IMEANDIKWA NA : CHANDE ABDALLAH
********************************************************************************
"Neema naona umeamua
kunifanyia makusudi, haiwezekani ukaingia siku zako leo wakati ndiyo unajua
kabisa unakuja kukutana na mimi baada ya maika zaidi ya saba," alilalamika
Cliff sauti yake ikifanya mngurumo mdogo ndani ya chumba cha hoteli ya kifahari
ya Red Spice iliyopo huko Arusha mjini.
"Hapana, sikujua
kabisa, kama itakuwa hivi, imeanza sasa hivi nakuapia Cliff sikuwezi kukufanyia
makusudi, hata mimi mwenyewe nimekumiss," alijibu Neema akijitetea ikiwa
ni baada ya mipango yao ya kufanya unzinzi kuonekana kuvunjika siku hiyo na
hata kesho na hata siku nne zijazo hadi pale bidada atakaporudi kutoka mwezini.
"hapana siamini
nataka nione," alisema Cliff akinusa harufu ya uongo wa Neema kuwa pengine
anambania makusudi baada ya kumlia vitu vyake; we fikiria makuku, mabia,
mastarehe waliyoyafanya usiku huo na kama haitoshi vile gharama za kulipia
chumba cha hoteli halafu eti anakuja kubaniwa kirahisi hivi, hapana kwa kweli,
lazima amkague.
"He, Cliff aya,
nitazame," alisema Neema akifumba macho yake kwa aibu na hasira,
akapandisha kisketi chake na kutanua miguu akionesha chupi yake ikiwa imeanza
kuloa tone la damu pale katikati.
Cliff akawehuka macho
yake yakitazama kitu anachonyimwa wala siyo maumivu ya mwenzie, zipu zikazidi
kungangamara badala ya kuvyondea, akamtazama Neema kwa uchu rohoni
akajisemea:"kwani damu nini bwana anipe tu kidogo naingiza kichwa
tu."
"tayari
umeamini?" alisema Neema akijiandaa kuishusha gauni yake.
"hapana,sijaamini,
nataka nione kabisa,je kama umejipaka lipstiki!?" "loh mimi nikufanyie
hivyo, aya ona, ona!" aliongea Neema akimsusia na chupi yenyewe, Loh Cliff
akatazama uroho ukimuisha, ni kweli Neema alikuwa kwenye siku zake, haitakuwa
ustaarabu kumlazimisha.
"Ndiyo uende tena,
ukaninunulie pedi," alisema Neema, Cliff akajizoazoa na mapombe yake
aliyomnywea mtoto wa watu na mkongo aliompakia mtoto wa watu, akatoka chumbani
kuelekea supermarket hali akitukana na kuilaani siku hii na siku nne zijazo.
akanunua na kurudi nazo
ndani. akampa Neema na kujifanya anampa pole.
kichwani akawa anapiga
mahesabu yake, ikiwa atamuachia Neema aondoke kesho yake, basi kumpata hapo ni
majaliwa, lazima ahakikishe anatembea naye kabla hajamuachia. Hela kwake siyo
tatizo kabisa akamtazama kwa uroho ulioanza kuamka tena, akamuuliza.
"Neema basi tukae na
mimi hapahapa hotelini hadi ukimaliza kubleed, pesa ipo,usirudi kwenu kwanza,
kwani baba yako anajua kama umesharudi?"
"mh we Cliff,
kubakia hapa ni noma, bora niende kwa baba kwanza halafu nikishamaliza
nitarudi," alisema Neema.
"wee hapana, sitaki,
yule mzee wako anakuchunga sana, na kukupata tu leo kama bahati, naomba ubakie
hapahapa kwani wewe unableed kwa siku ngapi?"
"siku nne tu nakuwa
poa, lakini ubaya baba anajua tumeshafunga kwa sababu ya huu ugonjwa wa corona
na nilishamtumia picha nipo airport," alijibu Neema.
"sawa cha msingi
tusitoke, na mzee wako akikuuliza we mwambie bado haujasafiri umesikia
eee!"
"tatizo
nilishamtumia picha nipo airport na najua atakua ananingojea nirudi kesho, sasa
sijui nitamdanganyaje?"
"we unajua bwana,
mwambie tu kuwa ndege ilighairisha safari,"
"aya sawa,"
" enhee kwani corona
ni nini na unakuwaje?
"taarifa tu kuwa
unapata mafua na homa na unaambukiza wengine, watu wengi wanaumwa Italia
wamefunga makanisa na vyuo ndiyo maana tumeruhusiwa kurudi, nasikia hapa hakuna
hata mgonjwa," alisema Neema.
"Afrika hatuumwi,
sisi tuna ngozi ngumu," alisema Cliff. Basi wakajikuta wanapiga stori za
Corona na kumpeperusha pepo wa ngono aliyewazingira siku hiyo.
kama ulikuwa ukijiuliza
ilikuwaje Cliff na Neema wakutane siku hiyo ni kwamba, hawa walikuwa wapenzi
tangu sekondari kumbukumbu halisi zilionesha tangu kidato cha tatu, Cliff
akamuomba penzi Neema lakini Neema akamwambia Cliff msimamo wake wa kutaka kuwa
sista na umuhimu wa kutunza bikra yake. Cliff alijua ni uongo tu wa Neema
kumkimbia lakini ni kweli hakuambulia kitu kwani Neema alivyomaliza kidato cha
nne, akapotelea seminari na kuenda huko Italia kusomea utawa na akawa mtawa
kweli.
walipotezana kwa miaka
saba, kwa njia ya ajabu akakutana Neema akiwa ni mtawa wa shirika la wa
Benedictini
Cliff yeye ni mfanyakazi
wa bodi ya utalii, kijana wa mjini mwenye uchu wa kulionja penzi la Neema maana
hakuwa tu na Neema bali alikuwa na msururu wa wanawake huko nyuma;
kilichomfanya amsubiri Neema kwa kiasi hicho ni jinsi alivyolivyo, maana kwanza
hafananii na kuwa sista jamani ni mzuri mno kufa na bikra yake. Lakini cha pili
ni hulka tu za Cliff, hakuwahi kumuonja Neema na ndiyo alitaka kumuonja kwa
gharama yoyote; na mpaka sasa alikuwa ameshagharamia vya kutosha na kumfanya
usiku huo sista wa watu avue kiremba na gauni la kitawa na kuvaa viatu vya
mchuchumio na vijinzi kisha kuingia club na hotelini kama hakuna kitu vile.
Huenda Cliff alishagundua
walakini katika tabia za Neema maana hakuonekana mgeni wa mambo ya kucheza
muziki wala vilevi. Alikunywa tu vilevi vikali na hakulewa kama Cliff
alivyotarajia. Muziki wa kidunia ulipopigwa na yeye nyimbo nyingine aliziimba
vizuri kabisa na kuzungusha kiuno chake. Mara kadhaa alijiuliza; Loh mtawa
anazijulia wapi nyimbo za aina hii? lakini akakausha akidhania pengine huko
utawani kama pombe huzinywa kwenye divai na kama nyimbo pengine huwa na
masherehe yao na huzisikiliza.
Usiku ule wakati wakiwa
wanalala baada ya stori akajua Neema atamsalisha sala za salamu Maria na Baba
yetu, lakini wapi! sista Neema alilala fofofo kama mpagani.
Siku ikapita na asubuhi
yake, Neema akatuma meseji ya whatsapp kwa baba yake akimtaarifu kuwa ndege
ilighairisha safari yake hivyo alitarajia kurudi nyumbani siku nne mbele. Baba
mtu, mzee Benson Swai akaitikia na kutuma voice note ya kumuombea mwanaye
safari njema na kuamuru malaika wamlinde.
Cliff alimkumbuka mzee
Benson enzi zile walipokuwa kidato cha nne na Neema, yeye alipenda kumuita
mkoloni, maana kila alipojaribu kupanga wakutane uchochoroni na Neema, Mzee
Benson angetokea na kuzua tafrani. Neema akawa anafungiwa tu hata kutembea
akiwa nyumbani alikuwa hawezi. Sehemu pekee Cliff angeweza kuonana na Neema ni
kanisani kwa kuwa hakukosa misa; daima na siti yake ilikuwa ya upande wa kulia
baada ya benchi za mbele za wanakwaya.
Cliff akawa anajibanza na
Neema huko walau, lakini kitu kibaya ni kwamba, baba yake Neema huyo mzee
Benson alikuwa pia ni mzee wa kanisa pale kigangoni, na alimzuia Cliff hata
huko kanisani ashindwe kupakanyaga. hivyo basi aliposikia voice note ya mzee
Benson, Cliff alikumbuka mbali akacheka kidogo huku akimtazama Neema.
"haha mzee wako
bwana hivi bado mkali vilevile?" aliuliza Cliff, Neema akakatisha ile
sauti ya maombi na kumtazama Cliff aliyejilaza bado.
"Ndiyo, tena
kazidi," alijibu Neema akionesha kuwa na huzuni. Cliff akagundua jambo
akaropoka.
"Neema, hivi baba
yako ndiyo aliyekutaka uwe sista au wewe mwenyewe tu?"
"mh kwanini
umeniuliza hivyo?
"hapana naona haupendezi
kuwa sista Neema, kiukweli roho inaniuma kukupoteza nilitaka nikuoe
ujue.."
"mh, muone! ila ni
kweli mimi sikupanga ni baba alinitaka niwe sista; no way ndiyo ilishakuwa
tena," alisema Neema akiinuka na kwenda kuoga.
Cliff wakati huo akawasha
televisheni kutazama habari za dunia. Huko duniani habari zilikuwa ni kuhusu
Corona tu.
Kipindi hicho ndiyo
kwanza ilikuwa inasamba ughaibuni, kwa Afrika ugonjwa huo ulikuwa ni ndoto
kuja, hivyo hakuna aliyeutilia manani na hata yeye pia aliupuuzia, akamsubiri
Neema alipotoka kuoga na yeye akaingia bafuni maana ni uungwana tu kumuacha
mpenzi wako aingie bafuni peke yake hasa akiwa katika siku zake ili ajiswafi
kwa nafasi sio kumganda kama kupe sugu.
Basi bwana baada ya kuoga
wakatoka zao hapo kwenye mgahawa wa hoteli na kunywa chai, Cliff akigharamia
kila kitu japo mara kadhaa akatoka kwenda kupokelea simu kwenye gari yake
aliyoiegesha kwenye parking akimzugisha mpenzi wake ambaye ni afisa wa polisi
Mwanza, Grace,;kuwa bado yupo kwenye vikao hivyo asimpigie sana kisha angerudi
kwa Neema kusubiria windo lake akihesabu siku kwa makini kuwa ni siku ya pili
hiyo ya Neema kubleed hivyo bado siku mbili tu mbele.
Neema wakati huo naye
alikuwa akichati na simu na kukwepa macho ya wanaume wa kizungu waliofika
hotelini hapo wakishangaa kumuona mtoto wa kike mzuri wa kipekee akiwa ameketi
peke yake, lakini kabla hawajafanya jitihada kumsogelea, Cliff angetokea haraka
na kuketi karibu na Neema; goma lake.
ITAENDELEA

0 Comments