Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo : Safari Sehemu Ya Tatu (3)



nae kijana kusikia binti BERALITA akiongea hivyo, huku kifua chake kikiwa kimejaa mno, akihema kwa speed ya hasira, basi nae alijibu kwa zarau kali kwa kuonesha yeye ni mvulana anaye jiamini, "Wewe binti mkate nisha uchukua, na nitafanya nitakacho, maana hata kwenye kiganja changu ukai, sasa jifanye mjuaji nije kukunyoosha vizuri"

hapo vika sikika vicheko toka kwa vijana waliokuwa karibu, vicheko vilivyo mvimbisha kichwa MWAIPAMBA huku binti BERALITA, akizidi kuchukizwa na zarau za kijana yule,hapo binti huyu alitulia kidogo na kufanya kama anamnongoneza MWAIPAMBA,"kaka naongea kwamala ya mwisho, nipemkate wangu, vinginevyo uta haibika, mbele ya hao mabwana zako" dah! ilo lilikuwa tusi kubwa kwa kijana huyu, atamimi nisinge kubari, "eti nini bwana zangu inamaana.." sasa ilikuwa zamu ya MWAIPAMBA, kusikia kicheko, toka kwa wale vijana, kicheko kilicho mpatisha hasira, "ujasikia au unazani naongea na simu, nipe mka te wandu anko, nita kuaribi sasa hivi" ndipo YOROBI alipoona kuwepo kwa dalili za kuwepo kwa, alipo tazama aliona fujo ndogo ndogo zikiendelea, naye pasipo kujuwa wanao gombana, akahachana nao na kuendelea na shuguri zake, lakini nyuma ya panzia toka anawahesabu watumwa, kijana YOROBI alionekana kumtamani sana, binti BERALITA, naalipanga akifika lazipa atafune kitumbua cha binti huyu, japo kidogo, huku kijana MWAIPAMBA aliona zalau zime zidi,akachukuwa uamuzi wa kumwadabisha yule bint ili nidhamu iludi, hapo kijana akalusha kofi kwenda usoni kwa binti BERALITA, 



 binti BERALITA alliona kofi likija kwa kasi usoni kwake,alinesa upande kidogo, kisha akausdaka mkono wa kijana MWAIPAMBA, na kuukunja kadri hasira zilivyokuwa zikimtuma binti huyo, vijana wenzake kuona hivyo na kubaki wakishanga,uwezo wa pinti huyu, huku binti nae alitaka kuwaonesha kuwa na yeye anaweza, kwani alimvumilia mno kumuomba mkate wake, na hakutaka kunyanyaswa wakati haki ni yake, "leo utajuta kuni chokoza, paka wewe" basi BERALITA aliachilia mkono wa kijana huyu, kisha kitendo cha alaka sana alilusha mgumi mbili mfululizo, zilizo tuwa usoni kwa MWAIPAMBA, na kumfanya apepesuke na kuyumbakidogo, alifanya hivyo huku akiwashangaza, vijana waliokuwa pembeni, huku nao wakiwa tumbo joto na kuona ya kuwa, binti mrembo anapigana kama mwanamume, hapo wakaogopa wasije kuingilia ugomvi huo, ikageukia kwao, basi walikaa wakiangalia mpambano uku kelele za kushangilia zikisikika, ndipo YOROBI ambae nae alikuwa pembeni akimtazama binti BERALITA akifanya ya kwake, akatulia kuona jinsi yule binti mrembo anaye mtamani, anavyo mwadabisha kijana wawatu, mpaka hapo kijana MWAIPAMBA, aliona yule binti siyo wamchezo, kimoyo moyo alijuwa ataahibika, endapo atasubiri mpaka ugomvi ufike mwisho, nikweli alimwona yule binti, akiwa amesha lizika na kuamua kuhachana na yeye, maana alimwona akiwa anarudi sehemu aliyo kuwa amekaa mwanzo nakuketi palepale alipokuwepo, na ndipo kijana alitokea kwa nyuma na kumpiga kikumbo, kwalengo la kumsukumia kwenye maji baharini, lakini binti alikuwa makoni sana, licha ya kuyumba kidogo nakujishikilia vizuri, pia aliweza kijitahidi na kusimama ni baada ya kufyetua teke moja lililo tuwa kwenye kengere za kijana MWAIPAMBA,iliyo msababishia maumivu makari nakumfanya ashikilie sehemuzake nyeti, hapo binti huyu akapata nafasi ya kunyanyuka na kumwongezea kifuti, cha usoni, kilicho mwinua MWAIPAMBA, nakumrudisha nyuma, huku akiachia mkono kwenye kengere zake zachini, hapo BERALITA,hakumwachia upenyo aliruka juu huku akiachia konde zito, ambalo lilitua kifuani kwa MWAIPAMBA, ambae alienda chini na kuwaangukia wenzake ambao walikuwa wana shangilia ugomvi ule, konde lile lilipeleka maumivu makali kwa kijana MWAIPAMBA na kumfanya kukata net work kwamuda uku wenge likitawala kichwani mwake, hapo kijana akajiuliza, "huyu ni mwanamke au mwanaume?"

