Siku ikapita na kesho yake ratiba yao ikawa ni hiyohiyo, kushuka
mgahawani na kuzunguka eneo la vivutio vya hotelini na kurudi kulala. hatimaye
siku ya nne ikatimia Neema akajikagua na kuona tone la mwisho likishuka kwenye
pedi yake, lakini akajikausha kimya.
"Ney, bado tu!" alisema Cliff mara baada ya kurudi
chumbani wakiwa wamemaliza kula chakula cha mchana.
"nitaangalia," alisema Neema akimtania Cliff.
"lete tuangalie," alisema Cliff akitaka kumkagua tena
Neema.
"wee Cliff bwana, nakutania, nitakupa.. ngoja nikaoge
kwanza.. na wewe jiandae maana nataka tumalizane mchana, usiku unirudishe
airport nijifanye ndiyo naingia Tanzania na baba nilishamwambia kuwa naingia
Arusha leo saa saba usiku."
Loh Cliff alifurahia huyo, akajikoki, akapiga hesabu za masaa
atakayomfaidi Neema akaona ni masaa takribani kumi,akajiapia hatoyaachia
hivihivi, hatosinzia wala kufikicha kope; ni shoo shoo. sasa wakati Neema
anaingia bafuni,yeye akajibust kidogo na mvinyo huku akitoa laptop kwenye begi
lake na kuweka muvi ya ngono kwa sauti ya kistaarabu ili ihamasishe tendo
litakalofanyika dakika chache zijazo, kisha akatulia kama nyani ngabu.
Kila sekunde kwa Cliff zilikuwa zikithaminishwa na nenge
alilokuwa nalo juu ya Neema, akaona anachelewa japo kiukweli hata dakika tano
hazikupita tangu Neema aingie bafuni. sauti ya maji yakitiririshwa bafuni ndiyo
aliyokuwa akiyasikia; akausihi moyo wake utulie na usiwe na pupa; na kwa wakati
huo akawaza staili za kumla bata wake wa anayenukia ukanisakanisa.
Basi ule muda aliokuwa akiusubiria ulitaradadi, Neema akatoka
huko bafuni na kitaulo kifuani kwake, akamtazama cliff na kumsogelea akijifuta
kiuchokozi na uchokonozi vimajimaji vilivyobakia mgongoni.
Neema akapanda kitandani na kumkabili CLiff aliyekuwa hajauwazia
huu mwenendo kabisa kichwani pake, Cliff akampokea sista wa kanisa kama mtoto
akamuonesha kuwa yeye ndiye kituji mrina asali akamgeuza na kuanza kumpangua
tawi mojamoja akipuyanga kuelekea kwenye mzinga wa asali.
Kila Cliff alivyomkwanyua vikonyo mtoto wa watu ndipo Neema
alitamka majina ya watu wa kwenye biblia na watakatifu kadhaa
Haikuwa inaendana na eneo la tukio kabisa na pengine malaika wa
dhambi wangemuandikia adhabu kali; lakini utamu ulimfanya aropoke neno lolote
lilikuwa karibu na ncha ya ulimi wake, naye ni sista sasa ungetegemea ataje
pombe pale au?
Basi robo sentimeta tu kufikia utamu na hatamu zake, ghafla
mlango ukapigwa hodi kwa nguvu, Cliff na Neema wakashtuka maana ni nadra mlango
wa hoteli kudundwa konzi zito namna hiyo. Cliff akaghafirika kwelikweli
akaizima laptop yake; lakini akasita kufungua mlango kwanza; pengine ni tego
hili! aliwaza akimtazama kwa jicho kali Neema; Neema naye alimtazama Cliff
vivyohivyo akijiuliza kama alivyojiuliza yeye.
mara mlango ukagongwa kwa mara ya pili tena kwa uzito uleule.
"we Cliff mkeo nini amekuja?" aliuliza Neema
akijivalisha nguo zake himahima.
"hapana; sina mke mimi?"
"au basi mpenzi wako.."
"hapana hawezi kuja huku hajui.." alijibu Cliff roho
ikimuuma jinsi Neema alivyovaa tena wakati mambo yalikuwa tayari siyo mambo.
mara hodi ikakoma kama ilivyokuja awali kukawa kimya tena; Cliff
akamtazama Neema aliyejivisha kama vile hakuna kilichokuwa kikiendelea humo
ndani.
"watakuwa wamekosea room!" alisema Cliff moyoni
akitukana kuanzia aliyegonga mlango wa chumba chake, wahudumu na hadi mmiliki
wa hoteli kwa kumharibia gemu yake.
lakini kabla wazo hilo halijamea kichwani pake kumshawishi Neema
aliyekuwa tayari na wasiwasi, mara simu ya chumba chake ambayo imeungwa na kule
mapokezi ikaita. Cliff akahesabu sekunde kumi kisha akaipokea kwa hofu na
ghadhabu.
"hallow, samahani mteja wetu;kuna tatizo limetokea
tunawapigia wateja wetu wote waje ukumbi wa hoteli floo ya tatu sasa hivi, ni
jambo la kiusalama tafadhali," alisema mhudumu wa kike aliyesikika akiwa
na hofu mno.
Haraka Neema alikimbilia kutoka nje ya mlango akimuacha Cliff
ameduwaa. Akilini Neema alijua pengine ni tukio la ugaidi linaendelea hotelini
hapo kiasi cha mhudumu kutoa taarifa ile, lakini kwa Cliff ilikuwa ni saa
nyingine ya kulaani; kwanini vikwazo vinatokea asifanye mapenzi na Neema; au
Mungu anamlaani asitende dhambi na mtawa?
Basi naye Cliff haraka akavaa nguo zake na kukimbilia huko floo
ya tatu alipopanda Neema, hapo varandani kundi la watu wakiwa ni wateja wa
vyumba vingine vya hoteli hiyo, wazungu, waarabu kwa waafrika wote wakikimbilia
pamoja naye kwenye floo ya tatu kila mtu akijiuliza; nini kimetokea?
wakaingia kwenye ukumbi huo wa mkutano wao wakionekana ni kundi
la mwisho kabisa maana watu walikuwa wengi sana hapo ukumbini, wengine na
mashuka kabisa ya kulalia wakiwa wamejizungusha nayo, wengine na mataulo na
mabaki ya mapovu masikioni kuonesha kuwa walikurupuliwa na hilo tangazo la
dhalura wakiwa wanaoga. Kuona hivyo ndiyo angalau Cliff alituliza pepo lake,
akajipenyeza mpaka alipokuwa ameketi Neema naye akaketi pembeni yake macho
yakiwa mbele ya ukumbi.
Watu wanne walionekana wakiwa wamevalia suti kuonesha kuwa ni
watu wa heshima au viongozi fulani, sura ya mmoja wao ndiyo iliyomshtua Cliff
akajiuliza amewahi kumuona wapi mtu huyo, lakini kumbukumbu zake zilimsaliti.
Ghafla kidogo kundi la maaskari polisi waliingia ukumbini hapo wachache wakiwa
na viziba pua kama madaktari wa oparesheni au wahudumu wa mochwari, na kufanya
ukumbi uzidi kuwa na hofu waliingia madaktari sasa wakiwa na makoti ya nailoni,
glovuzi za mipira, miwani ya kuziba macho mfano ya watu wanaopiga mbizi chini
ya maji na wakipumulia mashine fulani, migongoni mwao wakiwa na mabegi ambayo
walienda kuyaweka mbele kabisa kisha nao wakajiunga na wale wengine waliosimama
pale mbele ukumbini wakiwatazama wakina Cliff na kundi la wateja wa ile hoteli.
"Naitwa Mrisho Gambo, mkuu wa mkoa wa Arusha, samahanini kwa kuvamia hapa
hotelini, hawa ni madaktari kitengo cha kuzuia magonjwa ya mripuko. Kama
tunavyofahamu dunia ipo vitani dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona ambao
unaambukiza kwa njia ya kugusana au kukaa karibu na muathirika wa ugonjwa huo
"Ugonjwa huu ni hatari kwa kuwa unaua haraka kama utakosa
matibabu; kwa Afrika hadi jana nchi ya Nigeria, Algeria na Kenya zilikuwa
zimekumbwa tayari na ugonjwa huu.
Kwa bahati mbaya sana leo naripoti kuwa ugonjwa huu umeingia
rasmi Tanzania na mgonjwa wa kwanza amepatikana mchana huu hapahapa
hotelini." alisema mkuu huyo wa mkoa kauli yake ikitafsiriwa kiitaliano na
kiingereza na meneja wa hoteli na palepale minong'ono ikasikika mle ndani, hofu
ikatanda.
Cliff akamtazama Neema aliyejikunyata,akamsogelea na
kumkumbatia. "Kwa kauli hiyo basi, hoteli hii itafuata taratibu za shirika
la afya la dunia kuwa itawaweka karantini ya siku 15 wagonjwa wote kabla ya
kuwaruhusu ili kama kuna mtu atakuwa ameambukizwa bila kujijua asiende
kuwaambukiza wengine huko nje. Kuanzia leo hii ninavyotamka hoteli hii
naifungwa hakuna atakayetoka wala atakayeingia. Baada ya hayo ninawaachia timu
ya madaktari na wanausalama watawapeni maagizo zaidi natumai mmenielewa,"
alisema mkuu huyo wa mkoa na kuondoka haraka.
Loh kauli ya kutotakiwa kuondoka mle hotelini ilimvuruga kidogo
Cliff akawaza demu wake Grace yule polisi atamueleza nini, lakini mwenye mawazo
sanasana alikuwa ni Neema akamfikiria baba yake na alivyomdanganya kuwa
ataingia Arusha usiku huo je, akisikia alikuwa hotelini atamfikiriaje? kwanza
watamuuliza alifuata nini na hata kama aliamua kulala, vitabu vya hoteli si
vitamuumbua kuwa alifika Arusha siku nne nyuma? aliwaza Neema macho yake pia
yakiwa makini kuona kama kutakuwa na makamera ya waandishi maana sehemu kama
hizo waandishi hawakosekanagi. Akafarijika kutomuona hata mmoja akakumbuka
kumbe yupo Bongo nchi ya waandishi waoga kama kunguru wa Zanzibar,ona alivyokuwa
na hatari mtawa wetu hata hofu juu ya Corona hakuwa nayo, yeye aliwaza
kujilinda tu asiumbuke kwa baba yake.
"Naomba wageni waliofika kutoka nchi zilizoathirika wakae
upande huu wa kushoto, wale walioingia hapa hotelini kutokea Tanzania hapahapa
wakae upande wa kulia," ilikuwa kauli ya meneja wa hoteli aliyeitafsiri
vizuri kiasi cha kueleweka na wote waliokuwa hapo.
Haraka kundi likagawanyika, lakini Neema akawa ametatizika
hakujua aelekee wapi maana aliona kujitaja kama ametokea Italia ambapo ugonjwa
huo wa COrona umeshika kasi ingekuwa ni kuzidi kujichelewesha kukaa hapo
hotelini pia akawaza uwezekano wa kuruhusiwa kwa wageni wa hoteli waliotokea
hapohapo Tanzania na hakutaka fursa hiyo aikose.
Kwa upande wa Cliff yeye alikuwa tayari anaelekea upande wa
kulia na akashangaa kumuona Neema anaelekea huko pia.
"We Neema, si wamesema uende kushoto?" aliuliza Cliff
kujiridhisha na sababu ya maamuzi ya Neema.
"Cliff sitaki nibakie hapa Hotelini, lazima nirudi nyumbani
leo!" alifoka kichinichini Neema.
"sawa,lakini si unaona hali halisi tunatokaje sasa,"
alisema Cliff akitazama saa ya simu yake kuwa ni saa 9 kamili za mchana.
"sijui kwanini nilikubali kuja hapa hotelini na wewe
agh!" alilalamika Neema akionekana kujilaumu mno.
"usiseme hivyo Neema mimi mwenyewe naona kama vile nina
gundu na wewe; majuzi ulianza kubleed,leo corona dah!" aliamua kusema yake
pia Cliff.
"hapana labda Mungu ananiadhibu mimi," alisema Neema
akikaribia kujibanza kwenye hilo kundi la wageni kutokea Tanzania;lakini
akashtuka kuona mmoja wa wahudumu wa mapokezi wa hoteli hiyo akifika na daftari
la register kwa yule meneja wa hoteli ambaye alikuwa nyuma yake na maaskari
wenye maski zao usoni sambamba na madaktari kama wote.
Haraka Neema akajua ujanja wake wa kujibanza upande wa Cliff
utabainika na watamtilia shaka na kama wakimpekua na kugundua anatokea Italia
tena ni mtawa ndio kabisa watamgeuza kituko na mbaya zaidi alivyovalia hapo
ukumbini ilikuwa kichekesho maana alikuwa na kiskini jinzi na kingwabi
kilichomchoresha hadi ncha za matiti yake; akageuza harakaharaka na kurudi
upande wa kushoto akijiunga na wahabeshi wenzake akitengana na CLiff aliyekuwa
ametumbua macho asielewe mchezo wa Neema.
Basi kama kweli alivyotabiri Neema, majina ya register sasa
ndiyo yakatumika kuwatenganisha wageni kutokana na nchi mbalimbali tena kundi
la kwanza kupimwa likawa la wale waliotokea nchi zenye maambukizo ya COrona
wakianzia Uchina, Marekani na kundi litakalofuata kupima lilikuwa na wageni
kutoka Italia ambapo hapo Neema alikuwemo.
Mkojo wa wasiwasi ulimbana Neema wakati akishuhudia foleni
ikipungua kuelekea kwenye sehemu ya kupimia, akajua ataumbuka safari hii;
akamuomba Mungu amsaidie asiumbuke na akaapa kutorudia kufanya uzinzi huu tena.
"jina na umetokea nchi gani na chumba namba ngapi?"
aliuliza meneja akimkazia macho mzee wa kizungu aliyekuwa akipiga chafya
mfululizo mbele ya Neema, maana akitoka huyo tu ndiyo Neema angefuatia.
"Diego Poisant, Italy, room 13," alisema huyo Mzee kwa
kingereza kilichoathiriwa na kiitaliano cha ndani kabisa. "where is your
passport?(passport yako ipo wapi)" aliuliza yule Meneja akipandisha maski
yake imzuie vilivyo usoni maana shuku la wote mle ndani lilikuwa juu ya mzee huyo
kuwa ana corona maana hata wale maaskari walitetemeka.
"I left it in my room, hey I came in a hurry i didnt know
we have to come with it{ nimekiacha chumbani, nilitoka kwa haraka, sikujua kama
nilipaswa kukibeba)."
Basi alivyosema hivyo yule meneja akasema kwa sauti,
"tafadhali walioacha passport vyumbani wakachukue na warudi haraka
hapa."
Loh alivyosema hivyo, Neema akaona ni chansi akarudi haraka kule
chumbani; akawaza kutoroka hotelini lakini nje umati wa mapolisi na waandishi
wa habari ulimrekebisha wazo lake haraka. Basi akavua viwalo vya kishenzi
alivyovivaa na kuvaa vazi lake la usista akabeba na simu yake na kumtumia
meseji, Cliff.
"Sikia nitasema wewe ni dereva wa parokia uliyetumwa
unipokeena unipeleke nyumbani," aliandika meseji hiyo Neema ikadeliver kwa
Cliff maana alikuwa na uhakika alimuona na simu yake pale ukumbini.
"He sasa wakiuliza ilikuwaje jina la pale reception
niliandika jina langu, nisemeje?"
"sema ulikuwa umeona usumbufu kubook kwa jina langu,kwakuwa
ndege ilighairishwa mara nyingi, sema nilifika jana usiku, nina uhakika
muonekano wangu nitakavyotoka huku ndani,hakuna atakayesema aliniona mahali
popote.
ITAENDELEA

0 Comments