Dula kabla hajajibu
kunamzee mmoja akaingia akiwa anahema naitwa juma nimesikia mke wangu na
mwanangu wameletwa hospitali hapa wakiwa mahututi bado wazima? Mzee juma
aliongea huku jasho linamtoka dokta ikabidi amtulize na kumwambia mke wako na
binti yako anaitwa nani.
Aaaaanaitwa mama jeni na
mtoto wetu anaitwa jeni
Ile kutaja jeni Dula
akashituka kumbe huyu ndio baba yake jeni
Dokta aliweza kumweleza
vyema na kumtoa wasi wasi na kuwa wanaendelea vyema ila mtu ambae anaruhusiwa
kumwona ni mkewe tyu ila jeni hadi kesho basi mzee juma alienda kumwona mkewe
pamoja na akina dula na nasra.
Ndipo dula na nasra
walivyomaliza maongezi na mgonjwa waliaga wanaondoka hadi kesho
Mzee juma aliingiza mkono
mfukoni akatoa laki mbili akawapa Dula na nasra na kuwashukuru kuokoa maisha ya
familia yake
dula alipokea kisha
akatoka nje
Ndipo alimgawia nasra
laki moja.
Dula hizo hela chukua
zote mimi sina shida na hela baba yangu anapesa nyingi nasra alikataa kupokea
japo alimlazimisha ila hakupokea
Dula alizitia mfukoni na kumwaga
nasra kua yeye anaenda nyumbani
Nasra alimwambia Dula
apande gari ili ampitishe anako kaa basi dula alikubali.
Dula na nasra walisogea
hadi mahali waliko paki gari nasra alifungua mlango akaingia na kumwambia dula
apande
Kitendo cha dula kushika mlango
wa gari alishangaa kitu kizito kikatua shingoni puaaa ,dula akayumba kabla
hajakaa vyeama akapigwa tena na nondo nzito kifuani dula akayumba na kudondoka
nasra akapiga kelele baada ya kumwona mpenzi wake ambae mchana aliwafuma
wamekumbatiana na Dula baada ya kumsaidia kurudisha simu yake kwa vibaka.
Jemba ilimtandika Dula
balaa mudy akiwa hajielewi yule mwanaume wa shoka akatoa panga na kuliweka
shingoni mwa dula kisha sauti nzito ya yule mwanaume ikitetemesha "
akasema shenzi boya wewe nakata shingo mchana ulibahatisha kunipiga wasalimie
kuzimu.
Tulipoishia jana baada ya
Dula kupigwa na jemba kisha akadondoka chini ile njemba ikiwa na kundi lake
alitoa panga na kuiweka kwenye shingo ya dula.
Nasra alianza kutetemeka
wakati Dula hajielewi anaona marue rue baada ya kupigwa na nondo kifuani na
shingoni
Yule jemba alianza kuonge
"mimi ndio RAMSONI gaidi wa dar es salam wewe nyau mchana uliniotea
ukanizimisha ukajiona wewe ndio hatari kwa taarifa yako nakata shingo wasalimie
kuzimu
Ile anashikilia panga ili
amkate Dula, Tayari dula kengele ya hatari ishagonga kichwani dula alihisi
kichwa kinazunguka alijituliza akakuta panga ipo shingoni.
Alichokifanya aliikamata
ile panga kwenye makali , ramso akashtuka kumbe huyu bwege hajafa tyu ramso
aliinama ili amkandamize dula asisimame kitendo cha kuinama dula yuko shapu
aliinuka kwa stail yake na kumtandika hedi ya maana kwenye utosi ramso akapiga
yowe la uchungu yani kichwa alotandikwa ni balaa ikawa zamu yake kuona marue
rue,
Dula akafanikiwa kuinuka
huku kashikilia panga kwenye makali
Ikawa vuta nikuvute
aliachia ile panga akaruka na kudunda juu ya gari akajizungusha na kuachia
mateke mawili yaliyompata ramso vyema kichwani ramso akayumba na kudondokea
kwenye gari yake
Kabla hajakaa sawa dula
katua kifuani na kumtandika makonde ya ngumi nzito.
Ramso ulimi ukamtoka
wakati ngumi zikiendelea kurushwa bibie nasra kashikilia mapigo ya moyo na
kujisemea" mungu msaidie dula asiuawe nampenda hakika ni handsome anioe
mimi walai nimempenda hayo ndio yalikua maombi ya nasra" hakujali kama
dula anapambane yeye ombi lake ampate dula.
Ramso nae alijitahidi
akarusha ngumi na kumpiga dula shavuni kama karudisha mashambulizi hapo ndipo
alipokosea dula aliruka hewani akajizungusha kama kamba na kumtandika mateke ya
double kifuani ramso alirushwa na unene aliojazia kwa kunyanyua vyuma na kwenda
kujibamiza kwenye mstimu puuu, taya zikapishana akajaribu kuongea hakuweza
akajaribu kuinuka hakuweza.
Dula akaenda na kumwambia
ramso "kaka yangu mimi staki kukuua huenda utajirekebisha shika panga lako
ukipona utaenda kufanya shughuli za shamba na ukiendelea kunifuatilia
nitakupoteza kwenye huu ulimwengu nakuheshimu sana "
Dula aliongea na kumtupia
panga lake kisha akaondoka na kuingia gari ya bibie nasra ,ramso na wenzake
hawaamini kama wamepata mbabe wao ,mwanzo walijua jiji lakwao wananyanyasa watu
ile kwa sasa imekuwa tofsuti.
Hospitali ilijaa watu
wakishuhudia pambano live simu ilipigwa polis ile dula anatoka akapishana na
gari ya polisi
Ramso na wenzake
wakawezwa kukamatwa wakati huo dula washaondoka na kuelekea nyumbani ilikua
tayari ishatimia saa moja jioni.
Musa nae akiwa getoni kwa
Dula alichoka kulala akaamua atoke akatembee ili apunguze mawazo musa alifunga
mlango na "kujisemea huyu Dula kaenda wapi?" Au nisitoke huenda
atakuja na akikuta sipo atamaindi maana jamaa mwenyewe anajua kupigana kama
wachina yaani nishida .
Aliwaza huku akizidi
kusonga na kuzidi kufika mbali sehem waliko kulikua na mageti makubwa nyumba za
kishua.
Mara kuna mdada mzuri
kaumbika balaa akiwa anatembea haraka haraka kashika simu kashika mkoba mkononi
kashika pochi ndogo sijui ndo inahela .
Akiwa anaharaka haraka
anataka kuiweka ile pochi ndogo kwenye mkoba bahati mbaya hakuiweka ndani yeye
alifungua zipu na kuweka kumbe hakuweka ile pochi ikadondoka chini puuuh!.
Kulikua na mwanga wa
mbala mwezi na taa za majumbani
Musa aliiona ile pochi
wakati huyo dada ashafika mbali kaiacha
Musa akafika mahali iliko
dondoka hio pochi akaiokota "mmmmh mbona nzito hii pochi kuna nini?"
musa alijisemea na
kufungua akajikuta anatoa macho "mmmmh " akaguna na kusema kumbe watu
wanalalamika vyuma vimekaza watu wameweka mahela ivi .
ile pochi ilikua imejaa
minoti miekundu tyu musa hakuhesabu aliitia mfukon akaangalia kulia na kushoto
hamna mtu
Musa akasema tayari
nishakuwa tajiri mimi umaskini bai bai.
Musa akasema hizi hela
kazidondosha kwa haraka zake acha nikaziweke geto musa akiwa anawaza. Hivyo
mara sauti ya mama yake ikamjia angali mtoto "mama yake alikua akimwambia
"
"Mwanangu ukiokota
kitu na ukamwona aliyeki,dondosha iwe ka bahati mbaya mrudishie usifsnye
dhuluma , usiibe wala kufanya uhalifu ili utajirike,
Utajiri huja taratibu ila
sio kwa kuzulumu kuiba na kupora
Yale maneno yalimuuma
akasema yawezekana hizi hela alikua anapeleka mahali acha nimkimbilie
nikamkabidhi hela zake ,alianza kukimbia kumtafuta yule dada.
Wala hakua mbali aliweza
kumwona akiwa anaongea na simu huku anatembea haraka haraka
Musa alimwita "dada
nisubiri wee dada nisubiri" musa alimwambia cha ajabu yule dada aligeuka
na kumwangalia musa kisha akaendelea kuongeza mwendo ,si unajua ukiwa umebeba
pesa nyingi basi kila mtu unaemwona mbeleke yako unahisi ni kibaka
Eneo hilo hapakuwa na
watu palikua pametulia sana mageti tu ya nyumba za kishua
Musa alikimbia na
kumkimbilia yule dada
Cha ajabu yule dada nae
akakimbia huku akiongea na simu ,hufu ya yule dada anajua anapesa hivyo
anahofia kuibiwa ama kuporea ndio maana nae akazidi kujihami.
Yule dada akimtizama musa
mwonekano alijua ni kibaka anataka ampore simu na hela alizokuwa nazo
Basi dada aliendelea
kujihami kukimbia alikimbia na kufika kijiwe cha kahawa akiwa anahema juu juu
watu wote walimwambia dada kulikoni mbona unakimbia hivo.
Yule dada akiwa anahema
akasema kuna mtu ananikimbiza sijui ni kibaka anataka aninyang'anye simu yangu
yule dada aliwaambia vijana kwenye kijiwe cha kahawa
Vijana walisimama kila
mtu na zana zake yuko wapi huyo kibaka anataka kukaba saizi mapema saa mbili
watu walijiandaa kwa ajili ya kumfundisha adabu huyo kibaka mara musa
akajitokeza akiwa anamfuata yule dada akampe pochi yake .
Kitendo cha kufika
kijiweni yule dada akamnyooshea musa mkono huyo hapo jamni
Musa alivamiwa na kuanza
kupigwa pale pale kijiweni" we kibaka kudadeki zako unataka kuiba ,watu
kama ninyi tunawatafuta , musa alishambuliwa na watu wengi vijana kwa wazee
wahuni wote wa sinza walimpiga musa na mbao, nondo viti hakika ndani ya dakika
tano musa hatamaniki damu kila mahali.
Mimi sio mwizzz musa
alijitetea "aah wapi wala watu hawakumwelewa alitandikwa mbaya".
Mara gari ya nasra akiwa
na dula, ilitokeza mahali pale dula aliweza kuona rundo la watu wakimshambulia
mtu akiwa ana gara gara chini huku wakimpa kipigo kikali dula, alimwambia nasra
hebu simamisha gari pale kuna nini mbona kama mtu anapigwa ebu simamishe gari
nikacheki kuna nini.
Nasra akakataa
kusimamisha gari na kumwambia dula," staki wasije wakakupiga mi nikakukosa
bure kwani hujui kama saivi upo moyoni ,yaani natamani nikufungie ndani usitoke
nasra aliongea huku akikataa kusimamisha gari".
dula akaona hii tabu
kutembea na mwanamke anae waza mapenzi muda wote akajaribu kufungua mlango
nasra alikua amelock.
Ikabidi atumie nguvu
simamisha gari lasivyo nakufumua sasa ivi nasra alivyoona dula kakasirika ndipo
akakanyagw breck gari ikasimama.
Sema walikua washapapita
dula,alifungua mlango upesi na kutoka alienda lile eneo alikuta rundo la watu
likiendelea kumpiga musa.ki ukweli musa nyota yake mbaya kila mahali yeye wa
kupigwa anamkosi.
Musa aliishiwa nguvu damu
mwili mzima. Dulaalifika na kusema acheni acheni acheni huku akiwasukuma ili
wasiendelee kumpiga huyo mtu kuna kijana mmoja alikua kabeba tofali la block na
tayari alijiandaa kumpiga musa kichwani.
Yule jamaa aliachia lele
tofali bahati nzuri dula alikua tayari ashafika alilidaka lile tofali kidogo
angezubaa musw angepasuliwa wakati huo hajui kama anaepigwa ni musa na
alishaambiwa na jeni amlinde musa aishi salama.
Watu wote walimshangaa
dula baada ya kudaka lile tofali ,akiwa anahema "aliwiwauliza mnampiga
kafanya kosa gani ?" Huku anamwinua mtu aliyekuwa akiipigwa alizidi
kushangaa baada ya kuweza kumtambua yule ni musa.
Dulabaliita kwa nguvu
musa ndugu yangu kulikoni ,musa alikua hawezi hata kuongea aliongea kwa tabu
kaka dula sielewi nimefika hapa wakaanza kunipiga alimwambia dula.
dulw akiwa haamini
aliwaukiza watu huyu kafanyeje mbona mmempiga watu wakasema alikua anamkimbiza
huyu dada ili amupore simu.
Musa hali yake ilizidi
kuwa mbaya wema wake umemponza musa analoa damu kuongea hawezi ukimtizama kama
unaroho nyepesi lazama utamwonea huruma.
Musa alijaribu kusimama
hakuweza akajikakamua na kusimama aliingiza mkono mfukoni akaitoa ile pochi
ndogo ya yule dada musa aliongea maneno machache.
"Dada mimi sio
kibaka wala mwizi na hii mara yangu ya pili kusingiziwa mwiz ulidindosha pochi
yako na mimi ndio nimeiokota nilikua nakukimbilia ili nikukabidhi pochi yako
nasi kukupora simu"
musa aliongea kwa shida
yule dada baada ya kuona ile pochi kwa musa akimpa alitumbua macho hakuamini
ukweli ilikua pochi yake,
Alifungua mkoba mkubwa
pochi haikuwepo ,ndio ile musa alompa
Yule dada alianza kilio
nisamehe sikujua kaka yangu nimekuponza umepigwa yule dada alilia kijiwe chote
walishangaa na kujilaumu uamuzi waliouchukua
Wote walinza kumwomba
musa msamaha
Kwa kipigo alichopigwa
musa gafla alidondokea kwa dula na akawa kimyaaa akiwa anavuja damu.
Yule dada aliyepewa pochi
yake alilia na kujiburuza chini akiomba msamaha.nimeponza mkaka wa watu anakufa
kww ajili ua uzembe wangu.
dula alimwita nasra alete
gari upesi amuwahishe hospitali
hatimae musa alifumba
macho na kuwa kimyaaaa
yule dada ambae hatujajua
ni nani,akasema nimeua ,nimeua akiwa analia,dula nae akamtizama wkamuuliza
"unasemaje?
Hakika yule dada alilia
sana na kujilaumu kwanini aliwaambia watu kuwa anataka kumpora
Watu kijiwen walimlaumu
yule dada na kumwambia usiwe unamhisi mtu tu ukajua ni mwizi ona tulivyompiga
kijana wa watu sijui kama atapona yule dada alipewa lawama zote. Watu kijiweni
walijilaumu sana , haikuwezekana tena kwa muda ule kuomba msamaha kwa kipigo
wapichompiga musa maana alidondoka na kuwa kimya .
Musa alipakiwa kwenye gar
na nasra na kuwahishwa hospitalini gafla sim ya yule dada ikaita bila shaka
kuna mtu alimpigia aliitoa kwenye mkoba na kuipokea "haloo upande wa pili
akaitikia" yes"
mwanangu uko sawa?
Mbona kama unalia yule
dada akasema" niko saawa japo alibabaika maana waliwasiliana na baba
yake" na kuambiwa awai kinondoni biafra .
yule dada alikodi piki
piki akaelekea aliko ambiwa aende dada yule alichanganyikiwa alikua akilia sana
aliweza kufika biafra alifuta machozi ili kuzuga baba yake asijue kipi
mimemkumba njiani ,aliweza kwenda moja ya baa iliyoezekwa kwa makuti alinyoosha
hadi akaunta aliweza kumkuta baba yake .
"Dady shikamoo"
" marhaba mwanangu
"
vip mbona kama ulikua
unalia?
Yule dada alitikisa
kichwa na kusema "hapa "
"Irene mwanangu
unanificha ee ok sawa "
kumbe huyo dada alikua
anaitwa irene, basi almkabidhi mzigo alioupeleka kisha akamwaga baba yake kua
anarudi nyumbani baba yake alimruhusu na kumpa hela ya usafiri .
Irene alirudi nyumbani
moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani mama yake alikuwa kakaa sebuleni lakin
irene aliingia chumbani kwake na kuanza kulia
"Hiiii hiiiii nimeua
jamani mungu nisamehe sikujua kwamba yule kijana hakua na nia mbaya na
mimi"
Kijana wa watu kaokoa
pesa za baba endapo zingepotea baba angeniua mimi wala asingenielewa.
Kijana wawatu kaokoa
maisha yangu mimi nimemsababishia kifo
Eeeh mungu muokoe asife
nitafanya chochote kwa ajili yake niko tayari kuokoa maisha yake hakika irene
alilia na kujilaumu
Mama yake alimwita akale
chakula irene alisema ameshiba.
Tukija hospitali ambako
jeni na mama yake kalazwa musa nae alipelekwa pale .musw alipokelewa haraka na
kupelekwa chumba cha watu mahututi hali yake ikiwa haitambuliki kama amekufa au
yu hai madaktari walianza kumshughulikia walimuwekea oxygen na mambo kadha wa
kadha
Ilionekana mapigo ya moyo
yako mbalii sana dokta alijitahidi usiku kucha
Musa alikesha na nasra.
Nasra alirudisha gari
nyumbani kisha akachukua koti na dula nae akampelekea koti
Nasra alikaa pemben ya
dula ,wakiwa kimya dula alikua hana ata hamu ya kuongea akifikiria hali ya musa
anashikwa na uchungu na kujikuta machozi yanamtoka walikesha wakisubiri majibu.
Ilifika saa nane usiku
nasra alichoka akajilaza miguuni kwa dula, alilala huku akipata joto.
dula hakua na hisia
zozote , aliingia kwenye msongo wa mawazo nasra alianza kukoroma japo kulikua
na feni ila mbu bado walikua wana muuma dula pamoja na nasra.
Hadi pakapambazuka kila
akiwauliza madaktari vip anaambiwa cha msingi ni kumwomba mungu kwani hali yake
sio nzuri
Palivyopambazuka jua
likachomoza
Irene alishidwa kuvumilia
irene alilia hadi macho yakamvimba jua lilivyochomoza alitoka na kuanza
kumtafuta musa kila hospitali za pale sinza
Hakika irene
alichanganyikiwa alijuta alicho kifanya ilifika mida ya saa tatu
Chumba alichokua jeni
kilifunguliwq jeni alikua kapona japo sio sana ila aliruhusiwa akaendeleze dozi
nyumbani jeni pamoja na mama yake.
Chumba aliko musa
alipimwa na ikaonekana damu iliyopo ni chache hivyo anahitaji kuongezewa damu
Dokta aliwafuata dula na
nasra ili akawape taarifa za mgonjwa wao kuongezewa dam.
Jeni walitoka na mama
yake pamoja na baba yake walishangaa kuwakuta dula na nasra wako pale.
"Hee nyie toka jana
hamjaenda nyumbani?" Baba yake jeni alimuuliza ,dula aka wajibu" baba
hapana kuna mgonjwa mwingine tumemleta ok baba yake jen akaitikia".
Jeni alivyomwona dula
alimkumbatia na kumwambia asante kwa msaada wako kitendo cha jeni kumkumbatia
dula, roho ya nasra ikaenda juu na kuhisi jeni anafaidi joto la dula, maana
anampenda dula balaa.
Mara dokta akafika na
kumwambia dula, mgonjwa wenu anahitaji kuongezewa damu upesi kama kuna mtu
atajitolea kumpa damu aje tumpime ili tuweze kuokoa maisha yake anahali mbaya
,dula alisema sawa twende ukanipime jeni akamuuliza dulwla" nani anahali
mbaya"? dula akamjibu jeni "musa anahali mbaya jana kapigwa
usiku."
Jeni kusikia jina musa
akachanganyikiwa na kusema dokta kama damu yangu itafaa kumuwekea musa nitoeni
damu yote hata sasaivi haiwezekani kila siku musw wa kupitia mateso hayo
nitoeni mimi damu nife musa apone .dunia hii ni mara chache kuona mtu anatoa
uhai wake kwa ajili ya mtu mwingine kama bahati aliyoipata musa licha ya kuwa
na bahati mbaya kila muda yeye wakupitia mateso.
Jeni aliongea huku analia
alikua hawezi kutembea vizuri sababu ya kukanyagwa tumbo, baba yake jeni na
mama yake jeni walimshangaa mwanao na kumuuliza huyo musa" unamjua jeni
aliwajibu namjua".
Kweli hali ilikua tete
jeni kagoma kwenda nyumbani anataka atolewe damu apewe musa si mchezo ,dula
alipimwa damu hazikuendana magroupn hivyo haitawezekan.
Jeni alisisitiza yeye
apimwe ili damu yake yote apewe musa ,lait anfejua mtu anaeyetaka kumpa dwmu
yake tayari keshaonjeshwa tunda bafuni na mpangaji basi asingelisubutu ila kwa
kuwa hajui basi alitaman kumsaidia musa apone,
yeye yupo tayari kufa na
endapo watakataa kumtolea damu wakasababisha maisha ya musa akafa basi yeye
yuko radhi kujiua na yeye endapo tu musa atakufa na yeye atajiua ki vyovyote
vile.
Hakika jeni alizidi
kuwaacha wazaziwake midomo wazi wakashidwa namna ya kumshauri jeni hakusikiliza
chochote anachotaka damu yake ipimwe apewe musa.
Wazazi waligonga mwamba
ikabidi wakubali apimwe maana wakikataa endapo musw atakufa na yeye atakufa si
mchezo jeni alichukuliwa damu na kupelekwa kwenye vipmo.
Ile dokta anaenda maabara
mara irene akaingia wakakutana uso kwa uso na dula .hasira za dula zilipanda
baada ya kumwona irene pale hospitalini maana irene ndiye aliyesababisha hayo
yote hadi musa kuwa katika hali ile.
Macho ya irene yalikua
yamevimba na kulia alivyofika alipiga magoti huku akilia akimwomba dula
amsamehe na hakujua kua musa hakuwa na lengo la kumpora irene alilia huku
akiomba msamaha,hospitali ilijaa majonzi na kuacha watu vinywa wazi.
Kaka kama yule kijana
anahali mbaya anaitaji kuongezewa damu au moyo au mapafu nitoeni mimi ili huyo
kijana atibiwe mimi ndiye niliyesababisha awe katika hali ile. irene aliongea
mashavu yake yakitiririsha machozi
Irene akiwa analia na
kusema kama musa anahitaji kupewa moyo ili asife yeye yupo tayari kutoa moyo
wake iwe figo hata damu hakika irene aliwashangaza watu.
Mara dokta alirejesha
majibu na kusema damu ya jeni inafaa kwa musa wapo group moja jane akaitwa ili
akatolewa damu kama alivyosema awali.
Irene alisimama na kusema
hapana wewe dada niache mimi nife dokta pima damu yangu nikamuongezee huyo
kijana irene alimzuia dokta dokta nae aliongea kwa msisitizo endapo tutaendelea
kuzozana tutampoteza huyo mpedwa.wenu.
Irene akarudia kuongea
kama huyo kaka atakua anahitaji moyo chukua wangu kama figo chukua hata damu
chukua .
Dokta alichanganyikiwa
ikabidi akampime irene endapo damu zitaendana achukue ya irene maana jeni bado
anaumwa.
Damu ya irene ikapimwa na
majibu yakaletwa kuwa inafaa kumwongezea musa
Dokta akamwita irene
akamtoe damu ili amuongezee musa, jeni aliwaza anampenda sana musa na yuko
tayari kwa lolote sasa jane alimkaba irene na kusema mimi natolewa damu
nimsaidie musa
Irene akamkaba na yeye
jeni akasema yeye hastahili kuishi kwani alichomfanyia musa hana thamani ya
kuishi kwenye sayari hi kwel ikawa vuta nikuvute mimi natolewa damu jeni
anataka irene anataka.
Dokta alitazama saa yake
mkononi na kuwambia zimebaki dakika kumi tu endapo mtachelewa basi musa
atapoteza maisha
Mwa upande wa jeni
ilikuwa ni vigum mno aligoma hadi kufikia baba yake kukasirika kwani ashampinga
mwanao vikali asijihusishe na wanaume na hii ndio madhara yake .
Baba yake jeni ikabidi
aulize musa ni nani na alipenda aunane nae, akaoneshwe ili amjue hata kwa sura
dokta alimruhusu akaenda pamoja na mkewe ile mama ireni kuingia chumba aliko
musa na akaweza kuona uso wake akajikuta anakumbatia mdomo kwa hofu kisha yule
mama akaanza kutiririsha machozi jambo lililofanya baba jeni ashidwe kuelewa
kuna nini kati ya familia yake na huyu musa.
Mama jeni alitoka nje
akamvuta mwanaume na kusema hata yeye ashawai kumsaidia huyu kijana mwezi mmoja
ulopita alipigwa maeneo ya mwenge mimi nilimchukua na babu mmoja nilimpeleka
massana hospital alitibiwa na alikua anaendelea vyema sasa sijui binti yetu
wamejuana vipi vipi huyu kijana .
Mama jeni aliongea kisha
baba jeni hasira zilipanda alimshika binti yake mkono na kumvuta kwa hasira
hakujali yakua jeni anaumwa alimkokota hadi kwenye gari .
Jeni alilia na kusema
baba niache hadi nisubiri nione musa anapona ila baba yake aliwaka mbaya
alimchukua na kuingia kwenye gari aliongea neno hamna kutoa damu wa msaada wote
twendeni nyumbani aliweka kikomo na maneno yake kwenye familiw ni sheria .
Jeni utanieleza huyo kinyago
mwizi sijui musa mmekutana vip na nilishakukataza kutembea na wanaume leo ndio
utanitambua mimi ni nani mzee aliwaka mbaya, jeni wala hakujali alikua akilia
tyu,kupande bwana kunamfanya mtu anakuwa chizi.
Hospitali baada ya jeni
kuchukuliwa ki nguvu na baba yake ndipo dokta aliweza kumtolea damu irene
haraka haraka na kumpatia musa
Na tayari ilikua
zimesalia dakika chache musa apoteze uhai wake kutokana na hali aliyokuwa nayo.
Hapo ndipo musa
aliongezewa damu, irene alikua ni mtu wa kulia na kumwomba mungu musa apone
amwombe msamaha kwa kweli ilikua ni wakati mgumu kwa irene .
Dula na nasra walikuwa
wakikaa pale hospitali walikua wananunua chakula wanakula wote nasra hakutaka
kukaa mbali na dula nae moyo ushatawala kwa yule kijana ,sijui kww mwonekano
wake ama ujasiri alionao wa kupambana na kuwa mshids ,huenda nasra aliona hio
nafasi ndio nzuri kumpenda mwanaume ambae anaweza kumlinda.
Nyumbani kwa irene
alianza kutafutwa ,na familia hake haonekaniki kibaya zaidi simu aliacha
chumbani alitoka yeye kama yeye mama yake alianza kuwaza huyu binti yangu sasa
kaenda wapi maana toka jana simwelewi.
Alijaribu kupiga simu kwa
mmewe , "akamuuliza vp irene amekuja huko?" mme akasema" toka
jana alivyompelea zile hela yeye aliondoka na yupo mlandizi kwenye shughuli
zake za ujenzi ,mama irene alibaki njia panda.muda mwingine kulewa mabinti ni
kazi kweli kweli.
Tukirudi hospitalini
baada ya jeni kutolewa damu alipewa wosia ale sana mboga za majani na matunda
ila irene hakuwa na hamu ya kula
Musa alianza matibabu
hatimae hali yake ikawa nafuu.
kila siku irene anakwenda
kumtembelea musa hospitalini vile vile dula na nasra wakawa wanamtembelea nao
kila siku na kumpelekea chakula musa alikaa miezi miwili hatimae alipona na
kurudi katika hali yake.
musa alipona majeraha na
mwili ukaimarika ,vile vile alimsamehe irene irene kwa yote yaliyotokea kwake
aliona ni sahihi hata asingelimsamehe isingesaidia maana tayari hali ishatokea
,pia kumshukuru kujitolea kumwongezea damu na kuokoa maisha yake.
Musq aliruhusiwa na
kwenda kwa nyumbani mwenye geto la dula
nasra na dula tayari
walikua wapenzi toka jeni atoke hospitalini hakurudi tena wala hata simu
haipatikani sijui kitu gani kilitokea ,kwa upande wa irene akawa kili siku
lazima aende kwa akina musa alimfulia musa nguo kumpikia kila kitu alikua
anafanya hivyo walau kulipa kew kile alichifw ya ,musa alijaribu kumkataza ila
irene hakukubali alilazimisha kufanya vile..
Maisha yaliendelea kama
kawaida , kuna siku musa alikaa nje akawa anamfikiria jeni na "kusema jeni
nitampata wapi nimemisi nimwone akiwa kakaa kaegemea ukuta" alisikia dula
akiongea na simu.
"Halo we nani?"
" Mimi jeni
hunikumbuki?"
jeni yupi dula alikua
anaongea huku kaweka laudi spika musa aliyasikia vyema maongezi jeni .
pia aliahidi leo anakuja
kumwona musa
dula alimwelekeza mahali
anamoishi ili iwe rahisi kufika eneo lile.
Ilivyofika mida ya saa
nane gari aina ya nissan ilipaki mahali akina dula wanaishi mrembo matata
alishuka kwenye gari marashi alopuliza kila mtu aliuliza nani huyo kapuliza hio
pafyum nzuri wapangaji walitoka kuangalia huo ujio wa nani? kama mjuavyo wambea
lazima waangalie kila kitu.
musa alikua kajilaza
kwenye mfuko wa roba na alikua akivuta usingizi wa mchana maana ndani ya chumba
dula alikua na bibie nasra wakipeana mavitu roho inapenda ,hio ni kawaida kwa
watu wanaoshare chumba ,mwenzako akipata mwanamke basi unampisha unaenda
kuzururs hadi atakapomaliza mambo yake utarudi ,ila kwa musa ilikuwa ngumu hana
nahali pa kwenda hivyo aliona ni vyema alale.zake nje tu.
Jeni alikua kabadilika
kawa mweupe nywele ndefu hadi mgongoni jeni aliangaza macho akatoa simu kubwa
akabonyeza namba alimpigia Dula.
Dula alipokea kisha
akatoka ndani ya chumba chao huku akivaa vest nyeupe huku jasho likimtiririka
bila shaka alikua kwenye shughuli ya kumkuna narsa.
dula alipagawa baada ya
kumwona jeni ikabidi aite jeni?
"Yes dula "
jeni aliitika na kujibu ni mimi , vipu musa yuko wapi jeni aliitika na
kumuuliza".
Dula alicheka na
kumwambia inamaana humwoni kweli au unanitania? jeni akauliza tena "yuko
wapi "
Dula alimwonesha kwenye
ukuta ule pale kalala wala hana habari alikua kajilaza kwenye roba kajikunja
vilivyo.
Jeni baada ya kuambiwa
ndio yeye musa haraka alienda mahali aliko musa na kukaa kwenye roba hakujali
kama linavumbi jeni alikaa kisha akamugusa musa shavuni .
musa alijivuta akiwa
usingizini jeni alirudia kumtingisha hapo ndipo musa aliamka ,alishangaa
kumwona msichana mrembo sura haikua ngeni alimtambua vyema.
Jeni alimkumbatia kwa
nguvu baada ya kumwona mzima wa afya taratibu machozi yakaanza kumtoka musa na
jeni nae alilia kwa furaha.siku zote upendo huanzia moyoni hata bila kutamkiana
mnapendans,ni dhahiri hisia za muss na mrembo jeni ,mioyo yao ishapendana.
Jeni aliita musa
musa kinywa kilikuwa
kizito yote ni furaha ya kumwona msichana ambae kila kwenye majanga amekuwa
akiokoa maisha yake .
Musa alimkumbatia jeni na
kumshukuru kwa msaada wake.
jeni nae alifurahi
kusikia sauti ya musa walikaa nyuma ya nyumba kwenye gunia lenye vumbi jen wala
hakujal dula nae walitoka na nasra wake wakaenda kukaa nje pamoja na akina
jeni.
Jeni alicheka kidogo
akasema samahanini. dula, musa na wifi yangu nasra ngoja niwaletee chakula kipo
kwenye gari.
jeni aliongea na kuinuka
na kufanya uwazi kwenye mapaja yake ,musa aliweza kuona nguo ya ndani aliyovaa
bibie jeni na kusababjsha mjsa ameze mate mengi.
Jeni alifungua gari
akatoa furushi kubwa kwenye kapu kulikuwa na sahan hotipot na jagi kubwa la
juice ya matunda .
Jeni aliwapakulia chakula
wote na yeye akajipakulia kwenye sahan akatoa glass akamimina juice wote
walianza kula.
Wapaangaji walianza
kubinua midomo na kusema dula anatumia kizizi sio bure apendwe na wadada wenye
pesa zao ,kutwa wanapishana ma magari wakati dula ni masikin tu.basi maneno ya
wapangaji yalianza chokochoko.
basi wapangaji walilala
mika kuona vyakula vitamu mapochopocho tambi kidogo ,pilau nduzi nyama yaani
vilikua vyakula vikinukia hata mimi ninaekula wali kisamvu kila siku nami
ningeongea tu.
Wakati dula musa , jeni
na nasra wakiendelea kula huku wamekalia gunia
Kwa mbali bibie irene
alikua anatembea taratibu kwa maringo mkonon kashika kapu bila shaka alikuwa
anaweletea musa chakula maana ndio kawaida yake kila siku hua anapika chakula
na kumpelekea musa.
Hatimae irene aliweza
kufika kwa akina musa maana anakokaa yeye na kwa akina musa hapana umbali.
Ile irene anafika na
kuwasalimia wote dula akainuka ili ampokee kapu la chakula jeni aliinua kichwa
ili amtizame nani anasalimia
Gaflaa macho ya jeni na
irene yakakutana .kama unavyojua mwez ulopita walikuwa wanagombana kumwongezea
damu musa leo tena wamekutana kwa , kila mmoja kampelekea musa chakula
jeni alitupa sahan ya
chakula ile anainuka amwangalie irene .
Irene nae ile anampa dula
kapu ampokee .
mwili wa irene ulikosa
nguvu irene alishuka kama gunia na kudondoka chini puuuu na kuwa kimya .
Irene alipata mshituko
baada ya kumwona jeni sijui nini ama hawa wanauhusiano upi
Musa akabaki kaduwaa dula
alianza kumpepea irene na kanga ambae alipewa na nasra.
Wakati wote wakishangaa
kudondoka kwa irene kuna bibi aliingia akijiburuza na makalio .
kucheki mguu wa yule bibi
alikuwa kachomwa na msumari kwenye unyayo na kutokeza hadi juu ya mguu
Yaani damu zilichuruzika
mno.
Bibi huyo akiwa amechoka
alisema wajukuu zangu nisaidien nakufaa msumari umenichomaa huku akitokwa na
machozi.
Watu wote walimwangalia
bibi ambae alikua akilia ,
Jeni aliwai kwa yule bibi
ili akamsaidie kitendo cha kumsogelea tyuu bibi
Gafla bibi alipotea kwa
mazingira ya kutatanisha hakuonekana wala ukitizama hamna bata tone la
damu,kilichowashangaza zaidi ni mchana kweupe inawezekana vipi bibi atokee na
kupotea,au ndio chanzo irene kuzimia?
Hii story nafanya kwa
mashabiki zangu tu kama una 500 njoo whatsap unaipata hadi mwisho
Je nini kitaendelea?
Irene akizinduka
itakuwaje?
Huyo bibi vp mchawi?
Gafla akaingia bibi akiwa
anajiburuza na makalio mguu ukiwa umejaa damu .
Bibi alikua kachomwa na
msumari kwenye unyayo hadi kutokeza kwa juu
Jeni aliwai ili
akamsaidie yule bibi ampeleke hospitali ile anataka kumshika,Gafla bibi
alipotea jeni nae alipata mshtuko pale pale akadondoka akapoteza fahamu.
Kaka vp mbona sielewi
mbona jeni nae kadondoka kuna nini musa alimuuliza dula, wakati dula yuko bize
anahangaika kumpepea irene nasra alikua kasimama haelewi chochote na yeye.
Kumbe wakati yule bibi
anakuja akijiburuza na makalio ni jeni pekee ndiye aliye mwona wengine
hawakuona chochote .
Hakika ni jambo la
kutisha musa aliinuka nae akaanza kumpepea jeni hawakuchukua muda sana wote
walizinduka na wakawa wako poa .
Ilibidi wakae chin
wajadili watafanyeje. Ili waishi kama ndugu wasitengane
dula alimuuliza irene ni
kitu kipi kilikufanya paka ukapoteza fahamu
Irene alitoa machozi na
kusema kitu alichokishuhudia irene alianza
kuongea "dula
unafikiri mie nilimwogopa huyu dada sijui ndio jeni mie sikumwogopa tena
nilikuwa nataka nimsalimie ila Nilivyomtizama musa nyuma yake kuna bibi kizee
alikua kakaa amejifunga masantula kiunoni huku shingoni kachomwa kisu
kimetokeza kwa nyuma pia yule bibi alikua analia kwa uchungu huku damu
zikimchuruzika ndio aliyenifanya nikashtuka kwani ninyi hamkumwona?"
Irene alimaliza kuongea
na kuwauliza swali nasra waliangaliana na dula kisha kwa pamoja wakasema hawakumwona
mtu "musa nae akasema hakumwona huyo bibi"
Alibaki jeni ndio
hakujibu jeni aliinuka akageuka kulia kushoto akiwa na hofu kubwa jeni
alishidwa kujizuia ikabidi akamshikilie dula huku analia
Hali iliyomfanya dula
azidi kuchanganyikiwa jeni alilia huku akimwomba dula ampeleke nyumbani maana
alichokiona kina tisha .
Ikabidi dula amtulize
jeni ili nae aeleze kuna nini ,jeni alitulia kisha akaanza kusimulia
"dula wakati wewe
unamapepea irene kuna kabibi kikogwe kalikuja kametokea nyuma ya hii nyumba
kakiwa kanajiburuza na makalio mguuni kamechomwa na msumari yule bibi aliomba
tumsaidie cha ajabu nainuka ili nikamsaidie ile nataka kumshika yule bibi
akapotea".
story na irene na jeni
zinafanana ,kulikoni wao wawili wamwone huyo bibi tu halafu bibi anapotea kuna
nini nyuma ya hili jambo? bibi ni nani kwanini anajitokeza kwa jeni na irene?
swali ambalo halina majibu tuzidi kusonga mbele na story yetu.
Jeni alisimulia na
kumfanya irene ashidwa kuelewa
Musa na nasra wao walikua
kimya hawajui kinachoendelea
jeni alivyomaliza
kusimulia kisa cha huyo bibi,sijui mzimu dula kuna kitu alikumbuka akacheka na
kusema sasa mambo yameiva wakuu walichoniambiaga huenda sasa kinatimia dula
alijiongelesha kimoyo moyo kisha akatabasam na kusema nimepata msaidizi sasa .
We dula unawaza nini
mbona unatabasam mwenyewe musa alimshtua dula na kumuuliza ivo .
Dula alishtuka na
kumwambia musa mdogo wangu hawa wadada wanasimulia ndoto tyu .bibi gani kaja
hapa wamwone wao tyu na sisi tusimwone kisha dula alicheka na kumwambia nasra
amsubiri kuna mahali anaenda dula aliondoka. jeni alimwita dula ila dula
hakutaka kusikiliza mtu.
Dul alikimbia na kuingia
uchochoron musa akashidwa kuelewa dula ananini.
jeni alimwaga musa na kumwambia
anaogopa kukaa tena hapo atamtafuta siku nyingine wapige story jeni aliwasha
gari akaondoka
Sasa akabaki musa na
irene walikaa tena kwenye roba .
musa akiwa na mawazo tele
irene alianza kumuongelesha musa kwa lugha ya upole mbona leo jeni kaja na mambo
ya ajabu yameanza kutokea au jeni nimchawi sielewi mim ,Maana kila jeni ukiwa
nae lazima upate matatizo itakuwa jeni sio binadamu wa kawaida anakuchezea
akili irene alimwelezea musa na kumwambia.
jeni sio bina damu wa
kawaida atakua anatuchezea mchezo nishamshtukia baada ya irene kumaliza kuongea
musa alisapoti maneno aliyoyaongea irene.
Na kukumbuka mateso
aliyeyapitia lazima jeni amwokoe yawezekana jeni ni jini aliyejivika sura ya
binadamu au inakuweje? ,
Wakati mazungumzo
yanaendelea cm ya irene iliita alipokea sauti mama yake ilisikika akimwambia
aende nyumbani hali yake sio nzuri ,pale pale irene alimwaga musa na kutudi
nyumbani.
Alibaki musa peke yake
alianza kuwaza mambo mengi nae akaamini jeni atakuwa ni jini tyu haiwezekani
kila nikipata mkosi jeni anatokea kunisaidia pia mbona haya mambo kama nishawai
kuota halafu nashangaa wao wanasema kuna bibi sijui kachomwa na kisu shingoni
mara amechomwa na msumari mguuni usiku hii ndoto niliiota iweje waseme
wamemwona huyo bibi??.
Bila shaka jeni atakuwa
jini tu musa alijiwazia akakunja roba lake vyema kisha kuingiza ndani chumbani
musa alifunga mlango alivua shati na kubaki kifua wazi.
Mgongoni kwa musa kulikua
na alama "m' imejichora katikati ya mgongo musa aliwaza na kusema hili
geto la ndugu yangu bwana halina hata kioo jana niliota ndoto ya haka kabibi
ambacho wanasema eti wamekaona leo
Yule bibi aliniambia nina
alama mgongoni imeandikwa "m".
Na haitafutika milele
sasa nitaonaje na kuniambia nimefuzu mafunzo ya kupigana sasa mie nilikua
najifunzaga wapi ndoto zingine bana ni uongo tu.
Ukweli musa usiku aliota
ndoto mbaya sana alitokewa na bibi mwenye sura ya kutisha mara ajitokeze
amechomwa na kisu shingoni mara amechomwa na msumari mguuni mara tumbo
limepasuka hakika yule bibi alikua anatisha bala neno moja alilomwambia musa ni
kwamba kuanzia sasa amefuzu mafuzo ya mapigano asaidie kisasi namba yake ni
alama M
Ipo kati kati ya mgongo
Musa alivaa shati
akafunga mlango na kwenda saloon moja. Karibu na anakokaa, lengo lake alitaka
akaangalie kwenye kama ile ndoto inaukweli ili ajue endapo atakuta alama M
Basi ataamini ile ndoto
na kama hataikuta basi itakuwa hio ndoto sio ya ukweli .
Musa alifika saloon
aliingia akawasalimia watu aliyewakuta mle , alivua shati kisha akajiangalia
kwenye kioo hakuona hio alama 'm'
Musa aliguna na kusema
lini ndota ya alfajiri ikawa ya ukweli.
Hamnaga ndoto ya ukweli
labda mtu uote umekojoa ukiamka asubui mkojo utaushuhudia musw alijiongelesha
mle kwenye saloon kisha akatoka na kuwaacha Watu na maswali watu walihisi musa
ni chizi maana kaingia saloon kavua shati kaongea halafu katoka bila kuaga.
Watu walijisemea huyu boy
atakuwa kalogwa maana sijamsoma ni maneno aliyeongea kinyoz.
Musa alirudi geto
akaingia na kulala hadi saa mbili usiku dulq alikua hajarudi bado.
Tukija maeneo ya kawe
beach tunamwona dula amekaa pembezoni mwa bahari aliongea maneno yasiyo
julikana
Dula aliaanza kuita jina
bibi ! Bibiiii
Bibii dula aliita kwa
nguvu
Mala gafla upepo mkali
ulivuma kwa kasi sana baharini mawimbi yakawa yanapiga kwa kasi Dula aliendelea
kuita bibi!!! bibi !!!!
Mara radi ikabiga paaaa
na mngurumo ,Juu upepo ukaongezeka dula akiwa ameangalia Bahari inavyozidi
kuchafuka.
Nyuma aliko kaa dula kuna
kiumbe cha kutisha sijui kimetokea wapi kilisimama nyuma yake kikiwa
kimejifunga shuka jeupee miguu yake ni kwato za punda mdomo meno marefu
yametokeza macho mekundu kile kiumbe kilikua kinafuka moshi.
dula akiwa haelewi
anaendelea kuita bibi kile kiumbe mikono yake ilikua na kucha ndefu kilinyanyua
makucha yake na huyo kiumbe alikaa tayari kuyazamisha mwilin mwa
dula.,inawezekana ,kile kiumbe ama bibi aliyewatokea irene na jene ,huenda dula
anajua kitu kuusu huyo bibi
dula aliendelea kuita
bibi sijui anamwita bibi yupi kile kiumbe kilinyanyua makucha yake kikataka
kuyazamisha mwilin mwa dula
Mara dula aligeuka nyuma
akamwona yule kiumbe akifuka moshi
dula wala hakushituka
alimwambia yule kiumbe mbona wewe umekuja bibi yuko wapi?
ITAENDELEA

0 Comments