kuona ina tosha YOROBI alitoa amri ya kuwa hachanisha, hapo watu wakamzingira BERARITA na kumshawishi akakae kwenye sehemu aliyokuwa amekaa mwanzo, lakini wengine walipiga kelele, kuwa wamwache binti BERALITA azidi kumtandika kijana huyo, kwani alikuwa akileta jeuri nyingi, kijana MWAIPAMBA akiwa ametulia pale chini hakili zikianza kumrudia, alisikia zile kelele za kumkashifu, aakatazama upande aliopo binti BERALITA, akamwona anaelekea sehemu aliyo kuwa amekaa mwanzo, hapo MWAIPAMBA akawaza namna ya kujipatia pinti moja itakayo mfutia haibu, akiamini kuwa endapo ata fanikiwa kumkumba BERALITA, nakumtupia kwenye maji baharini atakuwa amefanikiwa kufuta haibu maana alikuwa anaimani yakuwa, binti huyo hasingeweza kujiokoa na maji mengi kwakuwa yeye anaweza kuogelea, itakuwa lahisi kwake kurudi chomboni akimwacha binti huyu anakufa kwa maji, alitokea kumchukia vibaya sana, hapo kijana huyu akakaa tayali, pasipo mtu yoyote kufikilia ujinga anao taka kuufanya MWAIPAMBA,ghafla walishuhudia kijana huyu akitoka mbio na kumfwata BERALITA,.



MWAIPAMBA.alichomoka speed na kumkumba binti huyu ambae alikuwa karibu na ukingo wa jahazi, kitendo ambacho BERALITA hakukitegemea alijikuta yupo juu,akiwa amekamatwa na kijana huyu, ambae ametoka kumwazibu mda mchache uliopita, wakielekea baharini, hapo bint akarudisha mawzo mchezoni, akijuwa kuwa kizubaha amekufa maji, Basi watu wote waliokuwa wakitizama pambano hilo walishangaa, hakili za usiku za kijana huyu, hawakuamini kilichotokea wakati huo.walishuhudia wote wawili wakitumbukia kwenye maji na kuzama kabisaaa bila kuonekana ata nywele, wote wakasogea kwenye kingo za jahazi huku wakingoja watakapo zidiwa na maji warudi juu, zika pita sekunde kumi, hapo walishangazwa sana na tukio hilo na kuanza kuchungulia ndani ya maji lakini hawakuona chochote zaidi ya maji yale.walikosa majibu, hapo kila mmoja wao wa vijana wale walibaki hawaelewi nini kimetokea na kushika tama tu! na kujua wameshawapoteza, kumbe binti BERALITA pamoja na kijana MWAIPAMBA.

Waliendelea kuvurugana ndani ya maji, huku kila mmoja akionekana kuwa na pumzi nyingi, na alivyokuwa akufikiria kijana MWAIPAMBA kuwa ataweza kumpiga vizuri binti huyo, haikuwa hivyo bali kalionekana kuwavizuri zaidi, kwani kila alipo jaribu kumng'ang'ania aliambulia teke nakumsababishia maumivumakari, huku damu ikianza kumvuja kijana MWAIPAMBA, akutegemea kuwa kipigo cha kwenye maji kingemgeuzia yeye mwenyewe kijana MWAIPAMBA.Ndipo kijana mwongoza jahazi, YOROBI alipo taka kuingia, kwenye maji ilikutoa msaada asa kwa binti BERALITA, ambae alisha mkolea sana binti huyu, lakini alizuiliwa na vijana wenzake asifanye kitu kama hicho, kwani kuna hatari ya papa wengi sana kwenye maji yale, nae kuona hivyo basi ilimbidi abadili maamuzi ya kuingia ndani ya maji hayo....

Lakini japo alikatishwa tamaa ya kuingia ndani ya bahari, ili kuwaokoa kijana pamoja na binti, lakini moyoni mwake YOROBI hakuridhika na kile walicho amua wenzake, yeye alitaka kuwasaidia watumwa hao.alibaki akiwa mtu mwenye unyonge flani, ambao uliwatia shaka wenzake, kumbuka pia alitokea kuvutiwa na binti BERALITA, japo kuwa alitaka kumwambia tokea mwanzo, lakini alikuwa ajapata nafasi nzuri, na huku akihisi hii ndio nafasi ya kumsaidia na kupatana vizuri, maana lengo lake lilikuwa ni kumchomoa kwenye utumwa na kumfanya mke kabisa, basi mbinu zake ziliishia hapo, akapoteza ata uwezo wakufanya kazi vizuri, huku akifikiria tukio lililo tokea kwa binti mrembo kudumbukia majini na kijana, na pili alihofia sana mda waliotumia ulikuwa ni mwingi kwa kwaida ya binadamu kuwa na pumzi nyingi kiasi hicho.

Sakata lilikuwa likiendelea majini huku binti akiendelea kuongoza kwa kumsurubisha kijana MWAIPAMBA, kwani maji yalianza kumzidia kijana huyo kwa kuchoka sana, kwamaumivu ya vipigo na pumzi, kiukweli hakutegemea kufanywa mfuko wa mazowezi na binti, kwa kichapo kile maana binti aliendeleza kumtwanga mpaka alipoona huyu atazidiwa, na ndipo kwa mbali binti aliona PAPA mmoja akikatiza katiza maeneo walipo, kwa mbali kidogo na maeneo hayo walipokuwa wakizipiga na kijana mwaipamba, basi aliogopa na ndipo kumshitua mwenzie, naye alipoona, hapo MWAIPAMBA jicho lilimtoka na kupata nguvu nyingi, kwani alijua ndio mwisho wake, kwani PAPA hakuwa mmoja , sasa walionekana wakija kwao kwawingi, na walionekana kuwa na njaa kali, ambayo itawafanya wapate hamu ya kuwala vijana hao.Basi kila mmoja alionekana kuwa mtulivu, iliwasi wajulishe papa kuwa wao ni msosi wao, na ndipo kijana MWAIPAMBA alipoonekana kuanza kunyata mdogo mdogo, lakini ghafla alishituka na kugeuka, na kukuta PAPA wamewazingira kila kona, huku wakikosa namna ya kutoka kwa wakati huo, mwaipamba akiamini kuwa, ndio mwisho wao, akaanza kujilahumu kwaujinga wa kujitumbukiza baharini, lakini kwa binti BERALITA alionekana kuwa shujaa, alionekna kupata wazo flani ambalo lingewasaidia, alianza kunyata na kumsogelea MWAIPAMBA, ili watakapo toka watoke wote, japo kuwa walikuwa maadui, lakini binti huyu hakuwaza hilo, nae roho ilikuwa safi, ili wajipange wapambane na hao PAPA, lazima bifu likae pembeni,

MWAIPAMBA kuona hivyo binti akisogelea akatulia, na ndipo waliposhikana na kuoneshana ishara nini wafanye, ili kutoka kwenye msitu huo wa mdudu PAPA. ndipo walipo anza kupiga maji kwa kasi na kwenda chini zidi, kwani PAPA hao walionekana kuwa juu yao,.


ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments