ILIPOISHIA
“Mh! Haya bwana.
Waswahili walisema mtu chake. Tutaona hiyo jioni kama hizo sifa unazompamba
kweli anazo?”. Mama Careen aliongea.
SASA ENDELEA
“Hodi humu
ndani!”. Nilipiga hodi mara baada ya kufika nyumbani na kubaini kwamba mlango
ulikuwa umefungwa.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa upande wa
wakati ilikuwa ni majira ya mchana. Nilikuwa nimerudi nyumbani mapema ili
nipate kujiandaa kwa ajili ya safari yangu na Jasmine kwenda kwa dada yake kwa
ajili ya kunitambulisha.
Sikutaka kabisa
kumwangusha mpenzi wangu Jasmine.
Mlango
ulifunguliwa na mama Careen ambaye leo alinishangaza sana. Uso wake ulikuwa na
furaha kubwa sana tofauti na siku zote katika maisha yetu ya ndoa. Hakika
sijawahi kumshuhudia mke wangu akiwa katika hali hii ya furaha katika maisha
yetu ya ndoa.
Furaha ile
iliufanya uso wake uchanue na kuuruhusu uzuri wake uonekane dhahiri. Hakika mke
wangu alikuwa ni mwanamke mzuri sana ila uzuri wake siku zote ulikuwa
ukifunikwa na ukali wake.
Roho yangu sasa
ilianza kuniuma. Nikaanza kujilaumu ni kwa nini nilikuwa nikimsaliti mwanamke
huyu ambaye mwenyezi Mungu alikuwa amenipatia.
Ikafika kipindi
mpaka nikataka nighairi safari yangu ya kwenda kwa Jasmine lakini nikaamua
kukaza kwamba kwani nilimfahamu sana huyu mwanamke. Aliku-wa ni mwanamke ambaye
alikuwa hatabiriki.
“Leo tuna mgeni
mume wangu”. Mama Careen aliongea kwa furaha.
“Mgeni?”.
Niliuliza kwa staajabu.
“Ndiyo mume
wangu”. Mama Careen alijibu.
“Mgeni gani?”.
Name nikauliza.
“Mdogo wangu, yule
ambaye nilikuwa nikikupa habari zake kila siku”. Mama Careen akaongea.
“Anhaaaaaa! Basi
hamna tatizo”. Nilimjibu mama Careen mara baada ya kukumbuka kwamba amekuwa
akinieleza mara kwa mara kwamba ana mdogo wake ambaye anaishi katika jiji hili
la Kano.
Mama Careen
akatangulia mbele kuelekea sebuleni akaniacha mimi pale mlangoni huku
nikijiweka sawa mavazi yangu kwa lengo la kwenda kukutana na mgeni ambaye
nilikuwa sijawahi kukutana naye hata siku moja.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipoingia ndani
moyo wangu ulitaka kupasuka kwa mshutuko mkubwa sana ambao uliupata. Macho
yangu hayakuamini kile ambacho yalikuwa yakikishuhudia. Ubongo wangu ndiyo
uligoma kabisa kukubaliana na picha nzima ambayo ilikuwa ikionekana pale
sebuleni.
“He! Mayanja vipi?
Umekujuaje huku?”. Jasmine aliuliza swali ambalo lilileta utata kwa mama
Careen.
Mimi nikaiona hali
ya hewa imeanza kuchafuka kabisa pale sebuleni. Nikakosa kabisa nmana ya kuweza
kulinusuru lile balaa ambalo harufu yake ilianza kusikika.
“Vipi Jasmine,
kwani mnafahamiana?”. Mama Careen aliuliza kwa mshangao.
“Huyu ndiye yule
mchumba wangu ambaye nilikuwa nikikueleza hivi punde kwamba anataraji kunioa.
Mayanja huyu ni dada yangu mpendwa anaitwa mama Careen”.
Masikini Jasmine
alikuwa akiyaongea haya yote asijue ni siri gani ilikuwa nyuma ya pazia.
Hakujua kabisa kwamba aliyekuwa akimkaribisha alikuwa ni mwenyeji wa nyumba ile
na ndiye ambaye alipaswa kumkaribisha yeye.
Mama Careen
hakukiamini kile ambacho alikuwa akikisikia. Alibaki amesimama akiwa ameduwaa
huku macho akiwa ameyatoa mithili ya mjusi ambaye alikuwa amebanwa na mlango.
Ghafla mama Careen
alianguka chini na kuzimia. Kitendo kile kilizua tafrani kubwa mle sebuleni na
kufanya kila mtu ataharuki.
“Kwani ni nini
kinaendelea Mayanja? Mbona sielewi?”. Jasmine alihoji wakati huo mimi nikiwa
ninampepea mama Careen.
“Fanya utaratibu
tumuwahishe hospitali Jasmine. Huyu ndiye mke wangu niliyekuwa nakueleza siku
zote”. Nilimweleza Jasmine.
“Oooooooh!
Mamaaaaaaa! Jamani Mayanja. Ni kwa nini umenitenda hivi. Mbona umenitia aibu
ambayo nitashindwa kuibeba. Nitaiweka wapi sura yangu jamani?”. Jasmine naye
alikaa chini na kuanza kulia.
Mimi nikaona hapa
nikifanya uzembe nitampoteza mama Careen. Nikachomoka mbio kutoka mle sebuleni
na kuelekea nje ambako nilitafuta taksi.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulimpakia mama
Careen na kumuwahisha hospitali. Na kwa wakati wote huo Jasmine alikuwa
amempakata Careen huku akilia kwa uchungu.
Tulipofika
hospitali, tulimshusha mama Careen na manesi wakampokea na kumpeleka kwa lengo
la kupatiwa huduma. Hali yake haikuwa nzuri hata kidogo.
Mimi na Jasimine
tulikaa katika dawati la kupumzikia huku tukimwomba mwenyezi Mungu atende
muujiza wa kuyanusuru maisha ya mama Careen.
Baada ya dakika
kama ishirini hivi kupita, daktari alitoka na kutujia pale ambapo tulikuwa
tumekaa.
“Ok, wewe ndiye
mume wa mgonjwa?”. Daktari aliuliza hilo kwa kuzingatia maelekezo ambayo
tulikuwa tumeyaandikisha kwa nesi awali pindi tukimfikisha mgonjwa pale
hospitalini.
“Ndiyo dokta.
Mgonjwa wangu anaendeleaje?”. Nilimwuliza daktari kwa bashasha ya kutaka kujua
hali ya mama Careen.
Daktari hakunijibu
bali alinivuta na kunisogeza mbali kidogo na Jasmine. Moyo wangu ulikuwa una
hofu kubwa sana kwa wakati ule.
“Wewe ni mwanaume
hivyo unapaswa kujikaza kiume kwa taarifa hii nitakayokupa”. Dakatari alianza
kuongea huku akinigongagonga bega.
“Unataka kusema
nini dokta?’ Nilimwuliza daktari huku nikiwa nimemtolea macho.
“Kwa bahati mbaya,
mkeo tumempoteza. Amefariki dunia”. Maneno yale yaligota katika ubongo wangu na
kuniletea kizunguzungu ambacho kinilinifanya nile mweleka na kuanguka chini.
Baada ya hapo
nikazirai.
**********
Mazishi ya mama
Careen yalifanyika nyumbani kijijini kwetu. Ulikuwa ni msiba mkubwa sana ambao
ulinipa uchungu mkubwa. Msiba huu ulikuwa umekitikisa kijiji chetu kutokana na
umaarufu wangu.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jasmine kwa wakati
wote huo alikuwa akilia asijue ni nini cha kufanya. Kifo cha dada yake kilikuwa
kimemchanganya kabisa.
Baada ya mazishi
ya mama Careen tulikaa matanga.
Msiba ulipokwisha,
mimi na Jasmine tulirejea jijini Kano huku Careen tukiwa tumemwacha kijijini na
bibi yake.
Maisha yetu jijini
Kano hayakuwa ya furaha hata kidogo. Ile furaha ambayo mimi na Jasmine tulikuwa
nayo ilikuwa sasa imeyeyuka.
Baada ya wiki
mbili toka mimi na Jasmine tutoke kijijini, kuna tukio moja kubwa sana
lilitokea. Tukio hili lilizidisha ule uchungu ambao mimi nilikuwa nao.
Jasmine alikutwa
akiwa amekufa kwa kunywa sumu huku akiwa ameacha ujumbe wa kunituhumu mimi kuwa
ndiye msababishaji wa madhila hayo yote.
Polisi
walinikamata na kunifungulia mashtaka ya kusababisha vifo vya watu wawili ambao
ni mama Careen na Jasmine. Kesi hii ilikuwa nzito na ililalia upande wangu.
Hatimaye
nikapatikana na hatia na nikahukumiwa kifungo cha miaka ishirini gerezani.
MWISHO
FUNZO
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika mahusiano
ya ndoa yatupasa tuepuke tamaa. Turidhike na ndoa zetu. Siku zote tuishi katika
kuzijenga ndoa zetu na si kuzibomoa. Tuepuke kufanya maamuzi ambayo baadaye
huja kutugharimu sana.

0 Comments