitaani kumsaka. Askari kwa ushirikiano walijigawa makundi zaidi ya matatu kumtafuta Lady Amana pamoja na Foibe huko walipokuwa wamekimbilia.

*******

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments