“Mke wangu mimi
sielewi kabisa ni nini ambacho unakizungumza”. Niliongea huku nikiendelea
kusikilizia maumivu pale juu ya sakafu.
SASA ENDELEA
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninarudia tena
kwa mara nyingine, ninataka kujua vito na baadhi ya nguo zangu vimeenda wapi?
Haiwezekani vitu vyangu vikatoweka kiajabuajabu!”. Mama Careen aliendelea
kuongea huku akiendelea kunishushia kipigo kitakatifu.
“Mimi sielewi mama
Careen. Mbona wewe umekazania kwamba mimi ndiye ambaye nimechukua vitu vyako?”,
Niliongea kwa kujitetea katika sauti ya maumivu.
“Sasa humu ndani
tunaishi wangapi”. Aliuliza mama Careen baada ya kuwa amenitandika upawa katika
makalio yangu.
“Humu tunaishi
wengi na wewe mwenyewe unajua kabisa”. Niliendelea kujitetea.
“Kwa hiyo una
maana huyu mtoto mdogo Careen ndiye ambaye amechukua?”. Mama Careen alihoji kwa
ghadhabu sana.
“Huwezi jua mke
wangu”. Nilijibu hivyo kwa lengo la kumshawishi akubaliane nami.
Ukweli wa dhahma
ile yote mimi ndiye ambaye nilikuwa naufahamu. Mimi ndiye ambaye nilikuwa
nimechukua baadhi ya vifaa vya urembo vya mke wangu kama vile; bangili, herein,
pete n.k na kwenda kumpa Jasmine kama zawadi.
Nakumbuka nilimpa
Jasmine nikimdanganya kwamba nilikuwa nimemnunulia. Jasmine alifurahi sana na
kuamini kwamba kweli mimi nilikuwa ninamaanisha penzi la dhati kwake. Aliahidi
kulidumisha penzi letu hili changa na kunipenda milele.
“Nasema hivi baba
Careen, mimi sihitaji maelezo yako ya kitoto na yasiyo na kichwa wala miguu.
Ninachokihitaji ni vitu vyangu virejee hapa. Hii ni tabia mbaya kabisa”. Mama
Careen aliendelea kufoka huku sasa akibubujikwa na machozi na kuondoka kutoka
eneo lile ambalo alikuwa akinisulubu.
Nami kwa aibu na
fedheha kubwa nikajizoazoa kutoka pale chini huku mwili wangu ukiwa umelemewa
mzigo mzito sana wa maumivu yasiyomithilika. Nikaamua kwenda chumbani ili
nikayapunguze mawazo yangu.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********
Penzi langu na
Jasmine lilizidi kukua kwa kasi mithili ya moto mkali ulao nyika. Jasmine sasa
alikuwa ameiacha ile kazi yake ya ukahaba na nilikuwa ninajaribu kuiweka sawa
mipango ya kumfungulia mradi ambao utayaendesha maisha yake.
Nilikuwa nimeamua
kabisa kuimarisha koloni langu kwa Jasmine baada ya kuona mke wangu mama Careen
ananiletea mambo ambayo siyaelewi kabisa.
“Baby nina jambo
moja nyeti ambalo ninapenda nikushirikishe”. Jasmine aliongea siku moja tukiwa
nyumbani kwake tukiyafurahia mapenzi yetu.
“Jambo gani tena
mpenzi wangu?”. Nilimwuliza Jasmine.
“Ni jambo la
kawaida tu”. Jasmine aliongea huku akiniachia busu mwanana.
“Umeanza kunitisha
sasa mpenzi wangu”. Nilimwambia.
“Usihofu mpenzi,
ni kawaida”. Jasmine aliongea.
“Ok, ni jambo gani
hilo?”. Nilimwuliza.
“Katika siku za
hivi karibuni nilikuwa najihisi tofauti katika mwili wangu. Nimekuwa
nikijisikia uchovu wa mara kwa mara, kichefuchefu na miguu kuniuma”. Jasmine
aliongea.
“Aaaaah! Hayo
yatakuwa ni malaria”. Nilimjibu kwa kujiamini sana utadhani mimi ni daktari.
“Kwa nini wasema
hivyo mpenzi?”. Jasmine aliuliza huku akinitazama usoni.
“Unajua malaria
mimi naifahamu sana. Dalili zake ni kama hizohizo ambazo umezitaja. Itakubidi
uende hospitali ukapime ili uanze dozi mapema?”. Nilongea huku nikimfariji
Jasmine.
“Basi jana
niliamua kwenda hospitali kwa lengo la kupima. Baada ya vipimo, niligundulika
kwamba nina ujauzito wa mwezi mmoja”.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unasemaje
weweeeee?”. Niliuliza kwa taharuki utadhani ya kwamba nilikuwa sijakisikia kile
ambacho Jasmine alikuwa amekiongea.
“Nina ujauzito wa
mwezi mmoja mpenzi”. Jasmine alirudia kuongea tena kwa mkazo.
“Hapana
haiwezekani!”. Niliongea huku ubongo wangu ukiwa kama umeacha kufanya kwa
sekunde kadhaa.
“Sasa haiwezekani
nini?”. Jasmine alihoji kwa mshangao.
“Sasa wewe
unafikiri tutafanyaje?”. Nami nilimjibu kwa kumkandika swali.
“Tutafanyaje
kivipi?”. Naye alinijibu kwa kunirushia swali lilelile.
“Hivi wewe huoni
kama hili ni tatizo kubwa?”. Nilimwambia.
“Sasa kuna tatizo
gani hapo wakati wewe ulisema wanipenda na wataka kuanza maisha na mimi”.
Jasmine aliongea.
“Sawa, lakini vipi
mama Careen akiligundua hili? Huoni kwamba patachimbika?”. Nilijaribu kutoa
tahadhari.
“Hilo utajua wewe
maana tangu mwanzo mimi nilikwambia kuhusu hili. Je, wewe ulinijibuje? Si
ulisema nikuachie wewe ya kwamba utajua namna ya kufanya!”. Jasmine aliongea
huku sasa akionekana kukasirika kidogo usoni.
“Sawa la … la …
lakini ….”. Kigugumizi cha ghafla kilinijia.
“Lakini nini?”.
Jasminie aliuliza.
“Tena ulisema wewe
ndiye mwanaume wa nyumba na unaamua nini ukifanye na nini usikifanye. Hebu acha
kunichanganya bwana”. Moto wa Jasmine sasa ulizidi kupanda.
“Ok, mama wala
usijali. Mimi nitajua namna ya kufanya. Nakupenda sana Jasmine”. Niliamua
kumuweka sana ili kuisafisha hali ya hewa ambayo niliona inaanza kuchafuka
taratibu.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hayo ndiyo
maneno. Siyo unakuwa unaleta ngonjera zako hapa ambazo hazieleweki kama siyo
mwanaume bwana!”. Jasmine aliongea huku akionesha wazi kwamba alikuwa na furaha
kutokana na maneno yangu.
*********
Ujauzito wa
Jasmine ukazidi kuyaimarisha mapenzi yetu. Mimi nikampenda sana Jasmine na yeye
pia akanipenda sana. Tulithaminiana na kuheshimiana. Tuliweka ahadi na mipango
mingi na kabambe katika kuliimarisha penzi letu.
Ujauzito wake
ukazidi kukua kwa kasi. Miezi ikazidi kukatika. Kichwa changu kikawa na mawazo
mengi sana ambayo yalikuwa yakizidi kuongezeka kila uchao.
Nilikuwa nikiwaza
ni namna gani nitaweza kukabiliana na varangati la mama Careen pindi ambapo
atakuja kuyagundua mahusiano yangu ya kimapenzi na Jasmine.
Hilo lilikuwa ni
dogo kati ya yale ambayo nilikuwa nikiyawaza. Jambo kubwa ambalo ndilo
liliniumiza kichwa hasa ni suala la ujauzito wa Jasmine. Suala la mimi kutembea
na Jasmine niliona ningeweza kulizima endapo moto wa mama Careen ungewaka
lakini suala la ujauzito mh!
Hili lilikuwa
kubwa na nilishindwa kulibeba kabisa. Nilikuwa nikiliona kabisa jahazi likienda
mrama na mimi kama nahodha nilikuwa sina uwezo wa kulinusuru jahazi hili katika
gharika hili kubwa.
“Lakini haya yote
ameyataka yeye mwenyewe mama Careen. Mwanamke ni mshari balaa. Hajui hata
kuibembeleza na kuitunza ndoa. Kila siku ni ugomvi tu ambao hauna hata sababu
ya msingi”. Niliwaza siku moja nikiwa chumbani wakati mama Careen akiwa nje
uwanjani akicheza na Careen.
“Furaha ya ndoa
yetu ilipotea miaka mingi nyuma. Siku za mwanzo za ndoa yetu ndipo
nilipolifurahia penzi langu na mama Careen lakini baada ya hapo, ndoa yetu
ilibadilika na kuwa chungu kabisa”. Niliendelea kuumizwa na mawazo kichwani
mwangu.
“Na kila
nikijaribu kumsogeza jirani mke wangu ili tuitengeneze ndoa yetu, yeye alikuwa
mbali nami zaidi ya kuzidisha ushari wake. Hajali kabisa ustawi wa ndoa yake”.
Nilizidi kutiririkwa na mawazo lukuki mengine yakiwa ni maswali ambayo yalikosa
majibu.
Hatimaye taratibu
machozi ya uchungu yakaanza kuniporomoka. Niliumia kwa sababu mimi na mke wangu
tulikuwa tumeshindwa kuitengeneza ndoa yetu na hatimaye ilikuwa ikielekea
katika misukosuko.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadaye usingizi
ukanipitia na kunisahaulisha yale yote ambayo yalikuwa yakiniliza. Nilianza
kuota ndoto nzuri na tamutamu juu yangu na Jasmine. Niliota tukiyafurahia
maisha pamoja.
***********
Siku moja mama
Careen akawa amepata mgeni. Mgeni huyu alikuwa ni mwanamke. Mwanamke huyu
alikuwa ni mzuri na mrembo sana.
“Mh! Mdogo wangu
wewe una mambo makubwa sana”. Mama Careen aliongea pindi walipokuwa wamekaa
sebuleni.
“Kwa nini waongea
hivyo dada?”. Mgeni aliuliza.
“Yaani tumepoteana
miaka mingi sana hatuonani. Halafu jambo la kushangaza eti sote twaishi katika
jiji hilihili la Kano”. Mama Careen aliongea.
“Nisamehe dada
yangu. Ni maisha tu ndiyo yamesababisha yote haya”. Mgeni aliongea.
“Wala hata usiyasingizie
maisha. Maisha ndiyo yakufanye ushindwe hata kunijulia hali nduguyo?”. Mama
Careen aliendelea kuongea kwa kutoa lawama kwa mgeni ambaye alikuwa ni mdogo
wake.
“Halafu naona
mambo yako si mabaya. Yaani safari hii umeamua kabisa kutundikwa mpaka mimba.
Mbona siyaamini macho yangu!”. Mama Careen aliongea kwa mshangao huku
akilitazama tumbo la mdogo wake ambalo kwa sasa lilikuwa kubwa.
“Dada yangu. Mimi
safari hii ninataka kuolewa. Nimepata mchumba ambaye ananijali na yuko tayari
kabisa kunioa”. Mgeni aliongea.
“Ha ha ha ha
haaaaaaaa! Yaani Jasmine wewe leo hii unataka kuolewa?. Mh! Haya bwana. Je, na
biashara yako ya ukahaba unamwachia nani?”. Mama Careen aliuliza.
“Ile biashara
nilikwishaiacha dada. Huyu mchumba wangu ndiye ambaye amenibadilisha na
kunifanya niiache biashara hii kabisa. Nimeamua kubadilika kabisa na kuanza
maisha mapya dada yangu”. Mgeni aliongea huku machozi yakimlengalenga.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yaani leo ndiyo
unatambua kwamba biashara uliyokuwa ukiifanya ilikuwa ni mbaya. Je, wakati mimi
nakukanya juu ya biashara ile mbona hata ulikuwa hunisikilizi?”. Mama Careen
aliongea.
“Nisamehe dada
yangu. Na ndiyo maana leo hii waniona niko hapa mbele yako nikiwa nimebadilika
kabisa. Mimi si yule Jasmine wa zamani, kahaba. Mimi ni Jasmine mpya. Naomba
unisamehe kwa yote ambayo nilikukosea dada yangu mpenzi”. Jasmine aliongea huku
akiporomokwa na machozi.
“Haya nimekusamehe
mdogo wangu”. Mama Careen aliongea huku akimkumbatia Jasmine.
Ghafla simu ya
Jasmine iliita.
“Hallo! Baby”.
Jasmine aliongea mara baada ya kubonya kitufe cha kupokelea simu.
“Uko wapi? Mbona
nimefika hapa kwako sijakuona?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Nisamehe mpenzi
wangu. Leo nimeenda kumtembelea dada yangu yule ambaye nilikwambia”. Jasmine
aliongea.
“Sasa mbona
hukunitaarifu?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Naomba unisamehe
mume wangu. Mimi nilifikiri kwamba hutakuja nyumbani kwa wakati huu ndiyo maana
sikukutaarifu. Nisamehe sana mpenzi wangu”. Jasmine aliongea.
“Ok,
nimekusamehe”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Halafu mpenzi,
nilipenda jioni ya leo twende pamoja huku kwa dada yangu ili nikutambulishe
kwani dada ana hamu kubwa sana ya kukuona”.
“Ooooh! Hilo wala
usijali. Nitajaribu kuziweka sawa ratiba zangu ili kusiwe na usumbufu wowote”.
Upande wa pili wa simu uliongea.
“Ahsante sana
mpenzi”. Jasmine alishukuru.
“Ok, usijali”.
Upande wa pili wa simu uliongea.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Jasmine
kuongea na ile simu, basi maongezi yake na mama Careen yakaendelea. Wakaendelea
kupeana michapo ya hapa na pale ambayo iliwaletea furaha tele katika nyoyo zao.
“Ndiyo hivyo dada.
Hakika utampenda kwani ni mwanaume mzuri, mtanashati, anayejali na ambaye
anajua nini maana ya pendo la dhati”. Jasmine aliongea.
“Mh! Haya bwana.
Waswahili walisema mtu chake. Tutaona hiyo jioni kama hizo sifa unazompamba
kweli anazo?”. Mama Careen aliongea huku akicheka.
************
ITAENDELEA

0 Comments